Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ, leo tarehe 14.02.2022.
Jaji ameingia Mahakamani muda huu saa 4 kamili asubuhi
Kesi namba 16 ya mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa mahakamani muda huu
Wakili wa Serikali Robert Kidando Mheshimiwa Jaji ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili
Pius Hilla,
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka mawakili wa serikali waandamizi na wakili Tulimanywa Majige
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ikupendeza naitwa Peter Kibatala: nipo pamoja na wakili
John Malya
Faraji Mangula
Nashon Nkungu
Fredrick Kihwelo
Livino Haule
Edward Heche
Sisty Aloyce
Seleman Matauka
Jaji anaita washtakiwa wote wanne na wote wanaitika wapo mahakamani
WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa na leo shahidi namba 13 ameweza kufika kwa ajili ya kuendelea kutoa ushahidi wake ambapo upande wa utetezi walikuwa wanahoji maswali ya dodoso. Tupo tayari kuendelea
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi pia tupo tayari kuendelea
Inspector Tumaini Sosthenes Swila, anapanda kizimbani na kaunda suti ya kijivu kisha anasimama.
Jaji: Shahidi nakukumbusha kuwa kabla shauri hailijahairishwa ulikuwa chini ya kiapo na leo utaendelea kuwa chini ya kiapo
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Mheshimiwa Jaji nakumbuka nilipo ishia naomba nipewe kielelezo namba P4, P5 (risasi na maganda yaliyo tumika)
Kibatala: Shahidi unakumbuka mara ya mwisho zoezi lilisimama kwa sababu ulisema unataka kupata huduma za afya?
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Na kweli ulitoa Kauli hiyo Ukiwa kwenye Kiapo?
Shahidi: Ni kweli
Kibatala: Una daktari wako au una daktari wako mahususi?
Shahidi: Kimyaaaaaaa
Shahidi: Nahudumiwa na madaktari tofauti
Kibatala: Unahudumiwa kwa muda gani?
Shahidi: Zaidi ya miaka miwili
Kibatala: Wanaitwa nani?
Shahidi: Namkumbuka mmoja anaitwa Mohammed
Kibatala: Mohammed nani?
Shahidi: Simkumbuki
Kibatala: Na amekuhudumia kwa muda gani huyo usiyemkumbuka?
Shahidi: Miaka 2
Kibatala: Je unafahamu niliandika barua katika hospitali ambayo ulisema kwamba wanakuhudumia?
Shahidi: Sijapewa
Kibatala: Kwa hiyo hujui kwamba hospitali imesema ipo tayari kusema wapo tayari kuja kutoa ushahidi?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Ni hali ya kawaida kutomfahamu mtu anayekuhudumia miaka 2?
Shahidi: Kawaida
Kibatala: Ulilazwa au ulipumzika nyumbani?
Shahidi: Nilikuwa nimepumzika nyumbani
Kibatala: Nyumbani kulikuwa na daktari anayekuhudumia?
Shahidi: Hapana
Kibatala: :Tutoke hapo nitarudi baadae.
Kibatala: Unakumbuka nilikuuliza kwenye viashiria vya ufadhili wa ugaidi?
Shahidi: Nakumbuka
Kibatala: Ni sahihi tulikomea eneo la fedha?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Shahidi tulikubaliana kwamba mshtakiwa wa kwanza, wapili na watatu walitumia pesa zao kuja Morogoro
Kibatala: Je unafahamu kwamba nauli ya Mohammed Ling’wenya kuja Morogoro ilitolewa na baba yake?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Hukupeleleza hilo eneo?
Shahidi: Sikupeleleza
Kibatala: Uliona siyo muhimu?
Shahidi: Ndiyo siyo muhimu
Kibatala: Je kwa ufahamu wako baba yake Mohammed Ling’wenya alishawahi kuhojiwa ofisi ya RCO Mtwara?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Jeshi la Polisi kila mtu anajifanyia kazi yake au mnafanya kwa pamoja?
Shahidi: Tunafanya kazi kwa pamoja
Kibatala: Wewe kama mpelelezi source zako ni maelezo ya Denis Urio, Inspector Ndowo kutoka Cyber Forensic na washtakiwa wenyewe, Je ni sahihi?
Shahidi: Ni maeneo mawili siyo matatu
Kibatala: Yataje
Shahidi: Kutoka kwa Denis Urio na taarifa iliyo andaliwa kutoka maabara
Kibatala: Kwa hiyo taarifa ya maelezo ya watuhumiwa kuhusu pesa walizotumiwa siyo sehemu ya eneo muhimu?
Shahidi: Ni eneo muhimu
Kibatala: Kwahiyo ni eneo la tatu?
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Tukianza na Denis Urio, fedha ambazo anasema aliwapatia Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya aliwapatia kwa matumizi yapi?
Shahidi: Kwa lengo la kukutana na Freeman Mbowe
Kibatala: Ni sawa sawa na kusema aliwapatia fedha hizo kwa matumizi ya nauli?
Shahidi: Ni sawasawa
Kibatala: Kwa hiyo Wakili wa Serikali Pius Hilla alipo pinga kwamba nano nauli, je alipayia au alikosea?
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tunapinga hilo swali, sisi tunapinga alipokuwa ana refer kuna zile pesa zilikuwa za nauli
Kibatala: Mheshimiwa Jaji wacha niendelee eneo lingine, ila mtu akisimama awe na kitu cha msingi
Kibatala: Shahidi kwahiyo pesa hiyo walipewa sababu ya nauli?
Shahidi: Sahihi ya nauli na matumizi mengine
Kibatala: Ni sahihi kwamba washitakiwa wame elezea pesa hiyo katika maelezo yao?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ni sahihi kwamba fedha hizo pia zime zungumzwa katika maelezo ya Luten Denis Urio ambayo uliandika wewe?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Unakumbuka Luteni Denis Urio alisema aliwapatia Tsh ngapi
Shahidi: Ni Tsh 195,000 na kisha Tsh 199,000
Kibatala: Tsh 195,000 zinaonekana katika maelezo ya washitakiwa wote ya onyo?
Shahidi: Ndiyo zinaonekana
Kibatala: Katika figure hiyo?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Unafahamu hayo kwa sababu wewe kama mpelelezi makini na mzoefu kwa sababu ulitake trouble ya kusoma na kuelewa
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo namba P4 na P 13
Kibatala: Unafahamu kwamba Adam Kasekwa alisema kuwa sehemu ya fedha alizopewa alitumia kununua shati la mauamaua ambalo alikuwa amelivaa siku anahojiwa?
Shahidi: Nakumbuka maneno kwamba alinunua shati lenye maua maua
Kibatala: Kwa upelelezi wako wewe hilo shati lenye maua maua linahusika vipi na ugaidi (maana alitumia fedha kununua shati lenye maua maua)?
Shahidi: Ni fedha ambazo zilitolewa na Freeman Mbowe kwenda kufanya vitendo vya kigaidi
Kibatala: Kwa hiyo shati ambalo alikuwa amelivaa lilikuwa ni sehemu ya ugaidi?
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Kibatala: Na je kipengele cha yeye kununua shati mli’ rekodi chenyewe au hapana?
Shahidi Kilirekodiwa
Kibatala: Kwanini sasa unanikataza kuuliza kitu kimoja kimoja?
Shahidi: Ukiulizwa kimoja kimoja uwezi kupata ugaidi
Kibatala: Shika Maelezo ya Adam Kasekwa kwanza, katika eneo hilo kuna matukio kadhaa yalitokea, tafuta eneo la Luten Urio alitupa Nauli ya Tsh 87,000 /=
Shahidi: Nimeona
Kibatala: Soma kuanzia hapo tujue nauli ya kwenda Moshi ni Tsh ngapi?
