Wanajeshi waliofanya maafa Zanzibar warejea Bara

IDADI kubwa ya wanajeshi wa Jeshi la Wananchi na polisi waliokuwa wamepelekwa Zanzibar kudhibiti wapinzani, jana walirejea Tanzania Bara wakiwa katika botizaabiria zitokazo Zanzibar hadi Dar es Salaam.

Wakiwa katika makundi, wanausalama hao walipanda boti zote za asubuhi saa 1.30 na zile zinazoondoka machana kutoka Bandari ya Zanzibar.

“Jamaa sasa wamemaliza kazi zao kuja kutuonea, wanarejea kwao bara, wakituachia maumivu tele,” alisema raia mmoja akieleza wenzake nje ya bandari.

Uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, Rais wa Jamhuri ya Muungano, wabunge,madiwani na wawakilishi ulianza Oktoba 27, kwa makundi maalum ya wanausalama na baadhi ya watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar na kukamilika siku iliyofuata. Baadhi ya wanajeshi hao kutoka Bara, wanadaiwa wakupiga kura Zanzibar.

Uchaguzi huo ulitawaliwa na vurugu aambazo zilisababisha vifo vya baadhi ya raia katika maeneo kakdhaa ya Pemba.

Fujo zaidi zinaripotiwa kutokea baina ya raia na wanajeshi na polisi, ambapo wanausalama hao walitumia silaha za kivita dhidi ya watu wasiokuwa na silaha.

Tayari ZEC imemtangaza mgombea wa chama tawala, CCM, Dk. Hussein Mwinyi, mtoto wa Rais mstaadu, Ali Hasan Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar- kwa asilimia 76.25, akimshinda mgombea wa ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sbariff Hamad, aliyetajwa kupata asilimia 19.

Hii ni mara ya kwanza kwa uchaguzi wa Zanzibar kuwa na tofauti kubwa kati ya mshindi na Maalim Seif ambaye amegombea kwa mara ya mfululizo. Katika mara zote hizo, ZEC imekuwa ikitangaza tofauti ya asilimia zosizozidi tatu. Ni kielelezo cha kiwango cha wizi wa kura ambao haujawahi kufanyika Zanzibar.

Like