Corona yazuia Watanzania kuingia Uingereza

MADHARA ya serikali kukanusha uwepo wa maambukizi ya ugonjwa wa Corona nchini Tanzania sasa yameanza kuonekana baada ya Uingereza kupiga marufuku wasafiri wote watokao Tanzania wanaotaka kuingia nchini humo.

Jana – Alhamisi Januari 21, Serikali ya Uingereza kupitia kwa Waziri wa Uchukuzi Grant Shapps ilisema inachukua uamuzi huo ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo nchini mwake.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao jana, Grant alisema Uingereza imeamua kuzuia wasafiri kutoka nchi hiyo kwa kuwa kuna taarifa za kuwepo kwa maambukizi mengi ya Corona.

Baadaye waziri huyo, aliandika katika ukurasa wak wa Twitter kwamba Pamoja na Tanzania, nchi  nyingine ambayo imeangukiwa na uamzi huo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

“Wasafiri wote kutoka nchi hizo, hawataruhusiwa kuingia Uingereza, isipokuwa raia wa Uingereza, Ireland na watu wenye uhalali wa kuishi Uingereza,” aliandika kwenye Twitter.

Rais wa Tanzania John Magufuli amekuwa akisisitiza nchi yake haina ugonjwa wa Corona. Amekuwa akitamka hadharani kwamba Mungu ameiepusha nchi hiyo na ugonjwa huo unaoendelea kuondoa uhai wa watu.

Tanzania iliamua kuzuia taarifa za Corona kutangazwa kwa madai ya kutokwepo ugonjwa huo “baada ya maombi ya siku tatu kwa Mungu kujibiwa.” Dhana hii inapingwa na asili ya sayansi ya afya ya binadamu ikieleza kutokuwepo kwa Ushahidi wa msimamo huo wa Rais Magufuli.

Pamoja na taarifa hiyo ya waziri Grant, Katibu wa Kamati ya Bunge ya Uchukuzi wa Uingereza, Welwyn Hatfield alisema ili kuendelea kudhibiti maambukizi mapya, wageni kutoka Tanzania lazima wazuiwe.

Kuanzi alfajiri ya leo – Januari 22, saa 10:00, wasafiri wote kutoka au wale waliopita Tanzania ndani ya siku 10 hawaruhusiwi kuingia Uingereza.

Like