Shahidi: Tarehe 24 July 2020 nilikutana na Mohammed Ling’wenya kasisitiza tuende Morogoro tukakutane Luteni Urio tuliondoka siku hiyo hiyo na kukutana na Luteni Denis Urio alituambia kuwa kuna kazi ya kulinda VIP kwa Freeman Mbowe na Kwamba maelezo zaidi tutayakuta huko huko, kila mtu alipewa Tsh 87,000
Kibatala: kwahiyo kila mtu alipewa Tsh 87,000 kama nauli?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Na wewe kama mpelelezi uliona kuna kosa lolote?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Na wewe ukaona hapo kuna mantiki kama mpelelezi?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Jumla walipewa Tsh ngapi wote wawili kama walipewa kila mmoja Tsh 87,000
Shahidi: Walipewa Tsh 174,000/=
Kibatala: Tafuta katika maelezo hayo pesa iliyobakia katika Tsh 199,000 ambayo ni Tsh 25,000 kama utaona katika maelezo Ya Adam Kasekwa
Shahidi: Haijaelezwa humu
Kibatala: Na wewe kama mpelelezi ulifanyia vipi kuhusu hiyo Tsh 25,000,je uliandikia maelezo ya nyongeza?
Shahidi: Ya nani?
Kibatala: Kwani hapa tunamuongelea nani?
Shahidi: Adam Kasekwa
Kibatala: Je wewe kama mpelelezi uliandika maelezo ya nyongeza au kumtaka mtu amuhoji?
Shahidi: Hapakuwa na umuhimu huo
Kibatala: Mwambie sasa Mheshimiwa Jaji tunaipata wapi hiyo Tsh 25,000
Shahidi: Hutoiona
Kibatala: Uliwahi kufundishwa kuwa maelezo ya onyo ya mshtakiwa yanatakiwa yabebe kila kipengele ya fact inayounda shtaka?
Shahidi: Sijafundishwa, siyo lazima ibebe kila kitu
Kibatala: Na wewe hiyo Tsh 25,000 siyo muhimu kwako?
Shahidi: Siyo Muhimu
Kibatala: Ni sahihi kwamba Denis Urio anasema kwamba aliwapa Tsh 199,000 kama nauli kwa Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya, Je 199,000 ya Denis Urio inafanana na Tsh 174,000?
Shahidi: Zinafanana, Ni sawa na kusema 45 na mtu mwingine akasema ni 90 gawa kwa 2
Kibatala: Swali ni kwamba 174,000 na 199,000 zinafanama vipi?
Shahidi: Nishasema zinafanama
Kibatala: Kwahiyo figure zinafanama?
Shahidi: Nishasema zinafanana.
Kibatala: Shika na maelezo ya Mohammed Ling’wenya, soma pale baada ya mazungumzo Luteni Denis Urio alinipa..
Kibatala: Au anzia baada ya kufika tulikutana na Luteni Denis Urio Bar moja eneo la Msamvu
Shahidi: Nimeona
Kibatala: Soma mpaka ufike Tsh ngapi walipatiwa
Shahidi: baada ya kufika tulikutana na Luteni Denis Urio Bar moja eneo la Msamvu Bar hiyo sikumbuki, baada ya kufika Luteni Denis Urio alitueleza kuna kazi ya VIP kwa Freeman Mbowe, na siku hiyo hiyo alitutaka tusafiri siku hiyo hiyo
Baada ya mazungumzo Luteni Denis Urio aliniuliza huko Mtwara kwenye kibarua chako ulikuwa unalipwa Tsh ngapi, nikasema posho ya Tsh 15,000 basi akasema nikifika huko niombe mshahara wa Tsh 800,000 alitupatia Tsh 190,000 fedha ambazo tulinunua nguo ilituonekane nadhifu
Kibatala: Ni sahihi kwamba fedha hizo walinunulia nguo?
Shahidi: Sahihi
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Luteni Denis Urio aliwapa Tsh 190,000?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Ni sahihi yeye Denis Urio alisema kwamba alitumiwa Tsh 199,000 na hiyo Tsh 199,000 aliwapa Mohammed Ling’wenya na mwenzake Adam Kasekwa na Tsh 190,000 anayosema Mohammed Ling’wenya na walipatiwa na Denis Urio. Je hizo figure zote zinafanana au zinatofautiana?
Shahidi: Zina fanana
Kibatala: Sawa shahidi
Kibatala: Na maelezo ya Kasekwa na maelezo ya Mohammed Ling’wenya kwenye figure ambayo mmoja anasema jumla walipewa Tsh 174,000 na mmoja anasema Tsh 190,000 Je zinafanana au zinatofautiana?
Shahidi: Zinafanana
Kibatala: 199,000 ukito Tsh 190,000 zinabakia Tsh ngapi?
Kibatala: Je katika maelezo ya Mohammed Ling’wenya tafuta Tsh 9000 inafafanuliwa ilitumikaje?
Shahidi: Haijafafanuliwa
Kibatala: Na wewe kama mpelelezi uliyebobea wa zaidi ya miaka 20 na ukateuliwa na DCI, mwambie Mheshimiwa Jaji kuwa hiyo Tsh 9000 ulifanyiaje kazi?
Shahidi: Wote wanakiri kupokea fedha kutoka kwa Denis Urio
Jaji: Sikiliza swali vizuri unaulizwa hiyo Tsh 9000 ulifanyiaje kazi?
Shahidi: Ndiyo nilikuwa naeleza, wote wanakiri kupokea pesa kutoka kwa Luten Denis Urio
Kibatala: Kwahiyo hapo ndiyo umefanyia kazi?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Nikiuliza kwa namna gani utarudia maelezo ya awali?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Basi mahakama imesikia
Kibatala: Soma pale baada ya kupokea pesa hizo kutoka kwenye maelezo ya Denis Urio
Shahidi: Niliwapatia Tsh 195,000
Kibatala: Sasa soma maelezo ya washitakiwa wote wawili wanaizungumzia wapi.. katika maelezo ya Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Kibatala: Nikisema kuwa hawajazungumzia kuokoa muda nitakuwa nimekosea?
Shahidi Hawajazungumzia
Kibatala: Je unakubali kwamba hakuna sehemu waliyokiri kupokea?
Shahidi: Amezungumzia Denis Urio
Kibatala: Achana na Luteni Denis Urio, nataka hiyo refund kutoka walipotoka kuja Morogoro, Swali Je washtakiwa wali acknowledge? simple and clear
Shahidi: Hawajazungumzia
Kibatala: Na hiyo hali wewe kama mpelelezi uliona ni hali ya kawaida tuh?
Shahidi: Siyo mimi niliyeandika maelezo
Kibatala: Wewe kama mpelelezi?
Shahidi: Ni hali ya kawaida
Kibatala: Kwa hiyo hukuhangaika kutafuta fact ziada?
Shahidi: Nilichukua jitihada za kutafuta fact ziada
Kibatala: Kwakuwa ni hali ya kawaida hukufanyia kazi?
Shahidi Nilifanyia kazi
Kibatala: Haya ndo utuambie kuwa ulifanyia kazi vipi?
Shahidi Maelezo ya Denis Urio yalikuwa ya uhakika
Kibatala: Na maelezo ya washitakiwa?
Shahidi Na yenyewe yalikuwa ya uhakika
Kibatala: Lini ulianza kuona au kukufikia kati ya maelezo ya Denis Urio au watuhumiwa?
Shahidi: Maelezo ya washitakiwa
Kibatala: Wakati unamhoji Denis Urio ukiwa na faida ya maelezo ya Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya siku nne kabla?
Shahidi: Nilikuwa sijayasoma bado
Kibatalac Na uliyosoma lini sasa maelezo ya onyo ya washitakiwa
Kibatala: Baada ya kuandika maelezo ya Luten Denis Urio, ulifanya zoezi la kulinganisha?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ukaona kila kitu kipo sawa?
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Kibatala: Sawasawa, Haya Denis Urio anasema kwamba alitumiwa Tsh 500,000 akatoa 300,000 akawapa Bwire na Lijenje na baadae waka patikana vijana wawili akawapa akatoa Tsh 195,000 akawapa jumla ni Tsh ngapi?
Shahidi: Jumla ni Tsh 495,000
Kibatala: na Je 500,000 Ukitoa Tsh 495,0000 inabakia Tsh ngapi
Shahidi: Elfu 5
Kibatala: Ilienda wapi?
Shahidi: Ni gharama za mtandao
Kibatala: Hiyo gharama za mtandao ulitoa katika maelezo ya Denis Urio?
