Kesi ya Mbowe: Jaji Tiganga akataa mapingamizi yote ya utetezi

Kama ilivyowasilishwa na ripota raia BJ leo tarehe 14 Desemba 2021.

Jaji ameshaingia mahakamani. Ni saa 4:05, Desemba 14, 2021.

Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha jopo la mawakili wa Serikali.

  1. Pius Hilla
  2. Abdallah Chavula
  3. Jenitreza Kitali
  4. Nassoro Katuga
  5. Esther Martin
  6. Tulimanywa Majige
  7. Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala anatambulisha mawakili wa upande wa utetezi.

  1. Nashon Nkungu
  2. John Mallya
  3. Fredrick Kihwelo
  4. Dickson Matata
  5. Seleman Matauka
  6. Edward Heche
  7. Alex Massaba
  8. Gaston Garubindi
  9. Sisty Aloyce

Jaji anawaita washitakiwa wote wanne na wote wanaitika kuwa wapo mahakamani.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, shauri limekuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi. Tupo tayari mheshimiwa.

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji, nasisi pia kwa ruhusa yako tupo tayari.

Jaji anaandika.

JAJI: Shauri hili ni kweli linakuja kwa ajili ya uamuzi ambao ulikuwa really served. Mahakama ilielekeza mawakili walete hoja zao kwa maandishi ambapo wameleta. Wakati shahidi namba 08 ASP Jumanne wakati wa kutoa ushahidi wake alieleza kwamba alipewa kazi ya kuandika maelezo ya mshitakiwa wa tatu, na baada ya kueleza hivyo aliomba maelezo hayo yapokelewe mahakamani ambapo upande wa utetezi walipinga kwa sababu tisa. Sababu ya kwanza ni mshitakiwa namba tatu hakuwa kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, na hakuandika maelezo yoyote. Sababu ya pili mshitakiwa wa tatu alilazimishwa kuweka sahihi katika maandishi ambapo pia pamoja na kulazimishwa hakupewa nafasi ya kusoma maelezo yake.

JAJI: Alitshwa na Goodluck Minja na ASP Jumanne alimtishia kwamba asipoweka atateswa kama alivyoteswa Moshi. Sababu ya tatu ni kwamba maelezo yake yalirekodiwa nje ya muda. Yalirekodiwa siku ya tarehe 9 Agosti 2020 wakati amekamatwa tarehe 5 Agosti 2020. Sababu ya nne ni kwamba maelezo ya onyo yalikuwa yameandikwa kwa sheria ya kifungu 57((1) ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2020 ambapo sheria hiyo haipo. Sababu nyingine ni kwamba alionywa kwa Sheria ya Kuzuia na Kupambama na Ugaidi wakati sheria hiyo haipo.

JAJI: Sababu nyingine ni maelezo ambayo yanalengwa kutolewa mahakamani yapo tofauti na yale yaliyotolewa wakati wa Commital kwa kutofautisha subsection. Sababu ya saba hakuna kifungu kinachoonekana kwamba wamechukua maelezo na kushtaki kwa kifungu kipi. Kutokana na hoja zote mbili zilizoletwa zilikuwa zinaangukia katika Sheria ya Ushahidi ambapo ilipelekea kuwepo kwa kesi ndogo. Kwa hiyo mapingamizi hayo yalishughulikiwa kwa njia ya kuleta hoja Mahakamani.

JAJI: Na kwamba baada ya kesi ndogo submission ziletwe kwa kuleta hoja ya kuunga mkono kuhusu mapingamizi yanayoangukia katika Sheria ya Ushahidi. Katika kesi ndogo upande wa mashitaka wenye jukumu la kuleta mashahidi wa kuthibitisha, walileta mashahidi wanne. ASP Jumanne, Goodluck Minja, Issa Maulid na Msemwa.

JAJI: Na walileta vielelezo, barua ya Msajili kama kielelezo namba 1, Detention Register kama kielelezo namba 2 na kielelezo namba 3. Kwa upande wa utetezi walileta mashahidi watatu. Kielelezo namba moja maelezo ya Goodluck Minja, nakala ya Hati ya Mashitaka, Dispatch Book, nakala ya Hati ya Mashitaka ya Kesi namba 17/2020. Nakala ya Hati ya Mashitaka ya shahidi namba tatu kesi 63/2020.

