Kama ilivyoandikwa na ripota raia BJ, kutoka mahakamani, leo Jumatano 20.10.2021.
Mawakili wa pande zote wameshakaa sehemu zao.
Jaji ameshaingia mahakamani.
Kesi namba 16 ya mwaka 2021 inatajwa.
Robert Kidando anawatambulisha mawakili wenzake kwa kuanza na yeye mwenyewe.
- Robert Kidando
- Nassoro Katuga
- Ignas Mwanuka
- Esther Martin
- Tulumanywa Majigo
Peter Kibatala anawatambulisha mawakili wenzake kwa kuanza na yeye mwenyewe.
Mawakili wa utetezo leo
- Peter Kibatala
- Gaston Garubindi
- Seleman Matauka
- Idd Msawanga
- Michael Mwangasa
- Dickson Matata
- Maria Mushi
- Evaresta Kisanga
- Allex Massaba
- Jonathan Mndeme
- Fredrick Kiwhero
- John Malya
JAJI KIONGOZI: Wakili wa Serikali!
Robert Kidando: Shauri limekuja kwa ajili ya uamuzi. Tupo tayari Mheshimiwa Jaji.
JAJI KIONGOZI: Upande wa utetezi!?
Peter Kibatala: Tupo tayari Mheshimiwa Jaji Kiongozi
Jaji anachukua bahasha na kuichana.
JAJI KIONGOZI: Sasa nitajaribu kusoma kadri nitakavyoweza kwa ufupi yale yaliyosemwa hapa mahakamani kwa upande wangu ambayo ni umuhimu kama ufupisho. Na utakuwa ndio uamuzi wangu. Wakati anatoa ushahidi upande Shahidi Kingai alitoa Ushahidi kuwa Adam Kasekwa alikamatwa tarehe tano mweziu wa nane mwaka 2020.
JAJI KIONGOZI: Kwa mwa ushahidi wake, baada ya kuwakamata aliwachukua kwenda akubali asaidie kumtafuta Moses Lijenje. Na baada ya hapo alimsafirisha kuja Central Dar es Salaam. Kwa maelezo hayo ACP Kingai aliomba maelezo ya onyo yapokelewe kama sehemu ya ushahidi.
JAJI KIONGOZI: Ombi lake lilipingwa na upande wa utetezi. Na sababu ya pingamizi ni kwamba maelezo hayo yamechukuliwa kinyume cha muda wa sheria … sheria inayoongoza Mwenendo wa a Makosa ya Jinai kifungu namba 5 na 52. Na sababu ya pili ni kwamba Adam aliteswa wakati anatoa maelezo hayo. Mawakili wa pande zote mbili waliona kuna umuhimu wa kisheria fanya shauri dogo. Umuhimu wa kusikiliza shauri hili dogo. Mimi ni kubaliana nao. Kila upande ulikuwa na mashahidi watatu. Sikusudii kurudia kusema kila kitu ambacho mashahidi walisema hapa Mahakamani isipokuwa nitapitia yale ambayo nitarejea wakati wa uamuzi. Upande wa Jamhuri ulidai kwamba Adam Kasekwa ni kweli hakuweza kuhojiwa ndani ya masaa manne kwa sababu upelelezi wao ulikuwa haujakamilika.
JAJI KIONGOZI: ACP Kingai na Mahita wakati wamepewa taarifa mpango wao ultimate kuwa ni kuwakamata watu watatu. Licha ya hivyo hawakumkamata Moses Lijenje. Kwa mujibu wa Kingai ni kwamba Adam akijitolea kwenda kumtafuta Moses Lijenje sehemu mbalimbali kama Majengo, Boma Ng’ombe na Sehemu zingine bila mafanikio. Wakarudi Central Moshi. Kwa mujibu hiyo siku ya tarehe sita pia juhudi za kumtafuta Moses Lijenje zilindelea. Wakaenda mpaka Arusha maeneo ya Sakina kwa dada yake Moses Lijenje.
JAJI KIONGOZI: Tarehe sita amri ikatolewa kuwasafirisha kwenda Dar es Salaam. Kingai na Mahita wote wanakubali kuwa walisafiri kuja Dar es Salaam, na wakakabidhiwa kwa Msemwa. Kingai anasema baada ya kufahamishwa haki zake kisheria aliojiwa siku hiyo hiyo. Kwa upande wa utetezi, mshitakiwa anayetajwa (kama) Moses Lijenje, Adam Kasekwa alikanusha kuwaongoza Polisi wale waliomkamata.
