Kesi ya Mbowe: Shahidi ajikanyaga juu ya ‘ugaidi’ wa Mbowe na ujambazi wa Sabaya

Kama ilivyowasilishwa leo na ripota raia, BJ, leo tarehe 11 Januari 2022.

Jaji ameingia Mahakamani Muda huu Saa 4 Kasoro Dakika 3

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba kuwatambulisha:

Pius Hilla

Abdallah Chavula

Jenitreza Kitali

Nassoro Katuga

Esther Martin

Tulimanywa Majige

Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ikikupendeza naomba kuwatambulisha mawakili:

Nashon Nkungu

John Malya

Dickson Matata

Faraji Mangula

Sisty Aloyce

Michael Mwangasa

Gaston Garubindi

Seleman Matauka

Jaji anaita washitakiwa wote wanne na wote wanaitika wapo mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji shauri lina endelea kusikilizwa na upande wa mashitaka tupo tayari kuendelea

Mheshimiwa Jaji anaandika kidogo wakati mahakama ipo kimya

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji nasi pia tupo tayari kuendelea

Nje kuna kelele kufuatia timu ya mpira wa miguu Tanga sports Club (Timu ya Wananchi wapo nje na basi lao viwanja vya Law school wanafanya mazoezi)

Wakili Peter Kibatala: anasimama na kuendelea na kesi

Kibatala: Shahidi: tulikuwa tunaendelea kuhusu kesi yenu kuwa Mbowe alimpa maelezo Urio na Urio aweze kutafuta watu wa kufanya ugaidi

Kibatala: Shahidi, Urio bado yupo jeshini na mwanajeshi  aliye kwenye utumishi?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: katika Ushahidi wako uliwahi kuongea lolote hapa mahakamani kwamba urio akiwa kama. mwanajeshi wa jwtz kushiriki katika vitendo vizito vya ugaidi?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ulishawahi kuwasiliana na jwtz kuhusu mtumishi wao urio kushiriki katika ya matendo ya ugaidi?

Shahidi: Sijafanya

Kibatala: Je kwa ufahamu wako uongozi wa JWTZ unafahamu kuwa mwanajeshi wao Urio alikuwa anafanya vitendo vya kutafuta watu wa kufanya ugaidi?

Shahidi: Hilo Mimi sifahamu

Kibatala: Je unakubaliana na mimi kuwa vitendo vya ugaidi ni vitendo vizito na vinatikisia psychology na utulivu wa nchi?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je unafahamu kuwa JWTZ wanakitengo Cha Ujasusi cha Millitary Intelligence, kazi yao ni pamoja na kuchunguza matendo ya ugaidi?

Shahidi: Hapana sifahamu

Kibatala: Katika ushahidi wako ulizungumzia lolote kuhusu kushirikiana na vyombo vya usalama na kijasusi kama TISS?

Shahidi: Mimi sifahamu lakini viongozi wangu watakuwa wamefanya

Kibatala: Sasa viongozi wako unawapa hapo kwenye kizimba?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Unafahamu kuwa moja ya kazi ya hizo taasisi ni kushughulika na mambo ya ugaidi?

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unafahamu kuwa iwapo taasisi hizo zingeshirikishwa katika ngazi mbali mbali ya vyombo vya usalama na Idara ya Uhamiaji na wao wangeshirikishwa?

Shahidi: Hilo Mimi siyo wajibu wangu

Kibatala: Umeanza kuleta ujeuri mahakamani

Shahidi: Hapana

Kibatala: Sasa jibu, unafahamu au ufahamu!

 Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je Unafahamu kuwa mshitakiwa wa nne alisafiri kwenda nje mara kadhaa.? 

Shahidi: Hapana sifahamu

Kibatala: katika kikosi chemu wewe ulikuwa second command kama top leader, Je unafahamu katika timu yenu kuna mtu aliwasilina na Rais Samia Suluhu Hassan?

Shahidi: Hilo sifahamu

Kibatala: Unafahamu alipopata taarifa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mbowe alikuwa anajua  atashitakiwa kwa ugaidi ndiyo maana akakimbia nje ya nchi kukwepa upelelezi?

Shahidi: Hapana sifahamu

Kibatala: Kuna kikosi kazi zaidi ya chenu kilikuwa kinafanyia kazi suala hili labda wao walienda kumtaarifu Rais Samia Suluhu Hassan?

Shahidi: Hapana sifahamu

Kibatala: Katika kesi hii hii Rais Samia Suluhu Hassan alisema kuwa kuna watu wamefungua katika shauri hili, kwa ufahamu wako kuna watu wamefungua kwenye shauri hili?

