Hivi ndivyo Bashite, Ikulu walivyomponza Askofu Malasusa

Na Mwandishi Wetu

NGUVU iliyosababisha usaliti wa Askofu Dk. Alex Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), ambaye ametengwa na Baraza la Kuu la maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), imejulikana.

Kanisa lilifanya uamuzi wa kumtenga katika kikao cha maaskofu kilichomalizika Jumanne tarehe 24 Aprili 2018 mjini Arusha, Tanzania. Kwa kutengwa kwake huku, Askofu Malasusa ameondolewa katika kamati zote za maaskofu wa KKKT, na hawezi kushiriki vikao vya maaskofu. Anabaki kuwa “mtu wa Dar es Salaam tu.”

SAUTI KUBWA ina taarifa za uhakika kuwa mbali na udhaifu wa dhamiri yake mwenyewe, waliomponza Askofu Malasusa ni pamoja na Paul Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam (ambaye jina lake halisi ni Daudi Albert Bashite), na maofisa kadhaa wa Ikulu waliokuwa wanahaha kutengeneza mgawanyiko katika kanisa, ili waraka wa maaskofu uonekane si wa kanisa zima, na ukose mvuto kwa umma.

KKKT liliandika waraka maalumu wa maaskofu uliobeba ujumbe wa Pasaka kwa waamini na Watanzania wote mwaka huu, ukiwataka kuzingatia amani, na kuitaka serikali iwajibike kulinda amani ya raia wanaotekwa, wanaoteswa, na wanaouawa na “watu wasiojulikana,” ambao serikali imegoma kuwachukulia hatua. Serikali, hasa Ikulu, haikufurahishwa na waraka huo.

Kwa nguvu ya Makonda na maafisa hao, Askofu Malasusa alipuuza makubaliano ya kanisa yaliyotaka kila askofu asambaze waraka huo na kuusoma katika makanisa yaliyopo kwenye dayosisi yake siku ya Jumapili ya Matawi (Mitende).

Kilichotokea kati ya Ikulu, Bashite na Askofu Malasusa

Tarehe 24 Machi 2018, Jumamosi, (ambayo waraka ulitoka ili usomwe makanisani kesho yake Jumapili ya Mitende), Askofu Malasusa alikuwa na kikao kirefu na Bashite na maafisa wawili kutoka Ikulu.

Kikao kilifanyikia ofisini kwake. Baada ya kikao hicho, ambacho kiliisha usiku, maafisa wa Ikulu walifuata wahariri wa gazeti la UPENDO – linalomilikiwa na KKKT – na kuwataka waondoe habari iliyohusu waraka wa maaskofu, na waraka wenyewe ambao ulikuwa umechapishwa ndani ya gazeti.

Wahariri hawakukubaliana nao, bali walieleza maofisa wa Ikulu kuwa gazeti lilikuwa limeshapelekwa kiwandani, hivyo hawakuwa na njia nyingine ya kuondoa habari au waraka huo.

Wahariri walijitetea wakisema kwamba hata kama wangefanikiwa kuondoa habari hiyo na waraka, bado ingeweza kutoka kwenye magazeti mengine, na wao wangeonekana ni wasaliti.

Maafisa wa Ikulu walisema bora habari iandikwe na magazeti mengine, lakini gazeti la kanisa lisiwe nayo. Baada ya ubishi huo, maofisa hao walielekea kiwandani. Wanajua walivyofanya, wakachomoa habari hiyo na waraka wa maaskofu uliokuwa umewekwa gazetini.

Hatua hiyo ilihakikishia Ikulu kwamba kwa kuwa gazeti la kanisa halikutaja waraka huo, basi hata nguvu na athari ya waraka huo ingepungua.

Usaliti wa Askofu Malasusa ulileta taharuki katika kanisa hilo na kwenye jamii, huku serikali ikijitahidi kupotosha umma kwamba “waraka ule si wa kanisa bali ni maoni ya maaskofu wachache.”

Wachambuzi wa masuala ya dini wanasema kuwa kitendo cha Askofu Malasusa kutii mamlaka ya mkuu wa mkoa na kuzuia salaam za maaskofu, ni ukiukaji wa kiapo cha uaskofu wake kwa sababu “amemtii mwanadamu kuliko Mungu,” na kwamba  alijisafisha mbele ya Kaisari badala ya kujiweka mbele ya Mungu.