JAJI: Na kielelezo kingine ni Diary ambayo ilichukukiwa wakati wa shahidi wa mashitaka anatoa ushahidi wake. Sababu pande zote hawajazungumzia kwa kirefu kielelezo hiki basi na mimi sitoongelea kwa kirefu kielelezo hiki. Mahakama haina nia ya kurejea maelezo ya ushahidi wote. Suala la kutafuta ukweli kwa hoja namba moja na mbili na hoja namba tatu mpaka namba saba zilikuwa resolved kwa submission zilizopangiwa parties Mahakamani. Ni utaratibu wa kawaida mambo yanayohusu sheria kuamuliwa kwanza. Kwenda kwenye hoja za kisheria si sawa, ni vizuri kwenda kwenye hoja za ushahidi kwanza. Kwa sababu hiyo tutaanza na mambo yanayohusu ushahidi kabla mambo ya kisheria.

JAJI: Kwa mujibu wa Sheria ya Ushahidi Sura ya Sita kifungu 57 (1) pale ambapo utetezi wanapinga maelezo ni wajibu wa mashitaka kuthibitisha pasipo kuacha shaka. Kutokana na ushahidi wa shahidi namba moja na shahidi namba tatu ndiyo waliokwepo wakati wanaandika maelezo. Kwa mujibu wa ushahidi wao walimkamata mshitakiwa huko Rau Madukani, na kwamba wakati wanawakamata walikuwa na mwenzao Moses Lijenje, na washitakiwa kwa ridhaa yao waliongoza zoezi la kumtafuta Moses Lijenje katika maeneo ya Moshi na Wilaya ya Hai. Wakili aliwaongoza jopo la wakamataji, kwamba baada ya kushindwa kumpata siku ya tarehe 6 Agosti 2020 walianza safari kuja Dar es Salaam.

JAJI: Na kwamba walifika kesho yake alfajiri Kituo cha Central Police Dar es Salaam, na wakawakabidhi sehemu ya mapokezi na baada ya hapo waliondoka kwenda kufanya usafi, nwa kwamba wipokelewa na DC Msemwa, na walirudi tena kumhitaji mshitakiwa namba tatu kwa ajili ya kuandika maelezo yake ya onyo na kwamba mshitakiwa alitoa maelezo yake kwa hiari yake. Ushahidi wake uliungwa mkono na shahidi namba mbili, aliyeeleza kwamba aliwapokea baada ya washitakiwa kufikishiwa kwake na kuwaingiza kwenye kumbukumbu ya Detention Register._ Kwa mujibu wa ushahidi huo yeye anashuhudia kuwapo katika Kituo hicho.

JAJI: Anashuhudia kuwapokea na kumtoa tena kisha akumpokea tena mshitakiwa namba tatu. Mshitakiwa namba tatu aliporudishwa alikuwa kwenye hali nzuri. Na shahidi namba moja anaendelea kusema kwamba baada ya kumalizia kumuandika maelezo na kumsomea kisha akamrudisha tena mahabusu. Ushahidi huu ulipingwa na upande wa utetezi ambapo mshitakiwa wa tatu alitoa ushahidi wake kwamba hajawahi kufika katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam. Walipofikishwa Dar es Salaam walifikia Kituo cha Polisi Tazara na kupelekwa Mbweni ambapo alichukuliwa kwenye chumba alichokuwepo kupelekwa chumba kingine na kisha kulazimishwa kusaini maelezo.

JAJI: Maelezo yoyote yanayosema kwamba aliyatoa ni ya uongo. Akaendelea kusema kwamba upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kwamba Msemwa alikuwapo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam siku hiyo.

JAJI: Hata alipoulizwa alishindwa kusema aliwapokea zamu yake. Shahidi wa pili yeye alisema kwamba alikamatwa huko Wilayani ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro na kuletwa Kituo Cha Polisi Oysterbay alimkuta Msemwa na kwamba kwa sababu hakuwa amekula alimwagiza Afande Msemwa akamchukulie chakula na akaendelea kuwa rafiki wa Afande Msemwa na kwamba hata baada ya kupelekwa mahakamani alirudishwa tena Kituo cha Polisi Oysterbay kwa siku 19. Kwa muda wote huo si kweli kwamba Msemwa alikuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam na kwamba alipokuwa akifuatilia kesi aligundua kuwa Msemwa aliiongopea Mahakamani kwamba alikuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam. Aliwasilina na wakili wake kisha akapewa utaratibu wa kupata nyaraka kwa ajili ya kuzileta Mahakamani. Alipozileta upande wa mashitaka walipinga lakini Mahakama ikaona ni busara kuzipokea. Upande wa utetezi wakamleta tena shahidi wa tatu.

