JAJI AMEINGIA MAHAKAMANI MUDA HUU SAA 3 NA DAKIKA 40
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling’wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na
Abdallah Chavula
Nassoro Katuga
Esther Martin
Tulimanywa Majige
Ignasi Mwinuka
Wakili Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala
Nipo pamoja na
Nashon Nkungu
Gabriel Munishi kwa Niaba ya John Malya
Dickson Matata
Gaston Garubindi
Alex Massaba
Maria Mushi
Michael Mwangasa
Jaji Mshitakiwa namba Moja, Mbili, Tatu na Namba Nne
Wote wanaitika Wapo
Wakili wa Serikali Robert Kidando Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na tulikuwa tunaendelea Kujibu, Tupo tayari Kuendelea
Wakili Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji Basi pia tupo Tayari Kuendelea
Wakili wa Serikali Robert Kidando Mheshimiwa Jaji tunaomba Kuendelea, Tulikuwa bado tupo Kwenye Majibu yetu katika Swala Zima La Chain of Custody
Mheshimiwa Jaji tulikuwa tumefika kwenye Hoja ya Kwamba, Kadri ya Certificate of Seizure itakayokuwa imeitwa
Tunaendelea Kwa Kusema Kwamba Pamoja na Mawakili Wa Utetezi Kurejea Vifungu Vya PGO Vya 229 na 282,Sisi tunasema Kwamba PGO zote Mbili hazina Uhusiano na Pingamizi hili
Kwa sababu PGO namba 229 lina zungumzia Kuhusiana (2)a Kutoa Jukumu la Jumla la Utunzaji wa Vielelezo Kwa Polisi
Na hivyo katika PGO hiyohiyo ya 229 (4)c yenyewe inataka Askari aliyeondosha Vielelezo aandike alichokifanya Katika Notebook
Na PGO 282 ndiyo ambayo inaweza Takwa la Matumizi ya Notebook kwa ajili ya Kuandika Hatua Kadhaa ambazo Askari anazichukia Ikiwemo Uchukuaji wa Vielelezo
Lakini Vifungu Vyote Vya PGO havija we kwa Kuwa Ni Takwa linalo husiana na Admissibility
Mheshimiwa Jaji Hoja yetu inaenda Sambamba hata Walipo rejea Kifungu cha 22(4) katika Sheria Ya Uhujumu Uchumi, Kwamba Kielelezo baada ya kesi kirudishwe Kwa Mmiliki
Mheshimiwa Jaji Hoja yetu ni Kwamba Shahidi ameweza Kuonyesha Chain of Custody Kwa Viwango vinavyokibalika Kisheria
Tunaomba Kurejesha Mahakama Yako Katika Shauri La Tenatus MKOKA Vs JAMHURI, (Reported) TOR 2003 Katika Ukurasa wa 245
Kwamba Shahidi Wetu ameonyesha Kwamba Anaomba Kutoa Vielelezo na Kwamba ameonyesha Ni Vielelezo Vilevile alivyovikamata
Mheshimiwa Jaji tunaomba kukurejesha katika Shauri Lingine ya Mahakama ya Rufaa la KENNEDY SHAYO na WENZAKE Vs JAMHURI Rufaa ya Jinai ya Mwaka 2017 Kesi namba 84 Kesi Iliyoketi Arusha, Katika Ukurasa Wa 32
Kwa Kesi hii inasisitiza Kwamba Vielelezo Vilivyoletwa Mahakamani, kwa Nature Vile Vilivyo siyo Vile ambavyo unaweza Kuvibadili kiurahisi
Katika Viwango Vyake Shahidi Aliweza Kuna nyesha Swala hilo
Mheshimiwa Jaji Hoja yetu Nyingine Kabla hatuja maliza Chain of Custody, Pamoja na Wenzetu Kurejea zile GUIDELINES Walipo rejea Chapter 03 paragraph 02 point 08 walipokuwa wa nasisitiza Swala la Chain aof Custody
Ni Hoja yetu Kwamba hiyo paragraph 08 siyo Swala Pekee Linaloongoza Mahakama Katika Admissibility sibility isipokuwa tunaomba Kurejesha Mahakama Katika Chapter hiyohiyo ya tatu paragraph 03 point 02 inayotoa Mahakama kuongozwa na Authentication, Relevance na Competence
Irene Lema: Mheshimiwa Jaji Kwa Kumalizia tunaomba Mahakama Yako, Ione Kwamba Upande wa Utetezi Katika Hoja zao Hakuna Hata Moja ambaye ameweza Kuonyesha either Kwamba Upekuzi haukufanyika kabisa, au Kwamba zile items ambazo zimekuwa Sarved kama zilivyo onyeshwa Katika Kielelezo namba 14 ni Tofauti na ambavyo vimewasilishwa Mahakamani
Kwa hiyo tunaomba Uone Hoja zao Hazina Mashiko na Utupilie Mbali
Mheshimiwa Jaji tunaomba twende Kwenye Hoja Nyingine ya Kisheria ambapo Mawakili Wasomi Walichallenge Competence ya Shahidi namba 08 katika Kutoa Vielelezo ambavyo anavileta Mahakamani
Mheshimiwa Jaji Hoja hii ilishaingia jitokeza Wakati Wakili Msomi Nashon Nkungu anawasilisha Hoja yake
Na Vilevile Ili jitokeza Wakati Wakili Msomi Malya katika Pingamiz lake la Kwanza, Lakini Pia Pingamizi la Wakili Msomi Dickson Matata Na Lakini Pia Pingamizi la Wakili Msomi Kibatala Katika Pingamizi Lake la Kwanza
Mheshimiwa Jaji tunaomba Kujibu Pingamizi Hilo kwa Pamoja
Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho letu Kwamba Shahidi Namba 08 ASP JUMANNE MALANGAHE ni Competent Kutoa Vielelezo alivyo Vi Wasilisha hapa Mahakamani na Kuomba Kwamba Vipokelewe
Kwa sababu ya Jukumu alilolitimiza Siku ya Tarehe 10 August 2020, kwa sababu Ndiye aliyekuwa Afisa Mkamataji wa hizo Items
Na ni Wasilisho letu Kwamba Katika Hatua hii ya kutoa Vielelezo hivyo si haitaji la Kisheria Kwamba ni lazima aonyeshe Ujuzi
Yani Specialist ya Utambuzi Kwamba Kwa Items hizo na wala Hakutakiwa hata Kama aliwahi Kufanya kazi JWTZ
Isipokuwa Mheshimiwa Jaji katika Hatua yake hiyo ya Kukamata hizo Items inatosha Kutoa Utambuzi Kama ambavyo ameonyesha Katika Ushahidi Wake
