WACHAMBUZI wa uchumi wanasema kuwa iwapo uchumi wa Tanzania ungekuwa umesimamiwa vizuri, nchi ikafanya mauzo ya nje ya kutosha kuhakikisha uwiano wa kiwango cha kubadilisha fedha kati ya 2014 na 2022 inakuwa himilivu, bei ya lita moja ya mafuta jijini Dar es Saalaam ingekuwa shilingi 2,562.77 mwezi Mei 2022.
Kwa sasa, kutokana na hasara itokanayo na uwiano huo, Watanzania wanalazimika kulipa shilingi 585.04 zaidi. Bei ya mafuta (Mei, 2022) kwa lita jijini Dar es Salaam ni shilingi 3,147.81.
Kiasi hiki kilipaswa kupungua kwa shilingi 585.04, hivyo kuuzwa shilingi 2,562.77, pasipo kupunguza tozo za sasa ambazo ni mahsusi na muhimu kwa ajili kugharamia miradi ya maendeleo ya nchi.
Aidha, bei halisi ya mafuta kwa lita moja katika soko la dunia (CIF, Dar es Salaam), ingepungua kutoka shilingi 1,910.01 hadi shilingi 1,324.97 iwapo kusingekuwa na hasara ya uwiano wa kiwango cha kubadilisha fedha kiasi cha shilingi 585.04.
Takwimu halisi za uchambuzi huo hizi hapa: