Kesi ya Mbowe: Jaji aahirisha kesi hadi Jumatatu kwa ajili ya uamuzi wa pingamizi

Kama ilivyowasilishwa na ripota raia BJ leo tarehe 18 Novemba 2021.

Saa 03:33 asubuhi, Jaji ameshaingia Mahakamani. Kesi namba 16 ya mwaka 2021 ya Jamhuri dhidi Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe imetajwa kwa mara nyingine.

Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha mawakili wa Serikali.

 1. Pius Hilla
 2. Abdallah Chavula
 3. Jenitreza Kitali
 4. Nassoro Katuga
 5. Esther Martin
 6. Ignasi Mwinuka
 7. Tulimanywa Majige

Wakili Peter Kibatala anawatambulisha mawakili wa utetezi.

 1. Jeremiah Mtobesya
 2. John Malya
 3. Dickson Matata
 4. Idd Msawanga
 5. Hadija Aron
 6. Evaresta Kisanga

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji, shauri limekuja kwa ajili ya kusikilizwa na jana tulikuwa tunajibu hoja za pingamizi na tupo tayari kuendelea na majibu ya hoja.

Wakili Peter Kibatala naye anasema wapo tayari kwa ruhusa ya Jaji.

JAJI: Bwana Hilla Karibu.

WAKILI WA SERIKALI: (Pius Hilla) Asante Mheshimiwa Jaji. Naomba kujua niliishia wapi.

JAJI: Uliishia pale kwenye maamuzi kuhusiana na hoja zilizokuwa zinaendelea.

WAKILI WA SERIKALI: Nizungumzie kidogo kuhusiana na hiyo Disposal Order. Kwamba hakuna another getaway ambapo kielelezo kinaweza kutoka.

WAKILI WA SERIKALI: Na kwa kuwa kielelezo hakikuwa intendend kuwa disposed kwa maana ya disposal … Kwa namna ambayo upande wa mashitaka walikitumia, namaanisha ile administrative tuliyoitumia kwa kuomba kwa barua. Mheshimiwa Jaji, wasilisho la mwenzangu alivyowasilisha kwako kwamba proceedings za Trial Within a Trial ni bado ndani ya shauri hilo hilo, na kwa kuwa bado ipo ndani ya proceedings hizo Mheshimiwa Jaji na kwa kuwa hapakuwa na maombi au sababu kwa ajili ya ku- dispose basi knamna ilivyokuwa ilikuwa sahihi.

WAKILI WA SERIKALI: Naomba kurejea kesi ya … dhidi ya Jamhuri, ya mwaka 1996 … issue arising in a Trial Within a Trial inaweza kutumika in miner trial … Hii ku- cement hoja ya kwamba bado tupo kwenye kesi ile ile moja. Kinachotakiwa ni kuonyesha kwa Mahakama ni kwa namna gani kielelezo kimfikia shahidi. Na zile sheria au kanuni zimefuatwa. Mheshimiwa Jaji, Chain of Custody imeelezwa vizuri kwenye ushahidi, Foundation ya namna kielelezo hiki kimemfikia shahidi kimelezwa vizuri Mheshimiwa Jaji.

WAKILI WA SERIKALI: Mheshimiwa Jaji niongelee kidogo kuhusiana na powers za Deputy Registrar. Yupo sahihi kutoa kielelezo kwa sababu Mahakama ilishafanya uamuzi juu ya hatua za kufuata. Kwa maamuzi yale tayari ilikuwa ni maelekezo kwamba anaweza aka- performed majukumu yale. Hata kama siyo uamuzi wa Mahakama, ushughulikiaji wa kielelezo ni majukumu ya Deputy Registra.

WAKILI WA SERIKALI: Mazingira ya kesi yetu yalivyo ni sahihi Msajili wa Mahakama kushughulika movement ya kielelezo. Deputy Registra ndiye mtekelezaji wa amri za Mahakama. Kwa hivyo ni Mamlaka yake na jukumu lake kushughulika kielelezo kama alivyofanya. Ni wasilisho letu kwamba kama wenzetu wanakubaliana document ni authentic basi suala lingine halina nafasi.

WAKILI WA SERIKALI: Shahidi akishaonesha competence na akaonyesha imemfikiaje basi mengine hayana nafasi. Mheshimiwa Jaji, nimalizie kwa kusema kwamba kwa kutambua mazingira yote haya, kuhusu mapingamizi ya wenzetu, hakuna hoja nzito ya kuzia Detention Register kuingia hapa Mahakamani.

WAKILI WA SERIKALI: Tunaomba mapingamizi yatupiliwe mbali, kielelezo kiendelee na tuendelee na usikilizwaji wa shauri hili. Asante Mheshimiwa Jaji.