Shahidi: Hilo silijui na siwezi kuiongelea

Kibatala: Kama unajua sema najua au sijui, kusema uwezi kuongelea ni ujeuri nitaomba mahakama ikuzimishe 

Shahidi: Hilo silifahamu

Kibatala: Je unafahamu kuwa kingai alisema kuwa alimuwekea uangalizi Mbowe hata alipokuwa nje ya nchi.? 

Shahidi: Hilo Mimi silifahamu

Kibatala: Je kwa ufahamu wako wewe, Mbowe alikimbia nje ya nchi ilikuweza kukwepa upelelezi?

Shahidi: Hilo silifahamu

Kibatala: Je unafahamu nchi ambazo Freeman Mbowe kwenda nchi mbalimbali kutoka August 2020  mpaka mwaka 2021 July?

Shahidi:  Silifahamu nchi hizo

Kibatala: Je unafahamu kuwa mamlaka chunguzi/ pelelezi za Tanzania kuwasiliana na mamlaka chunguzi za hizo nchi?

Shahidi: Hilo sifahamu

Kibatala: Je unafahamu kuwa mtu ambaye akiwa kwenye uchunguzi na upelelezi wa kesi nzito huwa anazuiwa hata kusafiri.?

Shahidi: Hilo linategemea

Kibatala: Linategemea nini..?

Shahidi: Hilo sijui

Kibatala: Iambie mahakama ni uchunguzi upo huo uliokuwa unaendelea ambao uliwafanya usimkamate Mbowe wakati wote

Shahidi: Mambo ya forensic

Kibatala: Mlifanya mawasiliano kwa mara ya kwanza na Taasisi za Forensic mwezi july 2021 baada ya Mbowe kukamatwa je wewe unasemaje?

Shahidi: Sina ninachojua

Kibatala: Kingine kipi.?

Shahidi: Mambo ya intelligence

Kibatala: Intelligence ipi..?

Shahidi: Mambo ya intelligence mengi siwezi kuyazungumzia hapa

Kibatala: Kwa sheria ipi inayokuruhusu wewe shahidi usiseme hayo mambo halafu unataka kufunga mteja wangu?

Shahidi: Ni mambo ya watu wengine kwenye upelelezi ikiwemo watu wengine waliokamatwa

Kibatala: Kuna mtu alimakatwa baada ya September 2020.?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Sasa nani unayemzungumzia hapa?

Shahidi: Hakuna, ila wengine wa naendelea Kufuatiliwa

Kibatala: Kwa hiyo upelelezi wa kesi hii  unaendelea?

Shahidi: Hapana umeishia

Mahakama Kichekoooooo

Kibatala: Je unafahamu kwamba katika nchi ambazo viongozi wake ni madikteta, huwapa viongozi ambao ni wapinzani wao kesi ilikuwatisha?

Shahidi: Hilo silifahamu

Kibatala: Unafahamu kuwa nchi nilizo zitaja zina fuatilia  kesi hii kw a kutuma wawakilishi wao kuja kufuatilia haki ya Freeman Mbowe?

Shahidi: Hilo mimi sifahamu

Kibatala: Unafahamu kitu kinaitwa Travel Advisory

Shahidi: Sijawahi kukutana na kitu kama hicho

Kibatala: Askari mzoefu wa miaka 20 ujawahi kusikia kitu hicho?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Katika upelelezi wenu wote mpaka upelelezi unakamilika, urio si ndiyo alikuwa informant wenu?

Shahidi: Hilo sijaongelea hilo

Kibatala: Kwa hiyo alikuwa ni Whistler blower?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unaifahamu sheria inaitwa Whistler Blower and Protection Act, juu ya kulinda watoa taarifa.?

Shahidi: Hapana sifahamu sheria hiyo

Kibatala: Kwa hiyo wewe afisa wa polisi na kiongozi wa kikosi kazi ujui sheria ya Whistle Blower and Witness protection Act?

Shahidi: Miye sijawahi kulisoma natumia muongozo wangu

Kibatala: Kwa hiyo ufahamu kuwa whistle blower anapokuja kutoa taarifa umuandikishi maelezo ya onyo bali kwa taarifa za sheria hiyo?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Na bado mnataka tuendelee na kesi hii wakati whistle blower hajahojiwa kwa sheria hiyo?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kwa ufahamu wako wewe Mbowe aliwapa pesa washtakiwa wengine personally kutoka kwake?

Shahidi: Ndiyo aliwapa kutoka kwa Urio

Kibatala: Kwahiyo zikipitia kwa Urio ni personally.?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Sasa msomi mzima hujui maana ya personally?

