Tanzania sasa yasisitiza uvaaji wa barakoa

Waziri wa Afya Dorothy Gwajima

HOFU ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa Corona yameifanya serikali ya Tanzania iagize kila mwananchi kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo na kuvaa barakoa katika sehemu za mikusanyiko.

Corona, ugonjwa unaoendelea kusumbua dunia, pamoja na kupatikana kwa chanjo yake, umekuwa ukiibuka kwa wa “sura tofauti” – hali inayotia wasiwasi wa kusambaa kwake upya.

Tayari nchi Jirani na Tanzania, ikiwamo Uganda, DR Congo na Kenya zimerejea kwenye mikakati ya kudhibiti kusambaa kwa maambukizi mapya kwa kuweka masharti magumu ya kujumuika, ulazima wa kuvaa barakoa kila wakati na kulazimisha watu kunawa mikono.

Kutokana na hali hiyo, Tanzania nayo sasa inaweka masharti magumu na taratibu ngumu kwa wageni wote wanawasili kutoka nje ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Katika viwanja vya ndege, hasa vile vinavyopokea wageni kutoka ughaibuni, kila msafiri; hata akiwa mwenyeji anayetoka nje, anapaswa kupima upya ili kujiridhisha kwamba hana maambukizi mapya. Wageni nao hutakiwa kufanya hivyo.

Naibu Waziri wa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (anayehusika na afya) Dk. Godwin Mollel akizungumza na SAUTIKUBWA amesema pamoja nah atua hiyo kulalamikiwa na watu, lakini ni muhimu sana katika kudhibiti maambukizi mapya.

Amesema Tanzania imemaua kuwapima wasafiri wote wanaoingia nchini ili kuhakikisha kuna udhibiti mkubwa wa maambukizi ya ugonjwa huo wa Corona.

“Tanzania tulikuwa na sifa ya kutopima wasafiri, lakini sasa tulipoanza kupima kila anayeingia, hata kama amepimwa huko anakotoka, tunapa sifa nzuri kwamba  sasa tuko makini,” amesema k. Mollel.

Tanzania ilianza utaratibu huo wa kupima kila msafiri kwa njia ya haraka hata kama alipimwa alikotoka, ikiwa ni njia ya kudhibiti maambukizi mapya ya Corona, ugonjwa unaojulikana pia kwa jina la COVID-19. Kila msafiri hulazimikakuipia Sh. 59,000 (dola za Marekai 25) kupima na kupata majibu yake ndani ya dakika 10.

Wasafiri wanaokutwa na maambukizi hulazimika kujiweka karantini wenyewe huku wakishauriwa namna ya kujikinga ama kuwakinga wengine.

Sambamba na hatua hiyo, serikali pia kuanzia mwishoni mwa wiki, imeweka taratibu wa lazima kwa wananchi kuvaa barakoa sehemu zenye mikusanyiko ili kujikinga Corona.

Wakuu wa mikoa na wilaya wameagizwa kuhakikisha wanatimiza agizo hilo kwa kuzishirikisha kamati za afya ya msingi na kwamba watapimwa kulingana na utendaji wao.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima ameagiza pia wananchi kuchukua tahadhari kwa kuendelea na utaratibu wa kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na kutumia vitakasa mikono (sanitaiza).
Dk. Gwajima alisema utaratibu wa kuvaa barakoa ambao sasa unaonekana kuanza kuupwa, ni hatari zaidi kwani Tanzania imezungukwa na nchi ambazo “zinapigwa na wimbi la tatu” la maambukizi ya janga hilo.
Wakati wa utawala wa Rais John Magufuli, alikataa kutambua Corona kuwa janga na alikuwa akisema ni “kauggonjwa kadogo ka mafua,” ambak kalimalizwa na “damu ya yetu.” hivyo alitamka Tanznaia hakuna Corona. Hata hivyo, baada ya kifo chake, mrithi wake, Rais Samia Suluhu Hassan aliamua kuubeba ukweli kwamba janga hilo lipo, linaua na tayari amechukua taratibu kadhaa za kutahadharisha wananchi kujikinga nao kwa hatua mbalimbali.

Dorothy Gwajima
Like