Kama ilivyowasilishwa na ripota raia BJ leo tarehe 15 Novemba 2021.
Jaji ameingia Mahakamani. Sasa ni saa 4:05. Kesi namba 16 ya mwaka 2021 ya Jamhuri dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa.
Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha mawakili wa Serikali
- Jenitreza Kitali
- Abdallah Chavula
- Pius Hilla
- Nassoro Katuga
- Esther Martin
- Tulimanywa Majige
- Ignasi Mwinuka
Peter Kibatala anatambulisha mawakili wa upande wa utetezi
- Jeremiah Mtobesya
- John Malya
- Fredrick Kihwelo
- Sisty Aloyce
- Seleman Matauka
- Idd Msawanga
- Ladislaus Wongereza
- Evaresta Kisanga
9.Maria Mushi
Jaji anawaita washtakiwa wote wanne. Wanaitika kuonyesha wapo.
WAKILI WA SERIKALI: Shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa. Kuna uamuzi mdogo ulipangwa kutolewa tarehe ya leo. Tupo tayari kuupokea.
Peter KIBATALA: Mheshimiwa Jaji na sisi pia tupo tayari kupokea na kuendelea na shauri hilo.
Jaji anapekua nyaraka zake, kisha anaandika kidogo.
Ijumaa, siku ya tarehe 13 niliahirisha shauri hili na kutoa mwelekeo kuwa mahakama itatoa uamuzi mdogo leo katika kesi ya Trial Within Trial. Shahidi namba mbili ambaye alijitambulisha kuwa ni mwenye namba H4323 DC Msemwa akitoa ushahidi wake alisema akiwa Polisi Central Dar es Salaam alikuwa akifanya kazi kama General Duty, katika chumba cha mashitaka. Wakiwa katika chumba cha mashitaka kazi yao ilikuwa kupokea malalamiko. Akasema siku Agosti 7, 2020 alimpokea watu wawili ambao ni Adam Kasekwa Mohammed Ling’wenya.
JAJI: Na kwamba baada muda mfupi baada ya kuwakabidhi washitakiwa hao na kuwahifadhi walirudi Afande Kingai na ASP Jumanne na kwamba waliporudi aliwakabidhi washitakiwa. Na mshitakiwa namba tatu alimkabidhi kwa Afande Jumanne, na baada ya kuwakabidhi hakushughulika na jambo hilo zaidi ya kuwatembelea wakiwa Magereza, na wakati wote alipowatembelea walikuwa wazima wa afya. Alipata uhamisho kwenda kituo kingine cha kazi.
JAJI: Alipata wito wa kuja kutolea ushahidi, na kwamba alienda Polisi Central kwenda kuchukua kielelezo cha kuja kutolea ushahidi Mahakamani, akapapewa, na akaja kutolea nacho ushahidi Mahakamani katika kesi ndogo ya mshitakiwa namba mbili. Alipokea tena wito wa kuja kutolea ushahidi Mahakamani akaenda rena Central Polisi kuomba kielelezo, na kwamba alipoenda akaambiwa aende kuomba kwa Msajili.
JAJI: Na Msajili alimpatia kwa kusaini kwenye kitabu kielelezo na barua. Na baada ya hapo alikitambua kielelezo. Na baada ya hapo akaomba Mahakama ikipokee, jambo ambalo lilipingwa na mawakili wa utetezi. Mawakili wa upande wa utetezi walisema kwamba barua hiyo haikuwa inamuhusu yeye na hakusema namna ambavyo kielelezo kilimfikia na kwamba kweli ametajwa lakini barua hiyo imemtaja kwa jambo lingine.
JAJI: Na hapo waliiomba Mahakama kurejea kesi ya Sharif vs DPP na kesi ya Charles Gazilabo. Walisema kwamba maamuzi ya kesi hizo yameeleza namna gani ya kupokea nyaraka ya ushahidi na uthibitisho wa kukielewa kielelezo, na kwamba ithibitike kwamba siyo tu kwamba barua hiyo anaweza kuileza bali aeleze pia kwa namna gani alipata barua hiyo. Labda kama angetoa dispatch.
JAJI: Kwa kushindwa kuthibitisha ni kwa namna gani alipata kwa ofisi ya Mwendesha Mashitaka kielelezo kinaletwa kwa mujibu wa sheria, jambo ambalo angeomyesha alipataje kielelezo kingesaidia kuthibitisha kielelezo hicho. Sawa, ameonyesha baadhi ya Unique Features lakini alishindwa kutaja features zingine kama kumbukumbu namba.
JAJI: Shahidi anatakiwa kuwa competent, na kwa sababu hiyo wakasema kwamba kielelezo kinakosa Sifa hizo mbili na kwamba Mahakama ikatae kupokea. Kwa upande wao wa Mashitaka walipata nafasi ya kujibu. Wakaomba Mahakama itumie kanuni ya nyaraka kujizungumzia yenyewe.
JAJI: Barua kwa kuwa inaonyesha alipewa nakala basi anaweza kuiongelea Mahakamani, na kwamba kwa kuwa barua hiyo imetolewa na Msajili, basi hoja ya dispatch imekosa mashiko. Wapinga kielelezo hicho wameshindwa kuonyesha kwamba kielelezo hicho siyo Material wala Competent. Kwa shahidi kuweza kuelezea features za kielelezo hicho basi wao wanaona kwamba shahidi ni competent na ushahidi ni competent. Na wakasema kwamba kanuni za kupokea kielelezo zimetajwa katika kesi ya DPP vs Mizirahi kesi namba 493 ya mwaka 2016 ukurasa wa saba na wa nane. Wakaendelea kueleza Mahakama kwa mujibu wa maelekezo ya maelezo Iliyotoka kwamba wanaweza kufanya utaratibu wa kiutawala na kwamba wamefanya hivyo baada ya kuomba kwa utawala, na kwamba upande wa utetezi umefanya rejea ya kielelezo wakati kielelezo bado hakijapokelewa.
JAJI: Na kwa mujibu huo wakaomba Mahakama ione kwenye kesi ya Robison Mwangisi vs Jamhuri ya mwaka 2018 … Na kwa sababu hiyo basi kielelezo kinapaswa kiangaliwe Chain of Custody kama kielelezo kimemfikiaje shahidi. Hapakuwa na sababu ya kiutawala kwa NPS kunukuu Shahidi kwa sababu Shahidi alikuwa na nakala yake. Na upande wa utetezi walirudi kwa ajili ya utetezi wao, na kwamba katika utetezi wao kwamba nyaraka haiwezi kujizungumzia yenyewe lazima awepo mwingine wa kuisemea, na upande wa mashitaka wanajichanganya wenyewe. Mwingine anasema ijisemee yenyewe na mwingine anasema isemewe. Hakuna msingi uliolengwa kwamba kuna vitu kama unique features zilizotolewa mahakamani kuonyesha kama kweli vimesemwa kama vile mhusika angetaja tarehe na Kumbukumbu namba.
JAJI: kwamba hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya barua hiyo kielelezo na shahidi. Labda kama angekwepo Msajili kuthibitisha alimkabidhi kielelezo hicho. Kwa sababu hiyo waliiomba mahakama ione kama shahidi hakujenga misingi. Na ione kwamba shahidi hajaonyesha uelewa kuhusu nyaraka hiyo.
