Kama Kikwete angemjua vema Magufuli asingempa urais

HATA Rais Jakaya Kikwete anajilaumu kuhusu Rais John Magufuli. Rais Mstaafu Benjamin Mkapa naye vile ile; alimjua kwa upande mmoja kama “askari wake wa mwavuli.” Katika mengine wanayojuana, waliamua “kuchukuliana” ilimradi mgombea wa chama chao atangazwe mshindi; wapinzani wasiingie Ikulu.

Kwa kutomjua, Kikwete na Mkapa walidhani ingekuwa rahisi kumdhibiti Magufuli akiwa madarakani. Kwao ilikuwa nafuu kuwa na Magufuli waliyedhani wanamjua, kuliko kuruhusu Edward Lowassa, ambaye walidhani angelipa visasi.

Walikosea. Na iliwachukua mwaka mmoja tu kugundua kuwa Magufuli hakubali kudhibitiwa wala kushauriwa, na kwamba Lowassa si mtu wa visasi! Magufuli aliwasogeza mbali zaidi pale alipowaonya wasije “wakawashwawashwa!” Matokeo yake, nchi inadidimia mbele yao. Wao na wastaafu wengine wanasemea pembeni. Wanaogopa kumshauri.

Mbali na Mkapa na Kikwete, hata wanachama wa CCM walio wengi hawakumjua Magufuli hadi alipokuwa rais na mwenyekiti wao. Ujinga huu ulikumba pia baadhi ya wananchi waliokumbwa na kiwewe cha kampeni na ushabiki wa kisiasa.

Hili kueleza hali hii, nitawakumbusha kisa cha zamani kuonyesha kama Watanzania walikuwa wanamjua na kumpenda Magufuli au waliuziwa mbuzi kwenye gunia.

Mwaka 1981 iliyokuwa Soviet ilipata shida kwenye Umoja wa Mataifa (UN) kuamua nani awe Katibu Mkuu kati ya mwanadiplomasia wa Austria, Kurt Waldheim aliyekuwa anawania kipindi cha tatu na mwanadiplomasia wa Tanzania, Dk Salim Ahmed Salim.

Mwaka 1972 Kurt alifanya kampeni nzito akashawishi hata China na Uingereza zilizomkataa awali. Zikamkubali, akashinda. Mwaka 1976 China iliweka tena pingamizi lakini ililiondoa baadaye akachaguliwa kipindi cha pili.

Mwaka 1981 Soviet iliyomjua vema Kurt ilisema “heri shetani umjuaye” ikimaanisha heri Kurt wanayemjua kuliko Dk Salim, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania wakati huo, ilihali Marekani ilimpigia chapuo Kurt badala ya Dk Salim. Basi China iliondoa udhia kwa kumpigia veto Kurt.

Marekani ilimkataa Dk Salim ikilipiza kisasi kwa hatua ya Mwalimu Julius Nyerere ambaye huko nyuma alikuwa ameikatalia Marekani iliposhawishi Tanzania kususia Michezo ya Olimpiki iliyofanyika Urusi mwaka 1980. China ilitumia ripoti ya Tume ya UN ya Uhalifu wa Vita vya II vya Dunia iliyomtuhumu Kurt kufanya uhalifu alipokuwa katika Jeshi la Manazi wa Ujerumani.

Kabla ya China kutumia ripoti ya UN, Kurt alionekana muadilifu na msafi. China haikuweka uzito kumzuia Kurt kuongoza mara mbili UN lakini kipindi cha tatu ilisimama kidete. Safari hii haikutaka kufumba macho, ikaweka hadharani madudu ya Kurt na hakukuwa na njia zaidi ya kumtema na ndipo miezi mitano baadaye akachaguliwa Javier Pérez de Cuéllar kutoka Peru.