Na katika Ushahidi Wake aliongozwa Kuzungumzia Kuhusiana na Mwonekano Wa Items hizo, kwa a Maana ya Rangi na Physical Appearance
Lakini pia alienda Mbali Kwa Kuonyesha alama X/HD Kwamba Ndiyo alama alizoziweka na akazungumzia Katika Ushahidi Wake kabla amba ni hizo alama. Na zile alizo Semaa awali Kwamba Ndiyo zilimuwezesha Kuzitambua
Mheshimiwa Jaji katika Hoja hiyo iliibuliwa Shahidi Hakusema ni wakati Gani aliweka Ile alama ya X/HD, Mheshimiwa Jaji ni Kumbukumbu zetu Kwamba Shahidi alisema Kwamba alifanya hivyo baada ya Kukamlisha Upekuzi na kabla hajajaza Certificate of Seizure, Hivyo Ushahidi Wake unaonyesha
Irene Lema: Mheshimiwa Jaji katika Eneo la Competence iliibuliwa Hoja Kwamba Hizo Items ambazo Shahidi anaomba kuzitoa zinaweza Kupatikana Mahala Popote
Kwamba Shahidi alitakiwa aonyeshe Kwamba Items hizo zimetambuliwa na JWTZ au JKT
Wakati huo huo Mawakili Walikuwa wana admit (kukubali) kwamba Those are Complex Items na Hasa wakili Matata alidai Kwamba Shahidi alifanya Conclusion Kwamba items hizo ni za JESHI JWTZ badala la Kusema Kwamba alikuwa anazitilia Mashaka
Basi akaomba Mahakama Itamke Kwamba Shahidi Siyo Competent, Wakili Malya alienda Mbali zaidi Kwa Kuanza Kufanya Utambuzi Yeye Mwenyewe, Tena all the fikia Wakati ambapo alichallenge Kile Kilicho one kana katika Kielelezo namba 14 kama Ponjol yeye akasema Kwamba ni Rain Coat
Akaenda Mbali zaidi akasema Items hizo siyo za JWTZ Bali za UNITED NATIONS
Mheshimiwa Jaji Kwa Heshima Kwa Hoja hizi walijielekeza Vibaya
Kwa sababu Zifuatazo, Ya Kwanza
1.Maswala Waliyo yaibua no Factual na hayawezi Kutumika Katika Hoja hii ya Admissibility sibility
Kwa sababu Mahakama Katika Hatua iliyopo Haipo Katika Nafasi ya Kupima hicho ambacho Mawakili wamekiibua Kwa Sababu a Kinatakiwa Kije kwa Njia ya Ushahidi
2.kutokana na Ile attempt ya Kusema Vitu Hivi Vinaweza Kupatikana Popote na Wakili Malya akaja na Majina anayiyajua yeye, Katika Kuchallenge Competence ya Shahidi
Mheshimiwa Jaji Imeshajitoleza Mahakamani Mara Kadhaa kwa Mawakili Kuibua Vitu Kutoka kwake (Statement From the Bar) ambapo Kisheria Hazina nafasi kabisa Katika Hatua hii, na Ni Maneno ambayo Hayana Msaada Kwa Mahakama Katika Ku resolve Pingamizi la Kisheria la aina hiyo Kama lilivyoibuliwa
Mheshimiwa Jaji Swala la Competence ya Shahidi ilishatolewa Uamuzi katika kesi ya THE REPUBLIC Vs CHARLES GAZILABO NA WENZAKE WATATU ambayo ni Rufaa ya Jinai Namba 358 ya Mwaka 2019 Mahakama Iliyoketi Dar es Salaam Ukurasa wa 12 na 13
Vitu Vilivyotakiwa katika Shauri hilo tunaona Shahidi Wetu amevitimiza, Toka ametaja katika Ushahidi Wake Mpaka Hatua hii
Mheshimiwa Jaji ilikuwa Pia katika Hoja hiyo hiyo ya Competence katika Kutambua Hoja Hizo hapa Mahakamani, ilikuwa Kwamba Shahidi ajaonyesha Unique Features ya Kile ambacho Wakili Msomi Kibatala akikiita Kwamba Kile Kilivhosemwa na Shahidi namba 08 ni Inherent Features na akatofautisha na Unique Features
Mheshimiwa Jaji hata Kwa Maamuzi Kadhaa hapa Mahakamani hatuja kutana na Hilo Kitu Kinaitwa Inherent features, Maamuzi Mengi yamekuwa yakisisitiza Kuhusu Unique Features na Ni Wasilisho letu Kwamba Shahidi ameonyesha Unique futures
Sisi tunasema Kwamba Hizo ambazo Wakili Msomi Kibatala anasema ni Inherent Features ndiyo tunasema ni Unique Features na Shahidi Wetu amezionyeaha hapa Mahakamani
Na Shahidi Wetu akaenda Mbali akaonyesha alama alizoziweka Yeye za X/HD
Hivyo Mheshimiwa Jaji ni Hoja yetu Kuwa Kwamba Shahidi Namba 08 ameweza Kuonyesha Competence Yake ya Kutoa hizo Items ambazo aliomba Kuzitoa Hapa Mahakamani
Kwa Kuonyesha ni Jinsi gani alivyo vipata na Kuvishughukikia
Na ameonyesha Ujuzi wake wa Kuitambua (Identify) kwa Vigezo Vyote Viwili Vya unique features (Special Marks) na ameonyesha kuwa items hizo ni Competent na zinaweza Kupokelewa na Mahakama hii
Hivyo katika Vipingamizi Vyote Vinavyo husiana na Competence, Tunaona Kwamba Hayana Mashiko na Tunaomba uyatupilie Mbali
Mheshimiwa Jaji tunaomba tena Kwenda Kwenye Pingamizi Lingine ambapo Pingamizi hili lililetwa na Nashon Nkungu na Wakili Peter Kibatala ambapo walidai Kwamba hizi Items zinataka Kutolewa Mahakamani na Shahidi namba 08, Walidai Kwamba aina hiyo ya Ushahidi Kama ambavyo ilikuwa Listed Katika Kielelezo namba 14 ni Ushahidi ambao hatukuwa listed Wakati wa Commital Proceedings
Wakadia Kwamba Wanshangaa kwa Kuleta Ushahidi Wa aina hiyo bila Kuleta Kwa Kutumia Kifungu cha 289 cha Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai, Kwa a kutoa Notisi Katika Kutaka Kutumia Ushahidi huu
Mheshimiwa Jaji Hoja hii haina Mashiko Kisheria, kwa Sababu Ushahidi huo siyo Mpya kama ambavyo Mawakili Wanadai, Ushahidi Huo ulikwepo Tangu Wakati Commital Proceedings zinafanyika na Ushahidi Huo Ulisomwa Mahakamani kwa Mujibu wa Rule 8(2) ya Rules ya Mahakama hii za Mwaka 2016 na Swala hilo Mheshimiwa Jaji linajionyesha katika Ukurasa Wa 32 na 33 wa Proceedings Za Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu
