Kama ilivyowasilishwa na ripota raia, BJ leo tarehe 05 Novemba 2021.
Jaji ameingia Mahakamani
Kesi namba 16 ya Mwaka 2020 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe, imeshatajwa.
Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha jopo lake
2.Abdallah Chavula
3.Jenitreza Kitali
4.Pius Hilla
5.Nassoro Katuga
6.Esther Martin
7.Tulimanywa Majige
8.Ignasi Mwinuka
Wakili Peter Kibatala anatambulisha jopo la mawakili wa Utetezi
2.Jeremiah Mtobesya
3.John Malya
4.Fredrick Kihwelo
6.Idd Msawanga
7.Hadija Aron
8.Evaresta Kisanga
9.Maria Mushi
10.Nashon Nkungu
Kibatala anakaa
Jaji anaita washitakiwa kwa namba 1, 2, 3 na 4
Wote wanaitika wapo na kunyanyuka
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji, shauri linakuja kwa ajili ya kusikilizwa na leo tuna shahidi mmoja. Tupo tayari kuendelea.
Jaji anaandika na kuhoji, “upande wa utetezi?”
Wakili Peter Kibatala: Na sisi pia kwa ruhusa yako tupo tayari kuendelea.
Wakili wa Serikali: anaenda nje kumuita shahidi.
Jaji: atakuwa shahidi wa saba Siyo?
Wakili wa Serikali: Ndiyo
Tunamuona Inspector Mahita karejea
Jaji: Majina yako
Shahidi: Inspector Mahita Mohamed
Jaji: Umri
Shahidi: 36
Jaji: Kabila
Shahidi: Mluguru
Jaji: Kazi
Shahidi: Askari Polisi
Jaji: Dini
Shahidi: muislam
Shahidi: Wallah wabillah watallah, Nathibitisha Kutoa Ushahidi Wa Kweli
Wakili wa Serikali: Ataongozwa na Wakili Pius Hilla
Wakili wa Serikali: Mahita Wewe ni Mkazi wa wapi
Shahidi: Mkazi wa Morogoro
Wakili wa Serikali: Tangu lini
Shahidi: Mwezi 04 Mwaka 2021
Wakili wa Serikali: Kabla Mwezi wa Nne ulikuwa Ukiishi wapi
Shahidi: Arusha
Wakili wa Serikali: Kazi yako ni Ipi
Shahidi: Polisi
Wakili wa Serikali: Tangu lini
Shahidi: Mwezi wa 03 2011
Wakili wa Serikali: Upo Kitengo gani
Shahidi: Idara ya Polisi Upelelezi wa Jinai
Wakili wa Serikali: Kwa Muda gani
Shahidi: Kwa Miaka 08
Wakili wa Serikali: Arusha Ulikwenda Lini
Shahidi: Tangu Mwaka 2014
Wakili wa Serikali: Mwaka 2020 ulikuwa kituo gani
Shahidi: Central Police Arusha
Wakili wa Serikali: Ulikuwa na nafasi gani
Shahidi: Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Arusha
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama ukiwa Kama Afisa wa Polisi Majukumu Yako yalikuwa ni yapi
Shahidi: Ukamataji wa wahalifu, Upekuzi wa tuhumiwa na Maeneo, Kusafirisha Watuhumiwa
Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini
Shahidi: Kuwatoa Watuhumiwa kuwatoa na kuwapeleka Sehemu Nyingine
Wakili wa Serikali: Kingine
Shahidi: Kuzuia na Kupambama na Uhalifu
Wakili wa Serikali: Kingine
Shahidi: Uandishi Wa Maelezo, ya Mashahidi na Watuhumiwa pamoja na Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kusimamia Askari waliopo Chini yangu
Wakili wa Serikali: Tarehe 04 August 2020 nini Kilotokea
Shahidi: Nikiwa Ofisini Arusha Nilipogiwa Simu na Afande Wangu ACP Ramadhan Kingai, aliniita Ofisini kwake Aliniagiza Kutafuta Askari Wawili Ambapo niliwatafuta Detective Francis na koplo Goodluck Tulienda Ofisi ya Afande RCO akatuambia tunatoka Kwa ajili ya Safari ya kazi
Kuna kazi ya kwenda Kufanya
Wakili wa Serikali: Ilikuwa Majira ya Saa ngapi
Shahidi: Saa 11
Wakili wa Serikali: Kingai alisema mnapenda Kufanya kazi wapi
Shahidi: Tunaenda Kufanya kazi Moshi
Wakili wa Serikali: Ukiwa pale sasa na Goodluck pamoja na Francis kitu gani kilifuata
Shahidi: Tulijiandaa na Safari pamoja na Askari Mwingine anayetokea Ofisini Kwake ASP Jumanne alikuwa na Yeye anatusubiria pale tujiunge naye kwa Pamoja twende Moshi Alikuwa anatusubiria Arumeru
Wakili wa Serikali: Baada ya Kufika Arumeru Mlielekea Wapi
Shahidi: Tukiingiza Ofisi ya Polisi OC CID Arumeru, Mimi Afande Kingai, ASP Jumanne, PC GOODLUCK na PC Francis ili Kupata Briefing Ya kazi tunayo kwenda Kufanya
Shahidi: Tukiingiza Ofisi ya Polisi OC CID Arumeru, Mimi Afande Kingai, ASP Jumanne, PC GOODLUCK na PC Francis ili Kupata Briefing Ya kazi tunayo kwenda Kufanya
Wakili wa Serikali: Nani aliye fanya Briefing Siku hiyo
Shahidi: Afande Kingai ambaye ndiye alikuwa Kiongozi wetu wa Msafara
Wakili wa Serikali: Kwenye Briefing Mlielezwa Mambo gani
Shahidi: Afande Kingai alituambia Kuwa amepewa Maelekezo ya Kuunda Kikosi Maalum, na Kikosi Hilo Ndiyo MIMI, ASP Jumanne, Goodluck, Francis, na PC Aziz Kwamba Kuna Kikundi Cha Watu kinataka Kufanya Vitendo Vya kigaidi
Wakili wa Serikali: Vitendo gani hivyo Shahidi: Kuwa Kikundi hicho kinataka Kufanya Vitendo Vya Kigaidi Mikoa Mbalimbali ikiwemo Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya Uhalifu walipokuwa wanataka Kufanya ni KUCHOMA Vituo Vya Mafuta, Kuzuia Barabara, Kukata Miti, kuwadhuru Viongozi Wa Serikali Ikiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Hai, Ole Lengai Sabaya Maandamano ambayo haya Ukomo, na Pia alitueleza Washirika ambao wanataka Kufanya Matukio hayo
Wakili wa Serikali: Aliwataja akina nani
Shahidi: Afande Kingai alisema Mpango huo ulikuwa unaratibiwa na Mheshimiwa Freeman Mbowe
Shahidi: alisema Wahalifu Wengine wapo Moshi, Kwa hiyo tuwazuie Twende Mkoani Kilimanjaro Wilaya Ya Moshi Alisema Kuna watuhumiwa 4 ambao walikuwa Moshi
Wakili wa Serikali: Wakina nani
Shahidi: Walikuwa wanakamilisha Mpango wa kwenda Kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya
Wakili wa Serikali: Kingai alisema Madhumuni ya Mpango yote ni nini
Shahidi: Kuleta Taharuki, Ili Nchi is iweze Kutawalika Tunapoelekea Kwenye Uchaguzi Akasema tuzuie Matendo hayo, Ili Nchi eindelee Kuwa Salama
Wakili wa Serikali: Mengine
Shahidi: Hayo tu kwenye Briefing
Wakili wa Serikali: Baada ya Briefing?
Shahidi: Tukianza Safari Kuelekea Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro
Wakili wa Serikali: Ilikuwa Saa ngapi
Shahidi: Ilikuwa kwenye Saa Mbili Kuelekea Saa 03
Wakili wa Serikali: Mlipofikq Moshi Usiku huo kitu gani Kilifuata
Shahidi: Tuliendelea na Upelelezi wa watuhumiwa ilituweze Kuwakamata
Tulisubiri Taarifa Kutoka kwa Afande Kingai Lakini kwa Siku ile hatukupata kiru
Wakili wa Serikali: Mlifanya Ufutiliaji Kwa Muda gani Kuanzia Saa 6 Mpaka Saa 7 Afande akasema Tubreak tutaendelea Siku inayofuata
Wakili wa Serikali: Siku inayofuata ilikuwa Siku gani
Shahidi: Siku ya 05 Mwezi 08 Mwaka 2020
Shahidi: Ambapo tuliamka Saa 11 alfajiri, Afande akawa anacordinates, Ilipofika Saa 06 Afande alituita Wote,
Jaji: ukisema Afande ni Jumanne au Mtu gani
Shahidi: Afande Kingai Ambaye ndiyo Mkuu wa Msafara
Wakili wa Serikali: endelea Shahidi’ alipotuita alituambia Kuwa wale Watuhumiwa wameonekana Maeneo ya RAU Madukani
Wakili wa Serikali: Rau ya wapi Shahidi Moshi
Shahidi: Tulichofanya ni kupewa description ya Watuhumiwa Jinsi walivyo
Wakili wa Serikali: description ya nini
Shahidi: Muonekano wao
Wakili wa Serikali: Unakumbuka description Zao zilikuaje?