JAJI: Na nyaraka hiyo haiwezi kupokelewa kwa sababu ni msimamo wa sheria, na kwamba mahakama isishawishiwe na hoja iliyotoka kwamba mahakama ilisema fanya uamuzi na maamuzi siyo kwamba yalielekeza utaratibu huu bali maamuzi yalikuwa kuwakumbusha kufuata utaratibu. Kwa sababu hiyo basi wakaomba mahakama hii Ikikatae kielelezo hicho. Na huo ndio mwisho wa hoja za pzote mbili.
JAJI: Mahakama ikafanya uamuzi ambao ndiyo nafanya sasa hivi. Pingamizi hilo lilijengwa kwamba shahidi hakuweka misingi kwamba shahidi hakuweka msingi wa kutoa kielelezo na misingi wa competence ya kielelezo. Hayo ndiyo mambo mawili ya kuangalia. Kama ndivyo basi sheria kesi ambazo zimerejewa ambazo ni Sharif vs DPP na Charles Abel Gazilahabo zinaonyesha namna gani ya kupokea kielelezo. Zinasema kuangalia RELEVANCE, MATERIAL na COMPETENCE.
JAJI: Na hata hivyo competence yenyewe ni namna kielelezo kilivyofika mahakamani. Na competence kwa ujumla ni competence ya shahidi na kielelezo chenyewe. Sheria ya kesi zinasema kwamba ili kupima competence lazima tupatekungalia AUTHENTICATION. Kwa shahidi kutambua unique features, na Chain of Custody. Chain of Custody ni kuonyesha kwamba kama kielelezo kipo vilevile kama alivyokiacha mara ya mwisho.
JAJI: Mahakama hii inaona kwamba pande zote mbili wameziangalia kwa kina. Kwa upande wa utetezi, wao wanasema jambo hilo la unique features na unique objects zilijitokeza wakati wa kesi, na kwa namna hiyo basi tuache kutumia unique objects badala yake isomeke features. Kwa upande wa utetezi wanasema hakuna unique features kama tarehe na kumbukumbu namba. Kwa upande wa mashitaka wao wanasema kazitaja ambazo ni sahihi ya Msajili na Force Number zake. Kwa Mahakamani hii ili iweze kupata neno halisi la unique features ikaona kenye kamusi ya Kingereza ili kupata maana.
JAJI: Mahakama hii imeshindwa kupata tafsiri ya moja kwa moa kwa neno unique features. Hivyo mahakama ikaenda kwenye kamusi ya mtandao kwa kuangalia Htttps/Dictionary Universally. Kwamba ni kitu cha pekee
kwa namna ambavyo upande wa utetezi wamejenga hoja zao, sahihi ya Msajili haiwezi kuwa ni unique features, na kwa namna hiyo pia mahakama hii inaona kwamba jina na Force Number ni unique features. Kuhusiana na issue ya Chain of Custody hoja ya utetezi haikuwa Chain of Custody.
JAJI: Hoja yao ni kwamba barua hiyo imeelekezwa NPS na kwamba shahidi siyo mwaajiriwa wa NPS basi haimuhusu, na kwamba hajaonyesha ni jinsi gani alipata barua hiyo, na kwa jinsi hiyo alipaswa kuonyesha kwenye dispatch ambavyo Msajili alimkabidhi barua hiyo. Kwa kukosekana kwa mambo hayo mawili, basi imekosekana uthibitisho wa namna gani shahidi alipata barua hiyo kuleta mahakamani. Kwa upande wa mashitaka asuala la barua tayari shahidi kaonyesha namna gani alipata barua kutoka kwa Msajili. Maoni yao kwamba Chain of Custody ya kawaida haipswi kutumika.
JAJI: Na kwa maoni yangu kama ambavyo upande wa utetezi siyo Chain of Custody siyo wa kawaida. Tunachopaswa kungalia kama alipata kielelezo kwa utaratibu. Ni kweli alipaswa kutoa dispatch lakini tayari shahidi ameshaonyesha kwa mdomo namna gani ambavyo amepata ushahidi huo. Kwa Sheria ya Ushahidi inasema kwamba shahidi anaeleza ushahidi wake kwa mdomo na ataweza kuaminika, labda iamuliwe vinginevyo.
JAJI: Kwa kesi ya Goodluck Gado vs Jamhuri 118 2013 na kesi ya Sanga vs Jamhuri ya 2018, na kwamba shahidi atapaswa kuaminika kwamba ushahidi wake ni mkweli, na kwamba nafasi ya kuonyesha kwamba shahidi huyu si mkweli ni wakati wa dodoso. Mahakama inashindwa kuona shahidi huyu siyo mkweli.
JAJI: Upande wa utetezi wanayo nafasi wakati wa dodoso, wanaweza kumpima shahidi huyu kama mkweli au siyo mkweli. Kielelezo kinatakiwa kisomwe lakini ku- refer content ili aweze kutambua nyaraka hiyo. Kwa hiyo basi kwa Kesi ya Robison Mwangisi siyo sahihi kutumika kwenye kesi hii.
JAJI: Mahakama inaona kwamba tunapopewa nakala ya nyaraka, anamaanisha mambo mawili kwamba mtu anayepewa nakala kwa mhusika basi anataka mtu huyo ajue na pia anataka awe na haki ya kuitumia nyaraka hiyo. Mahakama inaona ni wazi kwamba kwa kutolewa nakala kwa shahidi juu ya nyaraka hiyo basi ni wazi lengo lilikuwa ni ili shahidi aweze kutumia nyaraka hiyo. Mahakama hii inaona haina sababu ya ku- fault shahidi huyo ambaye ameleta nyaraka hiyo.
JAJI: Kupokea nyaraka ni jambo moja lakini kupima uzito wa nyaraka ni jambo lingine. Katika kupima uzito wa nyaraka hiyo ni mahakama inaona kwamba ni wakati wa cross-examination. Kwa maana hiyo mahakama inaona barua hiyo iliyokuwa inaenda NPS na kwamba shahidi alipewa nakala. Basi Mahakama hii inaona ni nyaraka sahihi na kwa sababu hiyo mahakama inapokea barua.
(Mawakili wote wa pande zote mbili wanaamka na kukubaliana).
JAJI: Shahidi yupo wapi?
(Shahidi anaingia na kupanda kizimbani).
JAJI: Kwa mujibu wa kesi ya Robison Mwangisi nyaraka inapokelewa baada ya kusomwa, basi naelekeza shahidi aweze kusoma.
Mtobesya Objection! Siku ya Ijumaa mahakama ilitolea ufafanuzi kwamba kuna suala itatolea maamuzi leo. Tunaona ni muhimu kwa mahakama kutolea maamuzi hilo suala hilo kabla hatujaendelea.
JAJI: Upande wa mashitaka mna hoja yoyote?
WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji ulikuwa umeshaelekeza kwamba shahidi asome ili ile process ya admission iweze kukamilika. Kwa kuwa tayari kuna maelezo hayo sisi tunaona tuendelee na kusoma.
JAJI: Ni Kweli nilishasema hilo lakini kuna jambo nilishalitolea mahakamani, upande wa utetezi wanaona kwamba shahidi aliendelea kusoma kabla wakati wao wanapinga uhalali wa Mahakama.
WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa basi walete hizo hoja wakiruhusiwa.
MTOBESYA: Nitaanza mimi halafu kaka yangu Kibatala atamalizia. Mheshimiwa Jaji shauri hili ni shauri la uhujumu uchumi kwa mujibu wa ….