JAJI: Upande wa utetezi wakamleta tena shahidi wa tatu Bwana Mhina ambaye alikamatwa huko kwao Tabora na wakati wote huko alikuwa anaulizwa kama anamfahamu mshitakiwa namba nne na mshitakiwa namba tatu ambapo yeye alisema kwamba alifanya naye kazi wakati fulani. Pamoja na kuwaeleza ukweli lakini waliendelea kumshikilia na baadaye akashtakiwa na kupelekwa gerezani ambapo alikutana na mshitakiwa namba tatu. Akasema kwamba kwenye hati ya mashitaka palikuwa pameandikwa majina ya washitakiwa na pembeni gereza aliokuwa anashikiliwa. Yeye alikuwa anashikiliwa na mshitakiwa namba tatu Segerea. Kwa upande wa utetezi walionyesha kwamba kwa namna gani mshitakiwa namba tatu hakuwepo Kituo cha Polisi na upande wa mashitaka walikuwa wanaonyesha kwamba alikuwapo Kituo cha Polisi. Kama nilivyosema mwanzo kwamba upande wa mashitaka ndiyo wenye jukumu la kuthibitisha pasipo kuacha shaka, mzigo wa uthibitishaji wa shauri kutoka upande wa mashitaka, upande wa utetezi kazi yake kubwa ni kuonyesha mashaka ambayo yanaweza kuwa resolved kwa favour ya mshitakiwa.

JAJI: Hii ni kwa Sheria Kesi ya Joseph Vs Jamhuri Kesi 44 ya 1986. Jambo la msingi mshitakiwa alikuwa wapi. Upande wa mashitaka wanasema mshitakiwa namba tatu alikuwa katika kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam kwa kuleta Detention Register kuonyesha alifika Kituo cha Central Police. Shahidi namba mbili anasema kwamba alimpokea mshitakiwa na kumwongoza kwenye kielelezo namba 2 cha Detention Register. Kwa msingi huo wao ndiyo ushahidi wao. Upande wa utetezi wao wanakana na ushahidi wa kukana umejengwa kwa shahidi namba moja na shahidi namba tatu, kwamba ushahidi waliotoa haujaungwa mkono na maelezo yoyote kwamba kweli walikuwa kwenye Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam. Kwa upande wa utetezi wanaomba kwa mujibu wa PGO namba 284(4,5,6) kwa kusokekana kwa Occurance Book kuonyesha ni kweli kwamba Msemwa alikuwapo kazini siku hiyo.

JAJI: Hakuna ushahidi wa Polisi in charge pia. Wakaendelea kusema hata shahidi namba mbili alipoulizwa maswali alishindwa kuwataja aliwapokea zamu na hata waliompokea kinyume na Station Diary ambapo inatakiwa kuonyesha matukio yote. Hata kielelezo namba 2 kina mapungufu kwa kutolewa kwake kilipokuwa huko Polisi, kwa sababu hiyo Mahakama inatakiwa ione mashaka kwamba hakijakidhi. Kwa Kesi ya Isaya vs Jamhuri 115 ya mwaka 2019, upande wa utetezi walihitimisha kwa kuomba mahakama itizame kwa PGO 353 kwamba mshitakiwa anapofikishwa kituoni anatakiwa apelekwa kwa daktari, jambo ambalo lingefanyika lingeonyesha kweli kama mshitakiwa namba 3 hakuteswa.

JAJI: Kwa ushahidi ulitolewa na shahidi namba tatu, na kwamba walipokutana Mahakamani na gerezani aliambiwa na mshitakiwa namba tatu kwamba hakufikishwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam bali Tazara. Wakati napokea vielelezo nilisema mwisho nitaangalia na kuona kwamba vielelezo hivyo ni relevant.

JAJI: Niliombwa kuangalia kielelezo namba mbili Mahakama ichunguze ione kwamba hapakuwa na muunganiko wa kielelezo hicho na suala la kielelezo kimetolewaje Mahakamani. Ikumbukwe kwamba kielelezo hiki kilishapokelewa na Jaji Siyani. Nafikiri si sawa kuangalia kielelezo hicho tena wakati kielelezo hicho kilishatolewa uamuzi na Mahakama. Kwa sababu hiyo Mahakama inatupilia mbali hoja hiyo.

JAJI: Kuhusiana na hoja namba tatu kwamba mshitakiwa alikuwepo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam inahusu mashahidi namba moja na namba mbili. Namba moja anasema walipotoka Moshi walifika moja kwa moja Polisi Kati Dar es Salaam, na wanaonyesha kwamba jina la mshitakiwa namba tatu lipo kwenye Detention Register. Ushahidi unaonyesha kwamba mshitakiwa aliingizwa kwenye kituo hicho, na kwamba alitolewa kwa ajili ya upelelezi. Swali ambalo Mahakama inajiuliza ni je, ni ushahidi wa kuaminika?