JAJI: Mmemaliza?

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Tumemaliza Mheshimiwa Jaji.

Anaamka Wakili Mtobesya.

MTOBESYA: Tumesikia hoja za wenzetu. Nitajibu in chief na baada ya hapo nitaongezea vitu vichache, kisha atakuja kaka yangu Kibatala kujibu in chief.

MTOBESYA: Nimesikia wameongea kuhusu Disposal Order, lakini sijui ni kwa kakusudi au kwa bahati mbaya, kwamba wanavyosema kwamba proceedings za Trial Within a Trial ni sawa na main case, naomba kuwasilisha mambo manne ambayo yatakuwa ndiyo mtazamo wangu kwenye hilo suala.

MTOBESYA: Kwanza Mheshimiwa Jaji, ili kufanya Trial Within Trial ni lazima Mahakama husika kwa muda isitishe proceedings za main Trial iingie kwenye zoezi la kufanya kesi ndogo. Halafu baadaye regardless ya matokeo ya kesi hiyo ndogo, Mahakama husika itarejea kuendelea na kesi ya msingi. Kwa hiyo huo ni msingi wa kwanza.

MTOBESYA: Msingi wa PILI Mheshimiwa Jaji, Trial Within Trial. Proceedings za Trial Within Trial, it’s a factual exercise ambayo inalenga ku- achieve kitu kimoja tu. Ku- prove hoja ya mshitakiwa ambaye anakuwa under trial kwa kipindi hicho.

MTOBESYA: La TATU, kama ilivyo kwenye main Trial, mwenye jukumu la kutaka kuthibitisha kama yule aliteswa au la ni prosecutions, na kama ndiyo hivyo Mheshimiwa Jaji watatakiwa ku- lead evidence ku- prove na equally kwa mashitakiwa naye atatakiwa ku- lead evidence kama alitoa maelezo kwa hiari ama la. Kwa hiyo ni proceedings zinazojitegemea Mheshimiwa Jaji.

MTOBESYA: Jambo la NNE Mheshimiwa Jaji, katika Economic Case ya 16 ya Mwaka 2021, Mahakama hii ilishaingia ku- prove voluntariness ya mshitakiwa wa pili, Adam Kasekwa, na Mahakama ikaja na maamuzi ya kinachotakiwa kufanywa kwenye statement ya mshitakiwa namba mbili. Nirudi sasa kwenye submission ya kuwajibu kaka zangu wasomi ni kwanini sisi tulidhani kwamba kwenye kesi hii kielelezo hiki ambacho mshitakiwa anaomba kukitoa kiliiingia kwenye kesi ya Trial Within Trial na kwamba kielelezo hiki kiliingia na Mahakama ikafanya uamuzi wake.

MTOBESYA: Kwanini sisi tulirejea kwenye kifungu namba 353(3) of CPA cap 20, tofauti na kaka yangu Chavula alivyokuwa anatafsiri. Kinasema kwamba Mahakama ikisharidhika, ni vyema ikatoa amri kwa kielelezo hicho kutoka, itafanya hivyo baada au wakati Mahakama ikiendelea. Labda nisome.

(Wakili Mtobesya anasoma sasa).

MTOBESYA: Kwa hiyo sisi tulienda kwenye kifungu hiki tukijua kwamba kwa kuwa kielelezo hiki kilishatumika kwa kesi ya Adam Kasekwa, kwa kuwa kilishatumika kwenye different court proceedings, na kwamba kwa kuwa kilishaamriwa kwenye suala la hiari ya maelezo ya mshitakiwa wa pili, basi wao walipaswa wa- move Mahakama iweze kutoa kielelezo hicho.

MTOBESYA: Sasa wenzetu hawakufanya hivyo Mheshimiwa Jaji. Sisi tuna- submit kwamba kuna hatua za kisheria wameziruka. Kwenye sehemu E sehemu CAP 20 ndiyo inahusu Disposal of Exhibit. Mheshimiwa Jaji haihitaji kuzunguka sana kuhusu hoja hiyo. Kitu kikishaingia mahakamani procedure yake ya kukitoa ni ile ile kama ilivyokiingiza. Hiyo ni ‘court order.’

MTOBESYA: Na ukisoma kwa namna hii utagundua ni njia pekee ni ya ‘Court Order’. Kwa hiyo tunachokiona sisi waliruka utaratibu wa kupata kielelezo kwa Mahakama kujiridhisha sababu lazima pawe na maombi mbele ya Mahakama. Wenzetu hawajakisoma kifungu hiki vizuri wakaielewa. Sasa wakati wenzetu wana- submit walitaka kuonyesha kwamba proceedings hizi ni zile zile.

