Mashehe wamponza Mwigulu. Barua ya iliyomwingiza matatani hii hapa

PAMOJA na sababu nyingine zilizomfukuzisha Mwigulu Nchemba uwaziri wa mambo ya ndani, kubwa inayosemekana kumkasirisha zaidi Rais John Magufuli ni barua ya waziri kutengua zuio la idara ya uhamiaji dhidi ya mashehe wanane wageni waliotakiwa kuondoka nchini

Akijibu rufaa ya wenyeji wa mashehe hao na kuruhusu wageni wao waendelee na shughuli yao ya kueneza dini, waziri anamalizia barua yake kwa maneno matatu makali: “UCHAMUNGU SI UGAIDI.”

SAUTI KUBWA ina nakala ya barua hiyo, ya tarehe 27 Juni 2018, na imeambatanishwa hapa. Nchemba alifukuzwa kazi siku tatu baada ya kuandika barua hiyo.

Barua hiyo yenye kumbukumbu Na. 2SAB 134/313/01, iliyosainiwa na Nchemba mwenyewe, imeelekezwa kwa mwenyeji wa mashehe hao, Arif Yusuf AbdulRehman, mwenyekiti wa Darul Islamic Centre ya Dar es Salaam.

Ina kichwa cha habari kisemacho: “Kuzuia kuondoshwa kwa mashekhe na idara ya uhamiaji.” Waziri anaandika:

“Rejea kichwa cha habari hapo juu kuhusu mashekhe (08) kuondoka nchini ndani ya siku saba (07).

“Nimepokea maelezo yako, na kwa kina nimepitia sababu za rufaa yako kwangu na maudhui ya ujio wa mashekhe. Kwa kuwa taasisi yako imesajiliwa kwa mujibu wa sheria, na wageni wako hawa ujio wao unatambulika, wakiwa wamefanya kazi na taasisi rafiki iliyopo Zanzibar;

Nimefuta amri iliyotolewa na uhamiaji (ya) kuwataka mashekh hao kuacha shughuli yao ya kueneza dini. Kuna mapungufu yanayotajwa ya mawasiliano kati ya taasisi yako na BAKWATA; ni jambo la kushughulikiwa tu huku viongozi hawa wa kidini wakiendelea na madhumuni yao ya kueneza dini.

“Nimeelekeza taasisi za dini na ofisi zingine zote zinazohusika kuwa wanashughulikia masuala ya kiutawala kwa hekima, kuondoa kutiliana mashaka na kuathiri uhuru wa kuabudu kwa taasisi za kidini hapa nchini. UCHAMUNGU SIO UGAIDI.”

 

Mh. Dkt. Mwigulu L. Nchemba Madelu

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI

 

Soma nakala ya barua iliyosainiwa na Mwigulu:

Like
4

Leave a Comment

Your email address will not be published.