Shahidi: Mmoja alikuwa amevaa Jacket na Ndani Shati la kitenge, Wa pili alikuwa amevaa Shati na Wa tatu alikuwa amevaa Jezi
Wakili wa Serikali: Baada ya Kupata description Ilikuwaje
Shahidi: Kwenda Kujipanga kwa ajili ya ukamataji Detail ya kwanza alikuwa nayo Afande Kingai na Afande Jumanne Na Detail ya Pili nilikuwa nayo Mimi na Coplo Fransis
Wakili wa Serikali: Kwani hilo Eneo Likoje Mpaka Muwe na Details Mbili
Shahidi: Hilo Eneo lina Barabara ya Lami, Kushoto Kuna Flemu za Maduka
Wakili wa Serikali: Maduka Yametizama Upande Upi wa Barabara
Shahidi: Ukiwa unapelekea ni Kushoto na wale watu wa Madukani wanaangali Barabara
Wakili wa Serikali: Upande Mwingine
Shahidi: Kuna Kibanda ambapo Mbele yake a watuhumiwa ndiyo walipokwepo na Baada ya kuwaona wakina Afande kingai Wakaanza Kusimama Kuelekea Upande wangu
Shahidi: Mimi nikawasimamisha
Wakili wa Serikali: Hicho Kibanda cha Namna gani
Shahidi: Kama Cha Wazi tuh, Mtu akipita anawaona Ni kama Ki shelter alafu Pembeni yake kuna Ki Glocery
Wakili wa Serikali: Karibu palikuwa na nini
Shahidi: Pana Kiuwazi, MAma Mmoja alikuwa anapika
Wakili wa Serikali: Watu walipokuwa wamekaa kwenye Kibanda unasema walinyanyuka
Shahidi: Kwa Mujibu wa Taarifa tuliambiwa wapo Watatu lakini walipokuwa wanakuja wapo Watatu Nikawa simamisha Nikamwambia Wanyooshe. Mikono Juu, nikawaeleza Mimi Inspector Mahita natokea Arusha
Wakili wa Serikali: Ukiwaeleza Nini
Shahidi: SIMAMA, KAA CHINI
Wakili wa Serikali: Wakafanyeje
Shahidi: Walisrespond
Wakili wa Serikali: Sasa Baada ya Kuwa simamisha ukafanyeje
Shahidi: Nilijitambulisha Nikawaambi wanatuhumiwa Makosa ya Kutaka Kutenda Vitendo Vya Kigaidi
Baada ya Muda afande Kingai akafika Lakini baada ya Kutumia Sauti Kali ikazua Taharuki ikabidi Watu waaanze Kusogea
Wakili wa Serikali: Alifika afande Kingai na nani
Shahidi: Afande Kingai na Afande Jumanne Afande Kingai kamuamuru afande Jumanne kuwapeleka wale Watuhumiwa
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Baada ya Jumanne Kupewa Maelekezo, Jumanne alifanya nini
Shahidi: Kwanza aliwaita Mashahidi huru wawili walikuwa wanashuhudia
Wakili wa Serikali: Walikuja hao Mashahidi wa Namna gani
Shahidi: Wanawake
Wakili wa Serikali: Baada ya Mashahidi huru Kufika Kitu gani Kilifanyika
Shahidi: alijitambulisha kwa washtakiwa, akatoa Vitu vyake mfukoni, akaanza Upekuzi
Wakili wa Serikali: Alianza Upekuzi Kwa Mtu yupi
Shahidi: Alianza kwa Mtu anaye Itwa Adam Kasekwa
Wakili wa Serikali: Ulifahamu Adam Kasekwa Muda gani
Shahidi: Wakati Afande Jumanne anajitambulisha na wao walijitambulisha
Wakili wa Serikali: Matokeo ya Upekuzi yalikuwaje
Shahidi: afande Jumanne alitoa Pistol Upande wa Kushoto wa Mtuhumiwa
Wakili wa Serikali: Upande wa Kitu gani Shahidi Wa Suruali
Wakili wa Serikali: Ulitambua Vipi wewe Kwamba ni Pistol
Shahidi: kwa Mwonekano wake na ilikuwa na namba ya A5340
Wakili wa Serikali: Tofauti na Pistol Kitu gani Kingine Kilionekana
Shahidi: Ndani ya Hiyo post palikuwa na Magazine yenye Risasi 3, Ilikuwa aina ya Luger
Wakili wa Serikali: Tofauti na Pistol na Risasi zake, Je kitu gani Kingine
Shahidi: alikutwa na Unga unaosadikiwa kuwa ni Madawa ya Kulevya
Shahidi: Alikutwa pia na simu, Na Line za Simu, Airtel na Hallotel,
Wakili wa Serikali: baada ya Upekuzi ASP JUMANNE alifanya Kitu gani,
Shahidi: alijaza Hati ya Upekuzi
Wakili wa Serikali: Zilikuwa Hati ngapi
Shahidi: Zilikuwa Mbili
Wakili wa Serikali: baada ya hapo walifanya nini
Shahidi: Mtuhumiwa aliweka Sahihi na baada ya pale Akaendelea na Upekuzi wa Mtuhumiwa wa pili
Wakili wa Serikali: ambaye anaitwa nani Shahidi Mohamed Ling’wenya
Wakili wa Serikali: na Yeye alikutwa na nini
Shahidi: alikutwa na Simu, na Kete za Unga zinazosadikiwa kuwa ni Madawa ya Kulevya 25
Wakili wa Serikali: Madawa yalipatikana eneo gani
Shahidi: Kwenye Mfuko wa suruali
Wakili wa Serikali: baada ya hapo nini Kilifanyika
Shahidi: Afande Jumanne alijaza Hati mbili
Wakili wa Serikali: Baada ya Kujaza hizo Hati Mbili nini Kilifanyika
Shahidi: Mtuhumiwa aliweka Saini yake na wale Mashahidi huru
Afande Jumanne akampatia afande Goodluck Vielelezo, Afande kingai akaita Gari Nyingine
Wakili wa Serikali: Aliita kutoka wapi
Shahidi: Kwa Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro Kwa kuwa tulishakuwa wengi wale Mashahidi huru wakapanda Gari Nyingine
Wakili wa Serikali: Tueleze hapa Mahakamani
Uliowakamata wapo hapa?