Na to be Specific, ya Zile Rules inaonyesha zipo Items namba 10 na Kuhusiana na Order Za Mahakama Inaonyesha Ipo Kwemye Ukurasa Wa 32 katika 8(2)
Mheshimiwa Jaji Kama Ushahidi Ulikwepo Katika Item Namba 10 na Baadae Kielelezo namba 14 Kina kuja Kupokelewa na Mahakama hii, Ikiwa Ndiyo Shahidi ameomba Kuzitoa Items zilezile
Mheshimiwa Jaji Wakati Commital Proceedings zinaendelea palikuwa na Commitment Kuwa patakuqa na Physical Exhibit Wakati wa Usikilizwaji
Hatua ambayo Mheshimiwa Jaji tuliizingatia, Na Jambo hilo Mheshimiwa Jaji Kilifanyika Katika Mahakama Kuu ya Divisheni ya a Makosa ya Uhujumu Uchumi Katika PH ya tarehe 10 September 2021
Hivyo Mheshimiwa Jaji Pamoja na Wakili Peter Kibatala Kurejea Shauri La RAMADHAN Vs JAMHURI sisi tunaona Mazingira ya Shauri hili ni tofauti na Wala haiwezi Kutumika akatika Shauri Hili
Wala Jamhuri hatukutakiwa kutumia Kifungu cha 289 cha CPA Katika Kuleta Ushahidi huu
Mheshimiwa Jaji Kwa sababu Kuna Kanuni ya 8 ya Rules za Mahakama hii, Ni Wasilisho letu Kwamba Kanuni hii inajitosheleza na Hatuwezi tena Kutumia Kifungu cha 246 cha Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai
Hivyo Kwa Kusema hivyo Mheshimiwa Jaji, Tunaomba Hoja hii uione Haina Mashiko na uitupilie Mbali
Mheshimiwa Jaji tunaomba Kwenda Kwenye Hoja Nyingine Ambapo wakili Msomi Malya ambapo alidai kuwa Items hizi ambazo Shahidi namba 08 aliomba Kutoa Hapa Mahakamani ni Counter Evidence, Hivyo Visipokelewe
Na Hoja hii alisisitiza Kwamba Ile Notebook ambayo ipo Kwenye Items Namba 08 ya Kielelezo namba 14, Ionekane Kwamba alificha na ataki Kuleta Mahakamani Kwa sababu anajua Kilichopo Ndani
Ni Item ambayo pia no Kati ya vitu ambavyo Mashitakiwa amekutwa navyo Kwake
Mheshimiwa Jaji Hoja hii tumeijibu sana Katika Kujibu Hoja ya Kwanza ya Wakili Nashon Nkungu Ila tutaongeza Vitu Vichache
Kwanza Shahidi Namba 08 alieleza Kwamba ni Kwanini ajaleta Hicho Kielelezo items namba 08 Kwa sababu hakuhusisha na Tuhuma
Na Hayo Mambo Mengine ambayo Wakili Malya akiyaibua, Kwa sababu ni Statement from The Bar tunaona hayana nafasi kabisa Katika Swala la Admissibility
Tunaomba Kurejesha Mahakama Yako tukufu katika Maamuzi ya Mahakama Rufaa Kwamba Statement Ya Mawakili haiwezi Kutumika kwa sababu ni Kauli from The Bar katika Kesi ya TRANS AFRICA ASSURANCE COMPANY LTD Vs CIMBRIA (EA) East African Law Report 2002 Volume 02
Hivyo tunaomba Uitupilie mbali
Mheshimiwa Jaji Hoja Nyingine Ilikuwa ni Kuhusu Karatasi katika Kidaftari, akasema Kwamba hawakufahamishwa Kwamba pikuwa na Karatasi, Hivyo Imekuwa ni Strange Kwao na Hiyo ika angukia Katika Hoja yao Kwamba Ushahidi Umekuwa Ultered
Mheshimiwa Jaji Utaratibu uliopo na unaofahamika Kwamba Mkurugenzi Wa Mashitaka anapokamilisha na Kufungua Mashitaka Mahakama Kuu, Huwa anapeleka INFORMATION na Information hii ni
1.Hati Ya Mashitaka
2.Statement
3.Ushahidi ambao Jamuhuri utautumia Wakati wa Trial
Na Kwa Mujibu wa Utaratibu ni kwamba Mshitakiwa ama Wakili Wake Pia watapata Wakala wa Information pamoja na statement za Ushahidi na Documents Zote ambazo DPP atafile
Mheshimiwa Jaji Document za Commital Siyo sehemu ya Ushahidi Kama ambayo Shahidi Namba nane anatoa Ushahidi Sasa hivi Ikiwemo Ufafanuzi Wa Vielelezo
Mheshimiwa Jaji Kwa Mujibu wa Proceedings Za Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu katika Ukurasa Wa 33 Item namba 12 Daftari hilo lenye Five Star Limeorodheshwa na Kama Ilivyo kamawaida Mheshimiwa Hakimu alisema Kwamba Matakwa ya Rule 08 (02) a
yametekelezwa Ikiwemo Matakwa ya hicho Kidaftari
Na akama ivyo Utaratibu tunatoa Copy ya Nyaraka zote, Na Hakuna Sehemu yoyote ya Kidaftari hicho ambayo halikuwa Commited na sisi tuKiangalia hiyo sehemu ya hiyo Pinned ilikuwa Commited, Mheshimiwa Jaji Ndiyo Utaona hapa hiyo sehemu ya BIG BON Kariakoo, Inajionyesha wazi
Kwa Hoja hiyo haiwezi Kutumika Katika Kukataa katika a Kupokelewa Kwa Kielelezo hicho ambacho Shahidi Wa Nane ameomba Kutoa Hapa Mahakamani
Mheshimiwa Jaji tunaomba tena Kwenda Kwenye Hoja Nyingine aliyoibua Kaka yetu Wakili Kibatala Kwamba Kumekuwa na Ukiukwaji wa PGO 229 (10)
Kwamba Hakuna Matakwa Ya Kisheria Katika Ukuambatanisha na Kumtambulisha Items zilizopo Mahakamani
Mheshimiwa Jaji Ni Wasilisho letu Kwamba PGO 229 haina Jambo lolote la Kufanya Katika Swala la Admissibility
Mheshimiwa Jaji PGO 229 ni Muongozo Unaotumika Katika Upelelezi inapokuja Swala zima la Vielelezo hivyo Vichambuliwe (CLASSIFIED, na LEBELING)
Mheshimiwa Jaji Vielelezo ambavyo shahidi Wa 08 ameomba Kuvitoa Mahakamani amevilebel Yeye Mwenyewe
X/HD na Lebeling inafanyika Ili Kujihakikishia Kwamba Vielelezo Ulivyo kamata vinapofika Mahakamani no Vielelezo Vilevile Kama. Ambavyo Ukivikamata
Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho letu Kwamba Lebeling iyofanya Shahidi wa Nane ni ya Kisheria na Inakidhi Vigezo Vya Sura namba 08, Paragraph 3.8 (f)iv ya Exhibit Management ambayo inataja Mazingira ya aina tatu Kwamba Kielelezo Lazima Kiwe Lebeled
Mheshimiwa Jaji kama tulivyotangulia kusema PGO ya 229 haihusiani na Swala la Admissibility isipokuwa Kanuni za 08, Paragraph 3.8 zimetoa General Rule
Items hizi zimetimiza Kanuni zote za Kisheria, Tunaomba Uone Kwamba uhitaji na Vigezo Vya Kisheria kama alivyo fanya kulingana na Hizo Guidelines ambazo tumesharejea Vimekidhi
Hivyo Mheshimiwa Jaji tunaomba Uone pia Kwamba hiyo Hoja ya Vigezo vinakoaa Misingi ya Kisheria
Mheshimiwa Jaji ilikuwa Pia Hoja ya ushahidi wa namba 08 husiani na Shahidi namba 08 Kwa sababu Shahidi anasema Kwamba alifanya Upekuzi Yombo Kilakala lakini Kielelezo Namba 14 Kinaonyesha Upekuzi Ulifanyika Kilakala Temeke
Ni Wasilisho letu Kwamba Ushahidi Wa Shahidi namba 08 una Uhusiana na Kile Kilichopo Katika Kielelezo namba 14
Na siyo Kweli Kwamba eneo Lililoanyiwa Upekuzi Kama Wakili alivyo ihalika Mahakama Kupitia Kifungu Cha 59(1) kupitia Sheria ya Ushahidi Kwamba Kilakala ni Morogoro
Mheshimiwa Jaji Ushahidi Wa Shahidi Wa 08 upo wazi Kabisa, na Tangu anatoa Ushahidi alizumgumzia Kwamba Mtuhumiwa wa Kwanza anamakazi Temeke na Akaendelea Kusema Walifanya Upelelezi Mpaka walipofaniliwanKuoata a Makazi ya Mshitakiwa Wa Kwanza Temeke Huko huko, na Wakagika Eneo kinaitwa Kilakala na Upekuzi huo Ulifanyika Mbele ya Mashahidi Na Kwamba Baada ya Upekuzi Shahidi namba 08 anasema alimrudisha Shahidi Kituo Cha Polisi Chang’ombe
Sasa Wakili anahusisha Seizure Certificate Na Kilakala Ya Morogoro, Tunaona Mwenzetu ameshindwa Ku appreciate Ushahidi Wa shahidi namba 08 na ambao ndiyo Umetoa Kielelezo namba 14 ambapo Kipo Mahakamani Hivi Sasa
Mheshimiwa Jaji Shahidi namba 08 ukipata Kuona Ushahidi Wake, Shahidi alizumgumzia hili eneo la Kilakala ni Mtaa, Ndiyo a
Maana katika Ushahidi Wake alisema aliyeshuhudia ni Kiongozi wa Mtaa huo
Hivyo Mheshimiwa Jaji tunaomba Uone Kwamba invitation ya Wakili Kibatala Kuhusiana na Swala hili halina Mashiko Kisheria, Lakini hata Tafsiri ya Sheria hakuielewa
Mheshimiwa Jaji Mahakama hii Inachopaswa kama Kweli imekwepo au Ni sehemu ambayo Mahakama hii inge Hitaji kutumia Judicial Notice, Kifungu hicho cha 59(1) hilo Swala
Linahusiana na Muda na Geographical Division of the World
Mheshimiwa Jaji Unaweza Kuangalia, Kama tuliweza Kumsikia Vizuri, aliweka Hoja yake Kwamba Uchukue Hoja ya Geographical Division, Kwa Kutambua Kilakala ipo Morogoro
Mheshimiwa Jaji Kwa sababu Neno lilltumika na World, Ingekuwa ime intend kuchukua Mitaa Ingekuwa kitu cha Hatari Sana
Hivyo tunaomba Mheshimiwa Jaji Uone Kwamba Tafsiri aliyoitoa Mwenzetu hapa Siyo Sahihi
Na Kwa Vyovyote Vile tunaona Hoja hiyo Haina Mashiko Kisheria
Mheshimiwa Jaji naomba kwenda Kwenye point Nyingine ambapo Wakili Msomi Kibatala isema Kwamba PGO ya 226 (2) ilikiukwa wakati akisisitiza ile Hoja ya Kwamba Mwenye Mamlaka ya Kuingia Kwenye Upekuzi Ni OFICER COMMANDER OF STATION au OC CID, Au Maofisa Wanafanya kazi Chini yake Kwa Maelekezo yake
Kabla na baada ya Upekuzi Mnatakiwa Kuriport Kwa Hakimu Vitu gani Vimepatikana Kwenye Upekuzi
Mheshimiwa Jaji sisi tunasema Kwamba hiyo PGO ya 226 ina Mu accommodate Shahidi namba 08 kama alivyo fanya Upekuzi
Kwa sababu Baada tuh ya Maneno ya OC Station, PC CID Kuna Maneno Immediately ya Maafisa Upelelezi pale mbele
Mheshimiwa Jaji Shahidi Namba 08 anasema Tangu awali Kwamba alikuwa katika Jukumu lake la Kiupelelezi
Hivyo Upekuzi alioufanya Ulikuwa unaruhusiwa Kisheria, pamoja na Kwamba Katika Ushahidi Wake Hakuna Mahala alipo onyesha Kwamba ali Riport either Kabla au Baada kwa Hakimu, Hatuoni Tatizo hilo Kwamba Vielelezo alivyo kamata Vinaweza Visipokelewe Mahakama Vielelezo
Mheshimiwa Jaji Mahakama ya Rufaa Uamuzi Unaonyesha Kuhusiana na Swala la Kuto Riport kwa Hakimu ni la DPP Vs FREEMAN AIKAEL MBOWE la 2020,katika Ukurasa Wa 13 na 14 Mahakama Ya Rufaa Ilitoa Kifungu cha 38 cha CPA, Mahakama Ilisema hilo Pekee Haiwezi Kushusha Thamani ya Ushahidi huu
Hata Hapa Mheshimiwa Jaji Ukiangalia ni swala la Kwemda kwenye Ushahidi huo lakini siyo Wakati wa Admissibility
Hivyo Mheshimiwa Jaji tunaomba Uone Kwamba Hoja hiyo Haina Mashiko
Mheshimiwa Jaji tunaomba twende Kwenye PGO ya 226 (2)d Mheshimiwa Jaji tumeshalijibi hilobla Nexus kwa hoja ya Nashon Nkungu Wakati Wa Hoja yake kupitia Kifungu cha 38 cha CPA
Hoja yaoja ya Nyongeza ni Wakili Peter Kibatala alisema Kwamba Shahidi wa 08 Hakuongozwa Kuhusiana na Swala Zima La Risiti
Sisi tunaona Masharti yote Shahidi Wa Nane Alisha ya maliza Yeye Mwenyewe Kwa Kuandaa Risiti kwwnakuanda Hati ya Ukamataji Mali
Na Hoja Nyingine tumeshazisemea wakati tunajibu wakili Msomi Nashon Nkungu
