Ufisadi serikalini waota mizizi chini ya Magufuli

Na Mwandishi Wetu

MWAKA wa kwanza wa utawala wa Rais John Magufuli “uliotesha” ufisadi mkubwa serikalini kuliko awamu iliyomtangulia ya Rais Jakaya Kikwete.

Ukweli huu unapatikana katika uchambuzi mfupi uliofanywa na Dk. Marcossy Albanie kuhusu matumizi ya fedha za umma, kwa mujibu wa taarifa ya mdhibiti na msimamizi mkuu wa hesabu za serikali (CAG).

Dk. Albanie ni mkurugenzi wa taasisi ya kiraia ya kufuatilia mwenendo wa Bunge, Citizens Parliamentary Watch NGO.

Katika mwaka wa kwanza wa uongozi wake (2016/2017), serikali ilipata hati chafu tatu. Kabla ya hapo, mwaka uliotangulia, wakati wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete (2014/2015), serikali haikuwa imepata hati chafu.

Vile vile, hati zisizoridhisha ziliongezeka kutoka moja (2014/2015) hadi mbili katika mwaka 2016/2017.

Hati zinazoridhisha zilipungua kutoka asilimia 91 (2014/2015) hadi 86 katika mwaka 2016/2017. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, ukurasa wa xvii. Kutokana na hali hii, Dk. Albanie anasema hii ni aibu kwa serikali.

Anasema: “kitendo cha taasisi za serikali, wizara, idara na serikali za mitaa kuendelea kupata hati chafu, zenye mashaka na zisizoridhisha miaka zaidi ya 18 baada ya Mpango wa Maboresho ya Sekta ya Umma na Serikali za Mitaa kinatia aibu.

“Serikali ni lazima ichukue hatua si  tu kwa wenye hati chafu bali pia wenye hati zenye mashaka na zisizoridhisha.”

Akijadili utekelezaji wa maboresho ya nyuma (2015/16) kwa mujibu wa maagizo ya madhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali na Bunge, Dk. Albanie anabainisha yatuatayo:

Maagizo ya CAG

Kwa kuzingatia taarifa ya mwaka 2015/2016, mapendekezo ambayo hayajafanyiwa kazi mpaka mwisho wa mwaka wa fedha 30 Juni, 2016 ambayo yalihitaji kujibiwa na serikali ni 85 ambayo yalikuwa hayajashughulikiwa, 14 (16.5%) yalitekelezwa, 51 (60.0%) yalikuwa katika utekelezwaji, 9 (10.6%) hayakutekelezwa na 11 (12.6%) yalikuwa yamepitwa na wakati.

Maagizo ya Bunge

Kati ya maagizo 16 ya PAC (Kamati ya Bunge inayosimamia hesabu za serikali kuu) ambayo yalikuwa hayajafanyiwa kazi, moja (6%) lilitekelezwa, 10 (63%) yako katika utekelezaji, matatu  (19%) hayajatekelezwa na mawili (12%) yamepitwa na wakati.

Like
7

Leave a Comment

Your email address will not be published.