KAMISHNA Jenerali Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amewataka wananchi kuacha kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya kama bangi kwa kutumia mavazi, maneno na hata mitandaoni
Orodha inajumuisha ambao comment zao mitandaoni na mitaani huonesha kutetea bangi na amesema atakayefanya hivyo atapimwa na akibainika anatumia dawa hatua zitachukuliwa
Aretas Lyimo amesema: “Maabara ya kisasa ikikamilika tutashughulika na wote. Mtu akihamasisha matumizi ya dawa za kulevya tunamkamata tunaenda kumpima tukikuta anatumia dawa za kulevya tunampeleka Mahakamani.”
Nawaagiza DCEA wakiongozwa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo wanipe maelekezo, wapi niwafuate
Wanipime mimi, Martin Maranja Masese, MMM, Mtikila, kwa sababu nasema kilimo cha bangi (cannabis) ni manufaa sana kwa sasa kuliko mazao mengi sana ya biashara
Nitawapa mifano mingi, watu timamu watanielewa. Nitawaeleza kilimo cha bangi kilivyosaidia jamii zetu huko Tarime na hata kusaidia kujenga shule na vituo vya afya.
Robert ‘Bob’ Nesta Marley aliipenda wazi bangi na kuisifia na alisema watu wasiichafue kwa kusema ni kitu kibaya. Bob Marley alikuwa muumini wa Rastafarian. Bangi chakula.
Rastafarians wanaamini bangi imehalalishwa na kuagizwa na biblia kwamba siyo kosa kuivuta. Zaburi 104:14 inasema: “Huyameesha majani kwa makundi, Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; Ili atoe chakula katika nchi.”
Rastafarians kwa kutumia mstari huu wanaamini Mungu ameweka majani ardhini ili yatumike kwa matumizi ya binadamu. Hili ni kundi kubwa la imani linaloamini bangi katika mtazamo huo.
Bob Markey ni msanii namba moja duniani ambaye alijitolea maisha yake kuimba na kusema na kujitokeza hadharani kutetea haki za watu dhidi ya tawala kandamizi na mafashisti.
Muziki wa Bob Marley uliwaponya watu wengi waliokuwa wanaugua maradhi sugu ya ujinga. Bob Marley ndiye mwanamuziki wa Reggae ambaye anaheshimika zaidi Duniani.
One Love ni wimbo mkubwa sana duniani. Huu ni wimbo bora milenia (miaka 1000) hii ni kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC – British Broadcasting Corporation).
Kwa mujibu wa jarida maarufu la New York Times, Bob Marley anatajwa kuwa ndiye mtu mwenye ushawishi mkubwa zaidi duniani katika nusu ya pili ya karne ya 20 (1950 – 2000).
Katika orodha ya waimbaji bora wa wakati wote kuwahi kutokea duniani katika Rolling Stone, Bob Marley anakamata nafasi ya tisa, na katika hiyo orodha Michael “Wacko Jacko” Jackson yupo nafasi ya 25.
Mwaka 1976, Bob Markey alijitolea kufanya tamasha la bure, Jamaica. Ulikuwa ni wakati wa mgogoro mkubwa wa kisiasa kati ya vyama viwili vikubwa, Jamaica Labour Party (JLP) na People’s National Party (PNP)
Bob Marley akataka kufanya tamasha la kuwapa elimu watu wa Jamaica wapinzani wa Waziri Mkuu wa Jamaica, Michael Manley, aliyekuwa ameandaa tamasha hilo.
Siku moja kabla ya tamasha, Bob Marley akiwa kwenye mazoezi kwa ajili ya tamasha hilo, akavamiwa na watu wawili wenye silaha, wakamtandika risasi, mbili zikampata na kumjeruhi vibaya. Hii risasi ilibaki mwilini kwake hadi alipofariki.
Bob Marley akakimbilia Uingereza akiwa na Peter Tosh na Bunny Wailer. Huko ndipo alipojichimbia na kuandika nyimbo nyingi zaidi. Waiting in Vein na One Love aliziandika akiwa Uingereza.
Akiwa Uingereza akakamatwa na kutupwa gerezani kwa mwezi mzima baada ya kukutwa na viroba vya bangi. Unajua kisa cha kuandikwa kwa wimbo maarufu wa Bob Marley unaitwa Three Little Birds?
Alipotoka gerezani akapata pisi kali, Cindy Breakspeare, Miss World mwaka 1976. Huyu ndiye mama yake Damian Marley. Penzi likakolea, akaingia studio kuandika Three Little Birds. Ngoma ya nne album ya EXODUS.
