TANZANIA ina eneo lenye ukubwa wa 947,303 km² (30th Duniani). Eneo lenye maji ni 6.4% tu. 93.6% ni eneo la nchi kavu. 46% ya ardhi yote inafaa kwa kilimo. Eneo ambalo limetumika halijafika hata 30%.
Qatar ina jumla ya eneo lenye ukubwa wa 11,581 km² (158th Duniani). Eneo lenye maji ni 0.8%. 99.2% ni eneo la nchi kavu. 740 km² (1.8%) ya ardhi hiyo pekee inafaa kwa kilimo na wamelitumia kwa kilimo ipasavyo.
Kwa lugha rahisi tu ni kwamba; mkoa wa Lindi ni mkubwa mara tano (5) zaidi ya nchi ya Qatar. Lindi ina jumla ya eneo lenye ukubwa wa 66,040 km² wakati Qatar ina eneo lenye ukubwa wa 11,581 km².
Mkoa wa Lindi umegawanywa kanda kuu mbili za ikolojia ya kilimo; Pwani wanalima mazao ya miti kama korosho, nazi na maembe. Maeneo ya kati wanalima mahindi, mpunga, ufuta na muhogo.
Lindi, kati ya kaya 224,316, kaya 180,877 (81%) zinajihusisha na kilimo kwa kiasi fulani. Serikali haijawahi kuona sababu za kuwekeza katika kilimo cha mbogamboga na matunda kwa watu wa Lindi.
Leo, Rais wa Tanzania yupo Doha-Qatar anatembelea maonesho ya kimataifa ya kilimo cha mbogamboga na matunda (Doha International Horticulture Expo 2023).
Rais wa Tanzania ambaye nchi yake 46% ya ardhi yote inafaa kwa kilimo. Eneo ambalo limetumika halijafika hata 30% ametembelea maonesho Qatar ambao 740 km² (1.8%) ya ardhi hiyo pekee inafaa kwa kilimo.
Rasilimali za maji Tanzania zinakadiriwa kuwa mita za ujazo (m³) 126 bilioni kwa mwaka, ambapo rasilimali za maji juu ya ardhi ni (m³) 105 bilioni na zilizopo ardhini ni (m³) 21 bilioni. Maji ya kutosha.
Qatar ndiyo walitakiwa kujifunza Tanzania kuhusu kilimo cha mbogamboga na matunda. Eneo lenye maji Tanzania ni ni 6.4% wakati Qatar ni 0.8%. Kilimo cha umwagiliaji nani alitakiwa kuwa mwalimu?
January 2017 serikali ya CCM ilivunja shamba la Kilimanjaro Vegetable, mali ya @freemanmbowetz kwa sababu za hovyo tu kwamba lipo karibu na mto Weruweru. Bila kujali uwekezaji uliofanywa, walivunja.
Miaka sita (6) baadae, watu waliovunja shamba la Kilimanjaro vegetables kwa sababu za ajabu wanakwenda kutembelea maonesho ya kilimo cha mbogamboga na matunda nchini Qatar.
Gelasius Byakanwa baada ya uharibifu alipandishwa vyeo kutoka Mkuu wa Wilaya Hai hadi Mkuu wa Mkoa Mtwara. Akateuliwa kuwa Afisa Mkuu Ubalozi wa TZ, Korea Kusini sasa ni balozi Burundi.
Hakika inasikitisha ukiwa timamu. Penye miti mingi hakuna wajenzi.
Uchambuzi huu umeandikwa na Martin Maranja Masese.