JAJI: Siku ya Ijumaa ilikuwa off record naomba unikumbushe sasa.
MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji siku ya Ijumaa Novemba 12, 2021 upande wa utetezi kupitia Kibatala alisimama na kusema kwamba shahidi akiwa kwenye shauri dogo kizimbani shahidi alionekana akiwa na diary, kalamu na simu. Wakati Kibatala anatoa hoja hiyo diary hiyo ilikuwa wazi. Kufutia na hoja hiyo Mahakama ikaeleza kwamba viletwe Vitu hivyo mbele ya Mahakama. Wakati wa kufunga siku hiyo mahakama ilielekeza kwamba ni busara shahidi arudishiwe simu yake, na suala likabakia kuwa ni diary. Na asubuhi ya leo sisi tupo tayari kuelezea ni kwanini shahidi huyu asiendelee kutoa ushahidi wake na kisha Kibatala atamalizia. Mheshimiwa Jaji hili ni suala ambalo limejotokeza katika ya mwenendo wa shauri.
MTOBESYA: Kama tunavyojua kuwa shauri hili ni la Uhujumu Uchumi kama ambavyo inaonekana katika Sura ya 200, Sheria ya mwaka 2019, tumepitia Sura ya 200 ya sheria hii kifungu cha 28 na kanuni zake. Inasema kwamba labda patakapotokea jambo kubwa basi ndiyo Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ndiyo itatumika.
MTOBESYA: Ukienda sasa Sura 20 ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kwenye kifungu cha 264 kinaonyesha nguvu ya mahakama hii. Kwa vifungu hivyo viwili vya sheria hizo mbili kama ambavyo zimefanyiwa marekebisho mwaka 2019, kama nilivyosema kwenye utangalizi, kwamba kitendo cha shahidi kukutwa na diary hasa ikiwa wazi wakati mahakama inaendelea, shahidi aonekane hafai na hakidhi, Na tutaieleza mahakama kwanini tunasema hivyo.
MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji suala la kutoa ushahidi linaongozwa na sheria namba sita ya sheria zetu ambayo ni Sheria ya Ushahidi kama ambavyo imefanyiwa marekebisho mwaka 2016. Ukisoma Sheria ya Ushahidi na PGO inaonyesha kwamba shahidi ambaye atakuwa ni Polisi, kwa sasa tumzungumzia ambaye yupo kizimbani, kwamba shahidi huyo ambaye ni Polisi atakuwa na nyaraka zozote endapo tu ataruhisiwa na Mahakama.
MTOBESYA: Na kama ruhusa inatoka ni pale anapotakiwa ku- refresh memory tu. Tunayesma kwa kifungu cha 168 (1) ya sura ya 6 ya Sheria ya Ushahidi na PGO namba 282 (7) na aya saba paragraph A, B na C. Aya ya saba inasema kwamba afisa wa polisi anaweza kuwa na nyaraka baada ya kupata ruhusa ya Mahakama.
MTOBESYA: Ikitokea sasa kuna umuhimu w akiambatisho au nyaraka kuingia Mahakamani basi utaratibu utafuatwa na kwa utaratibu ambao umetajwa hapa katika Sheria ya Ushahidi na katika PGO 282(7). Shahidi alipaswa kuomba ruhusa ya Mahakama, na kibaya zaidi ikiwa wazi wakati mahakama ikiendelea. Tunasisitiza hizo tataratibu lazima zifuatwe Ili washitakiwa wapate haki yao wakati wa cross examination.
MTOBESYA: Na hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 172 cha Sheria ya Ushahidi
(Mtobesya anaanza kusoma).
MTOBESYA: Ilitokea shahidi anafanya kwa kificho inakuwa inamnyima haki mshitakiwa kujua shahidi anarejea kwenye nini. Angeomba wazi ku- refresh memory kwa sababu sheria inaruhusu. Na kwa kuwa hakuomba tu kwamba apatiwe hiyo diary, ni hisia zetu kwamba alikuwa nayo tangu anaingia. Ni msimamo wetu kwamba shahidi huyu alikuwa anatoa majibu kwenye diary wakati anatoa ushahidi wake.
MTOBESYA: Na kwa sababu amefanya hivyo kabla hajamaliza kutoa ushahidi wake, basi kwa kifungu cha 127(1) tunasema shahidi huyu ni incompetent.
MTOBESYA: Sababu zilizoelezwa kwenye kifungu cha 127 (1) ni nyingi lakini kuna moja inasema…
(Mtobesya anasoma).
MTOBESYA: Kwamba alichokifanya shahidi ni sababu ya kumfanye yeye aonekane hafai kuwa shahidi, na kwamba tangu alipoishia siku ya Ijumaa, asiendelee tena, na kwa sababu hiyo ushahidi wake wote aliotoa mahakama ufutiliwe ambali. Na kwa maana hiyo shahidi aondolewe.
MTOBESYA: Na mheshimiwa Jaji, kwa kusisitiza tu, hata sasa ushahidi ulioingia hivi punde kwa sababu umeingia kupitia shahidi huyu basi uondoke. Mahakama ambayo ina uwezo wa kumwondoa shahidi ni mahakama inayomsikiliza shahidi, ambayo ni mahakama hii.
MTOBESYA: Kama ambavyo imeelekezwa kwenye sheria, Kesi ya Emannuel Nanyaro vs Peniel Saitabau, ukurasa wa 57, Jaji ambaye anamsikiliza shahidi ndiye anayetakiwa kufanya maamuzi juu ya competence ya shahidi. Kwa mawasilisho hayo Mheshimiwa Jaji na hivyo vifungu vya sheria, ni kwamba shahidi huyu asiendelee kutoa ushahidi wake na ushahidi wake aliotoa uondolewe kwenya Mahakama.
MTOBESYA: Na kwamba kwa sababu ya nyaraka aliyokuwa nayo kwenye kizimbani cha mahakama uondolewe kwenye kumbukumbu za mahakama. Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.
Anaamka Wakili Peter Kibatala.
KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, zifuatazo ndiyo misingi ya kisheria ya utoaji wa ushahidi na uwepo wa shahidi kizimbani. MOJA, kisimba siku zote hakuruhusiwi kuwa na material (nyaraka) isipokuwa kifaa kazi cha uapishwaji tu. Kitu kingine chochote kinachoweza kuingia kwenye kizimba lazima kiwe na ruhusa ya Mahakama. Upande wa pili wawe na haki ya kutumia nyaraka iliyopo kizimbani. Kwenye Sheria neno tunalotumia kuwepo kwa shahidi kizimbani ni EXAMINATION au EXAMINE.
KIBATALA: Na hiyo inaenda mpaka panapokuwa na amri ya kumruhusu au kumuonya kumrudisha. Wakati unaandika uamuzi wako tunakualika utafute maana ya neno ‘EXAMINATION’. Kwa ile ambayo tumetafuta sisi ‘OXFORD’ ya online “a formal test of personal knowledge or efficient of knowledge or skills.” Test ambayo tunailila mahakama itumie ni kwenye chumba cha mitihani, ingalie je, unapopatikana na nyaraka isiyoruhusiwa, je, umepeatikana na “unauthorised material”?