Mheshimiwa Jaji Wakili Peter Kibatala alisema Kwamba PGO 229 (19) imekuwa Violated kuhusiana na ni nani hasa aliyekuwa anatunza Vielelezo hivi, na akadai Kwamba Yule Sarjent Johnstone ambaye alitaja na Shahidi Wa 08,Shahidi Wa nane Hakusema Kwamba Ndiye aliyekuwa Mtunza Vielelezo na Kwamba aka Question Swala la Chain of Custody kuhusu Vielelezo hivi
Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho letu Kwamba Shahidi Namba 08 ameonyesha Kwamba Sarjent Johnstone ndiye aliyekuwa Mtunza Vielelezo, Ushahidi Huo ameutoa, toa Ushahidi Wa Kumkabidhi na Ndiyo aliye mpatia Vielelezo hivyo Wakati akivileta Mahakamani
Na katika Ushahidi Wa Shahidi namba 08 Ameweza Ku Establish Chain of Custody na ameweza Ku authenticate katika Ushahidi Wake
Kwamba Nyaraka alizokabidhiwa alikagua na kuhakilki kama ni vyenyewe
Kwa Maana yale Mavazi, lakini pia ni Kidaftari, Ambapo anakiri Kuongezeka Lebel Kwenye Kile Kidaftari ambapo Hiyo Lebel Hakuweka yeye
Mheshimiwa Jaji yale Masharti Yaliyopo katika PGO ya 229 (19) Hatuoni kwa Vyovyote kama ya naweza Kutumika Kukataa Ushahidi
Tunaona Shahidi Wetu Katika Hoja ya Adminsibility ameonyesha ninwapi alipeleka na Vikatunzwa Mpaka Leo Kuvileta Mahakamani
Mheshimiwa Jaji Wakili Msomi Kibatala alikualika Kufanya Reconciliation Katika Maamuzi Uliyo kwisha Kutoa Wakati wa Kupokea Vielelezo
Anakualika Upya Kuhusiana NA Matakwa ya PGO
Mheshimiwa Jaji Maombi hayo hayapo katika Mfumo wetu wa Kisheria, Sehemu yoyote ile Hakunaga Reconciliation
Mheshimiwa Jaji tulijatibu Kufikiria, Hata a Kujaribu Kupata Maana yake, Haipo, Na Ombi kama hilo haiwezi Kuwa Entertained na Mahakama
Kwa sababu Mahakama Siku zote Inatakiwa Kutoa Uamuzi Kwa Mambo ambayo yameletwa kwa sahihi Mbele ya Hakimu au Jaji
Na Mahakama zetu zimekuwa na Coexistence Zinapotoa Uamuzi zimekuwa zinazingatia Sheria
Ni Ombi letu Mheshimiwa Jaji Ukatae Mwaliko huu
Mheshimiwa Jaji Kwa Kumalizia, Tunaomba Uone Kwamba Mapingamizi ayiye yaliyoletwa hayana Mashiko Kisheria na Yanastahili Kitupiliwa Mbali na Tunaomba Uone Kwamba Vielelezo hivi ambavyo Shahidi Wa 08 anaomba Kutoa Mahakamani ni Vielelezo Vinavyo weza Kupokelewa Mahakamani Kama Ushahidi Wa 08
Kwa sababu Vielelezo Hivi vimeshuhudiwa Kama Vielelezo Vikivyojazwa Katika Kielelezo namba 14
Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji
Wakili wa Serikali Robert Kidando akaa Chini baa submission yao
Wakili Nashon Nkungu Mheshimiwa Jaji Tumesikia Majibu Ya Mawakili wa Serikali
Kwa niaba ya Mshitakiwa Wa Kwanza, Kuna Baadhi ya Maamuzi ambayo yametumika Na wenzetu wakati Wa Kuwasilisha tungeomba na Sisi tupatiwe, Maamuzi ya Kama GEZILAHABO na KENNEDY SHAYO
Jaji Nakumbuka yalishawahi Kutoka kabla, Tumekuwa tukiyatumia
Wakili Nashon Nkungu Mimi Sijawahi Kupata
Nashon Nkungu Mheshimiwa Jaji Kwa Kuanza Wakili amesema Kwamba tumeshindwa Kuelewa Matakwa Ya PGO 229 (2) a na 229 (4)c ni Majibu yetu ni Kwamba PGO hizi zipo Very Clear na Msingi wake ni Kutaka Kuonyesha Inapotoka Pale eneo la Upekuzi Kwenda Kwingine
Sheria Imeonyesha Kwamba AliiLinda na Kuitunza Kabla havijaingia Mahakamani Na Kuja Kuonyesha alikuwa anatunza sana
Na Mheshimiwa Jaji hata Ukisoma Muongozo Wa Mahakama Inaelezea Hivyo hivyo
Ni Exhibit Management Guidelines 3.8 inasema Kwamba……….. “It Is chronological Paper…”
Hapo Sasa anataka Kigezo Kimoja Kimoja
Hapa Kinachosisistizwa na Chronological Paper Trade, Kama Kielelezo Kilitunzwa Sahihi
Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji ambacho hicho akijaongelewa kabisa Wenzetu naona walipitiwa, Kwetu ni Muhimu sana
3.8. “Chain of Custody
In a legal context, chain of custody means the sequential order which a piece of evidence is to be handled while the case is under investigation. It is a chronological paper trail that exhibits are collected, handled, analyzed, or otherwise controlled from seizure to exhibition. It contains the following principles:”
Ni Takwa la Kisheria Kwamba Shahidi lazima alete paper Trade
Na Mheshimiwa Jaji Nirudie Wasilisho langu Jana Kuhusu Sura ya 03 ya Exhibit Management Guidelines inasisitiza Kwamba Records inatakiwa kuwepo
Ni Takwa la Kisheria Kwamba Shahidi lazima alete paper Trade
Na Mheshimiwa Jaji Nirudie Wasilisho langu Jana Kuhusu Sura ya 03 ya Exhibit Management Guidelines inasisitiza Kwamba Records inatakiwa kuwepo
Mtu ambaye alihamisha, alihamisha Vipi na Kutoka Eneo Moja Mpaka Lingine
Shahidi amesema Kwamba aliona Kielelezo Namba 08 Hakina Umuhimu akaona akiache kwa Mdomo tuh
Section za CAP 200 zote zinaeleza namba ya Kudili na Vielelezo, Ilikuwa ni lazima Askari tumie Sheria
Na Sheria inasema kama Akiona haitaji Mara Moja alitakiwa Kumrudisha Muhusika Mwenyewe
Na Pia Kwamba Kuna Kielelezo Kilikuwa tempered, Tayari Kielelezo Kipo tofauti hapo na Kilivyochukuliwa
Mheshimiwa Jaji Ukisoma hapo Explanation inaweza Kutoka Kwa Mkuu wa huyo Askari Iwe Kwa Uzuri au Kwa Ubaya
