Hivi ndivyo serikali ilivyohujumu uchaguzi wa serikali za mitaa

Uchunguzi wangu umeonyesha kuwa hatua za kuharibu uchaguzi serikali za mitaa ulikuwa na hatua zifuatazo:
1. Maafisa wasaidizi wa kata waliagizwa na wakuu wa mikoa na wilaya, kuwashawishi wenyeviti wa vijiji, vitongoji na mitaa wa upinzani hasa Chadema, waunge mkono juhudi na kujiunga na CCM. Wakifanya hivyo watapewa fedha au nafasi ya kugombea endapo uchaguzi utafanyika.
Jitihada hizi hazikuzaa matunda makubwa.
2. Zilichapishwa fomu za aina mbili, feki na halisi. Maafisa waliagizwa watoe fomu feki kwa wagombea wa upinzani na fomu halisi kwa CCM. Feki hazikuwa na nembo ya Halmashauri.
Wapinzani walizigundua na kuzikataa. Ndipo amri ikatoka kuwa wote wapewe fomu halisi.
3. Zikaandaliwa fomu feki za kiapo cha maadili ya uchaguzi. Zikagundulika na kukataliwa. Wakurugenzi wakasisitiza kwa watendaji kuwa ni muhimu sana kuwaondoa wapinzani kwa sababu wanakubalika sana.
4. Ahadi ikatolewa kuwa Afisa atakayeokoa kijiji atapata 100,000/= na kitongoji/Mataa ni shiling 50,000/=. Wakuu wa Mikoa na Wilaya pia walikuwa na viwango vyao kwa vijiji na vitongoji watakavyookoa kwa kuengua wapinzani.
5. Wagombea wa CCM waliambiwa warejeshe fomu zao mapema, kisha maafisa wakaagizwa wajifiche. Endapo watabaini uwepo wa uvunjifu wa amani, wapokee fomu zote na kuzipeleka Halmashauri kwa ushauri zaidi.
6. Zilipofika Halmashauri, maafisa wasaidizi walifungiwa mahali pa siri na wakurugenzi waliingia kwa kificho (maana hawahusiki), na kuanza kuelekeza namna ya kuwatafutia sababu wapinzani ili waenguliwe. Kwa mfano, kwenye fomu palipoandikwa WILAYA, wao waliongeza neno “ya” kwa fomu za wagombea wa CCM na fomu za wapinzani zikaonekana hazina neno hilo na kikawa kigezo cha kuondolewa. Hali kadhalika maneno KATA, KIJIJI, n.k yaliongezewa maneno “cha”, “wa”, nk, wapinzani wakaonekana hawajui kujaza wilaya, kijiji, kata au mkoa.
7. Kwa baadhi ya wagombea wa upinzani waliokataa kuacha fomu zote za watendaji, ile waliyokabidhi ilinyofolewa fomu ya katikati na kuipoteza kisha uamuzi ukachukuliwa kuwaengua kuwa fomu zao hazikukamilika.
8. Kuhusu rufaa, leo 6/11/2019 limetoka agizo lenye vipengele vifuatavyo:
Watendaji wasionekane kupokea rufaa. Watakaoonekana wapokee lakini uamuzi umeishafanyika kwa maagizo yaliyo Halmashauri lakini watendaji hawakuambiwa ni yapi.
Kwa kuwa ni wao waliowaengua wapinzani, hawawezi kuwarudisha kwa sababu utakuwa ni ushahidi kuwa waliwaonea.
Kudhihirisha ukweli kuwa hakuna rufaa itakayobadili matokeo, watendaji wote leo wamepokea fedha zao za kukomboa vijiji na vitongoji. Hawawezi kupokea fedha halafu kijiji kikarudi.
Kwa hiyo kukata rufaa ni kupoteza wakati na Waziri Jaffo anatumika kutuliza hasira za watu.
Msingi wa maagizo ya boss ni kuwa, kuliko kupoteza fedha kufanya uchaguzi, afadhali awazawadie watendaji fedha za kuengua wapinzani ili uchaguzi usifanyike.
Like
1

Leave a Comment

Your email address will not be published.