Twitter yatambua rasmi Kiswahili

KISWAHILI kinazidi kukua, kuenea, na kutambulika duniani. Mbali na vyuo vikuu zaidi ya 100 vyenye programu za Kiswahili, na makumi ya vituo vya redio vyenye matangazo kwa lugha ya Kiswahili sehemu mbalimbali duniani, hata mtandao wa kijamii Twitter nao sasa umetambua rasmi lugha hiyo.

Awali, Twitter haikuweza kutofautisha maneno ya Kiswahili na Kiindonesia. Lakini sasa lugha hii, ambayo tayari ni moja ya lugha rasmi za Umoja wa Afrika, inayozungumzwa kama lugha ya taifa ya Tanzania, Kenya na ambayo ni lugha rasmi ya mataifa kadhaa ya Afrika Mashariki, imekuwa rasmi lugha ya Twitter pia.

Like
1

Leave a Comment

Your email address will not be published.