JAJI: Mahakama inatazama ushahidi huo kama ushahidi unapaswa kuungwa mkono. Mahakama imetizama katika aina ya ushahidi unapswa kuungwa mkono. Mahakama inaona ushahidi unatolewa chini ya kiapo unapaswa kuungwa mkono. Kwa Mujibu wa Kesi Mvumi Mpenda Vs Jamhuri 327 ya 2016, na maelezo ya marehemu wakati anafariki, maelezo ya mtoto pia, Sheria Kesi ya Frank Joseph vs Jamhuri, ushahidi ambao ime- base kwa habari ya kusikia unatakiwa kuungwa mkono.

JAJI: Ukiangalia aina ya ushahidi wa kuungwa mkono utaona ushahidi wa shahidi namba 2 hauangukii katika miongoni mwa ushahidi niliotaja kwa maelezo kwamba alipofika Polisi alimkuta shahidi wa pili. Mahakama inaona kwamba pamoja na kwamba ushahidi wa shahidi namba mbili siyo wa kuungwa mkono, basi ushahidi wake unaungwa mkono na shahidi namba mbili kama ilivyo kwenye kesi ya Goodluck Kyando vs Jamhuri ni ushahidi ambao unahaminika. Kama nilivyosema kwamba upande wa utetezi jukumu lao ni kuonyesha mashaka ili kusudi waweze kuleta mashaka. Walitakiwa watengeneze mashaka. Shahidi namba moja ambbaye ni mshitakiwa namba tatu anaposema kwamba alikuwa Kituo cha Polisi Tazara ndiyo mashaka yenyewe.

JAJI: Kwamba kwa mujibu wa sheria jukumu la kuthibitisha jambo lolote ambalo mtu analisema inakuwa kwake yeye labda kwa mujibu wa Sheria itatakiwa itihibitishwe na mtu mwingine. Kwa sababu hiyo basi, mshitakiwa alikuwa na jukumu la kuonyesha ni kweli alikuwa Kituo cha Tazara. Mzigo wa huo unakuwa mwepesi kwake. Wakati napitia ushahidi kuhusiana na jambo hili, ambapo yeye mshitakiwa alisema kwamba alikuwa katika kituo cha Tazara yeye na mshitakiwa namba mbili, kumbe alikuwa na mtu aliyemwona akiwa kwenye Kituo cha Tazara lakini kwa bahati mbaya mshitakiwa namba tatu ameshindwa kumwita shahidi huyo kutoa ushahidi wake Mahakamani. Badala yake alimwita shahidi namba tatu ambaye anasema alipofika Kituo Cha Tazara hakumkuta Kituo cha Polisi Tazara. Lakini pia katika ushahidi wake mshitakiwa namba tatu haikuelezea. Shahidi namba tatu kwa kutumia kielelezo ambacho ni hati ya mashitaka ambayo inaonyesha jina, mshitakiwa na gereza alilikuwemo.

JAJI: Kwa Kuzingatia hati hiyo hakuna sehemu inayoonyesha kwamba walikuwapo Katika Gerez la Segerea. Basi Mahakama inatilia mashaka ushahidi huo. Shahidi huyo namba tatu alikabidhiwa Detention Register ya Tazara alisema jina lake halikuwemo na pia jina la mshitakiwa namba tatu halikuwepo katika Detention Register. Kwa sababu hiyo Mahakama inapata mashaka kwamba mshitakiwa namba tatu alikuwepo Kituo cha Polisi Tazara.

JAJI: Na shahidi wa pili alisema kwamba hapakuwa na wwezekano kwamba Msemwa alikuwa anafanya kazi Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam. Na kwa maelezo hayo alileta vielelezo ambapo ni Dispatch, Hati ya Mashitaka na vingine. Ukitazama vielelezo vyote hivyo hakuna uhusiano wa moja kwa moja na kesi iliyopo Mahakamani.

JAJI: Na kwamba Mahakama inaona kwamba vielelezo hivi haviwezi kuisaidia Mahakama. Ushahidi unatolewa ni kuhusu tarehe 14 Mei 2020 wakati jambo linalobishaniwa hapa ni kuhusu tarehe 7 Agosti 2020. Labda kama ingekuwa shahidi huyo alikuwapo Oysterbay siku ya tarehe 7 Agosti 2020. Katika Mazingira hayo Mahakama inaona kwamba value yake ni zero na haiwezi kuisaidia Mahakama. Kwa upande wa mashitaka waliweza kueleza kwamba shahidi alikuwa ni shahidi mwenye maslahi, kwamba katika ushahidi wake ulikuwa wenye kujikanganya.

JAJI: Hasa pale aliposema kwamba alimuelekeza DC Msemwa akachukue fedha katika PPR yake wakati alishasema alipokamatwa hakuwa na kitu chochote huko Mwanga, na hakutoa PPR yake hapa Mahakamani, na hivyo ni ushahidi wenye kujikanganya. Mara ya kwanza alisema kwamba alimtambua DC Msemwa baada ya kusoma jina lake katika uniform na alipoulizwa mara ya pili alisema kwamba alitambua namba yake H4323. Alishindwa kuoanisha jina namba aliyosema mara ya pili kushindwa kuonyesha wajii wa DC Msemwa.