Na Mheshimiwa Jaji usisahau Kutolewa kwa Ushahidi Huu Kuna tokana na Kielelezo namba 14
Mheshimiwa Jaji Swala la Lebeling Sisi tulikataa Kwamba Kilicho fanyika siyo Lebeling Kwa sababu Lebeling Siyo zoezi ambalo Mtu anaweza Kujitungia Bali ni zoezi la Kisheria
Kilicho fanyika siyo Lebeling, Kilicho fanyika no Illegal Kwa sababu Tayari Umeshaanza Kuharibu Ushahidi Kwa kuchorachora, Lebeling Hakuna
Sisi tunakubalina nao Kwamba Kielelezo Must be Lebeled na Maana ya Lebeling Nimeeleza Katika Wasilisho langu, Uwezi Ku Lebel Kwa Aina Moja tuh X /HD KWA Vielelezo Vyote bila serial number
Hiyo Lebel ya X/HD anajua Shahidi peke yake tuh, Shahidi ameanza Kuharibu Ushahidi Kwa a kuanza Kuchora Chora wakati Hakuna Sheria Yoyote Inayomruhusu
Mheshimiwa Jaji Naomba Niondoe Fallacy Moja ambayo inatajwa Kujemgwa kwamba Issue Ya Chain of Custody Kwamba haitotumika Katika Admissibility
Mtu anaye weza Kusema hilo Ni Mtu ambaye hajawahi Kushiriki Kesi hii Mahakamani, Ni Kuipotosha Mahakama Kwa Kusema Kwamba Issue Ya Chain of Custody hautakiwi Kuwa applied Katika Admission ya Kielelezo
Dhumuni la Chain Of Custody ni Kuhakikisha Kwamba Kielelezo Kinatoa eneo la Tukio Mpaka Kinapogonga Milango ya Mahakama
Mheshimiwa Jaji Kuna Hoja Nyingine Mbayo Shahidi ameeleza Mazingira ni Jinsi gani ameleta Mahakamani
Especially Mimi Kwa Upande wangu nilihoji kwanini alipeleka Makao Makuu, Kitu ambacho ni wrong kwa sababu siyo Makao Makuu
Swali langu pia ilikuwa ni Vipi Kutoka Chumba Cha Mwendesha Mshitaka Kuja Mahakamani, na Shahidi Hakusema Kwamba alikiacha Kielelezo Chumba Cha Mashitaka Kwa Muda gani
Na Mahakama Yako unajua wazi Kwamba aliyetumwa Kuleta hakutujwa ana Shahidi Wala Hakutoa funguo na wala Hakueleza hayo Shahidi
Na Mheshimiwa Jaji Swala. Lingine ambalo linashangaza ni Kwamba Eti Kutoka na Nature ya Ushahidi wa wenyewe
Sisi tunasema Kwamba Vinaweza Kubadirika Kiurahisi kwa sababu Kwanza Havijawa Lebeled na Pili Hajavieleta Mwenyewe Hapa Mahakamani
Vilevile Mheshimiwa Jaji Ni kuhusu Seizure Certificate ndiyo Risiti, Sisi tuna Manta in Kwamba Sheria Haiku Kosa Maneno Kutumia maneno Mawili tofauti
Hawakutaka Kuchanganya watu tuh, Hizi ni Document Mbili tofauti na Purpose zake ni tofauti, Certificate of Seizure ni Nyaraka Ya Kukamatia Mali wakati Risiti Kazi yake ni Ku Acknowledge
Na haya Maneno siyo Yangu Mheshimiwa Jaji, Ukisoma Guidelines Zinasema Kazi ya Risiti ni Ku Acknowledge
Na Ukiangalia Kwenye Sheria, Makosa ya Uhujumu Uchumi Maswala ya Seizure Yatatumia Kifungu Cha 22(1) na Ukaenda Kusoma Utagundua Ndiyo Unazungumzia Juu ya Ukamataji Mali
Lakini Swala la Risiti Linaelezwa Katika 22(4) Kama Swala Tofauti
Mheshimiwa Jaji Wakili Msomi Robert Kidando Alianza Kusema hizo PGO haihusiani na Admissibility
Mheshimiwa Jaji huu ni Upotofu kwa sababu Mahakama Kuu hii kupitia Exhibit Management inasema Kila Kimoja na Kazi yake
Tulieleza Kuhusu Police Notebook ambayo Askari ataandika na ataibeba wakati wote akiwa Kazini na at atakiwa Kuja nayo Mahakamani Kwamba ni Kweli chain of Custody na Sheria ilifuatwa
Na Sheria ipo wazi Kwamba Askari atakiwi kuamini Kumbukumbu zake kwa sababu Haya Ni Maswala la Maisha ya Watu, na Pia Sheria Imemuonya Askari Kwamba atakiwi Kuamini Kumbukumbu zake kwa sababu Yeye ni Mwanadamu
Exhibit Admission inatakiwa a Kufuata hivi Vyote na Kama Haijafuata Mambo haya tunasema Kielelezo Kilikuwa Ilegally obtained
Mheshimiwa Jaji nitaenda Kwenye kesi ya Renatus MKOKA, Nimepitia Kesi hii yote Hakuna Jambo ambalo Wakili wa Serikali Robert Kidando amesema, Namimi na ihalika Mahakama Kusoma
Kinachosemwa ni Kwamba Prosecuton Wanalalamikiwa na Mahakama Kwamba Hawa kuweza Kufanya Jukumu lao La Vielelezo Kuingia Mahakamani Vikiwa Clear of Doubts
Hii Kesi naomba itumie Upande wetu
Mahakama Itumie Upande wetu
Mheshimiwa Jaji Swala la Upekuzi siyo sehemu ya Pingamizi Letu na sijui Kwanini Wakili Msomi Majibu hilo
Sisi tunasema Je Ni Kweli Vilivyochukuliwa ndiyo Vilivyoletwa Mahakamani, Huko Ndiyo Kuthibitisha Kwa Kuleta Paper Trade
Na Mahakama inaenda Kwa Nyaraka Siyo Maneno
ZNa Mheshimiwa Jaji Swala la Knowledge, Wakili anasema siyo katika Hatua hii shahidi aonyeshe Ujuzi, Hapana ahaikuwa Point yetu
Sisi tukichosema Kwamba Juu ya Ushahidi ulikuwa Unatolewa, Shahidi ajaonyesha Sufficient Knowledge, Kwa hakika Shahidi alikuwa anasema hizi ni Uniform za JWTZ, Sisi tunasema ilikusema Kwamba Hizo ni Uniform Za JWTZ pana Hitaji Knowledge
Na swala La Lebeling, knowledge ya Shahidi Bado Inayumba Sana
Mheshimiwa Jaji Kesi ya CHARLES GAZILABO Na MIZIRAHI ni Kesi tofauti na hazifanani
Ukiona Mle ndani Ilivyo Ilikuwa na Watu Competent Wa Kuja Kueleza Ushahidi huo na Identification
Mheshimiwa Jaji nakazia Wasilisho langu Kwa kuzingatia Kanuni Kwamba Nyaraka inapaswa kuwa Clearly Cleared