Shahidi: Kimyaaaaaaaaa
Kibatala: Kuna mahala popote katika maelezo ya Denis Urio ambayo umeandika wewe, kuna mahala popote ameielezea?
Shahidi: Hajaielezea
Kibatala: Uliambiwa kuwa Denis Urio alifafanua hiyo Tsh 5000 hapa mahakamani?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je hata wakili mwenzetu Gladys Fimbari aliwahi kuzungumzia hapa mahakamani hii Tsh 5000?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je upo makini na hii kesi?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je unafahamu kwamba kama kuna gharama za Tsh 5000 kama zimekatwa na mtandao zilitakiwa tuzione katika taarifa ya Mtandao
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Ndiyo maana nikamuuliza je wewe ni mpelelezi makini?
Shahidi: Ndiyo mpelelezi makini
Kibatala: Wa hadhi ya kesi ya Ugaidi?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwa ushahidi wako na mashahidi wengine wanaojenga kesi, baada ya kufika Moshi, mshitakiwa wa pili na watatu walikuwa wanapita maeneo ambayo Sabaya anapenda frequently kuyatembelea, ndiyo ulivyo sema?
Shahidi: Ndiyop
Kibatala: Katika ile 699 000 ambayo mnasema Mbowe alitumia kufadhili Ugaidi, ni Tsh ngapi Adam Kasekwa alitumia Kumtafuta Sabaya?
Shahidi: Kwa mujibu wa upelelezi wangu mbali ya Tsh 699 000 Kuna pesa zingine alikuwa anawapatia
Kibatala: Fedha hizo zipo katika hati ya mashitaka?
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Kwa hiyo fedha ambazo hazipo katika hati ya mashtaka unaona zinatusaidia sisi?
Shahidi: Aaaahhh zinasaidia
Kibatala: Weeeee kweli enheeeee?
Shahidi Anainama Chini kama anaona aibu
Kibatala: Unafahamu kwamba kuna mahala unazungumzwa Tsh 80,000 ambayo Khalfani Bwire wakibadilishana mikono na Freeman Mbowe?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Tsh ngapi?
Shahidi: Ni Tsh 80,000
Kibatala: Hiyo Tsh 80,000 kuiona katika shughuli zako za upelelezi?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Uliona wapi?
Shahidi: Katika taarifa Uchunguzi Wa Kisayansi
Kibatala: Kwani wao wanahusika na kutunza mihamala ya fedha ya simu?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba nipatiwe kielelezo namba P 15,16,17,18,19 Mpaka 20
Kibatala: Ni sahihi kwamba taarifa iliombwa chini ya ofisi yako hata kama ni DCI
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Nakuonyesha kielelezo cha barua namba P16 ya + 01 July 2020 Kutoka Forensic Beaural, Je unaitambua?
Shahidi: Ndiyo naitambua
Kibatala: Uliomba taarifa za lini hadi lini?
Shahidi 01 June 2020 – 31 July 2020
Kibatala: Barua ilisainiwa kwa niaba ya nani?
Shahidi Kamishina Wa Polisi Wa Uchunguzi wa Kisayansi
Kibatala: Anaitwa nani?
Shahidi NAFTALI J MANTAMBA
Kibatala: Unamfahamu?
Shahidi Hapana simfahamu
Kibatala: Wewe kutomfahamu huyo ni jambo la kawaida?
Shahidi: Ni jambo la kawaida
Kibatala: Kwani taarifa ya uchunguzi iliombwa kwa nani?
Shahidi: Na DCI
Kibatala: Ambaye DCI alimpa nani mamlaka ya upelelezi?
Shahidi: Mimi
Kibatala: Kwa hiyo ni sahihi kutomjua huyo?
Shahidi: Ndiyo, kuwajibika na hilo
Kibatala: Umeona hizo tarehe?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Hizo tarehe mliwapa au walijibunia wao?
Shahidi: Tuliwapa
Kibatala: Kwa kupitia barua ya tarehe 13 August 2020 Kumbukumbu CID/HQ/KUM/C. 8/VOL VIII/171?
Shahidi Ndiyo nafahamu
Kibatala: Barua ilikuwa ya muhimu au siyo muhimu?
Shahidi Ilikuwa muhimu
Kibatala: Katika ushahidi wako umeitoa barua hii kama ushahidi wako muhimu?
Shahidi Sikutoa
Kibatala: Ulitoa mahakamani sababu ya kwanini hukutoa mahakamani?
Shahidi: Sikutoa sababu
Kibatala: Uliongozwa kuitambua hapa mahakamani?
Shahidi: Sikuongozwa hapa mahakamani
Kibatala: Kwahiyo barua hii ndiyo ilipelekea simu 8?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je ulimwambia pia Mheshimiwa Jaji akuwa hakuna simu hata moja ya Mbowe katika simu mlizokamata
Shahidi: Sikueleza
Kibatala: Bado tupo eneo la fedha bado sijahama, lakini ilituzungumzie fedha lazima twende maeneo mengi
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Simu ambayo ilichukuliwa kwa Mohammed Ling’wenya, nilisikia ukisema kwa mujibu wa Seizure Certificate ya Mohammed Ling’wenya haikuwa na IMEI namba?
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Na ukatoa ushahidi namna ambavyo ulipata IMEI namba?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ulifanya nini tena ikumbushe mahakama?
Shahidi: #*06# OK
Kibatala: Ukapata IMEI namba?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Hiyo IMEI namba uliyopata ulimwambia Mheshimiwa Jaji?
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Ulimwambia mhe Jaji ni Manufacturer Directives IMEI namba Ikifutika ndiyo ufanye hivyo?
Shahidi: sikumueleza
Kibatala: Je ulimwambia Mhe Jaji Kwamba Manufacturer au agent wa TECNO ndiyo uliyekwenda kwake na akakupa ushauri wa kitaalamu?
Shahidi: Hapana sikumwambia
Kibatala: Unafahamu kwamba TECHNO wana mawakala wake Tanzania wanaofanya kazi hizo?
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Je ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba ukijifunza wapi namna ya kutafuta IMEI?
Shahidi: Sikueleza
Kibatala: Hiyo IMEI namba ndiyi uliweka katika barua ya kwenda Ofisi Ya Uchunguzi?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Unafahamu Kitu kinaitwa garbage in and garbage out?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Kwa hiyo wao wamenukuu IMEI namba ambayo wewe ndiyo ulipata?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Report ya Inspector Ndowo wewe uliona?
Shahidi: Niliona
Kibatala: Umemwambia Mheshimiwa Jaji kuwa hiyo IMEI namba, kwamba riport uliyopata ulilinganisha na IMEI namba ya mchunguzi ukaona zinafanana?
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Unafahamu maana ya authentication?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu kwamba simu zinaweza kuingiliwa?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu kwamba IMEI namba ni DNA ya simu?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Mwenye simu mwenyewe amezungumzia lolote kuhusu IMEI namba ya simu yake?
Shahidi: Naomba maelezo nijikumbushe
Shahidi: Hakueleza
Kibatala: Tafuta kwanza katika maelezo ya Mohammed Ling’wenya kuna mahala popote ametaja kuwa simu zake zote mbili ametaja ICCID?
Shahidi: Hakutaja
Kibatala: Na kurudisha kwenye barua ya kutoka Polisi kwenda Airtel, soma namba zote tatu zilizoombewa taarifa Airtel
Shahidi: 0784779944, 0782 237913 na 0787 555200
Kibatala: Nenda katika taarifa ya Gladys Fimbari, Je alitoa namba zinazo one kana katika mihamala alitoa taarifa za mihamala ya simu ngapi?
Shahidi: Namba mbili za 0784779944 na 0787 555200
Kibatala: Na hapo unasoma katika kielelezo namba P 15?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Unakubaliana na mimi Gladys Fimbari aliombwa miamala ya namba 3 ila yeye katika barua yake miamala ya simu 0782 237913 imeachwa?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Unafahamu record ya miamala ya Gladys Fimbari kutoka Airtel imetokana na barua ya Polisi Kwenda Airtel?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Nenda katika taarifa ya mihamala kielelezo namba P 20, mhamala wa mwisho kabisa wa tarehe 31 July 2020
Shahidi: Nimeona
Kibatala: Angalia namba iliyotuma fedha
Shahidi: 0784779944
Kibatala: Namba iliyotumiwa 0782 237913
Kibatala: Unakubaliana na mimi namba” 0″ inamiss?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Katika barua yenu ya kwenda Airtel, Je namba sifuri ilikwepo au haikuwepo?