Shahidi: Ndiyo wapo hapa Mahakamani
Wakili wa Serikali: Elezea Wapo wapi
Shahidi: Upande wa Pili
Wakili wa Serikali: Wamevaaje vaaje
Shahidi: Mohamed Ling’wenya ni yule aliye Vaa Shati na Adam Kasekwa ni yule Mwenye Tshirt yenye mistari Mistari
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Kwamba Kwemye Gari walipokuwa Watuhumiwa kuelekea Central Moshi Mlikuwa kwenye Gana akina nani
Shahidi: Afande Kingai, ASP Jumanne, Mimi na Watuhumiwa na Goodluck
Francis yeye alikuwa na wale Mashahidi
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kilifuata Mlipokuwa Njiani
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kilifuata Mlipokuwa Njiani
Shahidi: afande kingai aliwaambia Kwa Taarifa zake walikuwa watatu, akawa uliza yule Mwingine Yupo wapi
Wenyewe kwa Ushirikiano Kabisa wakasema Kuwa kweli walikuwa watatu
Wakili wa Serikali: Walikuwa na nani
Shahidi: Moses Lijenje
Wakili wa Serikali: Ambapo walisema yupo wapi
Shahidi: Kwa Maelezo yao walituambia wamemuacha pale Rau Madukani
Wakili wa Serikali: baada ya Kuelezea hivyo kitu gani kiliendelea
Shahidi: kwakuwa tulikuwa tumekaribia kufika Kituoni, tukiingia Kituoni Afande Kingai akatoa Maelekezo Francis aendelee Kuchukua Maelezo
Wakili wa Serikali: Kitu gani Kikafuata
Shahidi: Tukarudi na Watuhumiwa Mpaka Rau Madukani Lakini hatukupata, Watu wakawa wanasema Kapita hapa Kapita tuh
Tukarudi kwa Washitakiwa Wetu wakasema Basi watatu onyesha Maeneo anayopenda Kwenda
Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni sehemu gani
Shahidi: Naweza Kusema Ilikuwa ni Vibanda Umiza tuh pale Moshi Mjini
Wakili wa Serikali: Baada ya Pale Moshi Mjini, Kwanini Mlifika Mpaka Aishi Hotel
Shahidi: Kwa sababu walituambia wenyewe anaweza Kuwa ameelekea Kule
Wakili wa Serikali: Ufutailiaji huo wa Moses Lijenje Uliendelea Mpaka Lini au saa ngapi
Shahidi: Tuliendelea Mpaka Boma Majira ya Sa 4 au Saa 5
Wakili wa Serikali: Saa 4 au 5 ya Majira gani
Shahidi: Usiku
Wakili wa Serikali: Baada ya Kufika Boma
Shahidi: Tuliendelea Kumtafuta pale Boma, tukala nao Chakula. Afande Kingai akasema turudi kuwarudisha Lock up Watuhumiwa
Wakili wa Serikali: Lock Up wapi
Shahidi: Kituo cha Moshi
Shahidi: Kesho yake Majira saa 11 tuliamka na Kwenda kuwa chukua watuhumiwa pale Moshi Upelelezi Uliendelea Wa Kumtafuta Moses Lijenje Kama atakuwa amepanda Basi Kuelekea Sehemu Nyingine
Wakili wa Serikali: Matokea ya Upelelezi wenu Siku hiyo sa Tarehe 06 -08 -2020
Shahidi: Hatukumpata, ikabidi turudi tena Kwenye Vile Vijiwe Vya tarehe 05 Lakini wakati tunazunguka, Adam Kasekwa alisema Moses Lijenje NaDada Yake Sakina Arusha Safari Ikaanza Upya Kuelekea Huko Arusha
Wakili wa Serikali: Kitu gani kilitokea Huko Arusha
Shahidi: Tulifika Arusha lakininhawakuweza Kutambua Nyumba ya Dada yake Moses Lijenje Tukawarudisha Moshi Na Kisha Afande Kingai akasema tuwatoe Watuhumiwa tuwarudishe Moshi
Wakili wa Serikali: Safari ailianza Muda gani
Shahidi: Kuelekea Moshi Ilianza Saa 2 Jioni
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Baada ya Kutoka Moshi na Safari ya Kuja Dar Kitu gani Kilifuata
Shahidi: Tulilofila Njia panda Ya Himo Gari yetu ilipata Pacha, afande Kingai Ikabidi Aombe Gari Nyingine Tukiwa tunasubiria Gari tulipata Nguvu Tumbo (Refreshments) au Chakula
Baada ya Gari Kufika tuliendelea na Safari
Wakili wa Serikali: Kwenye Safari mlikuwa na akina nani Shahidi: Mimi, Afande Kingai, ASP Jumanne, PC GOODLUCK na wale Watuhumiwa
Wawili wa Serikali: watuhumiwa gani
Shahidi: Mohamed Ling’wenya na Adam Kasekwa
Wakili wa Serikali: Tangu tarehe 05 Mpaka tarehe 06 walikuwa Kwenye Uangalizi wa nani
Wakili wa Serikali: Walikuwa na Hali gani
Shahidi: Hali Nzuri
Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini Kusema Hali Nzuri
Shahidi: Walikuwa na Afya Nzuri
Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Dar es Salaam Mlifika lini
Shahidi: Tulifika Siku ya Tarehe 07 Majira ya Saa 11 kuelekea Saa 12 Asubuhi
Wakili wa Serikali: Mlipofika Dar es Mlielekea wapi
Shahidi: Tulifika Central Police Dar es Salaam Baada ya Kufika Central Police Dar es Salaam Tukiwakabidhi pale CRO ili wawaingize Lockup
Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa weka Luck up nini Kikifuata
Shahidi: afande Kingai alitoa Malekezo Kwamba tuka awe Uso alafu turudi
Wakili wa Serikali: Mlirejea Saa ngapo
Shahidi: Saa 1 Asubuhi
Wakili wa Serikali: Mlipewa Malekezo Gani sasa
Shahidi: Afande alituambia tujiunge na Assistant Inspector Swila tuendelee Na Ufutailiaji wa Mtuhumiwa Mwingine anayeitwa Bwire
Wakili wa Serikali: ambaye alikuwa wapi
Shahidi: Alikuwa Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Mlikuwa na akina nani
SHAHIDI: Mimi, PC GOODLUCK, Assistant Inspector Swila
Wakili wa Serikali: Mliendelea na nini
Shahidi: Tuliendelea na Upelelezi, Hatua za Upelelezi mbalimbali Kutafuta ma Informer
Wakili wa Serikali: Nini Kikatokea
Shahidi: Siku hiyo Hatukufanikiwa
Shahidi: Siku inayofuata ya tarehe 08 Afande Kingai akatoa Maelekezo Kwamba Tuwatoe Watuhumiwa pale Central tuwapeleke Kituo Cha Mbweni
Wakili wa Serikali: ulitekeleza Vipi hayo Maelezo
Wakili wa Serikali: Maelezo yapi Mengine Ulipewa
Shahidi: Afande Kingai akasema Kutokana na Mafunzo watuhumiwa walivyo nayo, Tuwapeleke Mbweni ilikila Mtuhumiwa akae Chumba Chake cha Mahabusu Wakili wa Serikali Unakumbuka zoezi la Kuwatoa Central Lilikuwa Kwenye Majira ya Saa 4
Shahidi: Nilienda Kuwatoa Mahabusu Watuhumiwa na Nikiwa na Afande Jumanne nikawapeleka Kituo cha Mbweni
Wakili wa Serikali: Maelezo yapi Mengine Ulipewa
Shahidi: Afande Kingai akasema Kutokana na Mafunzo watuhumiwa walivyo nayo, Tuwapeleke Mbweni ilikila Mtuhumiwa akae Chumba Chake cha Mahabusu
Wakili wa Serikali: Unakumbuka zoezi la Kuwatoa Central Lilikuwa Kwenye Majira ya Saa 4
Wakili wa Serikali: Tarehe 09 Mwezi wa 08 2020 nini kilitokea
Shahidi: Taarifa za Bwire tulizokuwa tumezipata kwamba Mtuhumiwa alikuwa anatokea Buguruni kwenda Maeneo ya Chang’ombe tukaweka Mtego
Wakili wa Serikali: Mtego gani huo
Shahidi: Tukiweka Askari Track wa Usalama Barabarani akalisimamisha Basi aina ya Costa ambayo Mtuhumiwa alikuwa amepanda Afande Kingai Aliniambia nipande Kumuangala Ndani Nikamkuta kakaa zile Siti za Kati
Wakili wa Serikali: Baada ya Kumuona Shahidi Nikajitambulisha Kwamba naitwa Inspector Mahita na Kwamba natokea Arusha na Kwamba anashitakiwa kwa Makosa ya Kutaka Kutenda Ugaidi Afande: Kingai na Yeye akajitambulisha akamuonya na baadae akawekwa Mahabusu ya pale pale Chang’ombe
Wakili wa Serikali: Ilikuwa Majira ya Saa ngapi
Shahidi: Saa 4 Usiku
Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Kwamba Baada ya Tarehe 09 ulishughulika namna gani na watuhumiwa
Shahidi: Tuliendelea Kuwatafuta Watuhumiwa na Kufanya Upelelezi akwa kwenda sehemu Mbalimbali
Wakili wa Serikali: Kama zipi
Shahidi: Mwanza na Tabora
Wakili wa Serikali: Unasema Ulishiriki Kumkamata Bwire, je yupo hapa Mahakamani
Shahidi: Ndiyo amevaa kanzu na Barakha Sheikh
Wakili wa Serikali: Mliwakamata watuhumiwa wote kwa tuhuma zipi
Shahidi: Kwa kula Njama za Kutenda Matendo Ya Ugaidi
Wakili wa Serikali: Umeshiriki Kumkamata watu watatu
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Mbowe yeye amekamatawa lini
Shahidi: Mwaka huu
Wakili wa Serikali: Kwanini yeye Kipindi hicho hakukamatwa
Shahidi: Afande Kingai alisema Mpaka Uchunguzi Ukikamilika
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji hatuna Swali lingine
Mtobesya ananyanyuka anaweka Joho Vizuri na Kumfuata Shahidi
Mtobesya: Afande Kingai alikwambia Siku ya Kwanza Kwamba Kuna watu wamepanga Kufanya Matendo ya Ugaidi
Shahidi: Ndiyo
Mtobesya: alikuwa anakwambia here say Kutoka kwa nani
Shahidi: alikuwa anaambiwa na Msiri wake
Mtobesya: Kwa hiyo Kingai ni Mtu wa Ngapi Kupokea Taarifa
Shahidi: Wa kwanza Kwa Uelewa wangu
Mtobesya: Mliweza Ku verify Source
Shahidi: Siyo Jukumu langu
Mtobesya: Nilisikia Unasema Kingai Aliwapa description Ya Mavazi
Shahidi: Ndiyo
Mtobesya: Mweleze Jaji Rau ina ukubwa gani na Ipo busy vipi
Shahidi: Ni Center ambayo ipo busy
Mtobesya: Nitakuwa Sahihi Nikisema Kuna Mwingiliano Wa watu wengi
Shahidi: Ndiyo sahihi
Mtobesya: Kwamba pale Rau Madukani pasingeweza kuwa na Mtu Mwingine Mwenye Shati Jekundu?
