Asante Mungu na Watanzania wema

Ndugu zangu, mwaka mmoja uliopita, tarehe 2 Oktoba 2017, nikiwa Mwanza, nilinusa kifo.

Hukumu juu yangu iliyokuwa imetolewa katika jumba kuu, siku tatu kabla, kwa shabaha ya kuninyamazisha kabisa, ilikuwa imebakiza muda mfupi kutekelezwa.

Movements zilizofuata baada ya hapo zilitegemea tukio hilo.

Namshukuru Mungu kwa kunipa watu wema walioshiriki kuepusha ajali hii, ili damu hii isimwagike.

Safari ndefu na chungu niliyoanza tangu siku hiyo ndiyo imenifikisha hapa nilipo, na bado inaendelea. Siku moja nitaiweka hadharani kwa andiko lisilofutika. Naamini Mungu bado ana mipango yake kwa ajili ya watu wake, kwa mikono ya wengine.

Tangu siku ile, maisha si yale yale tena. Tuendelee kuombeana na kusaidiana. Naamini tutafika salama.

Tuzidi kuombeana.

Like
23

Leave a Comment

Your email address will not be published.