Shahidi: Ilikuwepo
Kibatala: Wewe ndiyo ulimuandika maelezo Gladys Fimbari?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Uliandika sababu ya kutofautiana hiyo prefix ya “0”
Shahidi: Sikumuuliza, kwa sababu…
Kibatala: SITAKI SABABU HAPA MIMI
Kibatala: Nenda kwenye barua, ni sahihi kwamba namba iliyotumiwa hapo ndiyo namba ambayo ipo kwenye barua?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwanza imetumiwa Tsh ngapi?
Shahidi: 200,000
Kibatala: UNASOMA WAPI WEWE, KUWA MAKINI
Shahidi: Ni Tsh 80,000..
Kibatala: Je ni sahihi kwamba namba iliyotumiwa Tsh 80,000 ndiyo namba iliyokuwa kwenye Barua ya Polisi Kwenda Airtel?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Lakini hiyo namba katika covering latter ya Airtel hiyo namba haipo?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Je unafahamu legal implication ya suala hilo?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Lakini ulimuhoji Gladys Fimbari tarehe 05 July 2021?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Je ulifanyia kazi hiyo tofauti?
Shahidi: Sikufanyia kazi
Kibatala: Ndiyo maana nilikuuliza unafahamu maana ya legal implication?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Angalia muamala wa tarehe 20 July 2020, ukitumwa kutoka namba 0780 900174 kwenda namba 0787 555200, je ulisoma taarifa za miamala vizuri kama mpelelezi?
Shahidi: Nilisoma na kuzielewa
Kibatala: Na ni sahihi kwamba moja ya source zako za information mpaka kusema Mbowe alifadhili Ugaidi ilikuwa ni baada ya kusoma na kuelewa taarifa za miamala?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Ulifahamu, kwamba hii namba ni ya Wallet?
Shahidi: Hapana nilizingatia covering letter ya kutoka uchunguzi
Kibatala: Wewe unapeleleza faili, kupitia forensic beaural, na yeye kwakuwa hakuwa na utaalamu akaomba kutoka Airtel, Na ndiyo mwanzo nilikuuliza kwamba unafahamu hizo taarifa?
Shahidi: Ndiyo nilifanyia kazi
WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji shahidi amesha jibu hilo swali akasema hafahamu kuhusiana na hii namba, kwa hiyo tunaona swali linajirudia hapa
Kibatala: Mheshimiwa Jaji hakuna swala la kanuni hapo, kwa sasa kwa sababu ni mapema, wacha niendelee, ila baadae nitawahoji kwa sheria ipi kwa kanuni ipi
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji ilikiwa ni maamuzi yako, wala siyo sheria wala kanuni
Kibatala: Nishasema kuwa kwa sasa naendelea ila wakiendelea hivyo tutaomba ruling sababu hili ni zoezi la truth findings
Kibatala: Wewe binafsi kama Inspector Swila ulisoma na kuelewa au ulisoma hukuelewa?
Shahidi: Nilipitia lakini sikuelewa
Kibatala: Kwahiyo tuachane na hiyo taarifa, sababu hujaielewa?
Shahidi: Anayeweza kufafanua hiyo ni mtu wa Airtel
Kibatala: Sawasawa nimekuelewa?
Kibatala: Haya kuhusu KYC unazijua?
Shahidi: Kwa kiasi chake
Kibatala: Lakini ulizo fanyia kazi KYC za Denis Urio na Mbowe, Mohammed Ling’wenya
Kibatala: Kwa hiyo ulizielewa au hukuzielewa?
Shahidi: Nafahamu vitu baadhi
Kibatala: Unafahamu kwamba KYC inayo purport namba ya Mbowe, Denis Urio na Mohamed Ling’wenya zote Zina namba ya NIDA?
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Unafahamu Kwamba NIDA ndiyo primary source?
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Unafahamu kwamba wewe kama mpelelezi ulipokea taarifa ili uchunguze na kuthibitisha kwamba kweli i alikuwa na makosa ya ugaidi?
Shahidi: Sikuwahi
Kibatala: Kwani nani alikuwa mpelelezi kati yako wewe na Airtel?
Shahidi: Mimi pamoja na wapelelezi wengine
Kibatala: Kwa hiyo wewe hukufanya lolote la kwenda NIDA Kuona kama kweli zilikuwa taarifa zao?
Shahidi: Sikufanya
Kibatala: Je unafahamu Kwamba hiyo pesa iloyotumwa kwenda namba ya Tigo ilitumwa kutoka namba 071993338?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Ni sahihi kwamba mliomba TIGO taarifa ya namba hiyo?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Unafahamu namba ya faili ya Mbowe, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Khalfani Hassan Bwire ni CD /IR /2097 /2020?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Ni sahihi kwamba ndiyo ulisema wewe ulifungua faili hilo tarehe 18 July 2020
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Na wewe ndiyo uliandika maelezo ya Frank Kapala?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Ni sahihi pia ulisema katika ushahidi wako kuwa ulifanyia kazi taarifa za Tigo?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Na wewe ulisema ni mpelelezi makini?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Haya mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa jalada walilojibu Tigo ni lipi..?
Shahidi ni CD/IR/ 2097/ 2021
Kibatala: Tukumbushe kuwa jalada lako ulilofungua ni la mwaka gani?
Shahidi: Ni mwaka 2020
Kibatala: Je Tigo walijibu jalada lako kwa kunukuu mwaka gani?
Shahidi: Mwaka 2021
Kibatala: Je ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba ulifanya juhudi gani za kiupelelezi ku reconcile utofauti wa mwaka 2020 na mwaka 2021?
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Na mhamala unaobebwa na barua hiyo ni wa Tsh 500,000 ambao unasemekana kwamba Mbowe alimtumia Denis Urio?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Unamjua author wa hiyo barua?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Angalia aliyeandika hiyo barua pale chini ni nani?
Shahidi: Imeandikwa Mwanasheria ila jina halijaandikwa
Kibatala: Na wewe Tarehe 08 July 2021 ulimuhoji mtu anaitwa Kapala
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Sasa ulimwambia Mheshimiwa Jaji kwamba ulijuaje kwamba aliyeandika barua ile ni Frank Kapala?
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Nikisema kwamba ushahidi ulikuwa wa kupangwa kwa fact hizo nakosea?
Shahidi: Siyo sahihi
Kibatala: Je unafahamu kuhusu mihamala ya Tigo ambayo mnasema kwamba ilikuwa mihamala ya Freeman Mbowe?
Shahidi: Anafahamu mtu mwingine
Kibatala: Kwa hiyo ukiacha miamala ya Tigo hii hakuna kitu kingine unachokifahamu?
Shahidi: Kuhusu miamala anafahamu Denis Urio
Kibatala: Bado tupo Kwenye pesa, umetaja mara kadhaa kuhusu taarifa ya cyber kama moja ya kitendea kazi chako?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Tutaona nini na nini?
Shahidi: Taarifa za mawasiliano na usajili wa namba za simu
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba kielelezo namba P 23 na P 26 Na P22 ya Covering letter
Kibatala: Sasa shahidi nakuonyesha barua kutoka Uchunguzi Wa Kisayansi kielelezo namba P22
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Barua Imeelekezwa Kwa nani?
Shahidi: Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai
Kibatala: Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai ambaye ndiyo Mlalamikaji?
Shahidi: Inaenda Kwenye Ofisi
Kibatala: Kwani imesema “Kurugenzi ” au “Mkurugenzi “?
Shahidi: Mkurugenzi
Kibatala: Soma namba ya jalada iliyobeba barua
Shahidi: Ni CD/IR/ 2097/2020
Kibatala: Na barua iliyorejewa ni kumbukumbu namba ngapi?