Shahidi: Nilikuwa sijaelewa

Kibatala: Sasa nitafutie sehemu iliyo andikwa kwamba kuna pesa iliyotoka kwa Mbowe kuja kwa urio, kisha Urio akawapa wao 

Shahidi: Hakuna sehemu hiyo

Kibatala: Kwahiyo katika maelezo haya Ling’wenya alikabidhiwa pesa na Urio bila kuambiwa imetoka wapi?

Shahidi: Ndiyo

Shahidi: Baada ya kufika tukikutana na Ruteni Denis Urio bar moja ya Msavu sikumbuki jina, baada ya kukutana Ruteni Urio alisema kuwa kuna kazi ya kwenda Kufanya Moshi ambayo ni VIP PROTECTION

Kibatala: Soma hapa katika ukurasa wa tatu mstari wa mwisho. Baada ya kukutana na Ruteni Urio….. Je alifahamu anaenda  Moshi kufanya nini..?

Shahidi: Kufanya VIP PROTECTION

nitafutie Mahala ambapo Urio anamwelekeza Ling’wenya kuwa anaenda kufanya kazi ya ugaidi Moshi?

Shahidi: Hakuna sehemu hiyo anayosema kuwa alipewa kazi ya a kwenda kufanya kazi ya ugaidi

Kibatala: Ni wapi ambapo Ling’wenya anakiri Kuwa alipewa pesa na Mbowe kwenda  kufanya vitendo vya  kigaidi?

Shahidi: Hakuna sehemu ambayo anasema alipewa pesa na Mbowe kwenda  kufanya ugaidi

Shahidi: Hakuna Maelezo hayo

Kibatala: Kuna mahala popote katika statement ambapo Mbowe alipiga simu au kutuma meseji kumshawishi Ling’wenya kwenda kufanya kazi ya ugaidi?

Shahidi: Mimi kama mpelelezi sina sauti za Mbowe akipanga ugaidi

Kibatala: Kwa maelezo yenu ni kwamba Ruteni Denis Urio ndiye aliyeenda Ofisi wa ya DCI kuja kuleta taarifa na nyie ndiye akawa informant wenu, je nini kiliwazuia kumpa vifaa kazi mtu huyu kwa ajili ya kumrekodi Mbowe alitoa maelekezo ya kutenda ugaidi au kumdhuru Sabaya

Kibatala: Je tuna video yoyote ambayo inaonyesha mbowe akipanga ugaidi au kutoa maelekezo ya kutenda ugaidi au kumdhuru Sabaya?

Shahidi: Ndiyo hatuna video yoyote

Kibatala: Je mliwahi kumwambia  Luten Denis Urio kuwa amrekodi  Mbowe hata kwa simu alitoa maelekezo ya kutenda vitendo vya ugaidi au kumdhuru Sabaya ili zije mahakamani?

Shahidi: Hatuna voice record kutoka kwa Urio

Kibatala: Je mli-infiltrate mtu mwingine aweze kupata records za Mbowe hata kama kwa kutuma mwanamke aweze kumrekodi?

Shahidi: Miye siwezi kufahamu

Kibatala: Wewe ulifahamu lini kuwepo kwa  Luten Denis Urio kama whistle blower ?

Shahidi: Kwenye mwezi wa nane na wa tisa baada ya kuwa wamekamatwa wakina Ling’wenya

Kibatala: Mpaka tarehe hiyo mlikuwa mnafahamu kuwa Freeman Mbowe amemuagiza Luteni Denis Urio kutenda vitendo vya ugaidi, Je mpaka hapo alikuwa amefanya kosa au alikuwa haja fanya kosa?

Shahidi: Alikuwa amefanya kosa

Kibatala: Lakini mpaka wakati huo mlikuwa hamjaona sababu ya kumkamata?

Kibatala: Je ni sahihi nikisema kwamba mlitumia Luten Denis Urio kuwawekea  mtego vijana hawa ili kutengenezea Mbowe kesi ya kisiasa?

Shahidi: Si kweli, wewe siyo mpelelezi

Kibatala: Mimi na wewe nani hajui upelelezi wakati nimekuuliza hapa kuhusu mbinu za kazi

Kibatala: Upelelezi gani unaijua zaidi ya kuteswa vijana wa watu ambao walitumikia Nchi na Jeshi?

Shahidi: Upelelezi ni mambo mengi siyo hayo tuh

Shahidi: Sijatesa mtu mimi

Kibatala: Nakuuliza hapa chini ya kiapo, unamjua Tito Magoti au humjui?

