Mbowe ashinda kesi nyingine

Hukumu ya kesi ya Freeman Mbowe na wenzake katika shauri namba 3 ya mwaka 2020 katika mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki

Kesi imekuja kwa ajili ya hukumu

Mawakili wa Freeman Mbowe wanaongozwa na
John Mallya
Sheck Mfinanga
Jebra Kambole

Vivian Method ndie wakili wa serikali
Waleta maombi wali state kila nchi mwanachama wa EAC analazimika kufuata utawala wa bora na misingi ya Kidemokrasia

Na sheria inaruhusu Jumuiya kusitisha uanachama wa mwanachama ambaye atakiuka utawala bora au utawala wa kidemokrasia au atakayekiuka misingi ya haki za binadamu
Hukumu ipo tayari na itasomwa punde

Waleta maombi ni

Freeman Mbowe
Sharif Hamad (marehemu)
Zitto Kabwe
Hashim Rungwe
Salum Mwalimu
LHRC

Mjibu Maombi ni Mwanasheria mkuu wa Serikali
Katika shauri hili namba 3 la mwaka 2020 waleta maombi waliomba mahakama hii itamke kuwa sheria ya vyama vya siasa ni batili

Wote waliwakilishwa na mawakili tajwa

Waleta maombi walisema sheria inakiuka misingi ya kidemokrasia na kukiuka mkataba wa jumuiya ya Afrika mashariki
Ndio msingi wa kuundwa kwa Jumuiya,

Jaji anasoma vipengele kadhaa vya kisheria ambavo vilitumiwa na waleta maombi

Vipengele ambavo vinalalamikiwa kwenye sheria ya vyama vya siasa ni pamoja na kifungu kinachompa Msajili wa vyama vya siasa kuingilia wakati wowote shughuli za
chama cha siasa

Kifungu kinachompa mamlaka msajili awe na mamlaka ya kuingilia mafunzo mbalimbali ya vyama vya siasa

Kifungu kinachompa msajili mamlaka ya kuingilia uongozi wa chama cha siasa
Vifungu vyote hivi vinakiuka misingi ya utawala bora,misingi ya kidemokrasia na inakiuka mkataba wa EAC

Kifungu kinachompa msajili kumsimamisha uanachama mwanachama yeyote kushiriki shughuli za kisiasa
Sasa Jaji anasoma mambo ambayo mahakama imezingatia

Mosi, Kama mahakama ina mamlaka ya kusikiliza na kuamua shauri hili

Pili, Kama sheria tajwa imekiuka mkataba wa jumuiya

Na kama waleta maombi wana haki ya kufile case husika
Hivo waleta maombi wanaomba mahakama hii itamke kuwa sheria hiyo ni batili na mahakama hii itoe amri kuwapa kila aina ya nafuu ya kisheria

Mjibu maombi ambaye ni WS amejibu kuwa sheria hiyo haikusudii kukiuka mikataba ya kimataifa

Hivo anaomba mahakama itupilie mbali ombi hili
Mahakama hii ina mamlaka kamili ya kusikiliza shauri hili licha ya ukweli kuwa mleta maombi namba nne ametangulia mbele ya haki

Jaji anasoma kesi mbalimbali ambazo mahakama hii imefanya uamuzi kwenye mashauri yanayofanana na hili na ambayo yapo kwenye nchi wanachama
Mahakama hii inaona kuwa nchi wanachama wanapaswa kuheshimu mkataba pamoja na mkataba wa haki za binadamu wa Afrika.