KIBATALA: Kama jibu ni NDIYO, basi shahidi amekosa sifa. Hiyo ‘diary’ aliyokuwa nayo ni kwamba ipo katika Mahakama na imetoka kwenye kizimba moja kwa moja kwenye mikono ya shahidi, na haijapitia kingine kwamba inawaweza kuwa siyo, na kwamba nasema muda ambao ilichukuliwa diary alikuwa bado kwenye kizimba na kesi ikiendelea.
KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, Wakili Mtobesya amekurejesha kifungu cha 127 ambapo unakuwa na nguvu ya kumuondoa shahidi. Ni kweli tunakiri mle hakuna neno shahidi, isipokuwa Bunge limeweka maneno kwamba na vingine vinavyofanana na hivi … Mheshimiwa Jaji tunakurejeshe pia kwenye kifungu cha 62, kwamba shahidi atoe ushahidi ndani yake yeye, akitoa kwingine ushahidi unakuwa siyo direct oral evidence.
KIBATALA: Wenzetu wakija hapa na kwamba mahakama isizungumzie mambo ya presumption, mahakama imetoka kutoa uamuzi kwa kutumia presumption. Basi hata katika hili ni presumption kwamba shahidi alikuwa anatumia nyaraka kwa nia ovu bila ruhusa ya Mahakama. Naomba nikupeleke Katika sheria ya General Statute ya North Carolina, kwamba kwa shahidi ambaye ameingia na nyaraka isiyoruhusiwa siyo shahidi sahihi, KWANZA kwa kuingia nayo na PILI kwa kushindwa ku- declare.
KIBATALA: Wenzetu wanaweza kuja na suala kwamba shahidi anaruhusiwa kuwa na notebook akiwa ni polisi. Hakuna open check hapo, hata mwandishi wa PGO ameandika katika namna havurugi taratibu za kizimbani. Lakini hiyo notebook ya polisi ina masharti yake. Kwa mfano inatakiwa iandikwe kwa penseli, na kwa entry zilizopo katika PGO namba 282(5) A mpaka J, a PGO 282 (6), aliyeandika alilenga kwamba shahidi asibebe majibu kizimbani. Na hizo entry zake ziingizwe kwa penseli na siyo kwa pen kama shahidi wetu …
KIBATALA: Suala linaweza kuja kwamba hatakiwi mtu kuangalia notebook ya polisi, basi ndiyo maana alitakiwa ku- declare na ndiyo na sisi tungepewa nafasi ya kuikagua. Na kama Mheshimiwa Jaji, kama utafuta sehemu ukaona hakuna kifungu cha sheria moja kwa moja, basi fikiria kuhusu mashahidi million wengine watakaoruhusiwa kuingia na diary kizimbani.
KIBATALA: Na kama ikibidi ukaona kumwondoa ni hatua kali sana, basi turuhusiwe tuone je, aliandika nini humo? Ni majina ya askari aliowataja? Ni tarehe alizokuwa anazitaja? Ni information alizokuwa anazitoa?
WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, ataanza Mr Chavula
Wakili wa Serikali Abdallah Chavula anasimama.
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji tumesikikiza hoja za wenzetu. Na siye ni msimamo wetu kwamba hatukubaliani na misingi ya hoja za wenzetu. Lakini pili hatukubaliani na maombi yaliyitolewa na wenzetu. Wenzetu wanadai kwamba shahidi wakati yupo kizimbani alionekana kuwa vitu ambavyo wamesema ni diary pamoja na kalamu, na simu. Kwa mujibu wao kwamba vitu hivyo haviruhusiwi kuwa katika miliki yake katika sehemu ya kutolea ushahidi. Na wakaielekeza mahakama kwenye kifungu cha 168 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.
WAKILI WA SERIKALI: Na GPO 282, kwamba pia malekezo ikaelekezwa zaidi, kwamba kuna kanuni ya kizimba, kwamba kanuni hiyo inapiga marufuku au inakataza kuwepo wa kitu chochote kile kwenye eneo la ushahidi isipokuwa vile vitu ambavyo vitamwezesha yeye kwenye kutoa kiapo. Mheshimiwa Jaji ni utaratibu ni kanuni na ni utamaduni unapoielekeza mahakama kwenye kanuni yoyote ile walau ielekeze mahakama kanuni ile unapoielekeza mahakama inatambulika kisheria. Nasi walau ionyeshe mahakama kwenye Jurisdiction yetu kanuni hii inakubali kama inatambulikabila kuonyesha hayo inabakia kuwa tu ni maneno yasiyoungwa mkono na mamlaka za kisheria.
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji umealikwa kwenye kifungu cha 268(1) cha Sheria ya Ushahidi na ukaelezwa kwamba kifungu hiki kinamkataza shahidi anapokuwa anatoa ushahidi asiwe na kitu chochote. Naomba nisome kichwa cha habari, inapatikana kwenye ‘Part 4’. Sehemu hii tunapata kumbukumbu ama kurejea kupata kumbukumbu na la pili ni production of documents.
WAKILI WA SERIKALI: Na Kifungu cha 168 (1) …
(Wakili wa Serikali anakisoma kifungu hicho).
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, lugha iliyotumika hapa haina ukakasi. Ni lugha iliyonyooka. Hakisemi shahidi asiingie na simu wala karatasi. Kusema kifungu kinaweka katazo kubebeba kitu, tunasema hapana na kwa heshima zote hatukubaliani na wenzetu.
WAKILI WA SERIKALI: Na kingine ni PGO namba 282. Mahakama imeelekezwa katika PGO 282 (7) na (8). PGO hii inatoa maelekezo kwamba afisa wa polisi anapokuwa anatoa maelezo ya ushahidi wake lazima awe na notebook. Sharti la pili anapopewa kwamba kabla hajaenda mahakamani arejee kwenye notebook yake. Kwa hiyo kinachoonekana hapa, haitegemewi kwamba kwenye notebook ya shahidi ambaye ni askari kutakosekana jambo au taarifa ya jambo analoenda kulitolea ushahidi mahakamani.
WAKILI WA SERIKALI: Isifanywe maajabu sana kwa afisa wa polisi kukutwa na notebook ya jambo analokwenda kulielezea. Naomba niende kifungu B PGO hiyo hiyo ya saba. Kwa ruhusa ya jaji au hakimu, mmiliki anaweza ili kurejea kumbukumbu pekee na siyo kwa dhumuni la kusoma au kuelezea kilichoandikwa.
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, hapa nayo ipo wazi. Yaliyomo humu ama yalipo hapa kwa ruhusa ya mahakama ama jaji au hakimu, kwamba mwenye notebook “the holder” ikawa kuna haja ya kujikimbusha na kujikumbusha pekee na siyo kufanya quotation. Na hajaruhusiwa kufanya hivyo. Hivi vifungu viwili ukavitizama kwa pamoja havitoi katazo.
WAKILI WA SERIKALI: Havitoi katazo la yeye shahidi ambaye ni afisa wa polisi kuwa na notebook. Vifungu vipo wazi. Haihitaji kufanya presumption. Na kama pangekuwa na katazo pangewekwa wazi kwamba ni marufuku. Ndiyo maana huko huko unaona “the holder may refresh the memory”. Mheshimiwa Jaji PGO 282 (8) ingetanguliwa na kichwa cha habari “Inspection of Notebook”.