MTOBESYA: Logic ndogo sana mbona? Kwamba shahidi PW1 kwenye kesi hii ndogo, kule kwenye kesi ya msingi ni PW8. Na Mahakama ikirejea anarudi kuwa PW8 na ni kwa sababu shauri ni tofauti.

MTOBESYA: Hatuwezi kusema ni kesi moja hii. Niliwasikia wenzetu, especially kaka yangu Chavula, kwamba PW1 alipokuwa anaomba kielelezo, Mahakama iliwaruhusu wapewe. Bila kuingilia kilichofanyika, basi ni ukiukwaji mkubwa sana wa taratibu za Mahakama.

MTOBESYA: Kama walikuwa na ‘order’ ya kuomba kielelezo, hawakupaswa kuomba kwenye proceedings hizi, ni ukiukwaji mkubwa wa taratibu na Mahakama isingeweza kuombwa kitu ambacho kimechukuliwa kwenye proceedings zingine, na kama kweli walifanya hivyo, basi taratibu zingefuatwa kwa mujibu wa (section) 353 na mwongozo wa Mahakama. Na kaka zangu hawa ni mawakili wasomi, siwezi kuwafundisha. Lakini hilo halikufanyika na kama kilifanyika basi kimekiuka utaratibu ninaousema.

MTOBESYA: Pia Mheshimiwa Jaji, kama kweli proceedings hizi ni sawa, kwanini wanaomba Mahakama ipokee tena kwa mara ya pili kwenye shauri hili kama proceedings zote ni sawa na kesi ni ile ile? Na kitendo cha wao kuomba ipokelewe tena na Mahakama ni ushahidi tosha kwamba hili ni shauri tofauti.

MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji, kwenye hilo naomba kuishia hapo. Atakuja kumalizia kaka yangu Kibatala kama kuna kitu sijataja. Sababu walizotoa kupinga mapingamizi yetu zinakosa mashiko. Hivyo tunaomba isizigatie kabisa hoja zao zisizo na mashiko.

MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji naomba niende kwenye suala la PILI, kwamba Mahakama inakuwa ‘Funtus Officio’. Wakati wenzetu wanawasilisha wanaona suala la Mahakama kuwa ‘Funtus Officio’ kwa njia tofauti, kwamba wakati wa uamuzi wa Mahakama unatolewa Mahakama ilisema kwamba kielelezo kipo competent, relevant na material.

MTOBESYA: Kwamba PWI aliomba kuingia kama ID na PW2 anaomba kiingie kama kielelezo. Nadhani hawakuelewa suala la pingamizi letu. Labda nirudie kidogo. Mahakama ilishaitwa kusema jambo au kupokea exhibit hii. Na katika suala hilo Mahakama ilisha exercise haki yake ya kusema katika suala hilo. Na uamuzi wa Mahakama exhibit was rejected, ndiyo maana tunasema Mheshimiwa Jaji kwamba mwaliko huu wa mara ya pili kwamba Mahakama iseme tena lolote ni ukiukwaji wa taratibu, na unakuwa ukiukwaji kwa falsafa ya ‘Funtus Officio’.

MTOBESYA: The Court if Funtus Officio ilishafanya maamuzi, it’s done, kwamba wanachokifanya wenzetu ni kwamba Mahakama ilishakataa inaomba iangalie tena. Kibatala ananinong’oneza kwamba inakuwa ni review ambayo haijafuata utaratibu. Hapo ndipo tunasema wenzetu hawakuelewa maana ya ‘Funtus Officio’. Chavula anasema kwamba PW1 aliomba iingie kama ID na PW2 anaomba iingie kama exhibit. Mheshimiwa Jaji, Mahakama ilishasema kwamba procedure ni zile ile tunafunga tuna jambo ambalo Mahakama ilishatolea maamuzi.

MTOBESYA: Sasa kuna kesi walirejea hapa kaka zangu wasomi, Mawakili wa Serikali, ya NIBURO COSMAS kwamba sisi tumekosea kulinganisha parameters, kwamba Mahakama imepewa mamlaka ya kuamua kesi ni ‘Funtus Officio’ pale ambapo Mahakama inakuwa inasajili kesi nyingine. Mheshimiwa Jaji, Mahakama inakuwa Funtus Officio pale ambapo Mahakama inakuwa imemeliza jambo fulani, siyo lazima kesi nzima.