Nakumbusha kisa hiki kuonyesha unafiki wa CCM na badhi ya Watanzania wakati wa uchaguzi mwaka 2015. Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mamlaka ya Udhibiti na Manunuzi ya Umma (PPRA) zilibainisha wazi kwamba mgombea wa CCM John Magufuli hakustahili kuwa rais.

Wanahabari waliochambua ripoti kuhusu Magufuli walishutumiwa kwa maneno ya kejeli: “Wewe mwandishi uchwara!” “Umehongwa!”  “Unatumiwa!” Waliomwandika vizuri walisifiwa: “Wewe bonge la mwandishi!” “Hongera!”

Makada wa CCM walipenda kuona hata watoto wadogo wanachora kwenye mavumbi Edward Lowassa aliyehamia Chadema kuwa ni fisadi lakini watoto hao hao wakiandika Magufuli hafai walilalamika, “unatumiwa vibaya!” “Huo ni ushabiki wa kisiasa!” Vema, kwa nini kusema Lowassa ni fisadi haukuwa ushabiki wa kisiasa? Kwa nini waliomtetea Magufuli hawakuonekana wamehongwa?

Kabla ya China kufunua faili la maovu ya Kurt, machoni pa wengi alionekana mwadilifu, msafi. China ilipong’ang’ana na ripoti ikawa nafuu kwa UN, maana walimpata mbadala aliyekubalika na wote na kukipa heshima chombo hicho.

Kwa Tanzania haikuwa hivyo. Walimkataa Lowassa ambaye tuhuma zake kubwa ni kashfa ya Richmond wakamchagua Magufuli ambaye alikuwa na kashfa nyingi za ufisadi pamoja na nyingine moja iliyofichika ya udikteta.

Kwanza, alisimamia vibaya mchakato wa kuuza nyumba za serikali zaii ya 9000, nyingine akagawa kwa hawara zake na ndugu zake. Kumbukumbu zipo.

Pili, Magufuli ameisababishia hasara Tanzania ya shilingi trilioni 1.3 kwa papara zake kukamata samaki na meli ya wavuvi wa China. Wachina walifungua kesi, serikali ya Tanzania ikashindwa, na ikatakiwa kulipa kiasi hicho cha fidia. Walipokwenda kuchukua meli yao wakakuta nayo imezama baada ya kukatwa chuma chakavu.

Tatu, Mamlaka ya PPRA ilitoa ripoti ikisema Wizara ya Ujenzi iliyokuwa chini ya Magufuli ilisababisha Tanzania kulipa riba ya shilingi bilioni 124 kwa kuchelewa kulipa shilingi trilioni 5.3 za makandarasi wa barabara.

Nne, PPRA ilisema wizara hiyo ilifanya malipo hewa ya shilingi bilioni 951.7 kwa makandarasi ambao kazi hazikufanyika.

Tano, Ripoti ya CAG kuanzia mwaka 2013 inahoji zilikokwenda shilingi bilioni 253 katika Wizara ya Ujenzi aliyoiongoza kwa muda mrefu.

Sita, analaumiwa kwa ufisadi wa kununua meli mbovu kwa bei ghali. Wakala wa Ufundi na Umeme (Tamesa) chini ya Wizara ya Ujenzi ulinunua boti mbovu kwa shilingi bilioni 8 iliyobatizwa jina la Mv Bagamoyo.

CAG amehoji kwa nini boti hiyo ina kasoro tofauti na mkataba. Boti hiyo iliyolalamikiwa na wapinzani tangu wakati wa ununuzi ilifanya safari moja tu kwenda Bagamoyo Februari 27, 2015 na iliporejea Dar es Salaam ikashindwa kufanya kazi hadi leo iko ‘magogoni’ mbovu. Ilikuwa mbovu, lakini ilinunuliwa kwa  shilingi bilioni 10 za walalahoi; wakati boti mpya za Azamu zimenunuliwa kwa shilingi bilioni nne. Nayatekata kujua maana ya wapiga dili atafakari ununuzi wa boti ya Bagamoyo.

