UROHO wa fedha na hofu ya hadhi kwa baadhi ya timu na nchi, vinaweza kutajwa kuwa sababu kubwa ya kukwamisha kuanza ligi mpya na iliyotarajiwa kuwa na mvuto zaidi duniani; European Super League (ESL).
Hadi kufikia Aprili 21, mwaka huu, jumla ya timu nane, kati ya 12 zilizokubali awali kushiriki ligi hiyo ya timu kubwa kutoka Ulaya, zilikuwa zimejitoa bila kueleza sababu za msingi za kufanya hivyo. Timu zingine nane zilikubali kuwemo kwenye ligi hiyo na kuifanya kuwa na timu 20 zilizotarajiwa.
Yapo maswali mengi juu ya hatma ya ligi hiyo yanayoulizwa na wadau waliojiandaa kuipokea kwa shangwe na ushabiki mkubwa kuliko unaoshuhudiwa sasa kwenye ligi kubwa duniani, zikiwamo za Italia (Seria A), Uingereza (EPL), Ulaya (UEFA), Ureno (PPL)na nyingine.
Wengi wamekuwa wakiuliza; je, tatizo ni timu bnafsi, nchi zao, matajiri wao au sheria? Je ni nini hatma yake? Mashindano hayo yamekubalika kwa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), au yamekataliwa?
Ligi hiyo ya ESL lilikuwa wazo tangu miaka ya mwisho ya 1980 ambapo baadhi ya watu wenye nguvu ya fedha katika soka walipanga kuanzisha ligi yao, hususani timu za Bara la Ulaya hasa zile zenye majina makubwa na wafuasi (mashabiki) wengi katika ligi zao na duniani kuwa na ligi yao peke yao yenye ushindani.
Timu ambazo zilikubali kujiunga na ligi hiyo ni: Liverpool, Manchester United, Chelsea, Tottenham, Arsenal, Manchester City, Notts Forest & Aston Villa (kutoka England); Barcelona, Real Madrid, Atlético Madrid, Sevilla (Hispania); Juventus, AC Milan, Inter Milan (Italia); Bayern Munich, Dortmund, Hamburg (Ujerumani); PSG and Marseille (Ufaransa).
Lengo la kuanzisha ligi hii ni kutaka kuleta mvuto zaidi katika soka duniani, hasa kwa vijana, kusaidia timu hizo kupata fedha nyingi zaidi ili kuanzisha vyuo vya mchezo huo na pia kuchochea hamasa ya upendo kupitia soka.
Florentino Perez, Rais wa klabu ya Real Madrid ambaye amekuwa kinara wa kuanzishwa kwa ligi, akijaribu kujibu swali, “kwanini vijana wengi wa umri Kati ya miaka 16 – 24 wamepoteza matumaini na soka?” Alisema: “Wengi wamekuwa hawafuatilii kwa sababu hakuna mvuto, hivyo tunaanzisha ligi kubwa yenye mvuto zaidi na yenye uwazi wa hali ya juu katika uamuzi na ubora wa soka.”
Hata hivyo, pamoja na sababu nyingine, kumekuwepo kwa minong’ono kwamba huenda FIFA haipendi sana kuwepo kwa ligi hiyo mpya, kwa kuwa haikwa wazo leke, hivyo kujiandaa kupokea “malipo” kidogo ikilinganishwa na ligi ambazo zimeanzishwa na shirikisho hilo. Haiko wazi ni asilimia ngapi FIFA ingekuwa inapata kutokana na kuanza kwa ligi hiyo.
Mchambuzi mmoja wa masuala ya soka kutoka Uingereza, Steve McManaman, akizungmzia ligi hiyo iliyopigiwa chapio zaidi na matajiri wakubwa wa timu shiriki, alisema kuanza kwa ligi hiyo kunaweza kuinua zaidi soka, lakini haiondoi hatari ya kufifisha mchezo huo, ikiwa umakini hautafanyika na kuzigatiwa wakati itakapoanza.
Wapo pia baadhi ya wachezaji maarufu duniani ambao wanaona kuanza kwa ligi hiyo ni kuharibu mfumo wa ligi nyingine maarufu duniani. Wasiwasi wao ni “kutembezwa” kwa kiwango kikubwa cha fedha na si “utamu” wa soka lenyewe. Miongoni mwao ni Bruno Fernandez (Manchester United), Mesut Ozil (Fernabach) na mchezaji mstaafu wa soka, Gary Neville (Manchester United).
Mpaka sasa haijulikani nini hatima ya ligi hiyo ya Europe Super League (ESL), itakuwepo ama haitokutokuwepo japo FIFA na mashabiki wanaonekana kuipinga vikali.