MTOBESYA: Kwenye kesi tuliyoitumia jana ilikuwa overruled kwa sababu ilikuwa Funtus Officio ndiyo maana wakaendelea mpaka Mahakama ya Rufaa. _The court can’t go back, the court if Funtus Officio iwe kesi imeisha au haujaisha, lakini hapa kuna jambo ambalo Mahakama imeshalitolea uamuzi, kwamba kesi mpaka ifike mwisho siyo hoja ya msingi.

MTOBESYA: Sasa Mheshimiwa Jaji niishie hapo kwa kusema kwamba wenzetu hawakuelewa namna ambavyo falsafa hiyo ya Funtus Officio inavyofanya kazi.

MTOBESYA: Kwa sababu hiyo basi tunaomba basi Mahakama ikute kwamba haiwezi kuamua jambo hilo mara ya pili, na wakati Mahakama inafanya uamuzi zipatie uzito hoja zetu kwa kiwanho hicho. Mheshimiwa Jaji samahani kidogo…

(Mtobesya anateta kidogo na Peter Kibatala).

MTOBESYA: Mheshimiwa Jaji, kuna kesi ya Khatibu Gandhi aliyosoma kaka yangu Hilla, kwamba unaweza kutumia hoja za Trial Within Trial katika main case. Sivyo alivyotaka kutuaminisha kaka yangu Hila. Hoja ya kesi hii ni kwamba baada ya uamuzi wa kesi ya Trial Within Trial inaweza kutumika kama ushahidi katika main case. Kwa hiyo rejea hii ipo out of context. Haina uhusiano na kilichopo Mahakamani.

MTOBESYA: Kwa sababu hiyo naomba nimalizie hapo na nimuachie kaka yangu Peter Kibatala. Asante Mheshimiwa Jaji.

Anaamka Peter Kibatala.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji kwa ruhusa yako naomba niendelee hapo ambapo kaka yangu Mtobesya amemalizia. Kwa kweli ni mazingira tofauti kabisa na kesi hii.

KIBATALA: Hakuna sehemu yoyote katika shauri lile ku- ‘trans-exhibit’. Palikuwa hakuna kama wanachotaka kufanya wao hapa Mahakamani. Mheshimiwa Jaji, nirudi kule kwenye Disposal Order kama nilimuelewa Mr Chavula kama sijamuelewa atanisamehe. Anasema hatujashambulia kielelezo. Sasa kama hatujashambulia kielelezo tunafanya nini hapa?

KIBATALA: Hili siyo zoezi la ‘nomenclature’. Kwamba uamuzi ulikuwa juu ya shahidi siyo kielelezo, kwani wao walikuwa wa naomba shahidi aje…? Au walikuwa wanaomba kielelezo kuingia? Hapa katika suala la Chain of Custody, ni kwamba haikufuatwa kwa sababu mahakamani hakuna jambo linalofanyika kiholela.

(Peter Kibatala anasoma mwongozo).

KIBATALA: Kama tulivyowasilisha, walikuwa na nafasi tangu mara ya kwanza, kwamba kama watakitumia walipaswa kuomba _Disposal Order._Wanajiwekea sheria zao wenyewe na kurekebisha vifungu.

KIBATALA: Kama palikuwa na maamuzi ya Mahakama, ambapo maamuzi yakapelekea kupatikana kwa barua, hiyo haihalalishi kielelezo ambacho kimefika Mahakamani bila Disposal Order. Kwa bahati mbaya hakuna sehemu hata moja Wakili wa Serikali ametoa sheria wala sheria kesi kwamba Naibu Msajili anaweza kumkabidhi mtu yoyote yule kielelezo cha Mahakama.

KIBATALA: Iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi, na kupitiwa siyo dhambi kabisa. Wenzangu wanatumia uamuzi wako kwamba uliwafanya wafanye walichofanya. Hapana hakuna sehemu umesema Naibu Msajili aandike barua. Tunachojua Mahakama ilitupilia mbali kielelezo. Na sasa wanacho bila kufuata sheria na Chain of Custody.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, wakati nawasilisha kwa kutumia Mwongozo wa Jaji Mkuu, na walitaka kuukosoa lakini wakawa waangalifu.

WAKILI WA SERIKALI: (Abdallah Chavula) Objection Mheshimiwa Jaji. Ananichonganisha. Mie sikukosoa.

KIBATALA: Sawa. Siyo Big issue. Na wakati Hila anaongea alitaja kesi ya Gede ambayo ni ya mwaka 2017 na Mwongozo wa Mahakama ulitolewa mwaka 2020. Na hakuna Sehemu waliyosema kwamba kuna mgongano kati ya Mwongozo na Sheria au sheria kesi yoyote.

KIBATALA: Na ndiyo maana Jaji Mkuu wa sasa anasema alitoa Mwongozo kwa ajili ya kuleta ‘harmony’.