Shahidi: Nilisha Jiridhisha Kama Ulinisikikiza Vizuri, Ndiyo Maana tunafanya Surveillance
Mtobesya: Kwa hiyo kwa huo Ushahidi Wako kwa Siku ile Rau Madukani hapakuwa na Mtu Mwingine aliye Vaa Shati Jekundu
Shahidi: Ndiyo Kwa Siku hiyo
Mtobesya: Detail Mliyoenda nayo Moshi Mlikuwa watu wangapi
Shahidi: Sita
Mtobesya: Na Watu hao Sita Ndiyo Mlioshughulika kukamata
Shahidi: Ndiyo
Mtobesya: Kwa hiyo akitokea Mtu akisema mlikuwa watano kwenye ukamataji atakuwa sahihi au siyo Sahihi
Shahidi: Wakati Wa Ukamataji tulikuwa Wawili watatu wakaja baadae
Mtobesya: Unarukaruka swali, Nauliza Nyie Ambao Mlitoka Moshi Kwamba akitokea Mtu akisema Mlikuwa watano na siyo Sita atakuwa hayupo sahihi
Shahidi: itakuwa Hayupo Sahihi
Mtobesya: Baada ya upekuzi Jumanne alimkabidhi nani vielelezo?
Shahidi: PC GOODLUCK
Mtobesya: Unaifahamu fomu ya polisi inaitwa Fomu namba 45
Shahidi: Sifahamu
Mtobesya: Je, unafahamu kwamba hiyo fomu ndiyo anahitajika kujaza vielelezo anapotoa vielelezo sehemu ya tukio?
Shahidi: Ndiyo
Mtobesya: na unafahamu anayetokea vielelezo anatakiwa kujaza fomu+
Shahidi: Ndiyo
Mtobesya: Wewe Unasemaa umeona Jumanne Akimkabidhi Goodluck vielelezo, Je uliona wakijaza hiyo fomu
Shahidi: Ndiyo niliona
Mtobesya: hiyo fomu ya 145
Shahidi: Kimya
Mtobesya: na Unakumbuka ulichokiandika au Unahitaji Ku’ refresh Memory
Shahidi: Hapana nakumbuka
Mtobesya: Kwenye Maelezo yako uliyoandika Polisi Hakuna Sehemu ambayo umeandika Afande Jumanne alijitambulisha kabla ya Upekuzi
Shahidi: Ndiyo Hayapo
Mtobesya: Kwenye Maelezo yako wewe Ndiye Uliyemkamata Bwire hayo Maneno hayapo, Ni sahihi
Shahidi: Sahihi hayapo
Mtobesya: Kwenye Maelezo yako umeandika zile Kete kuwa ni Heroine, kwanini ulidhani ni Heroine na siyo Cocaine
Shahidi: Kwa uzoefu wa Kazi yangu Heroine Ina Mfano wake na Cocaine Kwa Mfano wake
Mtobesya: Kwa hiyo zikiwa in Powder form unaweza Kufanya Utambuzi, Mwambie Mheshimiwa Jaji
Shahidi: Unaweza Kufahamu zikiwa in Powder Form
Mtobesya: Umesema kwamba mlizurura na Watuhumiwa sehemu mbalimbali Moshi, Je unafahamu Kwamba Kuna Kielelezo Hapa Mahakamani Kwamba 24 July 2020 walienda Moshi halafu tarehe 31 July 2020 waliondoka Moshi Kuja Dar es Salaam
Shahidi: Hapana Sifahamu
Jaji anaomba atajiwe tena hizo tarehe
Mtobesya: Nikuulize sasa Swali la Mwisho, Wakati Mnamkamata huyu uliyemuita Bwire Ilikuwa Majira ya Saa ngapi
Shahidi: Saa 2 Usiku
Mtobesya: Wewe Uliacha Kuonana naye lini
Shahidi: Kwa Siku ile Hapana
Mtobesya: Kwa hiyo huwezi kuisaidia Mahakama Kwamba aliandika Maelezo au hakuandika
Shahidi: Wakati anaandika Maelezo Sikuwepo
Mtobesya: Je Upekuzi
Shahidi: Upekuzi wa Nini
Mtobesya: wa yeye Mwenyewe na alipokuwepo
Shahidi: Sikuwepo
Mtobesya: naomba Kuishia Hapo
Anasimama Wakili John Mallya
Mallya: Umewahi Pia kutoa Ushahidi Mahakamani Kwenye kesi zingine
Shahidi: Sahihi
Mallya: Ni sahihi Unapokuwa Shahidi Kama wewe, Kama arresting person Mnakuwa mnaandika Maelezo Kwa Kingereza baada ya kuwakamata Watuhumiwa
Shahidi: Ndiyo yakihitajika tunaandika
Mallya: ulisema Mlienda Mpaka Mwanza Mpaka TABORA
Shahidi: Ndiyo
Mallya: kunaruhusiwa Kuweka Maelezo ya Nyongeza
Shahidi: Additional Statement Inaruhusiwa
Mallya: Mwambie Jaji Kwa Mazingira yapi
Shahidi: Kama ikitokea kuna Maelezo umesahau
Mallya: Maelezo Ya Nyongeza yanasomeka Pamoja au Tofauti
Shahidi: Yanasomeka Pamoja
Mallya: Mtobesya alikuuliza Unakumbuka Uliandika Maelezo
Shahidi: Ndiyo nakumbuka
Mallya: Uliandika Mwezi gani
Shahidi: Tarehe 09 Mwezi 10 2020
Mallya: Sasa sisi tuna Maelezo yako Hapa Kwamba uliandika Maelezo Mwezi 08
Mallya: Tushike lipi
Shahidi: Mwezi wa 10
Mallya: Ulikuwa Lini TABORA
Shahidi: Mwezi 10
Mallya: Sasa Hapa Kuna shahidi kaja anaitwa Kaaya anasema Tarehe hizo Ulikuwa Arusha na siyo TABORA
Shahidi: Ndiyo niliitwa Kuchukua Maelezo
Mallya: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa huyo Kaaya wakati Unamkamata na Kumchukua Maelezo alikuwa anatuhumiwa kwa Makosa gani
Shahidi: Alikutwa na Noti bandia
Mallya: Kuhusu Ugaidi
Shahidi: Hakushtakiwa na Ugaidi
Mallya: Una uhakika
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Je Kaaya alishawahi kushtakiwa kwa Kesi ya ugaidi
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Je Kaaya anahusika na Kesi hii au hausiki
Shahidi: hahusiki
Mallya: Alikuja hapa kama Shahidi
Shahidi: Ndiyo anahusika
Mallya: Ulishawahi kuwakamata Magaidi wa Arusha
Shahidi: siwezi kuongelea Hapa
Mallya: naomba Mheshimiwa Jaji anijibu
Jaji: JIBU SWALI
Shahidi: Ndiyo nilishawahi Kuwakamata
Mallya: Sasa eleza Wakati Unawakamata Ulishawahi Kuonyeshwa na Gaidi gani Mwenzao
Shahidi: Sikumbuki
Mallya: Sasa Umesema hapa Kwamba Ulimkamata Bwire
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Ulimjuaje
Shahidi: Palikuwa na Informer Ndani
Mallya: ulisema Ulifanya Uhakiki kabla ya Kuwakamata, Je ulitoa description Kwamba walikuwa wanafanya Kitu gani
Shahidi: Sikueleza
Mallya: wakati unasema Umeona Cocaine Ulisema Rangi
Shahidi: Hapana
Mallya: Wakati Unasema Cocaine Ulisema ya Uzito gani
Shahidi: Hapana
Mallya: ulishuhudia Upekuzi Kwa Maelezo yako, Vitu Vyao kama Vitambulisho na Pesa vilikwenda wapi
Shahidi: Walikuwa hawana
Mallya: Wa Kwanza Ulifahamu Baada ya Jumanne Kujitambulisha kwake
Shahidi: Sahihi Kabisa
Mallya: na Hati za Uchukuaji Mali zilijazwa eneo la Tukio
Shahidi: Sahihi Kabisa
Mallya: Naomba Kielelezo Mheshimiwa Jaji
Mallya: we Umemtambua Adam Hassan Kasekwa, Je Soma Hati ya Kuchukua Mali imeandikwaje
Shahidi: Adam Hassan Kasekwa AKA Adamoo
Mallya: Umesema Sababu ya kuwahamisha ni Security yao
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Je Central Kuna Polisi Wangapi
Shahidi: Sifahamu
Mallya: hufahamu kwa sababu hujawahi kufanya kazi central?
Shahidi: Nishafanya kazi central..
Mallya: sasa elezea Central Dar es Salaam
Shahidi: Sijawahi kufanya kazi
Mallya: pale Central Mlikuta Polisi Wangapi
Shahidi: Mapokezi Kama wanne na Walinzi Nje
Mallya: Na Mbweni Mlikuwa wa ngapi Mapokezi
Shahidi: Kama wawili
Mallya: Kwa hiyo Mnawatoa Watuhumiwa Kwemye polisi Wengi ila wewe na Jumanne na Watu wawili tuh Mnawabeba Makomandoo
Shahidi: Tulikuwa tumewafunga Pingu
Mallya: Kwamba Ulinzi wa kituo ni kazi yako au Mkuu wa kituo
Shahidi: Mkuu wa Kituo ila Watakuwa waliwasiliana na Afande Kingai
Mallya: Wakati wakili wa Serikali anakuongoza Ulisema hayo
Shahidi: Hapana
Mallya: Wewe Ndiyo Mahita aliyekuja hapa kutoa Ushahidi Kwenye kesi Ndogo?