Na swala la Chain Of Custody, haitakiwi Kuwa Brocked Kwa namna yoyote ile
Na Vielelezo Vimetoka katika Mlolomgo ambao siyo wa Kisheria
Na Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho Langu Kwamba Vifungu Chumzima Vimekuwa violated( Kwa kuvunjwa sheria)
Kuchukuliwa Kwa Vielelezo hivi Kutakomaza Askari Kuchukua Vielelezo bila Kufuata Sheria
Kuchukuliwa Kwa Vielelezo Hivi Kunavunja Haki za Wateja wetu
Kutofuatwa Kwa Hizi Sheria pamoja na PGO, Mahakama ya Rufaa Ilisha Sema ni lazima Sheria hizo zifuatwe Je ni Kwanini Mahakama yake ichukue Vielelezo hivi alafu Isubiri tena Mahakama ya Rufaa itengue Uamuzi huo wakati Jambo Lipo wazi
Tunaomba Mahakama Yako Iangalie Sheria zote zilizovunjwa, Mahakama Iangalie inataka Ku archive nini kwa Kutaka Kuchukua Nyaraka ambazo zimechukuliwa kwa Kuvunjwa sheria
Mheshimiwa Jaji ni hayo tuh
Jaji Naona tuendelee Saa nane
Wakili Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji Wakili Dickson Matata anaumwa sana kama Unavyomuona, Naomba Tumalizie Kabisa tukiondoka tumeondoka, akapumzike
Wakili wa Serikali Robert Kidando Sawa Mheshimiwa
Jaji Sawa tuendelee
WAKILI GABRIEL MUNISHI (kwa Niaba ya Wakili John Malya)
Nimesikia Wakili wa Serikali akijibu Submission inchief ya Wakili John Malya, Naunga Mkono bado Hoja za John Malya alizotoa Kwenye Submission
Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji
Dickson Matata
Wakili Dickson Matata Mheshimiwa Jaji Naunga Mkono alicho Submit Wakili Nashon Nkungu, na Kutoka Na Hali yangu Namuachia Wakili Peter Kibatala
Wakili Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji Wakati anajibu Mapingamizi Yetu alijibu kutumia Kesi ya ILUMINATUS MKOKA,
Na Kesi ya MAYALA MBITI Kesi namba 177 ya Mwaka 2019 Ukurasa wa 6 na 7
Pamoja na Wewe Ulipoamua Kwenye Swala la Chain of Custody
Ulionyesha Kwamba hako Ka Components ni Muhimu sana na Ukawapa Faida Upande wa Mashitaka, Tunaomba tukualike Ufanye vilevile
Pia Kwemye Kesi ya KENNEDY SHAYO AND OTHERS Kwamba Items ambazo wamezitoa, Hakuna items Rahisi Kama Clothes ambazo Zimekuwa Lebeled Kwa Maandishi
Ndiyo Maana Wajuzi Wa Mambo Wakatunga PGO ya 229 (10) kwenye Lebeling Ya Nguo ili Kuzia Kutemper na Ushahidi
Sasa Shahidi ameamua Kuweka Aina ya Lebel zake yeye, Ku Legislate Ushahidi Wake, Je yeye ni Legislation Authority
Hii Mark Ame Apply Universally, Sheria imesema waweke Lebel Kutofautisha
PGO ya 229 ilitumgwa ilikuondoa Utata, Ilikuondoa Pre trial Legislation
PGO ni Public Police, Mtu anapokiuka ni against Public policy
Ndiyo Maana Nikasema Kwenye Submission inchief Kwamba kwamba kama tunakataa PGO tunaiua tuache Kuitumia Sasa
Mheshimiwa Jaji naikumbusha Mahakama Kwamba Shahidi Huyu alijivika Ufahamu zaidi, With certainity Kwamba Hivi ni Vifaa Vya Kijeshi, JWTZ
Kama aliamua Kuvitoa Vifaa Vile alipaswa amalize kabisa Kwa Kusema namna akivyogundua hizi ni Nguo za Jeshi
Kuna tufauti Ya Kupokea Nguo na Kupokea Nguo za Jeshi JWTZ
Sisi ndiyo Tunasema Kwamba hakuonyesha his Competence Ability
Sisi tunajibu Kwa Jinsi Ombi la Shahidi Kilivyo kuja, Anaomba Mahakama Ipokee Nguo za Jeshi, Je anaushahidi Huo.?
Tena Wenzetu hawajaelwa Kuhusu hizo alama, Siyo Naturally imposed Kama Mabaka, Bali ni Mark alizo weka Yeye Mwenyewe
Anasema aliweka X /HD kama alama
Je katika Ushahidi Wake Shahidi alisema Kwamba aliweka hizo alama Mbele ya Mashahidi Wa Ushuhuda
Je alisema Kwamba alizo weka Mbele ya Mashahidi..?
Kwanini alitofautisha Uwekaji wa alama na Ushuhuda wa Mashahidi
Je Shahidi alisema Kaba aliweka alama Mbele ya Mashahidi
Jibu ni Hapana na Jibu Kama Hapana, Haiwezi Kuingia Mheshimiwa Jaji
Jibu ni Hapana na Jibu Kama Hapana, Haiwezi Kuingia Mheshimiwa Jaji
Kwahiyo CHARLES GAZILABO haiwezi KuSaidia hapa
Na Mheshimiwa Jaji Wakati Inaangalia Kuhusu Muhuri, Wa Mahakama Ukaulizwa Kwamba Muhuri Wa Mahakama ni External Features sasa Kwa Vipimo Vilevile Maneno X/HD tunaomba yapitishwe Katika Tanuru lilelile kama Ulivyo fanya Kwenye Muhuri
Tunasisitiza PGO 229 (8,9,10 na 11) Wenzetu Wakati wanajibu wamejikita Kwenye PGO ya 229 (10) tuh
Mheshimiwa Jaji Pia Mwenzangu alikubali Kwamba Hakuna Mtu aliyeomba Kutumia 289 ya CPA
Hakuna Ubishi Kwamba Kifungu Hicho Kimetungwa Kwamba Panapokiwa na Ushahidi Wa ziada au Kielelezo Cha Ziada lazima Kufanyiwa Maombi
Sisi Mheshimiwa Jaji tunasisitiza Kwamba Katika Commital Proceedings Hutooona Ponjol wala Nguo za JKT, au JWTZ
Na Katika Commital Proceedings Kila Kitu Kinapswa Kutajwa Kwa Uwazi, Lakini Ukienda Kwenye hiyo Item Ya 10 kama anayosema, Ukienda Ukakuta haitaji basi inapaswa Kuwa ni Msaada kwa Upande wetu (in our favour
Pia Mheshimiwa Jaji Kwakusema Kwamba Walisema Kwenye Commital alafu hapohapo anasema Kwamba Walinotify Kwamba Kuna Additional Evidence Watatoa Mbeleni
Mbona ni Mambo Mawili tofauti yanajipinga , Walisema au walisema Wataleta.?