Siku ya uwekaji jiwe la msingi la uwanja wa ndege (Terminal Three) Dar es Salaam, Askofu Malasusa aliingia uwanjani hapo kwa gari la Ikulu lenye kimulimuli akitokea Mabibo alikokuwa amekwenda kufungua mkutano wa akina mama wa KKKT.

Ikulu ilimtumia gari limuwahishe kwenye tukio kwa sababu ya kuhofia kuwa msongamano wa magari barabarani ungeweza kumsababisha achelewe. Katika tukio hilo, mbele ya Askofu Malasusa na viongozi wengine wa dini, Rais John Magufuli aliwataka “maaskofu waombee viwanda badala ya kuandika nyaraka.”

Kwa uamuzi wa KKKT kumtenga Askofu Malasusa, kanisa limejenga heshima na kuhakikishia waamini na wananchi kuwa lipo imara, lina kauli moja isiyotetereka, na kwamba ujumbe wa waraka wa maaskofu upo pale pale kama kauli ya kitume na kinabii ya kanisa.

SAUTI KUBWA haikufanikiwa kujua “kifungo” cha Askofu Malasusa kinamalizika lini, lakini msaidizi wake ndiye anatarajiwa kuwa msimamizi wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Hata hivyo, baadhi ya wachungaji wa DMP wanasema kuna tetesi kuwa Askofu Malasusa anatafakari jinsi ya “kuondoa dayosisi yake katika KKKT.” Baadhi yao wanasema iwapo atafanya hivyo atakuwa amejitangaza rasmi kuwa “askofu wa serikali” badala ya kuwa askofu wa kanisa.

Like
101
11 Comments
  1. Daimon Mkocha 7 years ago
    Reply

    shetani humpa mtu hofu naye ikimuingia basi shetania anakua ameshinda ndicho kinachotokea kwa Dr Alex Malasusa

    1

    2
  2. Bichwa kubwa 7 years ago
    Reply

    Nchi sasa tunawahitaji watu kama ninyi kuikomboa na mikono ya mhutu, na sasa nimeamini kuwa huyu kiumbe hana damu ya kitanzania. Watanzania wa damu hawana roho kama ya huyu mtu. Na kwa nini atumie nguvu nyingi kuminya ukweli, haki na kupotosha watu kuwa anafanya mema?

    Ina maana vilio havisikii jinsi watu wanavyomzungumzia vibaya anashindwa kujirekebisha? Huyu rais tumeshajua ukweli sio damu ya kitanzania.

    3

    0
  3. Mzalendo 7 years ago
    Reply

    Ama Hakika viongozi waliompendekeza magufools awe rais wa nchi yetu walaaniwe wao pamoja na vizazi vya 40….mtu anaiuza nchi kwa mnyarwanda alaf wanamuangalia…

    2

    0
  4. Revocatus 7 years ago
    Reply

    Vizuri sana

    0

    0
  5. Shombokya 7 years ago
    Reply

    Aisee! Inasikitisha sana jamani, Yani ni Shetani aliyekalia kiti cha Musa.
    Kweli unamtii Binadamu kuliko Mungu?
    Unamwogopa Binadamu kuliko Mungu!
    Shetani aliyesimama kwa Waliteri mwaka huu ni hatari. Mimi namfahamu vizuri, hata Ndg zake pua, Imani si kitu kwao bali vitu

    3

    0
  6. Shombokya 7 years ago
    Reply

    Aisee, ni aibu kubwa hii jamani!
    Mimi yani hata sielewi, kweli Mtu mzima km huyu anamtii Makonda kuliko Mungu? Magufuli kuliko Mungu!
    Kweli Kanisa linaingia katika kali ngumu kiimani. Lkn ataja ona, kuna siku ataliona hili.

    2

    0
  7. Mange Kimambi 7 years ago
    Reply

    Magu ni mpumbavu kabisa

    1

    0
  8. mtima nyongo 7 years ago
    Reply

    tumekua na watawala wapuuzi kuliko awamu zote zilizopita,

    0

    0
  9. malcom 7 years ago
    Reply

    mwandishi kuna lile tukio la kutaja watu waliotelekeza watoto… katika list ya viongozi wa dini MALASUSA alikuwepo… na hiyo ndo hold walionayo juu yake. ungefuatilia vizuri kupata info.

    1

    0
  10. Mtanzania 7 years ago
    Reply

    Kuna kitu hapo. Makonda kamtisha askofu kwa namna moja au nyingine.

    1

    0
  11. Tongwa chungu 7 years ago
    Reply

    Pumbavu kabisa

    0

    0

Leave a Comment

Your email address will not be published.