Shahidi: Ndiyo mimi
Mallya: Ulisema Central ni Class A
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Kwa sababu anakaa RPC?
Shahidi: hapana
Mallya: Kwa sababu gani
Shahidi: Anakaa OCS na Mkuu wa Kituo na Idadi Kubwa ya Polisi
Mallya: Sasa hao OCS na Mkuu wa Kitu na hiyo Idadi wapo Mbweni
Shahidi: Hapana
Mallya: Ulielezea kwamba Madawa ya Kulevya mliyoyapata Kwa Adam Kasekwa Uliyatoa Upande Gani
Shahidi: Hapana
Mallya: Ulieleza Kwamba Madawa Ya kulevya ya Mohammed Ling’wenya mmetoa Upande gani
Shahidi: Hapana
Mallya: Kukaa Chini na Kuchuchumaa ni Kitu Kimoja
Shahidi: Hapana
Mallya: Sasa Kuna Mtu mmoja kaja mahakamani kasema ulisema wachuchumae siyo wakae Chini
Shahidi: Nilichokisema ndiyo Nilichokisema
Mallya: atakuwa anaongea Uongo
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Mpaka tunapoongea Maelezo Ya Bwire yameshachukuliwa
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Ulisema Umeenda Kuwachukua watuhumiwa Central Ukawapeleka Mbweni, Je Ulieleza Kwamba Ulifanya Nini baada ya Kufika pale mbweni
Shahidi: Sikueleza
Mallya: Ulieleza wakati Wa Upekuzi namna walivyo Hesabu hizo Kete
Shahidi: Sikueleza
Mallya: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu
Wakili Fredrick anasimama
Fredrick: Ulisema Baada ya ukamataji wa Khalfani Bwire Mlikuwa mnasubiri Maelekezo ya Viongozi
Shahidi: Sahihi
Fredrick: na baada ya hapo Mkaelekea Mwanza SHAHIDI: Ndiyo Fredrick: Mkumbushe Mheshimiwa Jaji ulienda Mwanza Tarehe Ngapi Shahidi Sikumbuki
Fredrick: Ulisema moja ya tuhuma ni kuwa dhuru Viongozi akiwemo Sabaya, wengine wakina nani
Shahidi: Sabaya
Fredrick: Wengine wakina nani?
Shahidi: Sabaya…
Fredrick: Sabaya ushamtaja hao wengine ni wapi?
Shahidi: nimemtaja Sabaya
Fredrick: Ulizungumza Kuhusu Kurudi Moshi Kutoka Boma, Je Ulieleza Mfika Saa ngapi
Shahidi: Sikueleza
Fredrick: Ulipowafikisha Moshi mkaandikisha
Shahidi: Ndiyo
Fredrick: Hiyo Register hapa Mahakamani Ipo au Haipo
Shahidi: Siyo Kazi yangu Kuitunza
Fredrick: Umezungumzia Kuhusu Afya za watuhumiwa, Kwamba walikuwa Vizuri
Shahidi: Ndiyo
Fredrick: ulijuaje
Shahidi: Kwa kuwaangalia na Majibu yao
Fredrick: Asante Mheshimiwa Jaji
Wakili Kibatala anasimama
Kibatala: Mahita mambo Vipi!?
Shahidi: Poa
Kibatala: Una elimu gani
Shahidi: Digrii
Kibatala: Ya Nini
Shahidi: Ya Sheria
Kibatala: ooohhh kwa hiyo naongea na learned brother
Shahidi: Wewe ndiyo learned brother, maana Mimi nimesema sheria tu..
Kibatala: Kuna Sehemu yoyote Kwenye Dictionary Grocery inasema ni sehemu ya Kunywa Pombe
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: katika Ushahidi Wako umetaja Popote Kuhusu Bar au Kufananisha Grocery na Bar
Shahidi: Hapana
Kibatala: kwahiyo wewe Hukutaja Bar
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: umesema kuhusu Kibanda umiza
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: umemfafanulia Jaji Maana Ya Kibanda Umiza
Kibatala: Je unafahamu Kingai aliambiwa na DCI Boaz Kuwa ndiye aliyetoa Maelezo Kwamba Baada ya Watuhumiwa Kukamatwa waletwe Dar es Salaam
Shahidi: Alituambia tarehe 6
Kibatala: Twende kwenye description sasa, Ni sahihi katika statement Yako mliweka mtego kuwakamata watuhumiwa wawili
Shahidi: Katika statement sikusema hivyo
Kibatala: Statement Yako ya Tarehe 10.8.2020 tulifika Moshi, Tuliweka Mtego mbalimbali kwa ajili ya Kuwakamata Watuhumiwa lakini hatukuwakuta….. Huu Mstari upo au Haupo
Shahidi: Upo
Kibatala: Kingai hajawahi Kuwaambia Kuwa ana Informer wake mwanajeshi anaitwa Urio
Shahidi: hajawahi
Kibatala: Kingai alikuwa anakwambia Kwamba ana wasiri wake au Informer wake
Kibatala: Hakusema hivyo
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Kibatala: Ushahidi Wako wewe Hukusema Neno wasiri au Informers
Shahidi: Nimesema
Kibatala: aliwaambia ana Informer Wangapi
Shahidi: Hakutuambia
Kibatala: Pale Rau Madukani Personally Ulifanya Surveillance
Shahidi: Tulifanya Kibatala Wewe Personally Ulifanya au Hukufanya
Kibatala: Wewe Personally Ulifanya au Hukufanya
Shahidi: Nilifanya
Kibatala: na Ukawaona Watu wote watatu
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je Kuna sehemu umesema Kwamba Ulibreak au Ukawa Divated
Shahidi: Hapana
Shahidi: Hapana
Kibatala: Kuna sehemu Ambayo umemwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Uliwaona watatu lakini Ghafla ukawakuta wawili
Shahidi: Nilieleza
Kibatala: Na Katika Ushahidi Wako Ulisema Kwamba Kuna Kibanda Cha Mbege
Shahidi: Hapana
Kibatala: Unafahamu wa Kibanda Cha Mbege Katika Kesi hii
Shahidi: Mimi nafahamu Kuhusu Kumkamata watuhumiwa
Kibatala: Kwa hiyo ufahamu lolote Kuhusu Kibanda Cha Mbege
Shahidi: Mimi sikwenda kukamata Kibanda Cha Mbege, Siyo Priority
Kibatala: Ulizungumzia Kuhusu Kibanda Cha Tigo?
Shahidi: Sikuzungumzia Kibatala: Ni Kuuliza pia Umuhimu wa Kibanda Cha Tigo Pesa Utasema siyo Priority Yako
Shahidi: Ndiyo ilikuwa My Primary Objective
Kibatala: Ulipokuwa Unawakamata Ukitumia Maneno gani
Shahidi: NILIWAAMBIA WASIMAME NILIWAAMBIA WAKAE CHINI
Kibatala: ilikuwa kwa Sauti Kubwa
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ukajitambulishaje
Shahidi: MAHITA OMARY MAHITA
Kibatala: Umezungumzia wewe au afande Jumanne kwenda Kuwaita kwenye Biashara zao
Shahidi: Nilieleza
Kibatala: kwa hiyo walienda Kuitwa Kwenye Biashara zao au Walitoka kutoka Kwenye Watu walipokuwa wameshuhudia
Shahidi: Walikuwa among the Crowd
Kibatala: wewe Yote Uliyashuhudia
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: na wote walipekuliwa kwenye Maungo yao
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Zoezi lilishuhidiwa na Mashahidi, Mwanamke
Shahidi: Ndiyo nilivyosema
Kibatala: Katika Ule Umati Wanamume walikwepo au hawakwepo
Shahidi: walikuwepo
Kibatala: ukiwa na suspect wa kike anatakiwa apekuliwe na nani?
Shahidi: Mtu yoyote
Kibatala: Kwamba upekuzi wa mwanamke unaweza kushuhudiwa na mtu yoyote
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwa sheria ipi?
Shahidi: sikumbuki
Kibatala: Upande wa Kulia wa eneo la Tukio palikuwa na frame 4, Moja Ni Duka la Vipodozi na Duka Moja la Jumla
Shahidi: Upande wa Kulia kama palikuwa na M-pesa na TigoPesa…. Mimi sifahamu.. mimi nilikwenda kuwakamata
Kibatala: Unakubaliana na Mimi kama Kweli Mliwakamata Pale Watuhumiwa pana frame 4
Shahidi: frame zipo Upande wa Kushoto
Kibatala: Upande wa pili pana frame?