Tunaomba Mahakama Ikapitie Hapo
Pia akuna Point Ndogo tunaomba utitumie Mheshimiwa Jaji Wakati wa Uamuzi wako, Kwa Mujibu wa Commital Proceedings Kuna Certificate of Seizure dated 05 08 2020 Kwamba ilikamatwa Bastola na Hiyo Bastola Ilikuwa Listed Separately
Je kwanini Bastola ambayo ina Certificate of Seizure Imekuwa Mentioned Separately kwenye Commital Proceedings, Je tutatofautisha Vipi Kanuni hiyo hiyo Kwa Kutaja Bastola alafu Huku usijate
Katika Ukurasa 32 Kuna Seizure Certificate Mbili za Tarehe 05 August 2020
Na Item namba 06 kuna Bastola Imetajwa
Vipi Kuhusu Item namba 10 ambayo inahusu Nguo Mbona hazitajatwa Zenyewe Kama Nguo
Mheshimiwa Jaji Hoja ya Tatu wanasema Kwamba Katika PH hizo Items ambazo Waliomba Kuzitoa zilikuwa listed
Hii naomba Kuita PH white Wash Evidence, Kwa sababu PH ni PH na Commital ni Commital
Na tunakazia Kwa Kesi ya RONJINO
Kuhusiana na Ultered Evidence Kwamba Kuna Daftari ameliondoa kwa hiyo Kinachoitwa sasa ni Ultered Evidence
Wenzetu wanasema Kwamba Ushahidi Huo Ulisomwa wakati Wa Commital
Wakili wa Serikali Robert Kidando Mheshimiwa Hoja ya Ultered Evidence ni Hoja ya Malya, Hatuoni Kwanini Kibatala ajibu yeye wakati Wakili Mwakilishi Wa Malya ameshasema anakazia
Wakili Peter Kibatala Naomba Mahakama inikumbushe Kwamba Kama Wakili wa Serikali Robert Kidando Hakusema Kuhusu Kidaftari
Jaji Siyo Kidaftari ambacho Kimeondolewa ni Kidaftari Chekundu
Hoja yangu Je ni sahihi kwa wao Kuchoma Vitu ambavyo Vimesomwa Kwenye Commital na Kuleta Baadhi, na Kama Hivyo Ndiyo Siyo Kuchezea Ushahidi Wa Commital
Kuhusu kwamba Hoja Malya nisijibu Mimi, Naomba Siku Nyingine Waje na Sheria ambayo inakataza Wakili Mwingine Kutokujibu Hoja ya Wakili Mwingine
Kuhusu PGO 229 (10) Sisi tunasema Ni part of Authentication kuhusu Admissibility Pamoja na Kwamba ni Kuhusu Upelelezi lakini aliyetunga hiyo PGO alijua Kwamba Ushahidi huo lazima Utakuja nao Mahakamani
Kama Una Ushahidi Unataka Kuleta Mahakamani Lazima tutakuuliza Je ume Comply na PGO kama Ni Ushahidi Wa Kukaa Ofisini sisi hatutokufuata huko
Na Mheshimiwa Jaji Kuhusu Kilakala Temeke, Kama Ushahidi Wa Shahidi, Katika Kielelezo namba 14 Mashahidi walijitambulisha Kwamba Wapo Kilakala, na Shahidi namba 08 Yupo Temeke Kilakala
Sisi tunasisitiza Kwamba Shahidi Wakati anaomgozwa Hakusema Kwamba Kilakala Ya pale Juu na Kilakala Temeke hapo Chini ni Kitu Kimoja, Hakuongozwa kufafanua
Wakati wa Uamuzi Wako Kuhusiana na Barua kuwa inapaswa ifafanuliwe
Kuhusu Hoja ya Kwamba Division of the World ni Kuhusu Maabara na Nchi, Hapana hiyo ni Tafsiri yake, Mimi nasema inashuka Mpaka Level ya Mtaa
Mimi nasema Kwamba Kuna Utofauti Wa Kilakala, Na Kilakala Temeke Kuna utofauti
Naomba Mahakama Ikatae
Mheshimiwa Jaji Kuhusu PGO 226 (2)4 Mwenzangu Hajapinga Kwamba Riport Haikwenda Kwa Hakimu
Na PGO hiyo Uliwekwa kwa sababu PGO ilitambua Polisi ni Shahidi Ni Shahidi Mwenye Maslahi ya Upelelezi Ndiyo Maana Ikaonekana Pawe na Authentication ya mtu huru ambaye ni Hakimu
Na Yeye Katika Kutetea hilo ameturejeaha Kwenye kesi ya Mbowe na Esther Matiko Kesi ambayo Tulikuwa tunaendesha Sisi
Hiyo ilikuwa ni Kuhusu Matumizi ya Maneno “Shall” Hakuna Permissive Rule ya Kuingiza Ushahidi Mahakamani ambao Haukupitia kwa Hakimu Katika Mahakama hii
Vyovyote itakayokuwa, alicho Sema hapa ni Impeachment na siyo Admissibility
Mheshimiwa Jaji Kesi ya TRANS AFRICA ASSURANCE COMPANY LTD ni Tofauti kwa Sababu Ilikuwa inazungumzia Wakili Kuzungumzia Mkataba
Lakini Bado haiokoi hizo Items, Tunasisitiza Kwa Mujibu wa PGO 226 (2)d no Fatal kwa sababu Risiti ni Part ya authentication, na Hii hatujajibiwa Vya kutosha
Kuhusiana Na 229 (19) kwamba anayepaswa Kutunza Vielelezo ni OCS au OC CID au Afisa aliyeteuliwa na na OCS sasa Shahidi Hakusema hilo na Kama Hakusema hatuwezi kumjazia Maneno kutoka Kwenye Prosecuton Bar
Na sisi tunasisitiza, a Kwamba hii Lebeling Inapaswa ifanyike kwa Mujibu wa 229 (10) KWA Mujibu wa Sheria Hata Swala la Serial ni Swala la Kisheria
Ndiyo Maana hata katika Guidelines 3.8, Kwamba kumlimda Mshitakiwa Dhidi ya Kumbambikia Mshitakiwa na Ushahidi lazima Kanuni hizi na Sheria zifuatwe
Na Kwa Maoni yetu Kwamba Vielelezo Vinaenda Kinyume Public policy, Guidelines na Sheria na Inawakosesha Haki zao Washtakiwa
Ni hayo TUH Mheshimiwa Jaji
Kibatala Nakala Chini
Jaji anaandika Kidogo
Wakati Jaji anaandika Kidogo, Hali za Ki Afya Mahakamani siyo Nzuri asilimia 60 Watu wanakohoa Kuanzia Askari Magereza Mpaka Watuhumiwa na Wahudhuriaji
Jaji naomba Mawakili Wa pande zote tuonane Ofisini
Jaji anatoka
Jaji amerejea Mahakamani
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Ling’wenya Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani
Wakili wa Serikali Robert Kidando Mheshimiwa Jaji Upande wa Jamhuri tupo Kama tulivyo kuwa awali
Wakili Peter Kibatala Na sisi pia Mheshimiwa Jaji
Jaji BAda ya Kukubaliana Pande zote Mbili Tumekubaliana Kuhairisha Shauri hili Mpaka Tarehe 10 January
Washitakiwa wataendelea Kuwa Rumande chini ya Magereza Mpka Mtakapoletwa Tarehe hiyo
Jaji anatoka Nje