Shahidi: Simfahamu Tito Magoti

Kibatala: Nikimleta hapa mahakamani  kam shahidi: akisema kuwa ulishiriki kumteka?

Shahidi: Miye sijawahi kumteka

Kibatala: Je unafahamu kuwa wewe ni Afisa wa Mahakama.?

Shahidi: Hapana sifahamu

Shahidi: Sijawahi kujua

Kibatala: Askari Mzoefu Miaka 20 hujui kuwa PGO inakutambua kama Afisa wa Mahakama?

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Nitafutie mahala popote ambapo Ling’wenya anakiri kukutana katika kikao cha kupanga vitendo vya kigaidi

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Nitafutie mahala popote katika statement hiyo ambapo Ling’wenya anakiri kuwa akipanga kwenda kulipua Soko la Kilombero Arusha

Kibatala: Nitafutie Mahala Popote ambapo Ling’wenya anakiri kuwa alipanga kulipua Mkoani Mwanza

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Nitafutie mahala popote ambapo Ling’wenya anakiri kuwa bastola mliyokamata kuwa ilikuwa inatakiwa kutumika vipi katika vitendo vya ugaidi

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Ni wapi ambapo Ling’wenya amezungumzia katika statement hiyo aina ya vilipuzi

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Kwa uzoefu wako wewe Kama afisa wa polisi, unaweza kulipua bila ya kuwa na vilipuzi?

Shahidi: Hapana lazima uwe na vilipuzi

Kibatala: Kuna mahala popote katika statement hiyo ambapo Ling’wenya ameelezea namna walivyo panga kumdhuru Sabaya?

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Unasema mliwakamata Ling’wenya na Adamoo Pale Rau Madukani?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je kwa upelelezi wenu, uwepo wao pale Rau Madukani Ling’wenya na Adamoo walikuwa katika matembezi yao au kwa kwenda kutekeleza mpango wa ugaidi? 

Shahidi: Walikuwa wanatekeleza mpango wa ugaidi

Kibatala: Nitafutie hilo katika statement ya Ling’wenya hapo sehemu ambapo anasema walikuwa Rau Madukani kutekeleza mipango ya ugaidi

Shahidi: Hapana hakuna sehemu hiyo

Kibatala: Lengai Ole Sabaya ameshahukumiwa kifungo kwa makosa ya ujambazi na kuzulumu watu mali zao

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ni nyie nyie ndiyo mlimshitaki sabaya kwa makosa ya ujambazi ambaye hapa mnasema alitaka Kudhuuriwa?

Shahidi: Miye ushawahi kuniona kwa Sabaya.?

Kibatala: Si nyie Jeshi la Polisi?

Shahidi: Aaah sawa hapo sawa kama Jeshi la Polisi, mwanzo hukuwa specific

Kibatala: Ulishawahi kuongea na Sabaya akamwambia kuna watu wanataka kumdhuru?

Shahidi: Hapana

Kibatala:  Turudi pale Rau Madukani, baada ya kuchukua bastola katika maungo ya Adamoo, na baadae ukamkabidhi Goodluck?

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala:  Na pale hakuwa na seizure certificate ikabidi atoke aende kwenye gari kufuata karatasi ya seizure certificate?

Shahidi: Sahihi

Kibatala:  Na Goodluck akaondola na Ile bastola kwenda kwenye gari, akarudi tena na ile bastola?

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala:  Lakini hukusema hapa kwamba Goodluck alisindikizwa na mashahidi: huru kwenda kuchukua seizure certificate Anita na Esther

Shahidi: Ndiyo sikusema, lakini tayari nilisha kuwa nimesema namba na kila mtu aliokuwa ameona namba

Kibatala:  Sasa ukiyasema hapa mahakamani?

Shahidi: Hapana

Kibatala:  Na Goodluck ile bastola uliyomkabidhi aende nayo ilikuwa na zile risasi tatu..?

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala:  Sasa unafahamu kuwa zile risasi zina calibre namba kwenye kitako?

Shahidi: Ni sahihi zina calibre namba

Kibatala:  Mwambie Mheshimiwa Jaji kama ulizungumzia hizo tofauti kuwa zile risasi zilikuwa moja haina namba na zile mbili zina namba tofauti

Shahidi: Hapana sikumwambia

Kibatala:  Na unafahamu kuwa kila silaha ina origination yake?

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala:  Je Ling’wenya alikwambia wamepata wapi hiyo silaha?