WAKILI WA SERIKALI: Hii kanuni ya nane inaongea habari ya inspection na kuna mazingira matatu
A. OC. District may examine the notebook … Wanaruhusiwa kufanya ukaguzi kama zinatunzwa vizuri. B. Note Book may be preserved by the …, kapewa jukumu la kutunza askari mhusika. C. Note book may only be shown to …, Police Officer, Magistrate or Judges. Hapa panatolewa mpaka haswa wa nani anapaswa kuziona kwa ajili ya ukaguzi. Kama siyo Police Officer basi ni Polisi alikuwa gazetted.
WAKILI WA SERIKALI: Wengine ni mahakimu na majaji. Ni wale tu ambao sheria imewatambua. Kwanini wanafanya hivyo? Ukielekea PGO ndogo ya saba kifungu C, kwamba notebook zinakuwa na mambo ya kesi mbalimbali na mengine ni mambo ya siri. Ndiyo maana wanaweka mpaka kwamba ni akina nani wanaweza kuonyeshwa. Nahitimisha hoja yetu kwamba PGO ya 282 sehemu ya saba haijaweka katazo kwa shahidi ambaye ni polisi kuwa na notebook. Kichwa cha habari kinasema pale anapofanya rejea. Haijaweka katazo kwa shahidi kuwa na notebook.
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, hoja nyingine iliyotolewa ni hoja inayohusu competence ya shahidi kwa kile kilichojitokeza. Mahakama ikaelekezwa kwenye kifungu cha 127(1). Na wakasema kwamba kwa mujibu wa kifungu hicho cha Sheria ya Ushahidi, kwa kile wanachokodai wao kwamba Mahakama ina uwezo wa kutaka maelezo ya shahidi yaondolewe. Mheshimiwa Jaji naomba nisome.
(Wakili wa Serikali anasoma).
WAKILI WA SERIKALI: Wakati wanatoa hoja walisema shahidi anaoekana ana vitu pale kwenye kizimba na ana pen ananukuu. Na wakasema ana simu. Wakati hayo yanatokea shahidi alikuwa hatoi ushahidi. Alikuwa amekaa anasikiliza malumbano ya hoja. Na hata hayo yanayosemwa alikuwa anayafanya, alikuwa hayafanyi. Mheshimiwa Jaji wakati shahidi anaongozwa kuanzia maapisho mpaka anatoa ushahidi wake, Mahakama ilikuwa ikimtizama. Hakuna hata mmoja wetu alisimama kwamba shahidi alikuwa anaongozwa na kuna vitu alikuwa anasoma kivirejea. Hiyo hoja haikuletwa.
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, kwa heshima yote, Makamana yako inaalikwa kufanya presumption. Je, ni kweli inaalikwa kwenye facts?
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, siye tunaona hiki kifungu 127 (1) cha Sheria ya Ushahidi, haya maneno “any other similar cause” ni maoni yetu hayaingii hapa. “Similar Cause” inayozungumzwa lazima iwe na uhusiano na yale yanayotajwa, ugonjwa, umri mdogo, ndiyo ’cause’ zinazoweza kufanya mahakama imkatae shahidi. Ni lazima shahidi huyo awe anashindwa kuelewa maswali na lazima awe anatoa majibu. Ili “cause” nyingine zije ni lazima kwanza ipitie hii test kwanza. Shahidi amekuwa akiongoziwa hapa, alikuwa anauliza maswali na alikuwa anatoa majibu kwenye masuala aliyokuwa akiulizwa. Hakuna mahala imeonyesha kwamba Shahidi alikuwa haelewi na majibu aliyokuwa anayatoa hayana mahusiano mbele ya Mahakama. Hilo lwa kwanza.
WAKILI WA SERIKALI: Lakini la pili Mheshimiwa Jaji, hakuna mahala Mahakama yako imeelezwa kwamba wakati akiulizwa maswali na mwendesha mashitaka kwamba shahidi alishindwa kujibu na akawa anafungua makabrasha kutoa majibu. Kwa sababu hayo hayapo na hatajajitoleza, Mahakama yako haiwezi kutumia hiki kifungu cha kumpoka sifa shahidi.
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, Mhakama yako umealikwa kumkosesha/kumtengua shahidi. Kifungu hiki hakikutajwa. Mheshimiwa Jaji, tuna kesi hapa ya Mahakama Kuu ya Uganda tunaamini itakuisaidia. Ni ya Uganda vs Okumu Regan na wenzake watano, Criminal Revison namba 003 ya mwaka 2018 ukurasa wa 12 kuanzia paragraph ya 10, 15, na 20. Naomba kunukuu …
(Wakili wa Serikali ananukuu kwa kusoma).
WAKILI WA SERIKALI: Na kama ni kweli shahidi alionekana wakati wa ushahidi wake wakati anasema, basi kinaenda kuathiri uzito wa ushahidi wake. Na ndiyo maana kwenye kifungu cha 127(1) kwamba alikuwa anasoma havikuomekana. Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji kwa kanuni hii ambayo tumeisomewa Mahakama, kwamba itumie mamlaka yake, haipo.
WAKILI WA SERIKALI: Hakuna nguvu ya kisheria kufanya mahakama yako iondoshe shahidi na iondoshe ushahidi wake. Mheshimiwa Jaji nashukuru kwa kunisikiliza na mimi nakomea hapa.
(Anamwalika mwenzake Pius Hilla)
JAJI: Bila kurudia uliyoyaongea.
WAKILI WA SERIKALI: (Pius Hilla) Nashukuru Mheshimiwa Jaji. Nianze kwa kusema kwamba hoja ambazo wameleta ni hoja ambazo hazipo sawasawa, na kwamba Mahakama yako haijawa moved kwa kujitosheleza. Vifungu vilivyotumika kui- move Mahakama kama nilivyowasikia wenzetu, ‘order’ walizoleta ni kumkosesha ama kumtengua shahidi na ushahidi wake utupwe. Ni kifungu cha 127 cha Sheria ya Ushahidi. Ni kweli waliongelea kwa hoja zao. Mheshimiwa kwa kuwa maombi haya yapo kwenye jurisdiction of the court kwa maana order ambazo zilikuwa moved, maombi yalipaswa kuletwa kwa vifungu ambavyo ni shahihi.
WAKILI WA SERIKALI: Kutokuletwa kwa vifungu hivyo hakuifanyi Mahakama kufanyia kazi. Mheshimiwa Jaji niendelee kuilaka Mahakama. Wenzetu hawakatai kwamba kile kilichotokea hapo kizimbani no factual issues. Hilo halina ubishi. Factual issues zinakuwa proved by evidence in this matter. Factual Issue imetoka from the back. Wote tuliopo kwenye bar na even from the bench hakuna aliyeona.
JAJI: Kwenye … nikukumbushe submission ya leo hajasema ilikuwa from the back.
WAKILI WA SERIKALI: Aliyesema hayo hakusema Mahakamani ni swali lipi na majibu yapi aliyatafuta from the … where. hajaeleza kwamba material yalipo kizimbani yalikuwa yamefunguliwa. Mheshimiwa Jaji, hakuna namna motion hiyo inaweza kuzingatiwa mpaka pale huyu anayeleta motion kuyazingatia hayo.
WAKILI WA SERIKALI: Tunayaeleza haya kwa sababu wote tulikuwapo mahakamani wakati namwongoza shahidi mimi ndiye nilikuwa karibu na shahidi kuliko mtu mwingine. Mheshimiwa Jaji nizungumzie kuhusu Presumption.
WAKILI WA SERIKALI: Hukuona shahidi anasoma wakati ana- testify. Wala Mheshimiwa hiyo haiwezi ku- qualify kuwa hiyo ni presumption.