Ni jukumu la nchi wanachama kuhakikisha ustawi wa watu, kulinda demokrasia pamoja haki za binadamu
Mahakama hii inaona kuwa ni lazima sheria inayotungwa kwenye nchi wanachama izingatie haki za binadamu, ni lazima sheria iwe wazi kwa watu wake wajue kipi kinakatazwa na kipi kinakubali
Section 4 ya sheria ya vyama vya siasa
Kifungu hiki kinahusu mafunzo ya makada wa vyama vya siasa,na sheria inataka kabla ya mafunzo lazima chama cha siasa kipeleke kwa msajili material yote ya kufundishia yeye msajili ndio akubali kama hayo mafunzo ni sawa ama la
Na kwamba sheria kumpa msajili uhuru wa kuingilia mambo ya ndani ya chama cha siasa!
Na kwamba msajili sio mtu huru kwa kuwa anateuliwa na mwenyekiti wa chama cha siasa.
Ni maoni ya mahakama hii kuwa sheria hii inampa msajili nguvu kubwa dhidi ya vyama vya siasa jambo ambalo ni kinyume cha mkataba wa Jumuiya
Kifungu hiki kinakiuka haki ya kujieleza na haki ya kukutana kinyume cha mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Kifungu hiki kinakiuka misingi ya Kidemokrasia na utawala bora kinyume cha mkataba wa Jumuiya kwa nchi wanachama
Waleta maombi walilalamikia hiki kifungu kwa kuwa kinatoa mamlaka makubwa ya msajili kupangilia nini chama kifanye

Na kiongozi cha cha siasa atakayekiuka sheria hii anatenda kosa la jinai na msajili atamfungia kwa muda atakaoamua yeye msajili
Mjibu maombi alijibu kuwa kifungu hiki kinalenga kufanya serikali itambue, ijue kila tukio linalofanywa na vyama vya siasa, Na kwamba

Mahakama hii inaona kuwa kifungu hiki kinakiuka mkataba wa EAC
Kuhusu kifungu cha tisa cha orodha ya wanachama au viongozi waleta maombi wanasema kifungu hiki kipo shallow mno na kinatoa haki upande mmoja na kuichukua kwa upande mwingine jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa chama cha siasa

Kifungu hiki kinaweza kutumiwa vibaya na msajili
Section 9, Kifungu hiki kinampa msajili mamlaka ya kuchukua orodha ya wanachama/viongozi kutoka kwa vyama vya siasa kwa muda wowote atakaona unafaa

Pia kifungu hiki kinazuia mafunzo ya ukakamavu kwa wanachama wake, mafunzo yoyote au kuunda vikosi kama green guard,etc
Hata hivo mjibu maombi alisema kuwa kifungu hakina shida kabisa na kinatekelezeka bila tatizo lolote

Waleta maombi wanasema kuwa sheria kusema kuwa maamuzi yafanywe tu na mikutano mikuu ni kuzuia haki hiyo ya kuungana
Hii ni kinyume cha haki ya kukusanyika

Kifungu hiki kinataka uamuzi wa vyama kuungana ufanywe na mikutano mikuu ya vyama vya siasa! Na ufanywe miezi mitatu kabla ya uchaguzi
Section 15, Waleta maombi wanalalamika Kifungu hiki ambacho kinahusu vyama kuungana kuwa kinakiuka haki ya kukusanyika kwa kuwa kinakosa uhalali hasa kwa kuwa kifungu kinataka muungano uwe tu wakati wa uchaguzi
Yaani vyama vinaweza tu kuungana wakati wa uchaguzi mkuu
Msajili ana mamlaka ya kuandika kusudio la kufuta chama cha siasa kitakachokiuka sheria hii na ataandika kusudio hilo kwa wanachama

Hata hivo mjibu maombi anasema kuwa kifungu hiki kimezingatia utawala bora na hakijakiuka mkataba
Waleta maombi wanasema msajili kuwa na mamlaka ya kuadhibu mwanachama/kiongozi na chama chenyewe ni kuminya haki ya ustawi ya vyama vya siasa

Pamoja na kukiuka haki ya kushiriki katika demokrasia kwa wanachama/wananchi
Ni sheria katili inayompa mamlaka ya kiimla Msajili
Section 29, Kifungu hiki kinasema mtu yeyote atakayekiuka sheria hii atapigwa faini ya 1mil ambayo haitazidi 10mil au kifungo kisichozidi mwaka

Chama cha siasa kikikiuka sheria hii kinaweza kupigwa faini hadi 30mil au kufutwa
Hitimisho

Mahakama hii ina declare kuwa sheria ya vyama vya siasa inakiuka vifungu vya mkataba sehemu 6d 72 ya Jumuiya ya Afrika

Jamhuri ya Tanzania inaamriwa kurekebisha sheria ya vyama siasa iendane na mkataba.

Gharama za kesi kwa kila mmoja

Jaji anahitmisha.

Like