Shahidi: Hajaeleza katika maelezo yake

Kibatala:  Katika upelelezi wenu mligindua Adamoo alipata wapi hiyo bastola?

Shahidi: Ilikuwa ni unlawful

Kibatala:  Sijakuuliza hilo, nimekuuliza, Adamoo alipata wapi hiyo bastola?

Shahidi: Hatujui alipata wapi

Kibatala:  Na haujasema kuwa alipewa na Freeman Mbowe?

Shahidi: Sijasema hivyo

Kibatala:  Na Hayo madawa ya kulevya aliyokutwa nayo Ling’wenya, mlichunguza amepata wapi?

Shahidi: Hatukuchunguza

Kibatala:  Je aliwaambia kuwa madawa hayo ya kulevya yana husiana vipi na njama za ugaidi?

Shahidi: Hatukugundua yana husiana vipi

Kibatala:  Turudi Dar ea Salaam. Je Mlifika Dar es Salaam saa ngapi kutoka Moshi ni saa 10  kwenda kwenye saa 11 au saa 11 kwenda saa 12?

Shahidi: Ilikuwa Saa 11 kwenda saa 12

Kibatala:  Kwahiyo ni range ya lisaa kimoja?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala:  Na jana ulisema kumbukumbu ni sifa ya askari makini? 

Shahidi: Ndiyo

Kibatala:  Wale vijana wengine watatu mliwakamata kwa sababu walipita 92 KJ?

Shahidi: Hapana

Kibatala:  Wewe si ndiyo mpelelezi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala:  Tuambie sasa Khalid ulimkamata na kukaa naye mwaka mzima kwa ushahidi: upi? 

Shahidi: Palikuwa na taarifa kuwa wataungana nao ila mpango haukufanikiwa

Kibatala:  Kwenye statement humo ya Ling’wenya ameeleza kwamba alikutana nao

Shahidi: Hapana

Kibatala:  Sasa uliwakamata kwa sababu ipi au ndiyo tuseme jeshi linaonea wanajeshi wake waliolitumikia?

Shahidi: Hapana kwa sababu walikutana  kabla, I kuwa mwezi July

Kibatala:  Kwa hiyo Walikutana wapi? 

Shahidi: Dar es Salaam

Kibatala:  Kwahiyo ni ushahidi: wako kuwa Ling’wenya alikuwa Dar es Salaam mwezi July?

Shahidi: Hapana Ilikuwa mwezi wa nane

Kibatala:  Je unafahamu kuwa Chadema ilishiriki uchaguzi Wa Rais na Wabunge nchi nzima?

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala:  Na Mbowe aligombea Ubunge kule Hai?

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala:  Hivi dhana ya mtu kuianga kufanya ugaidi kudhuru wananchi na kwenda tena kwa hao hao wananchi akiwa anagombea na chama chake?

Shahidi: Hiyo ni mtu mwenyewe sasa, miye sifanyii kazi dhana

Kibatala:  Kuna mahala popote wewe na kikosi kazi chako kuna mahala popote ulizungumzia kuriport kwa Kamanda wa Polisi Kilimanjaro na Moshi kuwa  mna kazi ya kitaifa mnafanya?

Shahidi: Hapana, sijazungumzia

Kibatala:  Kuna mahala popote kwenye PGO inasema kwamba maelezo kaandikishie mahala ambapo kesi imefunguliwa?

Shahidi: Hakuna

Kibatala:  Je kuna mwomgozo wowote unazungumzia hivyo?

Shahidi: Hapana

Kibatala:   Twende sehemu nyingine, jana nilisikia hapa unazungumzia kuhusu Lissu kupigwa risasi, Je Tukio la Lissu kupigwa risasi kwa Lissu ni ugaidi au siyo ugaidi?

Shahidi: Siyo ugaidi ni uhalifu wa kawaida

Kibatala:  Matata tufanye comperative analysis, inakuwaje kutaka kumdhuru mwalifu Sabaya iwe ugaidi ila kupigwa risasi kwa Lissu isiwe Ugaidi?

Shahidi: Kwa sababu ilikuwa inaendana na maandamano nchi nzima

Kibatala:  Kwani Chadema Wamefanya marangapi maandamano, je ilikuwa ni ugaidi?

Shahidi: Sijui

Kibatala:  Kuna mahala popote umesema kuwa mlipofika Dar es Salaam mlimfahamisha DCI?

Shahidi: Sijasema

Kibatala:  Kuna mahali popote ile umesema kwamba gari ilipoharibika mlimpigia simu DCI?