Shahidi: CID/HQ/C8/9/Vol viii/171/ ya 13 August 2020
Kibatala: Barua ambayo ujaitoa mahakamani kama kielelezo?
Shahidi: Sijaitoa Mahakamani
Shahidi: MHESHIMIWA JAJI NAOMBA NIENDE CHOONI
Mahakama ipo Kimya kusubiri Shahidi atoke chooni
Shahidi naambiwa Kakuta foleni Imebidi aingie Choo cha wanawake (kaingia choo cha kike)
Na Sasa Shahidi amerejea Kizimbani
Kibatala: Tunaweza kuendelea shahidi
Shahidi: Tuendelee
Kibatala: Je Barua ambayo haipo mahakamani Ya Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai Kwenda Ofisi ya Cyber imeandikwa lini?
Shahidi: Tarehe 13 July 2020
Kibatala: Na majibu yamekuja lini?
Shahidi: Tarehe 09 July 2021
Kibatala: Kama kipindi cha mwaka sasa?
Shahidi: Miezi 11
Kibatala: Walikwambia kwanini kufanya extraction tuh kesi kubwa kama hii vielelezo vinakaa miezi 11?
Shahidi: Walisema kuna vielelezo vingi
Kibatala: Unafahamu kwamba tarehe hizo ndiyo zilikuwa za vuguvugu za masuala ya Katiba?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Kwenu kesi hii ya ugaidi ilikuwa ni priority au mlianza hata kuchunguza maswala ya mapenzi kwanza?
Shahidi: Nishajibu
Kibatala: Unafahamu madhara waliyo pata washitakiwa wa kwanza, wapili na watatu kama vijana kwa kukaa ndani muda mrefu?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu a maana ya Polisi Impunity?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Ulifanyia kazi Extraction Reports?
Shahidi: Nilifanyia kazi kwa ufahamu wangu
Kibatala: Unafahamu zilikuwa ngapi?
Shahidi: Nne
Kibatala: unafahamu kwamba kuna extraction report siku ambayo covering latter imeandikwa?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: +Unafahamu walifanya extraction tarehe 09 July 2021 Saa 11 na Dakika 29 jioni
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Unafahamu kwamba walikuwa wanakimbizana na nini, hizo siku mbili za mwisho?
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Je unafahamu kwamba baada ya kukimbiza extraction report kwa siku mbili ndiyo baada ya siku 12 Mbowe akakamatwa?
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Na unafahamu a baada ya extraction report kukamilika na Mbowe Kukamatwa ndiyo Elia Kaaya akaachiwa na baadae akaja kuwa shahidi kwenye kesi hii?
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Haya nipeleke hayo maeneo ambayo yalokuingiza kufikiria kwamba Freeman Mbowe alifadhili Ugaidi
Shahidi: Ukurasa wa nne, bullet ya pili
Kibatala: Unasema nini?
Shahidi: Kwa mujibu wa report ya Tigo ya tarehe 20 July 2020, namba ya simu 0719933386 ilituma namba kwemda 0787 555200
Kibatala: Ni sahihi kwamba hapo amekopi kutoka Tigo?
Shahidi: Siyo sahihi
Kibatala: Tuambie sasa inspector ndowo alifanya nini?
Shahidi: Hapo bullet ya chini inaposema kwamba kwa mujibu wa report kutoka Tigo…
Kibatala: Nitafutie mahala ambapo Inspector Ndowo ali originate uchunguzi kutoka kwake, zaidi ya taarifa ya Tigo (Mbali na Primary Source kutoka Tigo)
Shahidi: Alifanyia kazi taarifa kutoka Tigo akaanda taarifa hii
Kibatala: Hiyo kazi ambayo alifanya yeye Inspector Ndowo nauona katika bullet ipi?
Shahidi: Ndiyo ungemuuliza yeye Inspector Ndowo
Kibatala: Kwa mdomo tena?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je unafahamu kwamba report inatakiwa kuiongelea yenyewe?
Shahidi: Ndiyo ungemuuliza yeye sasa
Kibatala: Nisionekane na kuharass, Je unakubaliana na mimi taarifa inayo tajwa hapo ni ileile ya Tigo ambayo kwenye barua ya Tigo ni CD/IR 2097 /2021
Shahidi: Hapana ni CD /IR/ 2097 /2020
Kibatala: Kwani barua kutoka Tigo imeandika jalada gani?
Shahidi: CD /IR 2097 /2021
Kibatala: Siyo kuuliza tena hapo.
Kibatala: Haya bullet gani nyingine inayo zungumzia kuwa mbowe akiwatumia pesa?
Shahidi: Ya pili kutoka mwisho, 0784779944 imesajiliwa kwa majina Freeman Mbowe ilituma pesa kwemda namba 0782 237913 ilituma kiasi cha Tsh 80,000
Kibatala: Je unafahamu unachosema hapo hakipo katika hati ya mashitaka?
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Sasa lengo la kuleta mahakamani kitu hakipo katika hati ya mashtaka ni nini?
Shahidi: Hizo ni fedha ambazo hazikuweza kutolewa maelezo na Denis Urio
Kibatala: Lengo la kuleta pesa hizo hapa mahakamani na nini, zilikuwa ni mahaba au ufadhili wa Ugaidi?
Shahidi: Ndiyo kufadhili Ugaidi, ambazo hazikuweza kuelezwa na Denis Urio
Kibatala: Namba 0782 237913 ndiyo namba ambayo haikuwa covered na Gladys Fimbari?
Shahidi Ndiyo
Kibatala: Haya nitafutie eneo lingine katika report
Shahidi: Fedha ambazo zimeonyeshwa katika report ni hizo tu
Kibatala: Ni sahihi katika maelezo yako uliyo andika wewe unaandika hivi, vilevile uchunguzi wa cyber ulikuwa unaonyesha mshitakiwa mbowe akiwatumia pesa wenzake na kutoa maelekezo nini cha kufanya?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Hiyo taarifa wewe ulipata wapi kwamba Mbowe alikuwa anatuma pesa na kutoa maelekezo nini cha kufanya
Shahidi: Kwenye report
Kibatala: Haya nitafutie kwenye riport mahala inaposema kwamba mshtakiwa Freeman Mbowe alikuwa anatuma pesa na kuelekeza wenzake nini cha kufanya (Vitendo Vya Ugaidi)
Shahidi anapekua report
Shahidi: Kwenye report hakuna
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kuwa katika report hakuna mahala ambapo Mbowe anatoa maelekezo nini cha kufanyia fedha hiyo
Shahidi: Mheshimiwa Jaji Katika report hakuna maelezo hayo
Kibatala: Infact ukisoma hiyo riport anayeomba pesa ni Denis Urio ukisoma pale Kwenye wamekwambia wanataka nini? Na wa umri gani (Katika Kielelezo G) page 3 mpaka page ya 4
Shahidi: Nimeona,
Kibatala: Ni nani anayesema naomba nitumie nauli kwa ajili ya kuwa mobilise nikutane nao Morogoro kwa mujibu wa riport ya Inspector Ndowo
Shahidi: Imetumwa na Denis Leo Urio
Kibatala: Ni sahihi meseji hiyo inaonyesha na matumizi ya hiyo pesa?
Shahidi: Ukisoma moja moja huwezi kupata maana halisi
Kibatala: Sijakubishia, ila tunazumgumzia kuhusu report ambayo wewe ndiyo umesema kwamba ni source ya conclusion yako
Kibatala: Sasa kwa mujibu wa Inspector Ndowo, Ni sahihi kwamba lengo lipo katika meseji ni kuwa mobilise?
Shahidi: Ni sahihi
Kibatala: Na kwa mujibu wa riport hiyo nani kasema “no problem kaka ni kwa namba ipi na kwa kiasi kipi”?
Shahidi: Ni Freeman Mbowe
Kibatala: Na kwa mujibu wa report hiyo nani kasema usiwe unatumia namba yako kaka?
Shahidi: Denis Leo Urio
Kibatala: Katika maelezo uliyokuwa unamuandika, ulimuhoji Denis Urio kwanini yeye kama mtu wa kumtoa gaidi pangoni aje aonekane ushahidi wake badala yake ndiyo anamfucha gaidi pangoni?