WAKILI WA SERIKALI: Tunawasilisha kwamba alichokuwa anakitokea ushahidi shahidi ni majibu kutoka kwenye knowledge yake na si vinginevyo. Mheshimiwa Jaji, Mahakama yako umealikwa kutumia examination room test. Sisi tunasema siyo sawasawa. Examination Room ina kanuni zake na sheria zake. Test ya kisheria ni Ile iliyopo kwenye section one ya Sheria ya Ushahidi. Wamesema kwamba Shahidi amekutwa na unauthorized material, lakini hilo pekee halitoshi kumwondoa au kumtengua shahidi. Haya ni masuala ya kisheria na yanapaswa kufanyika kisheria.
WAKILI WA SERIKALI: Kwa kuwa material yaliyopo hayajaonekana popote kama yalikuwa yanatumika kujibu majibu, ushahidi wake ulikuwa ni moja kwa moja kutoka mdomoni mwake. Mahakama yako ikaambiwa shahidi wako haja- declare. Kesi ya Goodluck Kyando imesema hayo. Je, mtu kutoka nyuma anaweza kuwa na bad faith?
WAKILI WA SERIKALI: Baada ya hayo naomba mwenzangu Robert Kidando amallizie kuwasilisha.
JAJI: Naamini yatakuwa siyo miongoni mwa mliyoongea.
WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji napenda kuwaongezea kwenye hoja ya Pius Hilla kwenye kifungu cha 264 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Siyo kwa njia hii. Kwa namna yoyote hatuoni kwamba kifungu hiki kilikuwa kuna mamlaka na maombi yaliyopo mahakamani. Tafsiri ambayo Mahakama Kuu ilitoa katika kesi ya EDWARD ISACK SHAYO AND ANOTHER vs REPUBLIC ambayo ni shauri la jinai namba 14 la mwaka 2019, Mahakama Kuu ya Tanzania iliyoketi Moshi, katika kutafsiri kifungu cha 264, alikuja na uamuzi kwamba
(Wakili wa Serikali anasoma).
WAKILI WA SERIKALI: Ni katika mazingira hayo tu ndiyo kifungu hicho kinaweza kuwa involved. Lakini unakwenda mbele zaidi katika kifungu cha 264 kwamba kimeipa mamlaka Mahakama Kuu lakini pia kwa mazingira maalumu. Namaliza kwa kusema kifungu hiki hakisomwi peke yake Mheshimiwa Jaji bali kwa kuangalia sheria zingine. Bila kuathiri mambo niliyotangulia kuyasema, Mheshimiwa Jaji … Tunaomba uone kwamba hiyo siyo njia sahihi ya kuomba forum, kwa sababu maamuzi ya mahakama yapo.
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji kuna ombi lingine ambalo wenzetu tunaomba wanaomba hifadhi, pale waliposema kwamba hata kama hakuna Sheria kwa maombi waliyosema kwamba is it a … game kwa shahidi kuingia na material kwenye kizimba. Sisi tunasema wasikimbilie huko. Ilikuwa ni kazi yao na kwa sababu kazi yao hawakufanya wasitafute huruma ambazo hazipo.
WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji, baada ya kuwa nimesema hayo naomba kuunga mkono hoja za wenzangu za Abdallah Chavula na Pius Hilla kwamba maombi haya uyakatae hata kama na sababu ambazo hatujawasilisha.
JAJI: Kwa kuwa leo tunaishia kwenye jambo hili basi tupumzike kidogo. Turudi hapa saa 8:20.
Jaji anaamka na kuondoka kwenye chumba cha mahakama.
Jaji ameingia mahakamani. Kesi namba 16 ya mwaka 2021 ya Jamhuri dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe imetajwa.
Wakili wa Serikali anasema column yake iko vile vile. Peter Kibatala anaomba kumjumuisha Wakili Dickson Matata kwa sababu alikuwa hospitali.
MTOBESYA: Naomba kujibu hoja za wasomi kaka zangu mawakili wa Serikali. Ningeanza na hoja aliyoiongelea kaka yangu Robert Kidando na Pius kuhusiana na kifungu cha 164 cha Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai na Kidando akaenda mbali kwamba Mahakama isipokee hoja yetu. Mheshimiwa Jaji sisi tunasisitiza kifungu cha 264 cha CPA ndicho kifungu kinachotupatia mamlaka. Kuna aina mbili za vifungu. MOJA, kuna Enabling Provision vinavyokupatia haki. PILI, kuna Prescriptive Provision vinavyoelekeza namna ya kuifikia haki. Kwa maoni yetu kifungu cha 264 cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ni Enabling Provision.
MTOBESYA: Kifungu cha 127 cha Sheria ya Ushahidi kinaangukia katika Prescriptive Provision. Nilisema kwamba kifungu cha 28 ndicho kinatoa mwanya wa kutumia vifungu vingine. Labda kwanini nieleze inatumika 264 ya Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai, ni kwa sababu vitendo vinavyotokea na kuipatia Mahakama kutumia vifungu … Kifungu cha 264 kinatumika kwenye proceedings. Huu ndiyo wakati wake sahihi, in the Cause of Proceedings. Siyo kitu ambacho ni extraordinary. Kuna kesi nyingi sana kuhusu kifungu hiki lakini siwezi kuzitaja kwa sababu wenzangu hawana nafasi ya kujibu na watasema ni jambo jipya.
Mtobesya: Kifungu hiki sawa na kifungu cha 95 Sheria ya Mwenendo wa Madai. Niende kwenye kesi iliyotajwa na kaka yangu Robert Kidando, ya Edward Isack Shayo. Mheshimiwa Jaji, ukiisoma kesi hii ya EDWARD ISACK SHAYO, mazingira yake ni tofauti na shauri ililolopo mbele yako. Kwenye kesi hii Edward alikuwa anaomba Mahakama iende kwenye masuala aliyoyaomba, Mahakama ilikuwa haijaingia kwenye Proceedings. In the first cause, katika mazingira hayo Mahakama ilikuwa sahihi kusema hivyo lakini siyo hapa. Hapa tayari Mahakama ipo kwenye proceedings. Tunaomba Mahakama ifanye jambo ambalo litakuwa sehemu ya mwenendo wa shauri. Alivyosema kaka yangu Robert Kidando tumenukuu kifungu nje ya context basi na yeye amenukuu kesi nje ya context. Tukizungumzia namna ya kuifikia haki sasa, ni pale mahakama inapoweza kuzuia au kumzuia shahidi wa upande wowote kutoa ushahidi. Mheshimiwa Jaji naomba itoshe kusema kwamba the court was properly moved na kwa sababu hiyo tunaomba Mahakama ifanye tuliloliomba Mahakama kufanya.
MTOBESYA: Sasa niende kwa Pius Hilla kwa hoja yake kwamba we made submission from the bar na made evidence from the bar. Wakati tunawasilisha Mheshimiwa Jaji tuliongelea mambo yaliyotokea hapa Mahakamani, kwa sababu hiyo hakuna ubishi kwamba shahidi alikutwa na diary na kwa sababu hiyo diary ipo kwenye mikono ya Mahakama, hakuna wakati wowote wakati wanasema kwamba shahidi aliomba diary wakati yupo kizimbani. Hizo fact (things speak for themselves in Latin). Ndiyo maana tukaiomba Mahakama kwamba shahidi kakutwa na diary, diary ambayo hakuomba formally. Na kwa sababu hakuomba formally na sisi tuna- submit kwamba shahidi akiwa kizimbani hatakiwi kuwa na material ya namna yoyote ile, na ndiyo maana alikuwa anaitumia kinyume na taratibu za Mahakama.