(Kibatala anasoma maneno ya Jaji Mkuu kuhusu suala la DISPOSAL ORDER).

KIBATALA: Na mwisho kabisa Jaji Mkuu amezungumzia suala la Exhibit Register. Na sijasikia wakili hata mmoja anazungumzia suala la Exhibit Register, na kwamba swaliu ni nani alitoa DISPOSAL ORDER.

KIBATALA: Hakuna mahala popote ambapo Mahakama hii ilifanya Disposal Order na kwamba wao wanasema kwamba ni suala la utawala. Ni sheria ipi imesema kwamba Disposal Order ni suala la kiutawala? Mheshimiwa Jaji, pia wamezungumzia suala la Gede Kondo kuhusiana na competence ya shahidi. Sasa shahidi mwenyewe hajafikia hata kwenye cross examination.

KIBATALA: Kwa hiyo kesi ya Abasi Gede Kondo ni rejea tofauti na haina uhusiano na kesi hii. Mheshimiwa Jaji, nakumbushwa kuhusu barua ya Naibu Msajili. Sisi tunasema kwamba alitakiwa kuandika barua ile baada ya kutolewa Disposal Order. Suala la mamlaka yake yatapimwa na taratibu za kisheria. Sisi tunashughulikia suala kuingia kwa exhibit. Hayo ya mamlaka yake siyo ajenda yetu. Kuna wakili wa Serikali amesema kwamba zoezi la kuingiza ID ni sawa. Hakuna. Kwamba wao walivyokuwa wanataka PW1 aingize ID ilikuwa ni sawa na hakuna.

KIBATALA: Sijui kama alikuwa serious au anatania. Nani alileta suala la ‘HAKUNAISM’ hapa Mahakamani? Mheshimiwa Jaji, pia suala la falsafa (doctrine) ya Estoppel. Kuna sehemu wenzetu wamesema kwamba siyo lazima kuitumia. Sasa kwanini palikuwa na hiyo falsafa ya Estoppel?

KIBATALA: Na wamesema kwamba kwenye kesi ya Issa Tojo Mahakama haikutumia despite walitaja tu. Nani kasema?

(Peter Kibatala anasoma uamuzi wa kesi anayoirejea).

KIBATALA: Kwa kutumia ‘Falsafa ya Estoppel’, na Principle of Estoppel inaweza kutumika wakati wa kesi au kabla ya kesi. Kesi ya Julius Michael pia walitumia Principle ya Estoppel ukurasa wa saba.

KIBATALA: Kwamba Kanuni ya Estoppel inatajwa. Kama unazungumzia specific issues basi kanuni hii lazima itumike. Na kwamba tunawasilisha kwamba kesi hii ipo sahihi. Msomi Pius Hilla alisema kwamba admission ni kitu kimoja na disposal ni kitu kingine. Sisi tunasema pamoja na kanuni tatu za Relevance, Competence na Veracity lakini hakuna ‘Paper Trade’.

KIBATALA: Mheshimiwa Jaji, tunawasilisha kwamba kama hawakuomba Disposal Order hawawezi kupata exhibit. Wakiomba wanapata wala hakuna njia ya mkato hapo. Tunakazia mapingamizi yetu. Asante Mheshimiwa Jaji.

(Kibatala anakaa).

JAJI: Nimesikia hoja zenu. Ninajaribu kutafakari kabla sijaamua kupanga maamuzi yawe lini na saa ngapi. Ningeomba dakika kumi nifanye tathimini kisha nitarejea kusema uamuzi ni lini.

Jaji anaondoka kwenye chumba cha mahakama.

Baada ya dakika kumi Jaji amerejea Mahakamani. Kesi namba 16 ya mwaka 2021 yA Jamhuri dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa tena.

WAKILI WA SERIKALI: (Robert Kidando) Mheshimiwa Jaji upande wa mashtaka tupo wote isipokuwa Mr Pius Hilla alitoka kidogo.

Wakili Peter KIBATALA: Mheshimiwa Jaji sisi quorum yetu ipo kama awali tupo tayari kusikiliza maamuzi.

JAJI: Nimefanya tathimini na uwezekano wa kusema mpaka kesho asubuhi utakuwa ni mgumu. Badala yake tuje Jumatatu ya tarehe 22 Novemba 2021. Shahidi unaombwa kurudi Mahakamani. Washitakiwa wataendelea kuwa Chini ya Magereza mpaka tarehe 22 Novemba 2021 Jumatatu saa tatu ssubuhi.

JAJI: Nawatakia week end njema.

Jaji anaondoka mahakamani.

Like
1