Shahidi: Ndiyo alieleza
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Maelezo Ya Luten Denis Urio
Kibatala: Haya tafuta mahala ambapo Luteni Denis Urio alifafanua katika maelezo yake kwanini anamwambia mbowe atumie namba ya wakala au wasaidizi wake
Shahidi: Wakati wa maongezi yetu afande DCI alifanya mawasiliano, na baada ya muda mfupi aliingia afande mwingine
DCI aliniambia ili tuweze kukusanya ushahidi niendelee kuwatafuta watu hao, ili kumweka karibu
Kibatala: Nitafutie mahala ambapo Denis Urio anasema alimwambia asitumie namba yake atumie namba ya wakala au wasaidizi wake ilikumweka karibu
Shahidi: Ili asiweze kumtilia mashaka
Kibatala: Hayo maneno yapo au hayapo, wewe umesoma kielelezo namba P23 meseji inasema usiwe unatumia namba yako, tumia namba ya wakala au wasaidizi wako, sasa nataka sehemu katika Maelezo ya Denis Urio sehemu ambayo amesema nilifanya hivi ili ku gain confidence
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tunapinga hilo swali, sababu limeshajibiwa
Kibatala: Naomba mwenzangu unisomee nione kama limejibiwa
JAJI: ulikuwa umeulizaje Mr. Kibatala?
Kibatala: Nataka kwa maelezo ya Denis Urio kwamba anitajie sehemu ambayo amesema kwamba ile meseji ya kumshauri Mbowe kuwa usitumie namba yako, tumia ya wasaidizi wako au wakala, je katika maelezo hayo kuna sehemu ambayo amesema?
Shahidi: Maneno hayo kwenye maelezo hayapo
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba kutoa hoja, naomba uridhie tupate break kidogo kama ilivyo utamaduni wetu, kisha turejee saa 8 kasorobo
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hatuna pingamizi
Jaji: Naahirisha kwa muda wa dakika 45, tutarudi tena saa 7 na dakika 45
Jaji amerejea Mahakamani Muda huu 02:18
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani tena
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ikupendeze Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wa Jamhuri Quorum ipo Kama Awali
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji nasi pia kwa Upande wet Quorum ipo Kama Ilivyo kuwa awali na tupo tayari Kuendelea
Shahidi Karejea Kizimbani
Mwenyekiti Freeman Aikael Mbowe amenyoosha mkono wake wa kulia hapa
Freeman Mbowe: Mheshimiwa Jaji naomba kuleta Kwenye Mahakama yako kuwa tumekosa haki ya kula chakula mchana kwa Miezi 5, Wakati nyie Mna’ break kwenda kula sisi hatupati chakula wala maji kwa miezi Yote 5
Pale mwanzo tuliambiwa kuwa kama chakula tuchukue Kutoka Jela, tutoke nacho Jela tuje nacho Mahakamani, tkitoka hapa tunakutana Magereza Wameshakula tunakwenda kulala na njaa siku zote.. Hawa vijana wanakonda kila Siku hata kusikiliza kesi ni geresha.. Ni hayo tu.
Jaji: sasa nyie Kibatala mnatoa uwakilishi gani hapa Mahakamani kama wateja wenu hawali miezi mitano?
Kibatala: sisi tulifkisha kwa Officer wa Magereza, Suluhu aliyotoa ndiyo hiyo Asubuhi Watoke na Chakula Kutoka Jela Kitu ambacho tulibishana na hatukufikia Muafaka kwa sababu haiwezekani.. Nafikiri hata Msajili Wa Mahakama analijua hilo, sutaki kumsemea.
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kwa Mujibu Wa Jambo lililo letwa naomba Tubreak Kidogo tuweze Kuishauri Vyema Mahakama.. Imekuwa ghafla sana..
Jaji: basi nawaita Mawakili Kuwakilisha Watu wote Ofisini Kwangu, Tuweze Kujadili
Jaji anatoka 02:27
Askari magereza wamemfuata Freeman Mbowe, anahitajika ofisini kwa Jaji katika kikao cha pamoja na mawakili wa pande zote (serikali na utetezi), Washtakiwa wengine watatu bado wamebakia kizimbani.
Jaji amerejea 03:56
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa tena Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji upande wa Jamhuri Quorum yetu ipo Kama awali
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi upande wetu Quorum ipo Kama awali
Jaji: Mshtakiwa Namba Nne aliibua Hoja ambayo tumekutana Mahakamani na Kuwatafuta Wa husika, Na tumemshirikisha yeye Mwenyewe Katika Mchakato Wa Kufikia Maamuzi, Kama una jambo la Kusema Mshtakiwa Wa Nne Karibu kabla ya Kusema Uamuzi.
Freeman Mbowe: Mheshimiwa Jaji Kwanza nashukuru Kwa kunisikiliza pamoja ni Nje ya Utaratibu, Siku washirikisha Mawakili Kutokana na Kutaka lishughulikiwe kwa Haraka Nashukuru sana..
Na Kilichoendelea kwa Mahakama Kuu nimeshirikishwa Kwa Hatua zote. Pamoja na Kwamba tuna Njaa ila Nguvu za Kuendelea Kusikiliza Kesi bado tunayo, Kwa kuwa bado Jambo litahusisha na Idara zingine linaweza lisiishe Leo, Kwa hiyo napenda tuendelee Na shauri Wakati tunasubiria Maamuzi
Jaji: Umeomba Radhi Mawakili Wako Mawakili wa Serikali Umewasahau
Freeman Mbowe: aaahh! Na wenyewe tunawaomba Radhi sana, Sasa tuendelee tu Mheshimiwa Jaji..
Freeman Mbowe anaketi kizimbani.
Kibatala: Shahidi Sasa tuendelee, Shahidi Utakumbuka tulipo Ishia, Nakuonyesha Kielelezo namba P 13 Maelezo Ya Inspector Ndowo na Wakati huo Ulikuwa na Maelezo Ya Luten Denis Urio
Kibatala: Ni sahihi Shahidi katika Matokeo Ya Uchunguzi, Ni sahihi Kwamba Kwamba Meseji Unazosema Ulieleza ni Kielelezo namba G
Shahidi : Ni sahihi
Kibatala: Na Katika Upelelezi Wako Uligundua hilo Kielelezo namba G ni simu ya Luten Denis Urio
Shahidi : Ndiyo
Kibatala: Utakubaliana na Mimi Kwamba Ukisoma Riport ya Uchunguzi, achosema Luteni Denis Urio, Kwamba Namba ya Simu ya Kielelezo namba G ni 0719933386 imehifadhiwa katika Kielelezo hiki kwa Jina Free
Shahidi : Ni sahihi
Kibatala: Na ni sahihi Kwamba hii namba ya 0754612518 ndiyi Simu Card ambayo Tarehe 11 August 2020 ndiyo Simu ambayo ulimpatia Denis Urio Kwa Maelezo kuwa ataiwasilisha baadae
Shahidi : Ndiyo Simu Card hii
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Sim Card hii Hujawahi Kuitambua hapa Mahakamani
Shahidi : Ni sahihi
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Kwa Vyovyote Vile hata Kama tuki assume wewe ndiye Uliyemrudishia Sim Card hiyo, lakini Hakuna Handover ya Simu Tatu (Hati za Makabidhiano ya Simu 3) ikiwemo hiyo Samsung Duo yenye Sim Card hiyo
Shahidi : Si Kutoa Hati Ya Makabidhiano
Kibatala: Na Shahidi Kwakuwa Una Kielelezo namba D4 Maelezo Ya Luten Denis Urio, Je Kuna Mahala Popote anazungumzia Namba ya Simu Zifuatazo 1130138344.?