Saba, mwendelezo wa madudu ya Magufuli ni ripoti ya CAG ya mwaka 2016/17 inayosema baada ya kufanya ukaguzi haoni kilipo kiasi cha shilingi trilioni 1.5. CAG anasema serikali ilikusanya shilingi trilioni 25 na imetumia shilingi trilioni 23.5.

CCM wote, kuanzia makada wake, mawaziri na hata Magufuli mwenyewe aliyeweza kueleza kiasi hicho kiko wapi. Je, kimeliwa au kimetumika kwenye miradi ambayo Bunge halijui?

Kama fedha hizo zimetumika katika miradi ambayo Bunge halikuidhinisha kwa nini serikali inashindwa kuitaja? Kama miradi haipo ina maana fedha zimeliwa, na kama zimeliwa basi aliyekula atakuwa mkuu wa nchi maana kama wangekuwa ni mawaziri angekuwa ameshawatumbua na kuwafikisha mahakamani ili apate sifa?

Ili kuficha ufisadi wake, Magufuli ameamua kuzuia maoni huru na ukosoaji wa asasi za kiraia, waandishi wa habari na vyama vya siasa. Yeyote anayetoa maoni huru anakamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi. Wengine wameuawa.

Wapinzani wanalia, CCM wako kimya, wanahabari wanalia. Mithali 28:16 inasema wazi “Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana; Bali achukiaye kutamani (kupata visivyohalali) ataongeza siku zake.”

Like
33
10 Comments
  1. Sebastian 7 years ago
    Reply

    Bw. Ngurumo, Siku tatu zilizopita nimebahatika kusafiri na meneja mkuu wa kiwanda kimoja cha nguo nchini, tukielekea Nairobi yeye alikuwa anaenda kwenye trade expo ya Tanzania na Kenya. Katika mazungumzo yetu amekuwa na masikitiko makubwa sana juu ya ubabe na uonevu wa serikali dhidi yao na wafanyabiashara kwa ujumla. Amedai Tanzania nzima vipo viwanda viwili tu vya nguo lakini vinafanya kazi kwa hasara sana na ameenda mbali na kusema tutarajie viwanda vingi kufungwa maana hakuna maana ya kuwa na kiwanda kwa sera mbovu za serikali. Wengi wafanyabiashara wanaamisha biashara zao kwenda nchi za jirani! Anasema kufanya biashara Tanzania ni dhambi kuwa.

    Tulijadili mengi sana naona alifurahi sana kupata mtu wa kumsikiliza maana alifunguka sana naona moyo wake ulikuwa umejaa sana amenipatia visa na adhabu wanazo pata kutoka kwa mamlaka za serikali OSHA, WCF, NEMC, Labour, Immigration, TRA etc.

    Anadai sasa hivi rushwa inayoombwa ni mamilioni na vitisho ni vingi sana ukikataa unaandikiwa faini za ovyoovyo na za kulipa papo hapo. Kupata vibali vya kazi ni kupita kwenye moto wakati kwa bahati mbaya technology nyingi zinazotumika kwenye viwanda vipya watanzania wengi bado hawajafahamu hivyo inakuwa taabu sana! Cha ajabu wachina wanaleta hadi mahouse boy wao hawapati shida!

    Fanya uchunguzi wako uwafungue macho watanzania waliolala

    Sebastian

    3

    1
  2. Kunta Kinte 7 years ago
    Reply

    Hakika huu mzigo waliotutwisha waTz wanastahili kuja kuutolea hesabu hawa wazee

    1

    1
  3. Tang Zhou 7 years ago
    Reply

    Magufuli is a lusty bald fraud….huyu mtu ni mpenda fedha mno hazina ya taifa haiko salama chini yake, na ndiyo mtu unajiuliza kwanini anahofia sana vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kama si mwizi?

