Huu ndio mwisho wa enzi za Barcelona?

KLABU ya soka ya Barcelona ‘haiwezi kuwasajili’ rasmi nyota wake wapya kutokana na wakati mgumu wa kifedha inaoupitia.

Klabu hiyo ina tatizo kubwa la kifedha na imeripotiwa kuwa mpaka sasa tatizo hilo linafikia Euro milioni 200. Barcelona imeshindwa kuwasajili rasmi kwenye La Liga, nyota wake wapya ambao ni Depay, Eric Garcia, Sergio Aguero na Emerson lakini na imeripotiwa kuwa hii ndio sababu kuu inayopelekea ‘kusuasua’ kwa dili jipya la kuongeza kandarasi ya Leo Messi kwa miaka miwili zaidi baada ya kandarasi yake kumalizika.

Utafiti kwenye masuala ya kifedha uliofanywa na Ruben Uria na Andria Soldevilla kutoka Goal Espana klabuni hapo, umethibitisha kuwa hali ya kifedha ya timu hiyo imefikia pabaya sana na kuieleza hali hiyo kama ‘sinema ya kutisha’.

Ili kutokiuka sheria ya mishahara ya La Liga, Barcelona hawana budi kupunguza mishahara ya wachezaji wake, inayofikia kiasi cha Euro milioni 200 ili kuweza kuwasajili rasmi wachezaji wake wapya. Katika juhudi za kupunguza mishahara hiyo, wachezaji kama Konrad de la Fuente, Jean-Clair Todibo na Francisco Trincao tayari wameondoshwa klabuni hapo ingawaje wachezaji wengine wengi watapaswa kuondoshwa kwa haraka ili kukata kiasi kikubwa cha mishahara klabuni hapo.

Baadhi ya wachezaji ambao Miamba hao wa Ctalunya wanataka kuwaondosha kwa ‘udi na uvumba’ ni Samuel Umtiti, Miralem Pjanic na Philippe Coutinho, ambao mpaka sasa hamna kabu iliyoonyesha hamu ya kuwahitaji kutokana na mishahara yao kuwa mikubwa.

Tatizo la pili ni kwamba hata kama timu hiyo itafanikiwa kuwaondoa wachezaji hao kutoka klabuni hapo, mishahara itapungua kwa jumla ya Euro milioni 64 ambayo ikiongezwa kwa wachezaji waliokwisha aga klabuni hapo (Konrad, Todibo,Trincao, Junior na Mathews) itafikia jumla ya Euro milioni 89 tu ambayo pia haitoshi kwani ili kutokiuka sharia za La Liga, ni asilimia 25 pekee ya pesa hiyo, inayopaswa kuwekezwa kwenye ununuzi na usajili wa myota wapya.

Hii yote ina maana kuwa wachezaji zaidi wa timu hiyo watapaswa kuondoshwa na tayari kuna minong’ono kuwa Barcelona wapo tayari kumuuza Antoine Griezmann na huku tetesi za PSG na Manchester City kumtaka Messi zikirejea kwa kasi.

Ni Shida!

Like
1