JAJI KIONGOZI: (Alikanusha) kwenda maeneo kadhaa Mji wa Moshi na Arusha. Alikanusha pia kupelekwa Central Dar es Salaam bali kituo cha Polisi Tazara. Ushahidi wa Adam Kasekwa unaonyesha alipofika Dar es Salaam siku ya tarehe saba mwezi wa nane alipelekwa Tazara na Mbweni. Na siku ya tarehe tisa alitishwa ilikuwekwa sahihi.
JAJI KIONGOZI: Ilishabihishwa pia kupitia shahidi wa pili Mohamed Ling’wenya. Kwa mujibu wa Moses Ling’wenya alisikia walipokuwa Moshi akilia kwa sauti ya zege. Lilian pia kama shahidi wa tatu ambaye ni mke wa Adam Kasekwa alithibitisha kuwa alimuona Adam Kasekwa kuwa kateswa na kwa kuthibisha kwa makovu na alivyokuwa anatembea.
JAJI KIONGOZI: Hivyo baada ya kupitia pia mawasilisho yao ya pande zote, nawashukuru sana.
JAJI KIONGOZI: Kwa Upande wa Jamhuri wao walisisitiza kuwa maelezo yao yalichukuliwa kwa mujibu wa sheria kwamba Kifungu cha 50(2) kinaondoa muda huo katika hesabu za masaa manne toka awekwe chini ya ulinzi. Hivyo kwa mujibu wa Robert Kidando muda uliotumika kusafirisha watuhumiwa haupaswi kuwa sehemu ya masaa manne.
JAJI KIONGOZI: Kuhusiana na shauri hili sasa ambao upande wa Jamhuri wanakiri sasa kuwa walikuwa na Adama Kasekwa, upande wa Jamhuri sasa wameniletea kesi mbalimbali kwa ajili kufanya rejea kuhusiana na uamuzi sasa kwanini Adam Kasekwa amekamatiwa Moshi na kuja kuhojiwa Dar es Salaam. Kwa mujibu wa Robert Kidando sasa anasema ni sababu ya uzito wa tuhuma, kuzingatia pia makosa yalitakiwa kufanyika sehemu mbali mbali. Kuhusu pingamizi la pili kuhusiana Adamoo kulalamika kwamba ameteswa, Wakili wa Serikali amesema maelezo hayo yaliandikwa siku ya tarehe saba mwezi wa nane na kwamba upande wa utetezi wameshindwa kuibua shaka.
JAJI KIONGOZI: Na sababu ni Adam Kasekwa maarufu kama Adamoo katika utetezi wake hana na pingamizi ambao alikuwa amelitoa, ushahidi umetofautiana na pingamizi aliloibua. Upande wa utetezi umeshindwa kuwahoji mashahidi wa Jamhuri. Mwisho ni uzito wa hoja walizotoa. Kwa maelezo ya Adam Kasekwa ni kwamba japo alitoa maelezo lakini hakutoa kwa ridhaa yake. Kuhusiana na ushahidi wake hauonyeshi kuwa alitoa maelezo au kuteswa akiwa Central Police Dar es Salaam.
JAJI KIONGOZI: Kwa hiyo kwa upande wa Serikali ni kwamba ushahidi uliachana na pingamizi. Badala yake ukawa ni wa kufikirika. Na wakanirejesha kwenye kesi ya Rugemalila vs Jamuhuri, kwamba Kingai hakuhojiwa kwa mateso aliyopewa Adamu Kasekwa akiwa Moshi. Hakuhojiwa pia kuhusiana na maelezo aliyoyachukua Dar es Salaam.
JAJI KIONGOZI: Kwa Mujibu wa Robert Kidando akaeleza athari za kutokuhoji mambo ya msingi. Pia amezungumzia kukinzana kwa maelezo ya ushahidi kati ya Adam Kasekwa na Mohammed Ling’wenya. Kuhusiana na upande wa utetezi, mawasilisho yaliandikwa na John Malya, kwamba maelezo yalichukuliwa siku ya tarehe saba ambayo masaa manne yalikuwa yameshapita.
JAJI KIONGOZI: Kuhusiana na mazingira yaliyowekwa na sheria kifungu cha 50 kwamba Mahakama inapaswa kuzingatia masaa manne na kuyaondoa yale ya kusafirisha watuhumiwa, Moshi palikuwa na nyenzo zote ambazo zingeweza kuwezesha maelezo kuchukuliwa. Kuhusiana na mateso, Wakili Malya anasema mateso si lazima yawe ya kimwili, bali fikra na utu, au mateso yanayotweza utu wa mtu. Akaturejesha kwenye Katiba pia, na pia akaturejesha kwenye tamko la Umoja wa Mataifa linalozingatia Mateso na Utu wa Mwanadamu. Wakili Malya ametutaka Mahakama tuzingatie nyaraka hizo.