Shahidi: Ndiyo nilisema

Kibatala:  Kuna mahala ukisema pale Aishi Hotel Kingai alishuka kwenda kumtafuta Moses Lijenje?

Kibatala:  Kingai alikuwa anamfahamau Lijenje..

Shahidi: Hapana ila…

Kibatala:  Hakuna Cha ila hapa, ushajibu Swali

Kibatala:  Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo P12

Kibatala:  Shahidi nionyeshe hapa sehemu ambayo umejeza discription za zile risasi tatu 

Shahidi: Sikujaza swala la risasi kwenye seizure certificate

Kibatala:  Lakini unajua kuwa seizure certificate ndiyo inaonyesha chain of custody ya mali mnazokamata?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala:  Kielelezo namba P12 imeandikwa jina na saini ya anayekabidhiwa?

Shahidi: Ni sahihi   

Kibatala:  Tusomee mtu anaye kabidhiwa

Shahidi: H 4347 Detective Goodluck

Kibatala:  Hilo ndilo jina lake..?

Shahidi: Ndiyo kwa mujibu wa kazi zetu

Kibatala:  Ulipo jaza wewe kuna signature au hakuna?

Shahidi: Hakuna

Kibatala:  Ulielezea mahakama kwanini hakuna signature ?

Shahidi: Hapana

Kibatala:  Mpaka mnaenda Arusha kwa dada yake Lijenje Arusha, je mnyafahamu majina yake? 

Shahidi: Hapana

Kibatala:  Mlikuwa mnajua Lijenje pale Moshi anakaa Hotel gani?

Shahidi: Hotel mbalimbali

Kibatala:  Tutajie Hotel mbili 

Shahidi: Hapana Sizifahamu

Kibatala:  Nafikiri nimemaliza Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali Robert Kidando anasimama

Wakili wa Serikali: Shahidi, ukionyeshwa kuwa sehemu ya jina la H4347 kuna jina na hakuna sahihi lakini kwenye jina lako umeweka sahihi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba kupatiwa vielelezo P11, 12 na 13

John: OBJECTION Mheshimiwa Jaji hiyo ni fact mpya ya ufafanuzi

Shahidi: Kwa sababu askari mdogo hatakiwi kuweka saini ya kukoroga anaweza namba yake ya kazi tuh

Jaji: Rudia swali ambapo halitaleta majibu mapya

Wakili wa Serikali: Shahidi ukionyeshwa kuwa sehemu ya jina la H4347  kuna jina na hakuna sahihi lakini kwenye jina lako umeweka sahihi?

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji sisi tuna haki hiyo kwa mujibu wa sheria, siyo kama tunakatazwa

Dickson Matata: OBJECTION bado ni fact mpya hiyo

Wakili Peter Kibatala:  Mheshimiwa Jaji nafikiri wapewe nafasi ila nasisi tunaomba kurudi upya kwenye swali hilo

Jaji: Sawa ulizeni nitawapa upande wa utetezi nafasi ya kirudi tena

Wakili wa Serikali: Shahidi, ukionyeshwa kuwa sehemu ya jina la H4347  kuna jina na hakuna sahihi lakini kwenye jina lako umeweka sahihi?

Wakili wa Serikali: Kuna hiki kielelezo cha P13  maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa tatu?

Shahidi: Kwa sababu askari mdogo atakiwi kuweka saini ya kuklroga anaweza namba yake ya kazi tuh

Wakili wa Serikali: Kwa mujibu wa statement hii uliulizwa swali kama mohammed ling’wenya kuhusiana na mpango wa kulipua vituo vya mafuta kuhusu vilipuzi ukasema hakukueleza 

Shahidi: Ni sahihi

Wakili wa Serikali: Sasa yeye alikueleza nini?

Shahidi: Alieleza nchi nzima haku specify sehemu moja

Wakili wa Serikali: Uliulizwa hapa kuhusiana na Deni Urio kuhusiana na kuweka mtego ilikumpa mshitakiwa wa nne kesi ya kisiasa

Shahidi: Si Kweli 

Shahidi: Alileta taarifa mwenyewe wala hakutumwa na mtu

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusiana kuwakamata wakina Gabriel na Khalid KUW mliwakamata sababu walipita 92 Kj,  Je unasemaje?