JAJI: Alishindwa kutoa description nzuri ya shahidi huyo. Mwanzo alisema kwamba ni mweusi na mnene na alipoulizwa tena akasema kwamba anaweza kuwa mnene au siyo mnene. Mahakama ya Rufaa iliyoketi huko Arusha inasema kwamba siyo kila mkanganyiko unafanya Mahakama isiamini ushahidi uuo. Mahakama inajiuliza kwamba je, mkanganyiko huo ni mkanganyiko wa kawaida ambao mahakama inapaswa kuupuuza? Ikumbukwe Mahakama inaangaliwa kuhusu maelezo yaliyotolewa.

JAJI: Katika mazingira hayo ukiangalia contradiction ni contradiction siyo nyepesi. Kwa sababu hiyo basi Mahakama inatilia mashaka ushahidi wake. Ni wazi pia ushahidi unaotakiwa kutengeneza mashaka hautakiwi wenyewe kutiliwa mashaka. Wote waliokuja kuzungumza wamejichanganya.

JAJI: Na juu ya maslahi kwamba ni shahidi mwenye maslahi, ni kweli amesema kwamba amekuwa haridhiki kuanzia kesi mpaka kwa Jaji mwenyewe. Mahakama inaona yeye ni shahidi wa hisia ambaye amekuja Mahakamani kutoa hisia zake. Mahakama inaona kwamba kuhusiana na ushahidi alikuwapo Kituo cha Polisi Oysterbay wakati mshitakiwa namba tatu alikuwa Tazara.

JAJI: Mahakama inaona kwamba ushahidi ulioletwa na upande wa Mashitaka haujaweza kutikiswa. Na kwa sababu hiyo pingamizi la kwanza kwamba mshitakiwa hakuwepo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam siyo la msingi na Mahakama inatupilia mbali.

JAJI: Kwa maana hiyo sasa, kwamba mshitakiwa namba tatu aliteswa na alilazimishwa kuweka sahihi yake na kwamba aliweka sahihi yake baada ya ASP Jumanne kumtishia kwamba angeteswa kama alivyoteswa Moshi, na kwa namna ambayo alikuwa ametishwa hakupewa kusaini, ikumbukwe kwamba maelezo yanayibishaniwa ni yale yaliyotolewa alipokuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam. Upande wa mashitaka unapaswa kuthibitisha kwamba hapakuwepo na mateso.

JAJI: Na kwa sababu ya upande wa mashitaka ulikuwa jukumu hilo, wao wanasema mshitakiwa namba tatu hakuteswa na kwamba wao tarehe 8 Agosti 2020 walipowakabidhi washitakiwa Mbweni hawakurudi tena. Na kwa mujibu wa maelezo yao, maelezo ambayo anataka ni yale aliyotatoa akiwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.

JAJI: Kwamba mshitakiwa aliteswa na Goodluck na Mahita kwa kuulizwa maswali juu ya uhusiano wake na mshitakiwa namba 4, mshitakiwa anasema walimuuliza maswali mengi na walikuwa wanamrekodi na baada ya hapo walimpeleka kituo cha Mbweni, kitu ambacho upande wa mashitaka unapinga. Wakati wa ushahidi wake hakusema alivyoteswa na alivyotishwa akiwa Kituo cha Polisi Mbweni.

JAJI: Kwa maelezo yake yeye kwamba alifikishwa Mbweni akitokea Kituo cha Polisi Tazara, na kwamba siku ya tarehe 10 walimpeleka kwemye Ofisi ya Upelelezi ambapo Jumanne na Goodluck ndiyo walimtishia, na kwamba alipokuwa wamekaa aligeuka akamwona Goodluck akiwa na pistol na kumwambia kwamba asiposaini … Upande wa utetezi haujaeleza kwamba namna gani upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kwamba hakuteswa.

JAJI: Wakaomba pia Mahakama kujikimbusha PGO 353 (2) kwamba mshitakiwa anatakiwa kufikishwa kwa daktari, hiyo ingeondoa mashaka kama mshitakiwa hajateswa. Kwa sababu hiyo basi upande wa utetezi wakaomba Mahakama ione kwamba mshitakiwa alitishwa. Mahakama inalo jukumu la kuangalia ushahidi wa mtu mmoja mmoja na maelezo ya mshitakiwa.

JAJI: Kwa ushahidi wa mshtakiwa namba tatu kwamba alitshwa alipokuwa Kituo cha Polisi Mbweni na kwamba kama asiposaini mateso ya Moshi yatajirudia, kwa sababu hiyo maelezo yanayopaswa kutolewa yeye hayatambui.