JAJI KIONGOZI: Na amaetupa kesi za marejesho. Kutokana na nyaraka hizo alizowasilisha Wakili Malya, amesema ingawa hapa kuwa na ushahidi wa kitabibu, lakini ametutaka tuzingatie ushahidi wa kimazingira
- Kuchelewa kuandika maelezo yake
- Kuchelewa kumsafirisha
- kuchelewa mfikisha mahakamani
- Ushahidi wa Lilian Kibonqa, mke wa Adam Kasekwa, wa kushindwakumwona mume wake pamoja na juhudi zote alizozifanya.
- Zoezi zima la ukamataji halikuzingatia utaratibu wa kisheria kama PGO
JAJI KIONGOZI: Na kwamba Jamuhuri wameshindwa kuthibitisha kwamba Adam Kasekwa alihojiwa kwa kuzingatia sheria. Kwa hiyo nimejaribu kwa ufupi kupitia yale yaliyosemwa mahakamani. Na baada ya mimi kupitia ushaidi uliowasilishwa mahakamani na mawasilisho, nitaanza na hoja ya kwanza kwamba maelezo yaliandikwa nje ya muda wa kisheria.
JAJI KIONGOZI: Mie nakubaliana kuwa muda ambao mtu anapaswa kuanza kuchukuliwa ni masaa manne. Exception pekee ipo maeneo mawili, kifungu cha 51 pale ambapo muda wa masaa umeongezwa. Na ni kuongezwa na askari polisi Mkuu wa Upelelezi au kwa kuleta maombi mahakamani. Masaa manne lazima yazingatiwe isipokuwa yale yaliyoelezwa yamezingatiwa. Ukishindwa hivyo ushahidi huo haupaswi kupokelewa.
JAJI KIONGOZI: Na mimi narejea kesi ya a Mahakama ya Rufaa kuwa kutokuzingatia sheria ya kifungu namba 51 katika kuchukua maelezo inaathiri ushahidi huo.
JAJI KIONGOZI: Pia kesi nyingine katika Mahakama ya Rufani palikuwa na ucheleweshaji wa kumsafirisha mtuhumiwa kwa siku mbili. Kwamba Mahakama ya Rufani katika shauri hili walikutana tena na mazingira kama haya ya ucheleweshaji wa kuchukua maelezo. Kwamba muda uliowekwa kisheria 51(a) ulipaswa kuzingatiwa na mahakama ikaondoa maelezo hayo.
JAJI KIONGOZI: Sasa Adam Kasekwa alikamatwa tarehe tano mwezi wa nane mwaka 2020 na maelezo aliandika tarehe saba mwezi wa nane mwaka 2020 bila shaka hapakuwa na uthibitisho wowote kwa upande wa mashitaka kuwa masaa manne yalishapita. Hivyo jambo pekee limebakia kama kuna exception.
JAJI KIONGOZI: Ni kweli wakati Adam Kasekwa anakamatwa palikuwa na mtu anaitwa Moses Lijenje. Kwa mujibu wa ushahidi upande wa Jamuhuri, mpango ulikuwa ni kuwakamata watu watatu. Lipo pia kwenye kumbukumbu za Mahakama.
JAJI KIONGOZI: Kwa maoni yangu, kwa kuwa Adam Kasekwa alikuwa na Moses Lujenje na Mohammed Ling’wenya alikuwapo Rau Madukani, ni maoni yangu kuwa jambo la kuanza kumtafuta linaleta mantiki kwamba palikuwa na juhudi za kutaka kujua alikuwa wapi. Ni vigumu kuondoa dhana kuwa Adam Kasekwa aliwaongoza kumtafuta Moses Lijenje. Na pande zote mbili hawabishani kwamba Adama Kasekwa alisafirishwa kuja Dar es Salaam.
JAJI KIONGOZI: Hata Lilian Kibona alitueleza kuwa alijulishwa kuwa mume wake alisafirishwa kuja Dar es Salaam. Kwa hiyo kwa upande wa Jamhuri ushahidi unaunga mkono jambo hili. Kuwa muda uliotumika kumtafuta Moses Lijenje na muda uliotumika kumsafirisha kuja Dar es Salaam Adam Kasekwa unapaswa kuzingatiwa kuondolewa katika masaa manne.