MTOBESYA: Na ku- draw advance advice ni kitu ambacho Mahakama imekuwa ikikifanya. Siyo jambo geni. Kwa hiyo ni submission yetu kwamba Mheshimiwa Jaji hatukuwa na haja ya ku- file affidavit kwa vitu ambavyo vipo obvious. Kwa hoja hiyo nisiongee sana. Niende kwa hoja ya kaka yangu Abdallah Chavula kwamba it’s their submission kwamba it’s a mare fact kwamba shahidi amekutwa na material kizimbani basi hilo halikoseshi sifa ya shahidi kuendelea kutoa ushahidi, na kwamba test za kumwamini shahidi or other wise zimekwekwa pale kwenye kesi ya Goodluck Kyando.
MTOBESYA: Hatuwezi kusema kwa sababu zipo pale kwamba shahidi ataaminika labda pawe na sababu za kutokumwamini. Sisi tunasema zipo sababu za kutokumuamini huyu shahidi na sababu zenyenwe zinatokana na two facts ambazo tumesema zinatokana na ukweli wala siyo zawadi. Na ndiyo maana tuliiomba Mahakama imkague kwa sababu alikuwa anafungua kwa kificho. Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji ni submission yetu kwamba Kesi ya Goodluck Kuando haisaidii chochote katika kesi hii kwa sababu shahidi huyu hajakidhi vile vigezo.
MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji, kuna submission ya kaka yangu Abdallah Chavula. Kwanza aliomba kabisa Mahakama…
WAKILI WA SERIKALI: (Abdallah Chavula) Objection!
MTOBESYA: Sawa lisitusumbue hilo. Twende kwenye PGO ya 2832(7)A. Alisema kwamba shahidi ambaye ni polisi anaruhusiwa kumiliki ‘notebook’ kizimbani. Na akasema inayofuata kwamba mmiliki ndiye anaweza kuwa na ‘notebook’. Sisi tunasema Mheshimiwa Jaji ni tafsiri potofu kwa sababu PGO 282 (7)A inasema “Prior to get in into court”. Wakati naongea mwanzo nilisema anaweza, MSISITIZO HAPO, kifungu hakisemi kwamba kuna ulazima wa shahidi kuja na ‘notebook’ kwenye Mahakama haisema eneo gani. Halazimishwi kuwa nayo muda wowote. Lakini hata neno “Holder” lililotumika Section 282 haimaanishi kwamba muda wote atakuwa nayo.
MTOBESYA: Kwa tafsiri ya hii PGO holder is the one who possess. Kama tunakubaliana “holder” ndiyo “possesser,” he will still possess it siyo lazima aingie nayo mahakamani. Kwa hiyo ni submission yetu Mheshimiwa Jaji kama alivyowasilisha kaka yangu Chavula, havisemi kwamba muda wote akiwa Mahakamami aje na diary yake. That’s submission tunaomba iwe disregarded kwa sababu nimenukuliwa katika sehemu isivyo sahihi. Nije kwenye hoja ambayo ameongelea kwamba ukisoma 282 (8) kwamba ukisoma vifungu hivyo notebook haiwezi kukaguliwa na mtu yoyote ambaye ajatajwa mle. Kwamba kwa sababu sisi mawakili au washitakiwa hatujatawa basi tunakosa uhalali wa kukagua au kuangalia hiyo notebook.
MTOBESYA: Kwa maana hiyo basi hata shahidi aki- refresh memory kwa namna ile hata kama entry itaingia ina maana kwamba mshitakiwa hatopata access. Ukisoma pamoja kifungu cha 172 cha Sheria ya Ushahidi ikisomwa kwa pamoja na Ibara ya 13 (a) ya Katiba ya Mwaka 1977 juu ya haki ya kusikilizwa, ni submission yetu kwamba Mheshimiwa Jaji haki ya kusikilizwa ni pamoja na kumhoji shahidi juu ushahidi wake.
WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa tunaomba Ibara ya Katiba isinukuliwe. Tunaona wanaipeleka mbali sana haya mambo. Sasa wapo kwenye haki ya kusikilizwa.
JAJI: Wanaipeleka wakina nani?
MTOBESYA: Nikisema kwamba Ibara ya Kabita juu ya haki ya kusikilizwa, je, nikisema watasimama.
JAJI: Sema tuone kama watasimama.
WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Hata kama ikiondoka bado jambo litakuwa palepale. Hawa hawajasema suala la kutokusikilizwa kwa kwa bahati mbaya, na siyo subject matter Iliyotufikisha hapa.
MTOBESYA: Hata nikiondoa Ibara ya 13 bado itabakia 175 ya Sheria ya Ushahidi.
JAJI: Wakati anazungumza alisema hakuna sababu ya hivyo vifungu kuletwa.
WAKILI WA SERIKALI: (Abdallah Chavula) Mheshimiwa Jaji ukisoma utagundua kwamba nilirudi 282(8)C.
MTOBESYA: Labda turudi kidogo kwenye misingi, kwamba tunachojibu hapa ni hoja walizoibua hapa. Hoja yetu ni credibility ya shahidi siyo haki ya kusikilizwa. Wasiwe na hofu.
JAJI: Kama nimeeleza vizuri, ulichokuwa unasema ulikuwa unasisitiza kwamba wakili wa utetezi na wateja wake kupata nafasi ya kumkagua na kama hatamkagua basi Ibara ya 13 itakuwa imevunjwa. Je, likikaa hivyo kuna tatizo?
WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Basi asiendelee zaidi ya hapo.
MTOBESYA: Sitaendelea zaidi ya hapo. Sasa kaka yangu Chavula alirejea kesi ya Uganda. Alikuwa anasisitiza kwamba ni ngumu sana kumwondoa shahidi hasa kwa misingi ambayo sisi tumeijenga. Alisisitiza kwamba mahakama isiwe presumptive. Hakuna mahala popote tumakuwa presumptive na hakuna jambo la kufikirika tuliloongea. Tumesema kuna facts mbili na siyo presumptive. Zipo kwenye kumbukumbu.
MTOBESYA: Ni kitu ambacho kipo vivid na kwanini sisi tumesema lazima Mahakama iseme neno kwa hii situation iliyotokeaa Mahakamani. Chavula emesema na amerejeea kwenye ufafanuzi kwamba washitakiwa hawana haki ya kupata nafasi ya kukagua diary isipokuwa eneo ambalo lina husika tu. Mbona tunaona wanajichanganya wenyewe kwa wenyewe kwa maelezo yao? Mbona hawajasema sasa ni sehemu zipi ambazo washitakiwa wanaruhusiwa kuziona?
MTOBESYA: Na mbona hawajafanya maombi kupitia Kifungu cha 168(1) au PGO 282 (7) b & c. Hakufanya. Katika mazingira hayo tunawezaje kusema kwamba washitakiwa wanaweza kupata hiyo haki wakati mwishoni wanasema diary yote haitakiwi kukaguliwa? Ndiyo maana Mheshimiwa Jaji sisi tulisema kwamba Mahakama i- draw negative influence kwa sababu zoezi analosema kaka yangu Chavula kwamba linaweza kumpatia mshitakiwa haki, haliwezi kufanyika katika mazingira hayo.
