NCHINI Rwanda, viongozi wa juu pekee wenye hadhi ya kuwa na gari la serikali la zaidi ya 2000cc ni ni rais, waziri mkuu, spika wa bunge, spika wa seneti na mkuu wa mahakama ya juu.
Gari yenye 2000cc (mfano Toyota Innova) hutumia lita 12.5-14/100km katika mizunguko ya mjini, wakati katika barabara kuu inaweza kwenda hadi lita 8-10/100 km.
Mawaziri na maofisa wengine wakuu serikalini hupewa mikopo ya kununua magari wanayotaka wao na posho za kudumu kwa ajili ya matengenezo.
Rwanda ina mawaziri 30. Mawaziri hawapati magari ya serikali au magari ya kuongoza misafara yao wakiwa katika shughuli za serikali. Tabia hiyo ni kosa la jinai.
Mtu anapoteuliwa kuwa waziri, anapewa gari la serikali ambalo waziri atakopeshwa na atalitumia wakati akilipia taratibu (kutoka katika mshahara wake).
Waziri atatakiwa kuajiri dereva ambaye atakuwa anamuendesha katika shughuli zake za serikali, lakini dereva huyo atalipwa mshahara wake na waziri.
Rais, waziri mkuu, spika wa bunge, spika wa seneti na mkuu wa mahakama ya juu ndio pekee wanaruhusiwa kutanuliwa njia barabarani ili wapite.
Wengine wote waliobaki, watatakiwa kutumia barabara kama wananchi wengine. Si mkuu wa majeshi, mkuu wa polisi, waziri au mke na mtoto wa kiongozi.
Ukiwa Rwanda, unaweza kukaa mwezi mzima hujasikia king’ora. Utakisikia iwapo watu wanne hao wanapita, au kama ni ambulance imebeba mgonjwa. Sheria zinafuatwa kweli kweli.
Kwetu Tanzania, hata waziri wa fedha au waziri wa mambo ya nje au mkuu wa jeshi la polisi – wakati mwingine hata wabunge tu – wanatembea barabarani wakiongozwa na ving’ora. Ni ufisadi na kuchezea raslimali na sheria za nchi.
Ni.ajabu kwamba hata katika jambo dogo hivi, Tanzania bado inahitaji kujifunza Rwanda.