JAJI: Wakati anatoa ushahidi wake, wakili wa Serikali alimuuliza ni kweli kwamba yeye alitshwa tarehe 8 Agosti 2020 Akauliza je, kama Adamoo alitolewa tarehe 9 Agosti 2020. Akasema hajui itakuwaje. Hoja za mawakili zinaonyesha kwamba shahidi aliteswa tarehe 9 Agosti 2020.

JAJI: Na kwamba hoja ya tatu ya maelezo yaliandikwa nje ya muda wao wameandika tarehe 9 Agosti 2020. Ni wazi pale panapokuwa na ushahidi unaopingana na submission ni wazi ushahidi unapaswa uaminike kwa sababu submission ni ufafanuzi wa ushahidi.

JAJI: Katika mazingira hayo Mahakama inarejea maamuzi yake wakati ina- resolve mgogoro wa kwanza. Mahakama imeshindwa ku- examine ni tarehe gani mshitakiwa aliteswa. Kwa sababu hiyo basi Mahakama inabakia na mkanganyiko. Na kwa PGO ya 353 ya kuhusu kumpeleka shahidi kwa daktari haiwezi kusaidia kwa sababu Mahakama ipo kwenye dilemma.

JAJI: Mahakama inaona sababu ya pili ya pingamizi inaona upande wa utetezi umeshindwa kujenga vizuri na kwa sababu hiyo Mahakama ina- overule na kutupa pingamizi hilo.

JAJI: Nakuja sasa kwenye hoja za kisheria kwamba maelezo yalichukuliwa nje ya muda. Mahakama inakubaliana kwamba mshitakiwa alikamatwa tarehe 5 Agosti 2020 na kwamba maelezo yalichukuliwa tarehe 7 Agosti 2020. Mahakama inarejea Sheria kwamba maelezo yanatakiwa kuchukuliwa ndani ya masaa manne.

JAJI: Na kwamba kinyume na hapo panapaswa kuwa na kibali maalumu. Ni kweli maelezo hayo yameandikwa nje ya muda wa zaidi ya masaa 40. Lakini kifungu kinachofuata kinasema kwamba pale ambapo mshitakiwa anakuwa amekamatwa na taratibu za kiupelelezi zinaendelea basi muda huo unapaswa uondolewe.

JAJI: Kwa maelezo kwamba Walikuwa na Moses Lijenje na kwamba hakukamatwa, walitumia siku iliyobakia ya tarehe 5 Agosti 2020 walitumia muda uliobakia kumtafuta Moses Lijenje. Na kesho yake waliendelea kumtafuta sehemu mbalimbali.

JAJI: Kwa ku- base kwenye ushahidi huo wa upande wa mashitaka, upande wa utetezi walieleza kwamba yapo mapungufu mengi yameonekana. Wanasema maelezo hayo hayaonyeshi kwamba palikuwa na katazo kutoka kwa DCI kuwafanya wasiandike maelezo hayo hapo Moshi.

JAJI: Kwamba zoezi la kumtafuta Lijenje lilijawa na mapungufu mengi. Wakaomba Mahakama izingatie hoja zao kwa kutumia kesi zifuatazo: DPP vs James, Massawe vs Jamhuri, Aphonce vs Jamhuri, Hamis Chuma vs Jamhuri.

JAJI: Kama nilivyoeleza kwamba 50(1) lazima mshitakiwa achukuliwe maelezo ndani ya masaa manne, wakati kifungu cha 50(2) kinasema kwamba muda hautahesabika kama mshitakiwa atasafirishwa. Uzito wa kesi yenyewe … Muda huo hautahesabika. Kesi ya Mendez inasema kwamba si kila kutofuatwa kwa sheria kunaondoa uzito wa ushahidi wenyewe.

JAJI: Mahakama imekwisha kusema kwamba mara baada ya washitakiwa kukamatwa palikuwa na taarifa ya kutokamatwa kwa Moses Lijenje, kwamba walikamata washitakiwa wawili na mmoja alikuwa ameshaondoka. Kwa namna hiyo basi washitakiwa walikuwa watatu na mmoja aliweza ku- dissappear. Kwa askari wanaojua kazi zao is asingeweza ku- relax na kukaa bila kumtafuta mshitakiwa wa tatu.

JAJI: Ni wazi kwa upande wa mashitaka ushahidi wao hautakiwi kutiliwa shaka. Ni wazi pia upande wa utetezi wameeleza kwamba kifungu 50(1) ni wazi kilitungwa kwa uwezekano wa kuondoshwa kwa kuteswa kwa washtakiwa.

JAJI: Katika hali hiyo ni wazi kwamba, kwa hoja ya upande wa utetezi ushahidi unatolewa na upande wa mashitaka hakuna mashiko kwa kutengeneza mashaka.