JAJI KIONGOZI: Kwa Upande wangu kwamba walipaswa kuomba muda nyongeza, kwa upande wa askari kama ameanza kumuhoji na akaona muda wa masaa manne hayatatosha, hivyo ni kwa maoni yangu ni kwamba Adam Kasekwa alikuwa hajaanza kuhojiwa.
JAJI KIONGOZI: Kwa upande wangu katika kesi ya Malya juu ya Albert Mendez ni tofauti na shauri hili kwa sababu kesi ile ilikuwa ni madawa ya kulevya.
JAJI KIONGOZI: Mahakama ilisema hapa kuwa na sababu ya kusubiri mshitakiwa atoe zile kete (pipi) katika shauri hili hakuna mazingira ya kusubiri bali walikuwa wanatembea na mshitakiwa sehemu moja kwenda nyingine. Kwa upande wangu naona kuwa ucheleweshaji katika shauri hili palikuwa na sababu.
JAJI KIONGOZI: Matakwa ya sheria yalikuwa yamezingatiwa.
JAJI KIONGOZI: Muda wa masaa manne hautajumuishwa kwa sababu za usafirishaji. Hitimisho la hoja ya kwanza ndilo hilo.
JAJI KIONGOZI: Sasa nageukia pingamizi la pili. Linahusu uhiari, kwamba Adam Kasekwa aliteswa kabla na wakati wa kuandika maelezo.
JAJI KIONGOZI: Kwa uelewa wangu, pingamizi linaonyesha mshitakiwa alikubali kuwa alitoa maelezo. Kingai anasema walipofika Dar es Salaam mshitakiwa alihojiwa siku hiyo hiyo baada ya kufika. Kwa mujibu wa shahidi huyu ni kwamba aliomba Mahakama ipokee maelezo yalichukuliwa Central Police Dar es Salaam.
JAJI KIONGOZI: Ili kutibitisha kwamba mshitakiwa alitoa maelezo katika Central Police Dar es Salaam, Mahita na Msemwa hawakushuhudia wakati Adam Kasekwa anatoa maelezo, na Msemwa alitoa Detention Register kwamba Adam Kasekwa alipokelewa Central Police Dar es Salaam siku hiyo hiyo. Alitolewa saa 12 kaso robo na akarudishwa siku hiyo hiyo saa tatu. Hapakuwa na pingamizi kwamba Mahakama isipokee kielelezo hicho.
JAJI KIONGOZI: Kutokipinga inaonyesha kwamba hupingi kilichopo ndani ya kitabu hicho. Maelezo ya Adam Kasekwa kwamba aliteswa na kuchukuliwa maelezo Mbweni, ushahidi unakinzana na madai yake.
JAJI KIONGOZI: ACP Kingai alidai kuwa maelezo yalichukuliwa Central Police Dar es Salaam. Upande wa utetezi ulitarajiwa kuweka pingamizi kuwa Adam Kasekwa hajawahi kufika Central Police Dar es Salaam. Kwa kukubali kuwa alitoa maelezo lakini kwa mateso anakubaliana kuwa ametoa maelezo akiwa Central Police Dar es Salaam na kwamna mshitakiwa hakufikishwa katika kituo cha Polisi cha Kati cha Dar es Salaam. Kwa hiyo kwa hitimisho langu naona mapingamizi yote mawili yamekosa mashiko, kwamba maelezo yalichukuliwa ndani ya masaa manne.
JAJI KIONGOZI: Kwa ushahidi pia upande wa utetezi walioutoa, na pia maelezo yalitolewa na mshitakiwa wa pili kwa ridhaa yake, na hilo ndilo hitimisho langu.
JAJI KIONGOZI: Wakili wa Serikali!?
WAKILI WA SERIKALI: Naomba utoe amri turejee katika shauri la msingi.
JAJI KIONGOZI: Upande wa utetezi?
PETER KIBATALA: Hatuna pingamizi Mheshimiwa Jaji Kiongozi.
JAJI KIONGOZI: Sasa kwa kuzingatia maelezo yaliyowekewa pingamizi nayapokea sasa maelezo haya kama ushahidi. Sasa tuta-break kidogo…
Baada ya mahakama kurejea….
JAJI KIONGOZI: Tunapaswa kunaendele na shahidi lakini nikaomba nishauriane na mawakili. Sasa nimeona kwamba shauri hili ni moja ya mashauri yanayopaswa kuisha kwa haraka. Kama shauri likienda mfululizo ingechukua miezi kama minne. Hivyo, kwa majukumu niliyonayo nimeona nijitoe aje jaji mwingine haraka iwezekanavyo.