Magufuli: Nimechoka

Rais John Magufuli amewambia wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mjini Mwanza kuwa urais umemchosha. Alikuwa anajibu maombi ya Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda aliyependekeza Magufuli aongezewe muda wa kuongoza Tanzania, walau miaka mitano (5).

Rais Magufuli ametoa kauli nzuri, kwamba hataki kuendelea kinyume cha katiba. Lakini maneno mazuri pekee hayatoshi, kwani kumbukumbu zinaonyesha kuwa wapo wengine kama yeye walioanza hivi hivi, wanatuma wajumbe kupendekeza, wao wanakataa, halafu baadaye wanawakubalia.

Rais Yoweri Museveni (Uganda) ameyasema haya mara tano tangu 1986. Yupo! Rais Paul Kagame ameyasema haya mara kadhaa tangu 1994. Yupo. Tumtakie Rais Magufuli utekelezaji mwema wa kauli yake. Ikimpendeza aondoke hata sasa ili apumzike.

Like
2

Leave a Comment

Your email address will not be published.