JAJI: Pamoja na hoja zao hizo za utetezi, lakini ni wazi kwamba ushahidi huo wa mashitaka umeletwa kwa uzito wake siyo wa kupuuza. Mahakama inapokuwa inataka kuyapa uzito maelezo hayo Mahakama inapaswa kungalia mazingira yote.

JAJI: Kwa maoni yangu hatua tuliyopo ni hatua ya kupokea maelezo ya onyo. Mahakama haiwezi kuzungumzia uzito wake. Hoja ya kwamba Mahakama ione uzito wa maelezo yenyewe Mahakama inaona imeletwa kabla ya wakati. Kesi mbalimbali zinasisitiza kwamba yakiwepo maelezo ya kutosha yanayoonyesha kama palikuwa na sababu ya kutosha kuandaa maelezo, basi sababu hiyo inatosha kupokea maelezo hayo.

JAJI: Maelezo ya kwamba shauri lilikuwa limefumguliwa Dar es Salaam basi palikuwa na sababu ya msingi maelezo kuyachukulia Dar es Salaam. Kuwasafirisha washitakiwa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine Mahakama ina maoni kwamba kwa namna maelezo yaliyotolewa, Mahakama inaona katika mazingira haya ilikuwa ni sahihi itumike.

JAJI: Kwa sababu hiyo pingamizi la tatu nalitupilia mbali. Kuhusu pingamizi la nne kuhusu verification katika upande wa utetezi wameomba Mahakama ione umuhimu wa verification, kwamba Mahakama ilisema kwamba kutoa kuandika Sheria kwa usahihi ni fatal.

: JAJI: Hakuna Sehemu yoyote ambapo ASP Jumanne alikuwa akisahihisha. Wakaomba Mahakama ikatae kielelezo hicho. Suala zima la uhuru wa mtu anapokuwa anachukiliwa maelezo, siyo lazima ionyeshe umeathirika Vipi. Basi wakaomba Mahakama ikikatae kielelezo hicho. Nakubaliana na upande wa utetezi kwamba Mahakama ilikuwa inapokea kielelezo mara ya Kwanza.

JAJI: Mahama inaona kwamba katika mazingira fulani fulani Mahakama ya Rufani imekuwa ikilaumu kutokupokea kielelezo. Basi kwa sababu hiyo pingamizi hili pia naona halina mashiko.

JAJI: Kwamba kwa sasa Mahakama ya Rufani imekuwa inachukua msimamo tofauti, kwamba unapokuwa umerejea tofauti Sheria kwamba jambo hilo haliwezi kupokelewa.

JAJI: Kesi ya James Mwamule na Sykes Mahakama inaona kwamba kurejea kimakosa kwenye verification kumeathiri haki ya mshitakiwa kwa namna gani. Basi kwa sababu hiyo natupilia mbali pingamizi hilo.

JAJI: Kwa pingamizi la tano pia kuhusu subsection na kunukuu Sheria ambayo haipo, katika kukosea kutaja Sheria, hakufanyi nyaraka kukataliwa Mahakamani. Katika maamuzi hayo nimezingatia kesi ya James na Songoroka. Basi kwa namna hiyo pia natupilia mbali pingamizi hilo.

JAJI: Mahakama imeelekezwa kurejea kitabu kitakatifu cha Yohana 7:51 kwamba hata Mungu mwenyewe hahukumu pasipo kusikiliza. Na kifungu namba 57 kinasisiatiza kwamba polisi anapokamata mtu lazima amwambie kosa alilofanya.

JAJI: Article 13 ya Katiba ya nchi yetu, 15(2A) zenyenwe zote zinaeleza umuhimu wa mtu kuelezwa kosa analoshtakiwa nalo pamoja na haki ya kusikilizwa. Kesi ya George Songoroka vs DPP inaelezea kwamba … Kwamba katika kifungu 50 (1b) mtu aelezwe kosa lake.

JAJI: Lakini kama ambavyo nimesema kesi ya Issa James kutokurejea kwa usahihi kifungu cha sheria hakufanyi kesi ifutwe kama hakuna ushahidi ambao unaonyesha mshitakiwa ameathirika vipi. Kwa maana hiyo Mahakama inaona kwa kukosea au kutokurejea kifungu cha Sheria hakufanyi kielelezo kukataliwa. Kwa sababu hiyo natupilia mbali hoja ya tano ya pingamizi.

JAJI: Hoja ya sita inanataka kufanana na ile ya tano, kwamba maelezo yanayotolewa hayafafani na yake ya kwenye Committal Bundle. Mahakama imeelekezwa kwamba kutolewa kwa ushahidi baada ya Commital Bundle, dhumuni la Committal Bundle ilikuwa inalenga kufanya mshitakiwa ajue ushahidi uliopo.