Shahidi : Haja zungumzia
Kibatala: Ni sahihi pia Katika Kielelezo Namba D4 Hakuna Mahala Popote Ambapo Luten Denis Urio anazungumzia chochote Kuhusu 729414989
Shahidi : Ni sahihi
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Katika Kielelezo namba P 23 Riport ya Uchunguzi Ya Inspector Ndowo Hakuna Mahala anapo zungumzia Kuhusu hizo namba
Shahidi : Ni sahihi
Kibatala: Zile Meseji uliokuwa unasoma Mawasiliano Kuhusu Fedha, Je unafahamu Kuhusu Extraction Report Kielelezo P26, Kuhusu Fedha, Je namba hizo 1130138344 na 729414989 zilipo Sababisha Kutafuta Extraction Report Kuhusu Mih+amala ya fedha
Shahidi : Ndiyo nafahamu
Kibatala: Wewe Kama Mpelelezi Kuna chochote ambacho ulifafanua Kwa Mheshimiwa Jaji Ulichogundua Kutoka Kwenye hizo namba
Shahidi : Siku fafanua
Kibatala: Naomba turudishe Kielelezo Namba P 23 hiyo Report, Kwa Ruhusa Ya Mahakama Nakuonyesha Kielelezo namba P26 ambayo NI Extraction Report
Kibatala: Zile namba ambazo Unasema Uligundua Kuwa Zina Meseji Ambayo zilikuwa za Freeman Mbowe zikiwa zinajadili Matendo ya Kigaidi.
Shahidi : Ndiyo nimeziona
Kibatala: Na hiyo Riport Ukisoma na Kuielewa
Shahidi : Nilisoma na Kuilewa Kwa Kadri ya Uwezo Wangu
Kibatala: Meseji zote hizo zimebebwa na namba ambazo umesema hukufafanua
Shahidi : Ni sahihi
Kibatala: Je unafahamu Implication za Kisheria
Shahidi : Kimya
Kibatala: Wewe Binafsi hjawahi Kuzichunguza Mahususi zinazoonekana Katika Extraction Report
Shahidi : Ndiyo
Kibatala: Hii Namba ya 0754612518 Ulishawahi Kuwaandikia Vodacom Kuweza Kupata KYC kuweza Kujua ilikuwa imesajiliwa kwa Jina la nani
Shahidi : Sikuwahi Kuandikia ila nilikuwa najua ni ya Luten Denis Urio
Kibatala: Na Ulijulia Wapi Shahidi , Je Denis Urio ametaja Katika Maelezo Yake Popote
Shahidi : Ndiyo ametaja
Kibatala: Wapi na Sehemu gani ametaja
Shahidi : Kwenye Particulars
Kibatala: Je ni sahihi Katika Maelezo Kuna sehemu Imeandikwa Kwa Herufi Kubwa “MAELEZO” halafu inafuatiwa na Maneno Jeshi la Wananchi
Shahidi : sahihi
Kibatala: Kwa hiyo Baada ya Neno MAELEZO huku ndani Hakuna Mahala Popote Luteni Denis Urio aja zungumzia lolote Kuhusu hii namba
Shahidi Upande Wa Maelezo haijatajwa
Kibatala: Ulipata nafasi ya Kufafanua Kwanini Ipo Juu lakini Haipo Kwenye Maelezo huku Ndani
Shahidi : Siku fafanua
Kibatala: Katika UShahidi Wako Kuna Mahala Popote Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Wewe una Utaalamu wa Mawasiliano ya Mtandao Wa Telegram
Shahidi : sikumueleza
Kibatala: Ulimfafanulia Mheshimiwa Jaji ya Kwamba Ulipata Wapi hiyo Knowledge au Information Kwamba Meseji ya Telegram zinabakia kwenye Simu
Shahidi : Sikumueleza
Kibatala: Nikiwa bado Kwenye simu, Twende Simu za Mshitakiwa Wa kwanza Khalfani Bwire, Ulishawahi Wahi Kufika Kituo cha Polisi Chang’ombe
Shahidi : Ni sahihi
Kibatala: Na Bila Shaka Ulishawahi Kufika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam
Shahidi : Ni sahihi
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Kutoka Chang’ombe hata Kama Una Priveledge za Kipolisi inaweza Kuchukua Dakika ngapi
Shahidi : Dakika 10 Mpaka 15
Kibatala: Ni sahihi Kwamba Simu za Bwire Zichukuliwa na Kingai Pamoja na Goodluck
Shahidi : Sahihi
Kibatala: Ilikuwa Muda wa Saa ngapi
Shahidi : Sifahamu
Kibatala: Ulipigiwa Simu Muda gani
Shahidi : Saa 2 Kamili za Usiku
Kibatala: Kwa hiyo tuseme Kuwa Ulipigiwa Simu Kujua Simu za Bwire Wanazo, Ilikuwa Saa ngapi
Shahidi : Saa 2 kwenda Saa 3
Kibatala: Toka ulipopigiwa Simu Kuwa Simu zipo, Je Ilikuwa Saa ngapi Mpaka Wanakuja Kukukabidhi
Shahidi : Ni Nusu Saa baadae
Kibatala: na tunakubaliana kuwa hizi Simu, Hapa Mahakamani hujaleta Makaratasi ya Makabidhiano
Shahidi : Ni sahihi Nilieleza Mahakama, Ila Sikutoa
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo namba P1 na P 13
Kibatala: Shahidi Nakuonyesha Maelezo Ya Onyo ya Adam Kasekwa Kama Moja ya Chanzo chako Cha Uchunguzi, Soma Hapo Kwenye IMEI namba
Shahidi : 3547289120275
Kibatala: Naomba namba P 23
Kibatala: Nakuonyesha Report Iliyoandaliwa na Inspector Ndowo Simu aina ya ITEL kwenye IMEI Namba ya Pili ni Namba ipi
Shahidi : 353736289120273
Kibatala: Je Inafanana na Kwenye Maelezo?
Shahidi : Zinafanana
Kibatala: Kwa hiyo Katika Maelezo ya Onyo ya Adam Kasekwa inasomeka 353736289120273
Shahidi : Haipo Kwenye Maelezo Ya Kukiri
Kibatala: Kwenye Maelezo Ya Adam Kasekwa Hakuna 36? na 298 Je tofauti hiyo ulitoa ufafanuzi
Shahidi : Sikutoa Ufafanuzi
Kibatala: Je Unafahamu Kwamba Namna katika IMEI namba Ukikosa namba Mbili Unaleta Utofauti
Shahidi : Kimyaaaaaaaa
Kibatala: Tafuta Katika Kielelezo namba P23 Je Kuna Mahala Popote Kuna Maneno yameandikwa PUK
Shahidi : Hakuna
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Sasa Ni simu card ipi ambayo Adam Kasekwa anai’ verify kama PUK
Shahidi : Maneno PUK ambayo ametatumia Katika Maelezo ya Onyo hayapo Katika Report ya Inspector Ndowo
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa katika Upelelezi Wako Uligundua Kuwa Maneno PUK ndiyo Sawa na IC +CID namba
Shahidi : Sikumwambia
Kibatala: Soma Maelezo ya Adam Kasekwa Namba zake za PUK
Shahidi : ni 892550509065499312
Kibatala: Soma Sasa Katika Report Ya Inspector Ndowo Simu D Yanaonekana Wapi
Shahidi : 892550509065499322
Kibatala: Ni sahihi huku Kuna 22 wakati Kule Kuna 12
Shahidi : Ndiyo ila ni hiyo hiyo
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Sasa Kama ulitoa Ufafanuzi
Shahidi : Sikutoa Ufafanuzi
Kibatala: Na Kutoa Eneo la Simu nakupeleka katika Eneo Lingine, Katika Riport ya Silaha aina ya Luger A5340 ya Tarehe 15 November 2021. Je ni sahihi Kwamba Taarifa hiyo ina rejea Jalada la CID/IR /2097 /2020
Shahidi : Sifahamu
Kibatala: Lakini Ulifanya Upelelezi Kwa Makini kisha Ndipo Kesi hii ikafunguliwa
Shahidi : Ni sahihi
Kibatala: Je hii Report Iliyoandaliwa kuwa ni Moja wapo ambayo Ulifanyia kazi
Shahidi : Sahihi Kabisa
Kibatala: Soma Hapa ni Jalada namba ngapi
Shahidi : CD/IR/2097/2021
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kuna Utofauti huo
Shahidi : Sikumwambia
Kibatala: Hilo Jalada la CD /IR /2097 /2021 Uliwahi kulifungua
Shahidi : Mimi nilifungua la CD/ IR /2097 /2020
Kibatala: Ukiwa Mpelelezi Makini, Je Ulipo wasiliana na Wakamataji, Walikwambia Adam Kasekwa alikamatwa Saa ngapi
Shahidi : Sikumbuki
Kibatala: Sasa Nikisema Walikamatwa Saa 7 Mchana utabisha
Shahidi : Nisha sema Kuwa Sikumbuki
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Sasa Kwa Maelezo Ya Adam Kasekwa alikamatwa Majira Ya Saa ngapi
Shahidi : Tarehe 05 August 2020 Muda wa Saa 5 Asubuhi Nikiwa Eneo la Rau Madukani, Glocery Nikiwa napata Kinywaji
Kibatala: Kwa hiyo alikamatwa Saa 5 Asubuhi
Shahidi : Ndiyo
Kibatala: Kati yako wewe na Adam Kasekwa nani anafahamu Muda Wa Kukamatwa
Shahidi : Mkamatwaji na Mkamataji
Kibatala: Wakamataji Washasema Saa 7 Mchana, Je Maelezo ya Mohammed Ling’wenya Ulifanyia kazi?
