MASHIRIKA matatu yenye dhamana mtambuka katika habari, sheria, na haki za binadamu leo yamezindua ripoti ya utafiti juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika maeneo ya hifadhi nchini Tanzania.
Mashirika hayo ni the Centre for Strategic Litigation (CSL) lenye makao makuu Zanzibar, SK Media East Africa lenye makao makuu Nairobi (Kenya), na Media Brains la Dar Es Salaam.
Katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena, Dar es Salaam, miongoni mwa walioshiriki ni wanahabari, watetezi wa haki za binadamu, wanasheria nguli, na baadhi ya waathirika wa ukiukwaji wa haki za binadamu kutoka maeneo mbalimbali Tanzania.
Utafiti uliozaa ripoti hii ulifanyika kati ya 2022 na 2023, ukishirikisha waandishi wa habari walioteuliwa kutoka mikoa yote ya Tanzania, Bara na Visiwani. Walipewa mafunzo maalumu ya utafiti, ufuatiliaji na ukusanyaji wa taarifa za ukiukwaji wa haki za binadamu katika mikoa waliyopangiwa.
Ripoti ya utafiti, ambayo imeambatanishwa hapa.chini, inaonyesha, kwa kifupi, hali halisi katika kila mkoa.
Mpiga picha wetu, Fidelis Felix, alikuwepo. Zifuatazo ni baadhi ya picha za hafla ya uzinduzi huo.
NAKALA YA RIPOTI INAPATIKANA HAPA:Conserving Our Rights -Uncovering Human Rights Violations in Tanzania's Conservation Sector
Habari kamili itachapishwa katika ukurasa huu, na uchambuzi wake kwa video utafanyika katika ukurasa wetu wa SK Media Online TV kwenye mtandao wa YouTube.