Shahidi: Kuna Barabara
Kibatala: Kumbukumbu zako Uliwahi Kutoa Ushahidi Kuhusu Juhudi Kufanyika Kumtafuta Kiongozi wa Mtaa
Shahidi: Juhudi zilikuwa kumtafuta Shahidi. Mashahidi tuliwapata
Kibatala: Ufahamu wako pale kuna Kiongozi wa mtaa au Hakuna
Shahidi: Kila Eneo lazima kuna Kiongozi Wa Mtaa
Kibatala: Hao Mashahidi wawili uliwahi Kuwafuatilia Kama ni Viongozi wa Mtaa
Shahidi: Kimya
Kibatala: Mpaka mnaanza Kupata Taarifa kwa Washtakiwa Wa Pili na Watatu, Si palikuwa na Maulizo ya Maswali
Shahidi: Sahihi kabisa
Kibatala: Unafahamu Unapoanza Kumuhoji Mshtakiwa Inakuwa ni sehemu ya Uchukuaji wa Maelezo
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Digrrii Yako ya Sheria umepata lini
Shahidi: 2009
Kibatala: unafahamu Mohammed Ling’wenya alikuwa hajaishi Moshi kwa zaidi ya wiki Moja
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Je kwa Uchunguzi wenu Lijenje au alitoroka baada ya kuwagundua na kuwaona
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Je wasiri wenu Walikwambia nini Juu ya kutoweka Kwa Lijenje
Shahidi: Mimi sifahamu
Kibatala: Hati ya mashtaka inasema hivyo Vitendo vilivyotakiwa kufanywa vinajumuisha MOROGORO, ARUSHA, DAR ES SALAAM na MWANZA… Je ulieleza Kama kuna Mpelelezi alifika Morogoro?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Je Katika ushahidi wako umeeleza kwenda mwanza Kwa kesi hii
Shahidi: Sikueleza
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji wewe Kama Msaidizi Wa RCO, Ulizungumzia Kuhusu Uwepo wa Njama za Kulipua Vituo Vya Mafuta Arusha… Kwa sisi wenyewe tuligundua kuhusu Arusha Kuna Mipango inaendelea
Shahidi: Ndiyo nimeongea
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama Arusha Kituo A na B kilitaka Kulipuliwa
Shahidi: Sijamwambia
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama ARUSHA Kuna Kiongozi A na B walitaka Kudhuriwa
Shahidi: Kimya
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kwa Mujibu wa Upelelezi watu tuligundua Maandamano haya yalipangwa Tarehe ngapi na Eneo la Kuanzia
Shahidi: Hapana Siku Mwambia
Kibatala: Unakumbuka Kuzungumzia Chochote Kuhusu Mkoa wa Mbeya
Shahidi: Nilitaja Mkoa wa MBEYA kuwa Upo Miomgoni Mwa eneo linalotakiwa Kufanywa tukio
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kati yenu Kuna Mpelelezi alienda Mbeya
Shahidi: Sijamwambia
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kuna Vituo Vya Mafuta MBEYA Vilitakiwa Kulipuliwa
Shahidi: Sijamwambia
Kibatala: Je, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kiongozi gani alipangwa Kudhuriwa
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Morogoro Vituo gani kwamba vinatakiwa Kulipuliwa
Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Maandamano yalitakiwa kufanyika Wapi Mkoa wa Morogoro
Shahidi: Si kumwambia
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Sabaya alitakiwa Kudhuliwa tarehe ngapi Mwezi Gani na Mwaka gani
Shahidi: Hapana Sikumwambia
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Vituo Vinavyotaka Kulipuliwa Kilimanjaro
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Mshitakiwa wa Kwanza alitakiwa anatakiwa kufanya katika Mipango hiyo ya Ugaidi
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je specific Role aliyotakiwa Kufanya ADAM Kasekwa Ulimwambia Mheshimiwa Jaji
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je Specific Role ya Mohammed Ling’wenya Kwamba alitakiwa Kufanya nini
Shahidi: Si kumwambia
Kibatala: Je Specific Role ya Freeman Mbowe katika Kutaka kutenda Ugaidi
Shahidi: Ndiyo nilimwambia
Kibatala: Ulimwambia Nini
Shahidi: Kwamba Ndiye aliyekuwa anaratibu
Kibatala: kuratibu ni suala pana, Nataka Kujua Kazi yake Katika huo Uratibu
Shahidi: Hapana Sijamwambia
Kibatala: Je unafahamu katika Maelezo yako Umemtaja ADAM HASSAN na Siyo ADAM HASSAN KASEKWA Maarufu Adamoo
Shahidi: Nimemtaja ADAM HASSAN ila nimemtambua
Kibatala: Je unafahamu Kwamba Mshitakiwa wetu hapa Mahakamani Anaitwa ADAM HASSAN KASEKWA Maarufu Kama Adamoo
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Hwa wote wawili ADAM HASSAN ndiyo ADAM HASSAN KASEKWA
Shahidi: Ndiyo Nimefanya Kwa Kumtambua
Kibatala: Unafahamu Kwamba Sabaya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya amehukumiwa na Mahakama kwa Makosa ya Ujambazi
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Je unafahamu Kwamba Sabaya Amehukumiwa Makosa ya Ujambazi Wakati wewe Ukiwa Afisa wa Polisi Arusha na ACP Kingai
Shahidi: Ndiyo natambua
Kibatala: Wewe Ulifanya Jukumu gani katika Kuzuia uhalifu Wa Sabaya
Shahidi: Siyo lazima Mimi lakini kuna wasaidizi waliopo Chini yangu walizipata
Kibatala: Na Unafahamu Kwamba Matendo Yake yalijirudia rudia
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji iwapo wewe na Afande Kingai Kama mlipata Taarifa za Intelijensia kuhusu Uhalifu wa Sabaya
Shahidi: Sikupata Taarifa
Kibatala: lakini unajua Mipango ya Uhalifu wa Wilaya ya Hai Nje ya eneo lako la kazi
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Kwanini tusiseme Kwamba Kesi hii ninyi na Sabaya Mlitengeneza Kesi Kwa ajili ya mambo ya Kisiasa
Shahidi: Siyo Kweli kabisa
Kibatala: Huyu ASP Jumanne Yupo wapi
Shahidi: Yupo Arumeru
Kibatala: Kwamba hufahamu kwamba Jumanne amesimamishwa kazi baada ya kumbambikia Mzee mstaafu kuwekewa meno ya tembo kwenye mzinga wake wa nyuki chini ya usimamizi wa ASP Jumanne ambaye ni shahidi wenu?
Shahidi: Sifahamu najua yupo kazini..
Kibatala: Muda huu tunapo ongea yupo Ofisini?
Shahidi: Sifahamu sababu siwasiliani naye siku nyingi
Kibatala: Unajua tukio lake la kusimamia kumuwekea Mzee wa watu meno ya tembo
Shahidi: Nafahamu
Kibatala: Je ulimfahamisha huyu aliyetaka kudhuriwa Sabaya
Shahidi: Sijamwambia
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Ukimfahamisha Kamati ya Ulinzi ya Wilaya Hai au Mkoa wa kilimanjaro
Shahidi: Hapana Siku Mwambia
Kibatala: katika Briefing zenu Je Kingai aliwambia kwamba kwamba ametoa Taarifa Kwa Kamati za Ulinzi na Usalama
Shahidi: Hakutuambia
Kibatala: Je katika Briefing Zenu Kingai aliwahi kuwaambia kuwa amemtaarifu Rais ambaye ni Kiongozi wa Nchi
Shahidi: hajatuambia
Kibatala: Labda Kufahamisha watu wa USALAMA WA TAIFA FA
Shahidi: Hapana hakutuambia
Kibatala: katika Maelezo Yako umezungumzia Kuhusu Jumanne Kuweka Sahihi yake Katika Hati ya Uzuiaji Mali
Shahidi: Hapana Sijasema
Kibatala: Statement Yako inasema “Tuliwa chukua watuhumiwa hao na kuwapeleka kituo cha Polisi Central kwa Mahojiano na tuliendelea Kumtafuta Mtuhumiwa Mwingine Moses Lijenje ambaye hatukuweza Kumpata, Je Kuna sehemu umesema Kwamba Mahojiano hayakufanyika
Shahidi: Hapo hakuna ila Ndiyo Maana Nimeelezea
Kibatala: Mheshimiwa Jaji tulikubaliana kuwa na health break, tunge’ Break kwa sababu bado ninayo maswali mengi na huyu shahidi.
Wakili wa Serikali: sawa mheshimiwa
Jaji: unategemea muda gani zaidi
Kibatala: Labda nusu saa na zaidi
Jaji: Mpaka saa 8:30 tutarudi kuendelea
Jaji Kaingia, Kesi inatajwa na Kibatala anaendelea na shahidi.
Kibatala: Nani alimpekua Adam Kasekwa!?