Shahidi : Ni sahihi
Kibatala: Na Unafahamu Kwamba Adam Kasekwa Na Mohamed Ling’wenya Walikamatwa pamoja
Shahidi : Ni sahihi
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Sasa Kuwa Mohammed Ling’wenya anasema alikamatwa Rau Madukani Saa ngapi
Shahidi : Majira ya Saa 7 Mchana
Kibatala: Ni tofauti ya Masaa Mangapi Kwa Watu Unaosema Walikamatwa Pamoja
Shahidi : Masaa Mawili
Kibatala: Wewe Kama Mpelelezi Ulifanyia Vipi kazi Kuhusu Utofauti Wa Muda
Shahidi : Nilifanyia Kazi, Ila Kila Mtu anaweza Kusema anachoona ni sawa
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji
Shahidi : Sikumwambia
Kibatala: Nakupeleka Eneo Lingine Kuhusu Sampuli za Maandishi Ambazo Unasema Ulichukua
Shahidi : Ndiyo
Kibatala: Na Unasema Ulichukua Sampuli za Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya
Shahidi : Nakumbuka
Kibatala: Ulichukua Sampuli ngapi Kwa Kila Mtu
Shahidi : Kwa Adam Kasekwa 8, Mohammed Ling’wenya 8 na Khalfani Bwire 8
Kibatala: Baada ya Kuzichukia Ukazipeleka Wapi
Shahidi : Maabara Ya Uchunguzi
Kibatala: Na Yakafanyiwa Uchunguzi na Mtu anaitwa Khamis Nankaa
Shahidi : Sahihi
Kibatala: Wakati Unaongozwa na Mr Kidando, Ile Taarifa Ulifanyia kazi
Shahidi : Ndiyo
Kibatala: Pamoja na Hukutoa ile Taarifa, Je Unafahamu Kwamba Nankaa anasema Kwamba Ulimpeleka Karatasi 9 ikiambatana na Barua Moja, Kwa hiyo anasema Kuwa Karatasi 9 na Barua Moja Jumla Barua 1 inakuwa 10 Wakati wewe Ulisema 8
Shahidi : Nilisema 8 ndiyo
Kibatala: Kwanza hiyo application Latter Ulitaja hapa Mahakamani
Shahidi : Sikumbuki
Kibatala: Je Uliongozwa Kufafanua Mfanano wa Karatasi 9 na 8 ulizotaja
Shahidi : Siku fafanua
Kibatala: Unakumbuka Wakati nakuuliza Maswali Nilikuuliza Kuhusu Maswali ya Sayansi ya Uchukuaji Wa uandishi wa Habari
Wakili wa Serikali Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Samahani hili Neno la Uandishi Wa Habari Sijui limetoka Wapi
Kibatala: Samahani Mr Chavula ni Uimi Uliteleleza
Kibatala: Unakumbuka Kwamba nilikwambia Ina shauriwa Kuwa Katika Sayansi ya Uchukuaji Wa Maandishi, Unatakiwa Kuwa na Sampuli 15
Shahidi : Nilisema Siyo lazima
Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Shahidi alizumgumzia Kuhusu Report Kwa Mambo aliyofanya, Shahidi Siyo Maker aulizwe yake aliyofanya, Wakili asiende Katika Details Sana Kwa Sababu Shahidi Siyo Maker wa hiyo Nyaraka
Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa Heshima Zote, Kwa Maneno ya Wakili Pius Hilla, Nakumbuka nilisimama hapa Mahakamani Kuwa Omba Pamoja na Kwamba hatuwezi Kuwapangia UShahidi Wao nilishauri Kuwa Haipo Mahakamani, Waachane nao
Lakini Wao Wakasema Kuwa ni UShahidi Wao, Walikuwa wana zungumzia Kuhusu Notebook ambayo miye Nikiwa naita Diary, Na haikuwa Mahakamani
Jaji: Notebook haikuwa tendered, Hoja yangu ni kwamba Wewe unafanya Rejea Katika Nyaraka ambayo Haipo Mahakamani
Kibatala: Kwa Heshima Mheshimiwa Jaji Wao wakati wanaongelea Kuhusu Kidaftari na Michoro Mpaka wake na Kituo cha Mafuta cha Morocco, Wao walileta Kwenye UShahidi Kuonyesha Kwamba Mwandiko Wa Bwire upo katika Kidaftari. Mimi siwezi Kujua kitatokea nini, Namimi siwezi Kuliacha hilo
Jaji: Hoja hapa ni Kwamba Wewe Unapo +uliza Maswali una Rejea Katika Report hiyo ambayo haijawa tendered
Yaani Unatakiwa Kurejea Maswali yote lbila Kurejea hiyo Rrport
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Univumilie, hii Report Wao wameshaitumia hapa Majina kama Khamis Nimepata Wao Baada ya Wao Kulitaja Kutoka Katika hii Report
Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji bora Kuweka Sawa, akichukuwa anarejea Kabisa Kwamba Khamis Nankaa anasema Kitu…. Wakili ajikite tu Kwa Kile ambacho Shahidi ajafanyia kazi
Jaji: Shida yangu Kubwa Mazungumzo Kuhusu hiyo Report ambayo Siku ya Mwisho Mimi Ndiyo naandika Hukumu Kulinganisha UShahidi Wa Serikali Na Utetezi wakati hiyo Report Mimi sina
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba niishie hapa, Kesho tukija naomba uturejeshe alichosema Kuhusu report
Jaji: tusilale na Kiporo, Wewe Unakumbuka Nini?
Kibatala: Alisema Kuhusu Sampuli, Kwa Kumbukumbu zangu Sioni tatizo, Mimi sina Shida na Maamuzi Yako, Ila soon kama Ni sahihi Kufanya Supress Kama Wao Kitu Walileta wenyewe Nina right ya Kufanya Cross Examination..
Jaji: Mimi Dhumuni langu siyo Kukuzuia Wala Siyo nia yangu, nimekuacha Uulize Maswali Mengi na Siyo Leo tu hata Siku ya Kwanza Uliuliza Maswali Mengi, Mimi Hoja yangu Mna refer katika Report ambayo Sina Uhakika Kama nitaipata au Mna mpango wa Kuleta Mahakamani.
Jaji: Musifanye Reference Kwa Report ambayo bado Haipo Mahakamani, Mimi nita’ refer nini?
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kwa sasa turidhie Ku airisha Mahakama yetu Kwa Muda ambao Utakuwa Umependekeza, Kutokana na Muda kwenda Sana
Wakili w Serikali: Mheshimiwa Jaji sisi hatuna Pingamizi
Jaji: Basi shauri linaahirishwa mpaka kesho Tarehe 15 February 2022
Shahidi unaonywa kesho Utaendelea Kuwa Kizimbani Kuendelea Kutoa UShahidi Wako
Washtakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya Magereza mpaka kesho Asubuhi saa 3