Wakili Malya: OBJECTION! Neno wapo tayari hakusema

Shahidi: Si kweli tukiwa kamata wakiwa sababu walizungumza na washitakiwa na wakawa wapo tayari kujiumga

Jaji anasoma na kumbukumbu haionyeshi kuwa walikuwa wanampango wa kwenda kujiunga

Wakili wa Serikali: Basi Mheshimiwa Jaji neno mpango wa kujiunga liondoke

Wakili wa Serikali: Tufafanulie exactly ni mwezi upi Khalid na Gabriel walikutana mshitakiwa wa tatu Dar es Salaam 

Shahidi: Ni mwezi wa saba

Wakili wa Serikali: Ulitoa taarifa hapa kwamba ACP Kingai kuwa hakwepo Tarehe 09 August 2020 hakwepo Mbweni, hebu tufafanulie hapo

Shahidi: Ni kwa sababu tulikuwa na shughuli ya kuendelea kumtafuta mtuhumiwa Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia kuhusiana na upekuzi na ukamataji pale Rau Madukani kwamba baada ya kukamata bastola ulimtuma Goodluck kwenye gari na ukasema hakuna aliyekwenda na Goodluck kufuata seizure certificate tufafanulie kwanini ikitokea hivyo

Shahidi: Baada ya kukamata nilisema namba na wote walisikia, ndipo nikamtuma Goodluck na yeye mwenyewe ndiye aliye rudi na hiyo silaha

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia kuwa kama unajua kuwa mshitakiwa Freeman Mbowe alikamatwa Mwanza akiwa kwenye mkutano wa katiba ukasema ufahamu, je nini unachofahamu?

Wakili Mallya: OBJECTION! Hayo ni majibu mapya tena yanajikoroga na majibu ya awali

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia kama ulikuwa na maslahi binafsi na washitakiwa

Shahidi: Ni nacho fahamu ni kuwa alikamatwa Mwanza kwa tuhuma za ugaidi

Shahidi: Niliwakamata kwa Sababu ya tuhuma ambazo zimekuwa riported Polisi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusu na askari aliyesimamisha daladala na kuhusu taarifa za yule dereva, ukasema hapakuwa na umuhimi 

Shahidi: Hapa kuwa na umuhimu kwa sababu tulimkamata kisheria na ndiyo maana mpaka sasa yupo mahakamani

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusu simu mbili za mshtakiwa ukasema hilo hujakitolea ushahidi

Shahidi: Ni kwa sababu siyo mimi niliyemkamata wala kufanyia upekuzi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusu mshitakiwa wa tatu Kufanya VIP protection ukasema siyo kosa, ulikuwa unamaanisha nini?

Shahidi: Kwa sababu siyo Kosa akama unafanya kwa nia njema ila ni kosa unafanya kama jinai

Wakili Dickson OBJECTION! Hapo mbele majibu mayapinga sababu hakusema mwanzo

Jaji: Kwa ufafanuzi huu sioni shida

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia katika kielelezo hicho pia, kuhusiana kile kilicho hamasishwa kufanya maandamano nchi nzima ni kosa au siyo kosa ukasema inategemea?

Shahidi: Kufanya maandamano kwa kufuata sheria siyo kosa

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia kuhusu Mkoa gani umetajwa kufanya maandamano, ukasema hakuna je ni kitu gani kimesemwa?

Shahidi: Kufanya maandamano nchi nzima na Mikoa ipo ndani ya nchi

Wakili wa Serikali: Sambamba na hilo katika statement hiyo umeulizwa kuhusiana na suala la mshitakiwa wa tatu kupewa pesa yaanauki pale Morogoro kwa jili ya VIP protection ukasema siyo kosa sababu inategemea na malengo

Wakili Dickson: OBJECTIO! N swali hilo siku sema hivyo

Shahidi: Nilikuwa namaanisha kwamba pale walipokelewa na kuweka mahabusu ndiyo wanaandikishwa kwenye detention register

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia kuhusiana na ule muda wa ukamataji ukasema ilikuwa ni saa 7 mchana na pia uliandika kwenye hati ya upekuzi

Na ukasema muda huo ulikuwa muda sasa sana je, ulikuwa umaanisha nini?

Shahidi: Nilikuwa namaanisha haijavuka hiyo saa saba

Wakili wa Serikali: Pia uliulizwa hapa kwamba siku ya tarehe 09 August 2020 ndiyo siku uliwapeleka kituo cha Polisi Mbweni wewe na Mahita, ukasema siyo kweli, je unamanisha nini? 

Shahidi: Siyokweli kwamba tuliwapeleka kituo cha Polisi Mbweni tarehe 09 August bali ilikuwa tarehe 08 August 2020

Wakili wa Serikali: Pia umeulizwa kwamba mlienda Arusha, ukaulizwa kama ikiwa unamfahamu majina ya huyo dada yake Lijenje, Nyumba au mtaa ukasema ufahamu, hebu tufafanulie

Shahidi: Ni Kwa sababu wao watuhumiwa ndiyo walikuwa wanatupeleka kila sehemu

Wakili wa Serikali: Uliulizwa a kuhusu kuto mkamata mshitakiwa wa nne baada ya wengine watatu kukamatwa zaidi ya mwaka mmoja ukasema upelelezi ulikuwa unaendelea, je ni upelelezi upi?

