MAHAKAMA KUU YANUSURU WANACHADEMA WALIOSINGIZIWA UBAKAJI

Na Martin Maranja Masese

WANACHAMA wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Katala Kikaja na Ng’hulima Lilanga, wakazi wa kata ya Dutwa, Wilaya Bariadi, Mkoa Simiyu, walihukumiwa kitumikia kifungo cha maisha gerezani.

Katala Kikaja na Ng’hulima Lilanga walikuwa mawakala wa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA katika jimbo la Bariadi, kamanda Benard Makoye Maendeleo

27.10.2020 kama wengine, walipokea vitisho wasiende kusimamia kura za CHADEMA katika vituo vya uchaguzi. Wao wakaamua kupuuza vitisho hivyo.

28.10.2020 wakawahi katika vituo vya kupiga kura kama mawakala wa CHADEMA. Dutwa A na Dutwa B. Wakaelezwa mawakala wamezuiwa wasiingie.

Wakaendelea kubaki ndani ya vituo vya kupiga kura wakisubiri zoezi la kupiga kura lianze. Ghafla wakaingia askari polisi. Wakatumia nguvu kuwakamata wote.

Wakapelekwa kituo cha polisi bila kuelezaa makosa waliyopewa. Uchaguzi ukafanyika. Matokeo ya uchaguzi yakatangazea wakiwa wapo mahabusu ya Polisi.

Mwezi mmoja baadae wakapandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu kwa tuhuma za ubakaji na unyang’anyi wa kutumia silaha. Wakashangaa sana.

Hati ya mashtaka inaeleza alfajiri 28.10.2020 katika kituo cha kupiga kura walimkuta msimamizi msaidizi wa uchaguzi ambaye walimbaka kwa zamu.

Baada ya kumbaka wakampora pesa taslimu TZS 300,000/- na baada ya kufanya hivyo wakaendelea kubaki kituo cha kupiga kura kama MAWAKALA.

Hati ya mashtaka bila kumtaja huyo mtu aliyebakwa na hakuwahi kuitwa mahakamani kutoa ushahidi, aliwasilisha ushahidi wake kwa njia ya maandishi.

Mahakama ikaeleza kwamba hiyo ni kulinda UTU wa shahidi huyo wa upande wa Jamhuri. Mahakama ikawakuta na hatia na kuwakuhumu kifungo cha maisha

Tangu 28.10.2020 wanahamishwa magereza ya mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mwanza. 12 April 2022 wakahukumiwa kutumikia kifungo cha maisha gerezani

Uongozi wa CHADEMA kanda ya Serengeti walikata rufaa baada ya hukumu hiyo ya kihuni iliyowatia hatiani makamanda Katala Kikaja na Ng’hulima Lilanga

Waliamua kukata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, kanda ya Shinyanga. Nitakupitisha katika hukumu, ujionee JAMHURI ilivyokuwa HOVYO.

Jaji Athumani Matuma

Jaji Athumani Matuma akisoma uamuzi wa Mahakama ya Rufani anasema upande wa mashtaka (Jamhuri) walifanya jitihada kubwa za kuficha taarifa zote.

Kwamba warufani (washtakiwa) walikuwa mawakala wa CHADEMA katika kata ya Dutwa iliyopo katika Jimbo la Bariadi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020

Jaji Athumani Matuma anasema hoja za Mawakili wa upande wa utetezi (mawakili wa washtakiwa zote zina Mashiko). Amezipitia na kuziona zimebeba misingi.

Jaji Athumani Matuma anasisitiza, Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu aliyesikiliza shauri hili hatua za awali, hakufuatilia Ushahidi kwa kina,

Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu aliamua kuwatia hatiani Watuhumiwa hao wawili kwa ushahidi wenye kutia shaka. Ushahidi usiothibitika.

Ushahidi wa upande wa utetezi kutoka kwa aliyekuwa mgombea udiwani wa CHADEMA, ulionyesha mshtakiwa namba 1 alikuwa kituo cha kupiga kura.