Shahidi: Afande ASP Jumanne alimpekua Akamkuta Adam Kasekwa na Karatasi yenye Majina Mbalimbali
Kibatala: Je Karatasi hii yenye namba za Simu mli’ connect na tuhuma au ilikuwa ya kwake binafsi
Shahidi: Ilikuwa Connected
Kibatala: Kwa hiyo Ipo kwenye Hati ya Kumiliki Mali
Shahidi: Ipo
Kibatala: Na Ikija Karatasi ya Hati ya Kushikilia Mali nitaiona
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Nani anayo Shahidi: Sijui
Kibatala: Unaweza Kujua Kama hizo namba za Simu zinahusika a na Shauri hili hapa Mahakamani
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Pale Rau Madukani, nani alikuwa Arresting Officer
Shahidi: Mimi hapa
Kibatala: Unafahamu au hufahamu kwamba ukisoma pamoja kifungu cha 23 cha CPA pamoja na PGO, arresting person ndiyo anapaswa kufanya search, Je unafahamu hilo?
Shahidi: Siyo lazima
Kibatala: Kwa ruhusa ya Mahakama nakuonyesha PGO 357(2) nakuletea Shahidi: KAA NAYO TU, SOMA TU
Kibatala: Anasoma 357(2) ya PGO
Kibatala: Kwa ufahamu wako nilivyosema anayetakiwa kushikilia mali ni Arresting Officer au Siyo?
Shahidi: Siyo lazima
Kibatala: Ukishapata offensive Weapon Ikishakuwa Seized inakabidhiwa CRO, Unakubaliana na Mimi
Shahidi: Inategemea na Kituo
Kibatala: Mwambie Jaji hii offensive weapon Luger C100 Iliingizwa Kwenye CRO
Shahidi: Atazungumzia Mwingine
Kibatala: Ufahamu wako ipo au haipo Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Chain of custody ikoje Imeanza kwa nani
Shahidi: Kwa Goodluck
Kibatala: Siyo Jumanne?
Shahidi: Jumanne
Kibatala: Unafahamu au hufahamu Kwamba Goodluck alikaa na hiyo Bastola kuanzia ameichukua kwa Jumanne Mpaka Dar es Salaam
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Je ulishuhudia watuhumiwa wakikabidhiwa kwa CRO Dar es Salaam
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Je Ulishuhudia Handing over ya Bastola Kutoka kwenu kwenda CRO
Shahidi: Sikushuhudia
Kibatala: baada ya Makabidhiano ya Watuhumiwa ulishuhudia Mpaka Mwisho au Uliondoka Kabla
Shahidi: Handing over unawapa Watuhumiwa na Karatasi ya Reference
Kibatala: Ulizungumzia Chochote kwamba Ulishuhudia Jumanne na Goodluck wakibadilishana Makaratasi
Shahidi: Sikushuhudia
Kibatala: Je kwa ufahamu wako Wewe Kama Askari Mwenye LLB, Je Palipaswa kuwa na Makabidhiano ya Makaratasi au Siyo lazima
Shahidi: Lazima yawepo
Kibatala: Je kuna kazi Nyingine 10 Mwezi 08 2020 ya Kiupelelezi ulishiriki Kufanya
Shahidi: Ndiyo nilishiriki
Kibatala: Na Kati ya hao ni Maafisa wa Jeshi wa zamani
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Mmoja wapo ni Gabriel Mhina
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji kama ni vikao gani vilifanyika Aishi Hotel
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Morogoro Katika sehemu fulani washtakiwa Walikaa Kupanga Ugaidi
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Mshitakiwa wa 4,3,2, 1 kwamba walikaa Mkoani Arusha Kupanga Njama za Ugaidi
Shahidi: Hapana Sijamwambia Kibatala: Ni wakati gani mlikuwa na description za Watuhumiwa Mlipata Muda gani kabla
Shahidi: Masaa 6 kabla
Kibatala: Ulisema kuhusu ku’ procure search warranty au hukusema
Shahidi: SIWEZI KUJIBU
Jaji: SHAHIDI JIBU SWALI
Shahidi: SIKUSEMA…….
Kibatala: Nilikusikia Kwamba Ulisema Arusha Lijenje alikuwa na Dada Yake, Je Mwambie Mheshimiwa Jaji Kama Ulimtajia Mheshimiwa Jaji
Shahidi: Hapana Sikumwambia
Kibatala: Je unayajua Majina ya huyo Dada
Shahidi: Hatukutajiwa
Kibatala: Kwa hiyo Mlienda Arusha Kumtafuta Dada Wa Lijenje
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: katika Maelezo Yako Ukiweka Muda ulifika Dar es Salaam Muda gani
Shahidi: Niliweka Muda
Kibatala: Kwamba Asubuhi au Uliweka na Saa na Dakika
Shahidi: Niliweka
Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba tupewe nakala halisi ya statement ya Mahita kwa mujibu wa 154 na 155 ya Sheria ya Ushahidi Mawakili wa Serikali Wananong’onezana hapa.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi
Kibatala: Shahidi Soma Kote kisha Taja Exactly Sehemu Uliyo andika Muda
Shahidi: Nisome Kwa sauti
Kibatala: Ndiyo kwa Sauti
Shahidi: Usiku wa Tarehe 06.8.2020 tuliondoka kuelekea Dar es Salaam na kufika 07.8.2020 Asubuhi
Kibatala: Hapo wapi Umetaja 11?
Shahidi: Leo kwenye kiapo
Kibatala: Mimi nakuuliza maelezo yako
Shahidi: Hakuna
Kibatala: Je ungependa maelezo yako yapokelewa MAHAKAMANI?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Mheshimiwa Jaji tunaomba Maelezo yake ya pokelewa Kama Kielelezo Cha Upande wa Utetezi
Wakili wa Serikali: Hatuna Pingamizi Mheshimiwa
Jaji: Yanapokelewa Kama Kielelezo namba p3
Wakili wa Serikali: Tunaomba kipokelewe na kusomwa kwa Ule ule utaratibu Shahidi Mahita Omary Mahita anasoma Kielelezo
Shahidi, Inspector Mahita Omary Mahita kamaliza kusoma Kielelezo…
Kibatala: Katika Maelezo yako hakuna mahala umezungumzia kuhusu kumpekua Mohamed Ling’wenya
Shahidi: Sijazungumzia
Kibatala: Na Ulishiriki au Hukushiri
Shahidi: Sikushirki
Kibatala: Na Hukuwahi Kufika Nyumbani Kwake Kimara ukiwa Chini ya Kiapo
Shahidi: Sijawahi
Kibatala: Katika Statement hujazungumzia lolote kwamba Gari iliharibika Njia panda Himo
Shahidi: Sijazungumzia
Kibatala: Pia katika Statement Yako Ujazungumzia kuhusu Kwenda Boma Ng’ombe Kula Nyama
Shahidi: Sikuzungumzia
Kibatala: Katika Ushahidi Wako hakuna Mahala Umezungumzi kuhusu Kuchukua Finger Prints katika Eneo la tukio
Shahidi: Sijazumgumzia
Kibatala: PGO ya 229 Order 4 ambayo Heading ni Handing of Exhibit Kibatala anasoma yote (ni makingereza)
Shahidi: Inazelezea Scene of Crime, Eneo ambalo Kimetokea Tukio, lakini siyo On Possession ambapo Mtu amekutwa Kizibiti
Kibatala: Kwa hiyo ni sahihi Kwamba PGO inasisitiza Kutunzwa kwa Finger Prints eneo ambalo Kielelezo kinakutwa
Shahidi: Kwa Eneo la Tukio (Scene of Crime)
Kibatala: Ulimwambia Mhe Jaji Kwamba ni sehemu ya Mpango wenu Kuweka Surveillance
Shahidi: Sikumwambia
Kibatala: Unakubaliana na Mimi Kwamba Freeman Mbowe alishiriki Uchaguzi wa Mwaka Jana Jimbo la Hai, sahihi
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Kwa kuwa tayari mlikuwa na Maelezo ya Onyo tayari ya Washtakiwa baadhi, Je Mwambie Mheshimiwa Jaji Kwamba Ulitaarifu Mamlaka zingine Kuhusu Mbowe Kwamba alikuwa na Tuhuma Za Ugaidi.
Shahidi: Kimya
Kibatala: Unakubaliana na Mimi Kwamba Freeman Mbowe alishiriki Uchaguzi wa Mwaka Jana Jimbo la Hai, sahihi
Shahidi: Ndiyo nafahamu
Kibatala: Kwa kuwa tayari mlikuwa na Maelezo ya Onyo tayari ya Washtakiwa baadhi, Je Mwambie Mheshimiwa Jaji Kwamba Ulitaarifu Mamlaka
Kibatala: Kwa ufahamu wako wewe Mpaka wewe Unauliza Majukumu yako Kuhusu suala hilo, Uliwahi Kujulishwa na Afande Kingai kuhusu Kuchukua Hatua kama hizi
Shahidi: Hapana Sijawahi
Kibatala: Uliwahi Kumshauri ACP kingai atoe Taarifa kwa Afisa wa Uchaguzi
Shahidi: Hapana
Kibatala: Uliwahi kumshauri ACP Kingai ili aweze kudhibiti huyu mastermind wa vitendo vya kigaidi kuhusu mienendo ya kusafiri nje ya nchi
Shahidi: Hapana
Kibatala: Kingai aliwahi kukwambia kwamba alishawahi kuwashauri watu wa USALAMA WA TAIFA kuhusu kumdhibiti Master Mind wa Ugaidi?
