Rais Samia vunja Baraza la Mawaziri – Wanasheria

BARAZA la uongozi la Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) limemshauri Rais Samia Suluhu Hassan avunje na kuunda upya baraza la mawaziri na ngazi nyingine za uongozi wa juu ili kutekeleza matakwa ya kikatiba.

Mwongozo wa baraza hilo uliotolewa kwa umma jana unaeleza namna Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyomtaka rais mpya, bila kujali amepata madaraka hayo kupitia sanduku la kura au njia nyingine halali kuingia Ofisi Kuu – Ikulu baada kiongozi aliyepo madarakani kupata madhila yoyote yanayomzuia kuendelea na majukumu, ikiwamo kifo.

Jana, Tanzania ilipata rais wake mpya, aliyekuwa Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia Suluhu Hassan baada ya kifo cha Rais John Magufuli. Alifariki Jumatano, Machi 17, 2021 katika Hospiali ya Mzena, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa baada ya kukumbwa na shambulio la ugojwa wa moyo.

Baraza hilo katika mwongozo wake uliosainiwa na rais wake, Dk. Rugemeleza Nshala linaeleza kwamba Rais Samia, endapo atafanya hivyo, atakuwa na uhalali wa kikatiba na kisheria kufanya kazi ya kuongoza nchi bila “mkanganyiko.”

Mwongozo huo unaeleza kuwa ni vyema mawaziri hao kula viapo upya mbele ya Rais Samia kwani kiapo lazima kifanywe kwa rais aliyepo na siyo aliyeondoka madarakani; kwani kiapo kwa raisi hakimishwi kwa rais mwingine.

Tafadhali sikiliza hapa na soma mwongozo huo.

Like
2