Wimbo huu wa Three Little Birds ulifikia 20 bora nchini Uingereza, na kushika nafasi ya 17 katika chati za muziki. Ni moja ya nyimbo maarufu za Bob Marley na imerejewa kwa kufanyiwa cover na wasanii wengine wengi.
Jamaica, vuguvugu la kisiasa likazidi kupanda, serikali ya waziri mkuu, Michael Manley ikatuma ujumbe kumbembeleza Bob Marley arejee Jamaica, ili kuwatuliza wananchi. Bob Marley akarejea Jamaica. Akawatuliza wananchi.
Kwanini nimetoa hii hadithi fupi ya Bob Marley?
Nimejaribu kuwaonesha jinsi mvuta bangi huyu alivyokuwa na heshima kubwa katika macho ya watu wengi. Kamishna Jenerali anayesema atasaka wanaotetea bangi wakapimwe, hana alama hata moja kijijini kwao, achilia mbali Tanzania.
Ni makosa makubwa sana kuchanganya cannabis katika kundi la dawa hatari za kulevya. DCEA, msiweke Cannabis kundi la Narcotics. Hizo ni sheria za kikoloni.
Dunia haipo huko tena. Dunia imewaacha. Mnatakiwa kushughulika na Heroin, Morphine, cocaine, Opiates, Demerol, Methamphetamine, Codeine na jamii zake
Narcotics inasababisha Loss of consciousness, Tremors, Slow, shallow breathing, Clammy skin, Convulsions, Coma, Death. Hizi sasa ndiyo dawa za kulevya
Lakini cannabis (marijuana na hashish) hakuna madhara hayo kwa kuvuta mkwaju mmoja tu. Kwani uongo? Hakuna kifo kilichosababishwa na bangi katika jamii zetu
Shule ya sekondari Kewamamba, Tarime, imejengwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji cha Nkerege kwa kutumia fedha za bangi na mwaka 2021 ikapokea kidato cha kwanza
Sekondari hiyo imejengwa kutokana na kilimo cha bangi katika bonde la Nkerege, kijiji cha Nkerege, kata ta Kiore, wilaya ya Tarime. Wananchi wametumia fursa
Kama serikali ya mkoa wa Mara haitaki walime bangi, wananchi wapewe elimu ya kulima ngano katika hizo ekari 1,600+ ambazo wameteketeza mazao ya bangi
Wafanyabiashara ya zao la ngano wale wote waliokuwa wakiagiza ngano kutoka nje ya nchi sasa waelekezwe kwanba wanunue 60% ya ngano hiyo nchini Tanzania
Hii itatumika kama njia ya kukuza soko la wakulima kwa kuwapatia soko la uhakika na kuhakikisha nchi inajitosheleza kwa ngano ambayo sasa tunanunua nje.
Tanzania inanunua tani 863,000 za ngano kutoka nje ya nchi huku uzalishaji wa ndani wa zao la ngano ukiwa chini ya tani 100,000. Tani zaidi ya 700k inatoka nje
Kwa kuwa bei elekezi ya serikali ya kununua ngano ni Sh800 kwa kilo, wananchi wa Nkerege wakilima ngano katika ekari 1,600 watapata fedha nyingi sana
Kama ngano inachukua muda mrefu, wapewe elimu na utaalam wa kilimo cha mazao ya muda mfupi kama pamba na Aluzeti.. au hata vitunguu wauze nje ya nchi
Lakini bangi imekuwa ‘legal’ nchi nyingi sana.. kwanini serikali isizuie ‘consumption’ pekee yake na ikawa ni ruhusa kutumika kibiashara, ku’ export? AKILI
Kuna fursa kubwa Duniani ambayo haidumu kwa muda mrefu.. pindi Dunia nzima ikianza kuruhusu matumizi ya ‘cannabis’ bei zitashuka. Sasa tungetumia fursa hii
Ardhi ya Tarime imependana na cannabis. Watu waruhusiwe kulima bangi. Atafutwe mwekezaji aweke plant kubwa ku’ extract the substance needed for medical cannabis
Watu wa Tarime watapata pesa, wataajiriwa, watapata maarifa, watakuwa na mtaji na kuanzisha viwanda. Wakulima wanakuwa outgrowers to feed the processing plan
SATIVA inalimwa sana Tanzania maeneo ya Tarime. Ingawa INDICA ndiyo ipo katika soko la Dunia. Inauzwa €4,000 (Sh 10,561,873) kwa kg Netherlands na wanalima indoor.
Akili ndiyo kitu watu katika serikali walinyimwa. Huu ushauri serikali ya kifarauni ya CCM haiwezi kuchukua… ni small minded.. wanaishi Dunia ya pekee yao. Wamejifungia.