Shahidi: Hapana
Kibatala: Ulishawahi wewe au wenzio kwa kesi hii kuwa na voice records za Mbowe au kuagiza zikachukuliwe kwenye makampuni ya simu?
Shahidi: Hapana sijawahi
Kibatala: Ulishawahi kumshauri Boss wako Kingai kuwasiliana na makampuni ya simu kuhusu kwenda kuchukua sauti za simu za Mbowe
Shahidi: Sijawahi kumshauri
Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama wewe wenzio mlishawahi kuweka vinasa sauti nyumbani kwa Mbowe au ofisini ilitusikie pasipo shaka alipanga mipango ya ugaidi
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Umesema mshtakiwa 1, 2 na 3 hawakuwa na mali zozote zile
Shahidi: Ndiyo Kibatala: Je unafahamu kwamba palifanyika jitaihada za kwenda kutafuta vitambulisho vyao vya kupiga kura na NIDA
Shahidi: Sifahamu
Kibatala: Wewe unaona Kwako ni sawa Kwamba washtakiwa hawana chochote hata Pesa
Shahidi: Mbona watu wengi wanatembea na Pesa
Kibatala: Umemwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba washtakiwa Walikuwa wanaishi Moshi pale Rau
Shahidi: Hapana
Kibatala: Wakati unafanya surveillance washtakiwa Walikuwa wanafanya nini
Shahidi: walikuwa wamekaa tu
Kibatala: ulisema ulimuona yoyote akifanya Usajili wa Simu
Shahidi: Hapana
Kibatala: wakati unawakamata walikuwa wanafanya nini?
Shahidi: Walikuwa wanatembea kuja kwangu
Kibatala: Wakati unamkamata Bwire, Kingai alikuwepo
Shahidi: Alifika Jioni
Kibatala: Je Urio alifika lini Mbweni
Shahidi: Sifahamu kabisa
Kibatala: Mpaka leo hujawahi kumuona Urio
Shahidi: Sijawahi kumuona kabisa
Kibatala: Mheshimiwa Jaji ni hayo tu
Wakili wa Serikali: Wakati mnaenda Moshi Kutoka Arusha Mlikuwa watu wangapi?
Shahidi: Wakati tunatoka Moshi tulikuwa watu sita ila wakati wa ukamataji tulikuwa watano. Mmoja alikuwa dereva
Mtobesya: OBJECTION Jambo la Dereva ni Jipya, Hakutaja Dereva
Jaji: Wewe Hukusikia, alitaja dereva. Mimi nilisikia. Na nilisikia akisema mmoja ya waliotoka Arusha, mmoja alikuwa dereva wa RCO.
Jaji: anasoma majina, DC Aziz likiwemo, lakini hakuna neno dereva
Mtobesya: Neno DC AZIZI nilisikia ila hakusema hapo DEREVA..
Mallya: Wale waliohusika na Ukamataji ni Sita Ndiyo alitaja
Mtobesya: Na akija mtu mwingine akisema mlikuwa watano siyo sita, yeye akasema watano?
Mallya: Wale waliohusika na Ukamataji ni Sita Ndiyo alitaja
Jaji: kama jibu Muhimu mnalihitaji tutawapa Re-examination.
Wakili wa Serikali: Sawa
Wakili wa Serikali: Elezea wakati wa ukamataji
Shahidi: Tulikuwa watu watano na Mmoja alikuwa Kwenye Gari
Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali huhusiana na surveillance ukasema ulijiridhisha mwenyewe. Uliulizwa kuhusu tarehe ya maelezo yako. Je tarehe sahihi ni ipi?
Shahidi: Baada ya kupita tukaona ndiyo wale, na ilikuwa hakuna description ya nguo ya watu kama wale.
Shahidi: Tarehe 10 Mwezi 08 siyo Mwezi wa 09.
Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Kwenye Maelezo umeandika Uhalifu na siyo Ugaidi, Je uhalifu ulimaanisha nini?
Shahidi: Uhalifu ni jumla inayobeba Matendo mbalimbali ya kigaidi kama kuchoma vituo vya mafuta, maandamano ambayo hayana kokomo na kuwadhuru viongozi wa serikali.
Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusu Kibandaumiza, ikaleta maneno. Hebu fafanua.
Kibatala OBJECTION itakuwa sawa kweli?
Jaji: Nakubaliana na wewe.
Wakili wa Serikali: Uliulizwa ukiwa Moshi uliwapiga, ukajibu hayo ni maoni yake. Je, ulimaanisha nini?
Shahidi: Sikuwapiga, tulikaa nao vizuri.
Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali kuhusiana specific role ya kila mtu. Ieleze Mahakama sasa wewe aulichoambiwa katika briefing ni kitu gani uliambiwa.
Shahidi: Niliambiwa kuhusiana na kikundi kinachotaka kufanya vitendo vya kigaidi, nikisema kuchoma moto vituo vya mafuta, maandamano ya Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Mwanza na Morogoro, kuzuia barabara na mamiti.
Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali kuhusiana kukabidhiwa kwa pistol, eleza ulichoshuhudia.
Shahidi: Nilishuhudia wakikabidhiana kama nilivyoeleza Mahakam
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa ya kwangu ni hayo tu.
Re-cross examination
Jaji: Kuhusiana na hilo ambalo mlikuwa mnahitaji kufanya re-cross examination.
Mtobesya: Mheshimiwa Naomba nifanye re-cross examination
Jaji: Specifically kwenye eneo hilo tu.
Mtobesya: Unakumbuka ulisema wakati mnamkamata Mlikuwa sita.
Shahidi: Nlikwambia watano
Mtobesya: Ni ushahidi wako kwamba hukusema watu sita?
Shahidi: Mimi nilisema watu watano. Ndiyo tulienda kuwakamata
Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba utukumbushe
Jaji: “Tulitoka Arusha kwenda Moshi tukiwa sote na sisi ndiyo tuliokamata.
Tuliokamata tulikuwa sita.”
Mtobesya: Ni sahihi, ndivyo nilivyokuuliza?
Wawili ndio tuliowazuia na kuwawekachini ya ulinzi.
Shahidi: wawili ndio tuliokamata
Mtobesya: Rekodi za Mahakama zinasemaje sasa?
Shahidi: Mheshimiwa Jaji, naomba maelezo yangu haya Ndiyo yachukuliwe
Mtobesya: Kwenye Maelezo Yako Uliyoandika Ulieleza Kama mlikuwa watano au Sita
Shahidi: Sikueleza
Mtobesya: Mheshimiwa, ni hayo tu.
Jaji: Shahidi tunakushukuru kwa ushahidi wako
Jaji: Shahidi tunakushukuru kwa ushahidi wako
Jaji: Kama jibu muhimu mnalihitaji tutawapa
Re:Examination
Wakili wa Serikali: Sawa
Wakili wa Serikali: Elezea Wakati wa Ukamataji
Shahidi: Tulikuwa watu watano na Mmoja alikuwa Kwenye Gari
Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusiana na Surveillance Ukasema Ulijiridha Mwenyewe
Shahidi: Baada ya Kupita tukaona ndiyo wale, Alikuwa hakuna description ya nguo ya watu wale
Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuhusu Tarehe ya Maelezo yako, Je tarehe Sahihi ni Ipi
Shahidi: Tarehe 10 Mwezi 08 siyo Mwezi wa 09
Wakili wa Serikali: Uliulizwa Swali Kwenye Maelezo umeandika Uhalifu na siyo Ugaidi, Je uhalifu ulimaanisha nini
Shahidi: Uhalifu ni jumla inayobeba matendo mbalimbali ya kigaidi kama a Kuchoma vituo vya mafuta, maandamano ambayo hayana kikomo na kuwadhuru viongozi wa serikali
Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusu kibanda umiza, ikaleta maneno, hebu fafanua
Kibatala: OBJECTION itakuwa sawa kweli
Jaji: nakubaliana na wewe
Wakili wa Serikali: Uliulizwa ukiwa Moshi uliwapiga, ukajibu hayo ni maoni yake, Je ulimaanisha nini
Shahidi: Siku wapiga tulikaa nao vizuri
Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali Kuhusiana specific Role ya Kila Mtu Ieleze Mahakama sasa wewe aulichoambiwa Katika Briefing ni Kitu gani uliambiwa
Shahidi: Niliambiwa Kuhusiana na Kikundi Kinachotaka Kufanya Vitendo Vya Kigaidi, Nikisema Kuchoma Moto Vituo Vya mafuta.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji huyo ndiyo Shahidi Tuliyekuwa naye. Tunaomba hairisho mpaka Jumatatu Tarehe 08 ya Mwezi wa 11 ilituweze kuendelea na mashahidi wengine
Jaji: Utetezi
Kibatala: Hatuna Pingamizi Jaji anaandika kidogo
Jaji: Maombi ya hairisho yamekubaliwa. Shauri linaahirishwa Mpaka Jumatatu 8/11/2021 Washtakiwa watabaki rumande chini ya magereza mpaka tarehe hiyo