Shahidi: Masuala la forensics na upelelezi mwingine ulikuwa unaendelea

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia maswali kuwa katika bastola hiyo uliyo kamata ilikuwa ina maeneo ambayo yangeweza kutoa finger prints ukasema ni kweli, lakini haujaleta mahakamani?

Shahidi: Nikweli sikuleta ushahidi wa finger prints kwa sababu hapakuwa na mahala kwamba silaha hiyo ilikuwa haina ubishi kuwa inamilikiwa na mtuhumiwa

Wakili wa Serikali: Jana uliulizwa kuhusu katazo la ku-unload silaha, ukasema  inategemea, je ulikuwa unamanisha nini?

Shahidi: Ni silaha ambayo imekuwa eneo la tukio ndiyo haitakiwi kuna unload lakini silaha ambayo unataka ku seize na umeioata kwa mtu unaruhusiwa ku unload kuona kuna kitu gani, ndiyo nilichomanisha

Wakili wa Serikali: Uliulizwa hapa kuhusu mshitakiwa wa tatu kuhusu kwenda kwa mlinzi wa amani ila ukasema hukuona sababu ya  kwenda  na wala hakuhitaji

Shahidi: Ni Kwa sababu alikuwa tayari kujaza maelezo na hakuona haja ya kwenda kwa mlinzi wa amani

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia Ktk Utendaji wa shughuli zenu mmekuwa mkishirikiana na mamlaka mbalimbali za kiserikali, sasa tufafanulie ni ushirikiano gani huwa mnapeana

Shahidi: Ni kweli tunashirikiana na vyombo mbalimbali vya usalama lakini ni kwa ngazi za juu

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba kukomea hapo hatutokuwa na swali linguine.

Jaji: Kuna maeneo mawili ambayo mnayarudia upande wa utetezi

Shahidi: Hayo Sikusema

Kibatala:  Uliposema kuwa maofisa wa chini ulimaanisha nini?

Shahidi: Kuanzia staff sarjent kurudi chini

Kibatala:  Je Detective Coplo anatakiwa Kusaini au Lah? 

Shahidi: Hatakiwi Kusaini

Kibatala:  Kwa ruhusa ya  mahakama naomba usome hapa

Shahidi: Ni afisa wa chini

Kibatala:  Amesaini au hajasaini?

Shahidi: Amesaini

Matata: jana wakati nakufanyia dodoso nilikuuliza mtu kupewa nauli na pesa ya matumizi njiani ni kosa au siyo kosa ukasema siyo kosa

Leo wakati unafanyiwa re-examination ukasema siyo kosa kama ulipewa kwa nia njema

Sasa chukua hiyo statement nionyeshe sehemu ambayo Mohammed Ling’wenya amesema alipewa hiyo pesa ya nauli na matumizi ya njiani kwa nia ovu

Shahidi: Hakuna aliposema

Wakili Matata: Mheshimiwa Jaji sina swali linguine.

Jaji aandika kidogo mahakama ipo kimya kidogo

Jaji: Baada ya maswali hayo kuulizwa upande wa serikali maswali lolote.?

Jaji: Mmemaliza na shahidi: wa nane?

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ndiyo Mheshimiwa Jaji

Jaji: Shahidi tunakuahukuru kwa ushahidi: wako

Shahidi: anatoka na kuondoka kizimbani

Hivyo tunaomba ahirisho la kesi hii ili kuja kuendelea kesho kutwa alhamisi tarehe 13 January 2022 ambapo tutaleta shahidi: mwingine kuja kuendelea na ushahidi.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji huyo  ndiye shahidi: tukiyekuwa naye leo

Na pamoja na kwamba sasa ni saa saba mchana hatukuweza kujua shahidi huyu angeweza kumalizia saa ngapi

Hivyo tunaomba ahirisho mpka kesho kutwa kama nilivyo omba, ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji

Wakili Peter Kibatala:  Hatuna pingamizi Mheshimiwa Jaji.

Washitakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpaka Siku hiyo

Jaji: Basi maombi ya ahirisho yanakubaliwa mpaka kesho kutwa Alhamisi ya tarehe 13 January 2022

Jaji anatoka

Like
2