MTOBESYA: Kwa namna hiyo tunasema shahidi na upande wa Mashitaka hawakufanya matakwa haya kisheria ili shahidi awe na material ambayo amekutwa nayo kizimbani. Mheshimiwa Jaji Mahakama imchukulie kwamba shahidi huyu si mkweli, hajiwezi na haaminiki. Ni hoja yangu na maombi yetu kwamba ombi letu tuliloleta Mahakama ione lina mashiko na itupatie nafuu kama ambavyo tuliwasilisha mwanzoni.
Anaamka Peter Kibatala.
KIBATALA: Mheshimiwa Jaji naomba u- note yafuatayo, kwamba hakuna wakili hata mmoja wa Serikali aliyegusa hoja ya kifungu cha 62 cha Sheria ya Ushahidi kuhusu sifa za shahidi. Na hawajajibu kabisa kwamba katika diary ya shahidi alikuwa anaweka mambo yake binafsi kama masuala ya Man U na Arsenal. Pia wakati natoa hoja zangu wakati natoa tafsiri ya kifungu cha 127 “any other similar cause” nilikupeleka kwenye ‘extract’ ya North Carolina evidence Statute. Na nikasema kwamba kwa shahidi kuingia na material kwenye kizimba kunamfanya aonekane siyo mwaminifu. Wenzangu hawajajibu kabisa kuhusuiana na hilo.
KIBATALA: Mimi nilikupa material ya kusoma na material yangu hayajapingwa wala kuguswa kabisa. Tunasisitiza kwamba duty to tell the truth inasisitiza kwamba unapaswa uonyeshe kwamba unamiliki haya material na hayana madhara.
KIBATALA: Sasa doubt ya kwamba may be kuna kitu hiki au kile tunatoa wapi wakati mtu amekutwa na nyaraka bila kipingamizi kutoka kwa shahidi? Sasa huo wasiwasi tunatoa wapi?
KIBATALA: Niende kwenye allegation kwamba kuna wrong citation. Kwa bahati nzuri kifungu hicho kimeshawahi kutumika na Mahakama hii na kesi hii kwa upande wao wa mashitaka walipoomba kurekebisha nyaraka mojawapo hapa Mahakamani. Hata maneno kama yanafanana fanana na kwamba Mahakama ilikuwa imetungiwa kifungu hicho kwamba haifungwi mikono na huo ndio umahakama wenyewe.
KIBATALA: Kifungu cha 127 kinatoa katazo, sifa za competent witness kama vile kifungu cha 62 ambacho hakijajibiwa kinatoa sifa ya competent testimony. Kesi ya Edward Isack Shayo ni kwamba kesi Ilishaisha na adhabu ikatolewa, hawa watu wakampeleka Mahakama kwamba wanaomba kufanya maombi ya kuongezewa muda wa ule walikaa mahabusu. Na kifungu cha 164 Mtungi amesema kabisa hakiwezi ku- support Judicial Application. Na sisi hatujaiomba Mahakama ifanye review na ndiyo maana wakaambiwa mkitaka kateni rufaa. Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji sisi tunaona kesi imerejewa isivyo sahihi kabisa. Mheshimiwa Jaji, swali ni je, shahidi amekutwa au hajakutwa na diary?
KIBATALA: Na tulitoa hapa suluhu kwamba twendeni tukaangalie hiyo diary kama ina vitu hatarishi, kuona kama kwenye hiyo diary kuna ushahidi au la. Wanasema suspicious wakati tuna material katika mikono ya Mahakama? Mheshimiwa Jaji, nimemsikia msomi Chavula akizungumza PGO namba 282(5 & 6) wao wamegusa 7.
KIBATALA: Tulisema kwamba hata Shahidi ambaye ni polisi kuna utaratibu wa kuwa na material hayo, ikiwemo suala la kuwa na penseli na kuomba ruhusa ya Mahakama. Niende kwenye 282(7), kwamba mamlaka ya kuwa na material kwenye kizimba ni “a prior permission of the court”. Sijasikia wakili (wa Serikali) hata mmoja akilijibu hilo. Badala yake wanakuja kusema eti ilikuwa muda wa submission.
KIBATALA: Nimesema kwamba ushahidi unaanza tu pale ambapo shahidi anakuwa ameapishwa. Na hii ni sheria na wala siyo maoni, kwamba afisa wa polisi atakuwa na hiyo ‘notebook’ baada ya ‘prior permission.’
KIBATALA: Naona Chavula alizumgumzia 282( 8) A na B makusudi kabisa akaruka 8C, kwamba wanaopaswa kumkagua ni akina nani na wakati gani. Hakuna kwenye mfumo wa utoaji haki kwamba shahidi tu ndiye anaruhusiwa kuingia na material hiyo mahakamani. A na B zilikuwa cited bila sababu yoyote ile ya msingi na tunaamini kwamba wenzetu wanalifahamu hilo.
KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, kwamba hivyo vifungu havitoi katazo, kama havitoi katazo kwanini walisema kwa ruhusa ya Mahakama? Kwanini walisema upate kibali? Anayesema hakuna katazo hana support ya sheria.
KIBATALA: Tulisema na tunasisitiza kwamba kizimbani ni sehemu safi ni strictly reliability kwa hiyo tunaongelea kuhusu quantum.
KIBATALA: Kwamba una material? Jibu ni NDIYO. Basi una- suffer concequence ya kuwa na material Mahakamani. Mmoja alikuwa anauliza affidavit, mwingine nusu ashike Biblia akasema alikuwa na shahidi karibu kabisa. Sasa swali hapa ni je, alikuwa na material na je, alimuomba nani ruhusa? Kuhusu presumption, hatujaomba mahakamani presume kuhusu kukutwa na diary. Mheshimiwa Jaji niende kwenye hii kesi ya wenzetu ya Uganda vs Okumu Regan and Others. Kama kuna kesi itakuisaidia basi kesi hii. Nakupeleka ukurasa wa tano. Sisi tumesema kwamba shahidi ni incompetent.
(Kibatala anausoma huo ukurasa hadi anaumaliza)
KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, kesi yenyewe inahusu masuala ya uhujumu uchumi na ugaidi, washitakiwa wanayo haki ya kuona ushahidi unaokuja ni msafi na siyo wakutengeneza kama ulivyotangazwa na siyo kuja Mahakamani na kumwona shahidi anasoma ushahidi anaso,a ushahidi kwenye diary. Kama unaona kuna ugumu wa kufanya uamuzi kwenye kesi hii naomba itumie kesi ya UGANDA Vs OKUMU REGAN AND OTHERS. Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.
Kibatala anakaa chini.
JAJI: Tumefikia mwisho wa hoja? Kama mnavyoona mmetumia Siku nzima. Inamaanisha na mimi nitatumia siku nzima kuandika. Kwa namna ambavyo hoja zimewasilishwa tufanye kesho saa tano asubuhi. Sawa?
(Mawakili wote wanasema SAWA)
JAJI: Basi Kesho tarehe 16 saa 5 asubuhi kesi itakuja kwa maamuzi madogo. Mjiandae kwa yote. Shahidi namba mbili naomba uwepo ili uamuzi ukiwa utaendelea kuwepo basi tutaendelea.
JAJI: Kesi mpaka kesho saa 5 asubuhi.
Jaji anaondoka mahakamani.