Ukweli wa nyongeza kuhusu kongamano la serikali na “viongozi wa dini” ni huu

Shehe Alhad Musa Salum - Kutoka Maktaba
Kongamano la baadhi ya viongozi wa dini na serikali limeisha. Tumesikia kauli zao. Lakini kuna mambo yafuatayo ambayo hawakutuambia. Sasa, sisi tunawambia, na tunawasihi hawa “viongozi wa dini” wayaweke kwenye maombi yao kwa Mungu yeyote wanayemwabudu:

1. Gharama za kongamano la viongozi wa dini zimelipwa na serikali. Mhasibu aitwaye Kasapira yuko ofisi ya Waziri Mkuu ndiye alikuwa anashirikiana na Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum, katika kusimamia malipo ya fedha yote kwa “wajumbe.”

2. Shehe Salum aliomba fungu lake la pekee. Akaombewa kibali kwa wakubwa, akakubaliwa na kupewa. Hakutaka wenzake wajue.

3. Kwenye orodha ya alivyoomba aliweka gharama za “mbuzi wa shughuli,” akadai  kuna mashehe amewaalika kutoka Tanga waje kufanya “shughuli” hiyo.

4. Ili kulipa uzito kongamano, Shehe Salum alipendekeza waalikwe viongozi wengine kutoka mikoani ili waongeze idadi na uzito wa kongamano. Akapewa nauli yao, lakini waliokuja wanadai hawajapewa nauli yao.

 5. Waliohudhuria wamepewa posho na walikuwa hawaruhusiwi kwenda wawili wawili. Kila mtu “alitendewa haki” peke yake.

Like
2