Rais Samia Suluhu ni AMIRAT JESHI MKUU

RAIS wa Tanzania, kwa mujibu wa Katiba, ndiye kiongozi mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama.

Mara zote, tangu kupatikana kwa uhuru – Desemba 9, 1961, marais wa Tanzania wamekuwa ni wanaume; kuanzia kwa Julius Kambarage Nyerere (1962-1985), Ali Hassan Mwinyi (1985-1995), Benjamin William Mkapa (1995-2005), Jakaya Mrisho Kikwete (2005-2015) na John Pombe Magufuli (2015-2021).

Hawa wote walikuwa wakivaa cheo kingine kikubwa; AMIRI JESHI MKUU.

Amiri ni neno la Kiarabu lenye maana ya “kiongozi mkuu mwanaume.”

Lakini sasa Tanzania imempata kiongozi mwanamke, hivyo badala ya kuitwa AMIRI (mwanaume), yeye anakuwa AMIRAT (mwanamke).

Amirat lina asili ya Kiarabu na lugha kadhaa za Afrika, na humaanisha “Malkia.”

Kwa sababu hiyo, SAUTI KUBWA inashauri wanasiasa, vyombo vya habari na wananchi kuwa, kama vile ambavyo kwa Kiingereza hatuwezi kumwita Mr President bali Madam President, hata katika cheo hiki sasa Rais Samia Suluhu Hassan hawezi kuitwa Amir Jeshi Mkuu bali AMIRAT JESHI MKUU.

Tulitumie, litazoeleka.

Like
8