    2

    1
  4. Saidi mponda 7 years ago
    Reply

    Mmmm! Tunashukuru kwakuyafahamu hayo tulikua atuyajui

    1

    0
  5. OpenMind Tz 7 years ago
    Reply

    Hii yote inatokana na Idadi kubwa ya waliopata elimu ya juu kupuuzia mambo hayo na kulizisha matumbo yao na hata kutarajia kugewa cheo fulani Ama Nyadhfa kwa huyo wanae mwona anaafaa kwa sasa…Ila inauma sanaa sametime unatamani hata kutopiga kula kipindi cha UCHAGUZI MKUBWA lakin unahofu ya kupoteza haki yako …….Nukuu ya Walio wengi Awatamani kuoiga kula Tena kwa Imani ya kwamba hata wakipiga kula Haitasaidia ????..Its pain Naisi hapa ndipo sehemu ya kuwaacha baadh ya watu kupiti maumivu ya juu ya maswala yanayo wakuta angalau wanaweza kubadilika kwa Imani

    1

    1
  6. Tao 7 years ago
    Reply

    hii ni ishara mbaya sasa. Kwa nini tumefikishwa hapa?

    1

    0
  7. OpenMind Tz 7 years ago
    Reply

    Hii yote inatokana na Idadi kubwa ya waliopata elimu ya juu kupuuzia mambo hayo na kulizisha matumbo yao na hata kutarajia kugewa cheo fulani Ama Nyadhfa kwa huyo wanae mwona anaafaa kwa sasa…Ila inauma sanaa sametime unatamani hata kutopiga kula kipindi cha UCHAGUZI MKUBWA lakin unahofu ya kupoteza haki yako …….Nukuu ya Walio wengi Awatamani kuoiga kula Tena kwa Imani ya kwamba hata wakipiga kula Haitasaidia ????..Its pain Naisi hapa ndipo sehemu ya kuwaacha baadh ya watu kupiti maumivu ya juu ya maswala yanayo wakuta angalau wanaweza kubadilika kwa Imani

    0

    0
  8. hatarious 7 years ago
    Reply

    Sjida ya tz co kubadili chama tunatkiwa tupinge na kubadil katiba iliopo sas na amendment zake zote ina loop hole nying sana
    Ushaur wang kwa watz wote jarib kupata nakala yko ya katiba hata kam hujui sheria ilq kaam unaja kusom na kuandika”ambacho ni kigezo cha wew kuwa mbnge, diwan, dc au rc” kwa mujib wa katiba plz and plz isome utaona madudu yaliyok hum ndan then utajua mwenywe km shida ni chama au katiba tunayotumia
    Katiba ndo sheria ya nchi, ukibadili na kuielewa katiba itaweza kumwajibisha mwao/mzaz wako au hata askar shirikish anaekusumbua utajua haki zako mtanzania
    #somakatibayasas

    1

    0
  9. Mtanzania 7 years ago
    Reply

    ?Maraisi waliopita walikuwa na mambo yao mabaya lakini Magufuli kamwe hata- enjoy uzee wake kama wenzake kwa usalama. Nina hakika atapigania kuendelea kwenye madaraka mpaka watz wamtoe kwa nguvu. Magufuli siku moja atasimama mahakamani akijibu mashtaka ya uvunjaji wa haki za binadamu Tz. Ninawalaumu sana maraisi wastaafu kushindwa kumuita na kumshauri ajiuzulu mapema na aache kuwatesa Wtz. Nawalaumu kwa kutuchagulia dikteta kuwa raisi ili tu CCM ichukue madaraka. Nawalaumu kwa kuwa wabinafsi, huku wakiangalia taifa linaanguka. Hawa maraisi wastaafu wasifikiri wako salama, kama watakuwa hai, akiondolewa huyu dikteta, siku moja WTz watawauliza.

    5

    0
  10. Freedom tz 7 years ago
    Reply

    Aisee

    0

    0

Leave a Comment

Your email address will not be published.