Mshtakiwa namba 2 alikuwa dereva wa mgombea udiwani katika uchaguzi huo. Hoja zote zilifichwa na Upande wa Jamhuri, kwa maelezo ya hukumu ya Jaji.

Jaji Athumani Matuma anasema mazingira ya kesi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu ilitakiwa kutambua kwa kina ushahidi wa Watuhumiwa, bila kupuuza.

Hususani kwa kuzingatia ilikuwa usiku. Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu hakuelekeza akili yake sawa sawa kwenye utoaji wa hukumu hiyo.

Upande wa mashtaka walipaswa kumleta msimamizi wa uchaguzi (returning officer) kuthibitisha kama kweli matukio hayo tajwa (ubakaji na uporaji) yalitokea.

Upande wa mashtaka hawakumleta msimamizi wa uchanguzi. Msimamizi wa uchaguzi alikuwa ni shahidi muhimu katika kesi hii, hakuletwa Mahakamani.

Msimamizi wa uchaguzi alikuwa lazima atoe ushahidi kwa kuwa kulikuwa na upotevu wa vifaa vya uchaguzi kwa mujibu wa taarifa yao ya upelelezi.

Hakuna ofisa yeyote wa Polisi aliitwa na kufika Mahakamani kuthibitisha kama kweli kuna tukio la wizi wa vifaa vya kupiga kura lilitokea katika kituo hicho.

Kutoitwa Afisa wa Polisi yeyote kutoa ushahidi Mahakaman katika shauri hili, kunafanya hata ushahidi mwingine wowote kutoaminika na kukosa nguvu.

Nani ambaye alithibitisha kwamba kulitokea wizi wa vifaa vya tume ya taifa ya uchaguzi na uporaji wa fedha kama Polisi hajafika? Afisa gani wa polisi alipeleleza?

Jaji Athumani Matuma anasema, katika hali ya kushangaza upande wa mashtaka walimkataa shahidi Pili Masunga ambaye alikuwa shahidi wao muhimu.

Na wao (upande wa mashtaka) walishindwa kumleta mahakamani na baadae washtakiwa walimleta kuwa shahidi upande wao, lakini alikataliwa na Jamhuri.

Jaji Athumani Matuma anaendelea kusoma uamuzi akisema, kushindwa kuwaleta mashahidi muhimu ni jambo baya katika ushahidi wa mashtaka ya Jinai.

Shahidi Pili Masunga alikataa kwanba hakuna tukio lililotokea nyumbani kwake ambapo walalamikaji walisema matukio yalifanyika nyumbani kwa Masunga.

Jaji Athumani Matuma anasema, upande wa mashtaka (Jamhuri) walishindwa kuleta na kuwasilisha mashahidi na ushahidi wao muhimu mbele ya Mahakama.

Walifanya kila linalowezekana kuzuia washtakiwa na mashahidi wao kutoa ushahidi Mahakamani. Jaji akakemea vikali sana tabia hii mbaya ya Jamhuri.

Jaji anasema utambuzi wa ubakaji ulifanyika nyumbani kwa Pili Masunga kwanini Jamhuri hawakumleta Pili Masunga kutoa ushahidi kama shahidi wao muhimu?

Jaji Athumani Matuma anasema ushahidi wa Jamhuri uliosalia Mahakamani, kamwe hauwezi kuwatia hatiani washtakiwa kwa tuhuma za ubakaji na uporaji.

Jaji Athumani Matuma anaamua kufutilia mbali ushahidi wote wa Jamhuri na anaamuru washtakiwa wote waachiwe huru mara moja kwa amri ya Mahakama.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kanda ya Shinyanga, Athumani Matuma ameacha ‘precedent’ nzuri, itatumika kama rejea kwa kesi za mchongo.

Watu wetu wanakamatwa, wanashtakiwa kwa makosa ya uongo, wanaishi gerezani kwa makosa ya kusingiziwa wakati wa uchaguzi. Nchi nzima. Hatari.

Ndiyo maana nafikiri tukipata REFORMS itasaidia kuwalinda watu wetu dhidi ya makosa ya kuzusha na uongo wakati wa uchaguzi #noreformsnoelection.

Like