Kichekesho cha “ushindi” wa John Pombe Magufuli


HAKUNA lugha yenye uwezo wa kueleza kilichotokea katika uchaguzi mkuu wa Tanzania 2020. Waweza kusema “haramu,” “unajisi wa demokrasia”, “ubakaji uliokithiri,” “uhaini dhidi ya mamlaka ya wananchi,” au ” uchaguzi ambao haukufanyika.”

Haya yote yamefanywa na binadamu wenzetu “walioapa” kutenda haki na wanaojinadi kwa kusema kuwa msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Hawa wanaenda kwenye nyumba za ibada kila mara, ni wajenzi wa misikiti na makanisa, na wanajitapa kuwa ni wapinga rushwa na ubadhilifu.

Kwa kutumia tume ya uchaguzi, jeshi la polisi, watumishi wa serikali na majaji, wamepanga na kutekeleza dhuluma hii ya kihistoria.

Walifanya nini?

Orodha ni ndefu. Bila kuvunja katiba, ikubalike mchakato huu uhojiwe, si na mahakama bali na wananchi wenyewe. Watu wengi wako tayari kutoa ushahidi mbele ya kiapo kueleza kile kilichofanyika. Zinatajwa hujuma kadhaa, kwa mfano:


1. Wasimamizi wanne wa kila kituo cha kupewa kura kadhaa zilizopigwa na kuzificha mifukoni, kwenye soksi na kwingineko na kuingia nazo. vituoni, wakasubiri fursa mwafaka ya kuziingiza katika sanduku la kura.
2. Kuchelewesha kuruhusu mawakala wa upinzani ili waweze kutumbukiza kura zilizokwishapigwa.
3. Kuondoa mawakala vituoni kwa kutumia polisi ili waweze kuingiza kura.
4. Kujaza vitabu vya matokeo na kuvipeleka vituoni vikiwa tayari na matokeo ya mshindi hata kabla ya kurakuhesabiwa.
5. Kuwapa polisi kura zilizopigwa nao wakazipeleka vituoni.
6. Kukata umeme na kuhamisha masanduku ya kura, k.isha kuingiza mapya baada  ya kurejesha umeme.
7. Kuwapa baadhi ya makada na wafuasi wa CCM kura zilizopigwa tayari ili wawawepe wapiga kura wengine waliopangwa wazitumbukize wakati wanapiga kura.


Mbinu chafu nyingine ambazo ni nzito zaidi zinazohitaji kinga kuzitamka kwa sasa


Matokeo ya hujuma hizi ni kukosa umakini na kufanya makosa ya kushangaza ambayo tumeyashuhudia, kama ifuatavyo:
1. Kura za majimbo kadhaa ya mikoa tofauti kufanana kw aidadi.
2. Idadi ya kura zilizopigwa kuwa ndogo kuliko kura walizopata wagombea.
3. Ujumlishaji wa asilimia kuzidi asilimia  100
4.  Kupunguza kura za upinzani bila kuziondoa kwenye masanduku.
5. Tofauti kubwa kati ya takwimu zilizo majimboni na zile zinazotangazwa na tume.

Tume ya uchaguzi na walioiagiza kufanya vituko hivi hawakujioanga vema. Kama ni wizi wa kura, wao si wa kwanza. Hata Rais wa Kenya wa zamani Daniel arap Moi na Rais wa zamani wa Zaire Mobutu Seseseko walikuwa wanaiba kura. Y

oweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda wanaiba kura. Hata marais Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete waliiba kura. Lakini walikuwa makini kuliko Magufuli na tume yake walivyofanya sasa, maana wametumia nguvu iliyopitiliza, na wameacha nyayo zisizofutika, hata katika takwimu zao wenyewe.

Kwa mfano, wakati Tume ya Uchaguzi ilitangazia wananchi mwezi uliopita kuwa wapiga kura waliojiandikisha ni 29,804,992, jana wakati wanatangaza “mshindi” walisema kuwa wapiga kura waliojiandikisha ni 29,754,699.

Wanaweza kuleta maelezi yoyote yale lakini yatakuwa yale yale kama ya kikokotoo cha Polepole. Hayaingii kwa wenye akili timamu.

Tume imempatia Magufuli kura 12,516,252 na ikampatia Tundu Lissu kura 1,933,271. Walisahau kuwa Chadema pekee ina wanachama wasioopungua milioni nane, na ina mashabiki na wapenzi wasio wanachama.

Katika mazingira yoyote, hata kama miongoni mwao wangekuwemo wasiopiga kura, Lissu asingekosa kura milioni saba za wanachama wake pekee. Hizo 1.9 milioni walizompatia ni za kanda mbili ndogo za chama zikiunganishwa.

Pale walipodhamiria kumdhalilisha yeye, CCM na Tume ya Uchaguzi wamedhalilika wao, kwani wameiba kwa misuli badala ya akili. ndiyo maana hata wao wanashindwa kushangilia vema ushindi wao. Kwa wale wenye dhamiri bado zinawasumbua.

Like
2