MESSI, RONALDO WAIBUKA VINARA WA MABAO 2021 KWENYE VILABU VYAO VYA ZAMANI

WACHEZA soka bora kwa miongo miwili mfululizo, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, wamemaliza kalenda ya soka ya mwaka 2021 wakiwa vinara wa mabao katika vilabu vyao vya zamani, Barcelona na Juventus, licha ya nyota hao kuondoka kwenye vilabu hivyo katika dirisha dogo la usajili barani Ulaya.

Messi aliondoka Camp Nou na kujiunga na miamba wa Ufaransa, Paris Saint Germain (PSG), tarehe 11, mwezi Agosti huku Cristiano akiwashtua wengi kwa kurejea Manchester United wiki tatu baadaye.

Mpaka sasa, msimu wa soka wa 2021-22 umefikia nusu huku timu za Barcelona na Juventus zikikisa mchezaji wa kufikisha idadi ya mabao waliyofunga wachezaji hao wawili kabla ya kuondoka.

Kabla ya kandarasi yake kutamatika, Messi alipachika mabao 28 akiwa Barcelona na hakuna aliyemkaribia kwa idadi ya mabao. Hata baada ya mechi ya juzi Jumanne kati ya Barcelona na Sevilla uliomalizika kwa sare ya 1-1 bado hakuna aliyefikisha idadi ya mabao ya Messi.

Mchezo huo ulikamilisha ratiba ya michezo kwa mwaka 2021 kwa timu ya Barcelona.

Upande wa pili, Cristiano aliipachikia timu ya Juventus jumla ya mabao 20 katika mashindano yote kabla ya kujiunga na timu yake ya zamani ya Manchester United katika majira ya joto.

Idadi yake hiyo, imemfanya abaki kileleni kama mcehzaji mwenye mabao mengi klabuni hapo baada ya Juve kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Cagliari juzi Jumanne, mchezo wa mwisho kwa Juventus kwa mwaka 2021 huku wakijiandaa kuivaa Napoli tarehe 6, mwezi Januari, 2022.

Kwa mwaka 2021, timu ya Barcelona, ilipachika jumla ya mabao 108 katika mashindano yote huku Messi akifunga mabao 28 kati ya hao kabla ya kujiunga na PSG mwezi Agosti.

Idadi ya mabao ya Messi inakaribia mara mbili ya mchezaji anayemfutia kwa mabao mengi klabuni Barcelona, Antoine Griezmann ambaye pia alijiunga na Atletico Madrid kwa mkopo mwezi Septemba.

Barcelona (Mabao 108 katika mashindano yote mwaka 2021)

Lionel Messi – 28
Antoine Griezmann – 15
Memphis Depay – 8
Frenkie de Jong – 7
Ousmane Dembele -6
Ansu Fati, Jordi Alba, Martin Braithwaite – 4
Gerard Pique, Ronald Araujo, Francisco Trincao – 3
Pedri, Oscar Mingueza, Sergino Dest, Sergi Roberto, Philippe Coutinho, Nicolas Gonzalez, (Bao la kuhifunga) – 2
1: Riqui Puig, Junior Firpo, Ilaix Moriba, Luuk de Jong, Sergio Aguero, Sergio Busquets, Abde Ezzalzouli, Ferran Jutgla, Gavi – 1

Juventus (Mabao 106 katika mashindano yote mwaka 2021)

Baada ya Cristiano kuondoka, Juventus wamepita katika kipindi kigumu sana hasa mbele ya lango msimu huu. Mpaka sasa wapo katika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi huku wakiwa ndio timu yenye idadi ndogo zaidi ya mabao ya kufunga katika timu nane kwenye msimamo wa ligi.

Cristiano Ronaldo – 20
Alvaro Morata – 17
Federico Chiesa-15
Paulo Dybala-11
Juan Cuadrado, Weston McKennie – 6
Dejan Kulusevski – 5
Adrien Rabiot, Moise Kean – 4
Alex Sandro, Leonardo Bonucci – 3
Aaron Ramsey, Matthijs de Ligt, Manuel Locatelli – 2
Danilo, Hamza Rafia, Arthur, Gianluca Frabotta, Federico Bernardeschi, (Bao la kujifunga) – 1

Like
4