JAJI: Mahakama kwenye hoja hii haitochukua muda mrefu kwa sababu kifungu 249, kinaelezea kwamba mshitakiwa anatakiwa kutolewa substance ya nakala. Kinachotakiwa mshitakiwa kutolewa ni ushahidi, juu ya ushahidi kuwa kwa kifungu Sahihi au siyo Sahihi hakuwezi kufanya Mahakama itupilie mbali kielelezo hicho. Kielelezo hicho Mahakama inaona ni kielelezo kile kile isipokuwa kimoja kina subsection na kimoja hakina ila vyote viko sawa.

JAJI: Hoja ya saba ni kwamba katika kifungu cha 57 mshitakiwa anapokuwa ameonyesha kukiri anatakiwa kuonywa upya. Na anapokuwa ameonywa basi hapo ndipo maelezo yanatakiwa kuandikwa. Ni wazi kwa kungalia hilo haionyeshi mshitakiwa alihojiwa kwa kufuata taratibu gani kati ya hizo mbili.

Jaji” Niseme jambo hilo na hoja hii pamoja na kwamba Ilikuwa raised mwanzo, mawakili wamesema kwamba hawajazungumza. Kwa Maana hiyo Mahakama inapata benefit ya pekee kutoka kwa upande wa mashitaka. Pamoja na kwamba hoja hiyo haijaelezwa na upande wa utetezi lakini Mahakama ameona ni vyema ipitie hoja hiyo.

JAJI: Kinachotakiwa ni format tu na siyo kifungu kipi kimetumika. Kwa hiyo iwe kwa kifungu cha 51 au 57 kwa kufuata utaratibu huo, kama akuna maelezo ya mshitakiwa alivyoathirika, … Basi kesi ya Seko vs Jamhuri, Mahakama inaona hoja ya saba haina mashiko na naitupilia mbali.
[12:31, 12/14/2021] William Shao: JAJI: Hoja zote saba hazina mashiko na hasa kwenye kesi ndogo ushahidi ulioletwa na upande wa mashitaka umeshindwa kutingisha. Kwa sababu hiyo basi mapingamizi yote nayatupilia mbali.

Natoa AMRI.

: Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na uamuzi Jaji kwa kusimama na kumuinamia.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji naomba sasa utoe amri tuweze kurejea kwenye shauri kubwa.

PETER KIBATALA: Mheshimiwa Jaji naomba utoe amri tuweze kurejeshewa kielelezo ambacho ni dispatch.

JAJI: Na hivi vingine?

KIBATALA: Vibakie kwa sababu vinaweza kutumika hata Mahakama ya Rufaa huko mbeleni ila hiki kinatumika na Ofisi.

JAJI: Nimepokea hoja zote, na kwa sababu hiyo kwamba vielelezo ambavyo vilitolewa kwenye kesi ndogo virudishwe kwa wenyewe na ninaelekeza maafisa wa Mahakama kabla hawajarudisha watoe copy. Natoa AMRI.

Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na uamuzi Jaji kwa kusimama na kumuinamia.

JAJI: Baada ya kumalizia shauri dogo, sasa natoa amri turudi kwenye kesi kubwa. Natoa amri.

Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na uamuzi wa Jaji kwa kusimama na kumwinamia.

JAJI: Mara ya mwisho tuliishia kwenye ombi la kutaka kupokea maelezo. Sasa Mahakama inapokea maelezo hayo. Natoa AMRI. Tuendelee na shahidi.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, shahidi wetu ASP Jumanne ameshindwa kufika mahakamani pamoja na kumpatia taarifa leo awe maeneo jirani.

JAJI: Hamkumpa taarifa kwamba leo anatakiwa mahakamani?
WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji alikuwa awe hapa ila sasa anaumwa na kashindwa kusafiri. Naomba ahirisho Mheshimiwa Jaji.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, shahidi alishaonywa na kwamba leo alikuwa awe hapa. Sisi wengine tulitakiwa tuwe likizo lakini kwa sababu ya maslahi ya wateja wetu tumekubaliana kuendesha kesi wakati huu wa Mahakama inapokuwa likizo. Tunaomba kutoa masikitiko yetu na kesho alifika ajieleze.

JAJI: Nakubalina na wewe. Kesho aonyeshe uungwana kwa kuonyesha uthibitisho kwamba alikuwa anaumwa kabla ya kutoa ushahidi wake.

JAJI: Basi shauri linaahirishwa mpaka kesho tarehe 15 Desemba2021. Washitakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya Magereza mpaka kesho saa tatu asubuhi.

Saa 6:44 mchana, Jaji anaondoka mahakamani.

Like