Ijue historia fupi ya Ronaldinho

LEO tunakuletea historia fupi ya mchezaji maarufu na mstaafu wa mpira wa miguu wa kulipwa ambaye wengi tunamjua kama Ronaldinho Gaucho.

Mnamo mwezi March 21,1980 huko Porto Alegre Brazil alizaliwa staa wa mpira wa miguu Ronaldo de Assis Moreira (Ronaldinho Gaucho).

Baba yake mzee Jóao Moreira alikuwa mchomelea vyuma wakati mama yake (Miguelina de Assis Moreira) akiwa muuza vipodozi wa kawaida kabla ya kuwa muuguzi.

Ronaldinho alizaliwa kwenye familia iliyopenda mpira kwani kabla ya kuchomelea vyuma na kuwa mlinzi (watchman) katika uwanja wa Grémio, Jóao ( baba ya ake) alikuwa mchezaji wa mpira . Mzee Jóao alifariki Ronaldinho akiwa na umri wa miaka 8.

Roberto de Assis Moreira ni (kaka yake Ronaldinho ambaye ndiye alikuwa meneja wake katika soka) alicheza katika club ya Grémio na alikuwa tegemeo kwa familia yake kwani waliamini ataweza kucheza vilabu vikubwa na kuikomboa familia katika wimbi la umaskini.

Haikuwa bahati kwao kwani Roberto alipata jeraha la goti lililopelekea kuharibu maisha yake ya soka. Pia ana dada yake anayefahamika kwa jina la Deisy.

Ronaldinho alipewa jina hilo( Ronaldinho) kutokana na udogo wake kimuonekano huku alicheza na watu waliomzidi umri na miili pia.

Akiwa na umri wa miaka 13 aliwahi kupata umaarufu kwa kuifungia klabu yake ya nyumbani magoli 23 kwenye ushindi wa 23-0.

Alipoanza kuchezea klabu kubwa, alikuta mtu mwingne mwenye jina la Ronaldo ambalo ndilo jina lake halisi. Hivyo aliamua kutumia Ronaldinho kama wengi walivyozoea kumuita.

Ronaldinho alianza mpira wa kulipwa katika club aliyocheza utotoni (Grémio) 1998 akiwa na umri wa miaka 20 akifunga magoli 47 kabla ya kujiunga na miamba wa Ufaransa Paris Saint – Germain akifunga magoli 17 na baadaye Barcelona 2003.

Akiwa Barcelona nyota yake iling’aa zaidi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusakata kabubumbu huku akiwachenga wapinzani wake kwa mitindo ( style) za aina yake.

Wengi walipenda umahili wake kwani hata ambao hawakuwa mashabiki wa timu yake walimpenda yeye.

Akiwa Barcelona aliweza kunawili na Kufika kileke Cha unawili kwani Ronaldinho alicheza kwa misimu mitano (5) akifanikiwa kushinda kombe la (La liga) mara mbili (2) na Champions league Mara moja 1(), Ballon d’Or 2005 pamoja na FIFA World Player Of The Year.

Mbali na mafanikio hayo , Ronaldinho alishinda Kombe la Dunia na timu yake ya taifa Brazil mnamo mwaka 20002 akiwa pamoja na wachezaji nguli kama Ronaldo na Rivaldo.(Na Makonbe mengine 97 akifunga magoli 33) Akiwa Barcelona alifunga magoli 70.

Mnamo 2008 -2011alihama kuichezea klabu ya AC Milan huku akifunga magoli (20). 2011-2012 Akiwa Flamengo akifunga magoli (23), Atletico Mineiro 2012-2014 akiwa na magoli ( 20) na baadae (Quertaro) na (Fluminense). Timu zote za mwisho alicheza akiwa kwao Brazil.

Ronaldinho alikaa kwa miaka miwili (2) bila klabu yoyote hadi alipoamua kustaafu soka la kulipwa mnamo mwaka 2018.

Ronaldinho anakadiliwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani $90 million zaidi ya billion mia mbili na million mia saba za kitanzania ( 208,710,000,000.00 TZS).

Alimuoa “Janaina Nattielle Mendes” amabye alikuwa mtangazaji wa vipindi vya televisheni Brazil. Walifanikiwa kupata mtoto wa kiume “Jóao de Assis Moreira” ambaye alimpa jina la baba yake mzee Jóao Moreira.

Katika mahojiano na vyombo vya habari, Ronaldinho aliwahi kusema kuwa baba yake aliamini yeye atakujakuwa mchezaji hodari wa mpira kuliko kaka yake Roberto, jambo ambalo alifanikiwa.

Hii ni historia iliyofupishwa ya mchezaji hodari wa kabumbu Ronaldinho Gaucho.

Like
7