Tume ya uchaguzi yatuhumiwa kuchapisha kura feki za rais

SERIKALI ya Tanzania inatuhumiwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchapisha karatasi za kura za urais katika kiwanda cha uchapishani cha Tanzania Printing Services (TPS) ili kuiba kura katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, 2020.

Kuna taarifa kuwa maboksi yaliyosheheni karatasi hizo zilizochapishwa na kiwanda hicho, yaliondolewa Jumapili iliyopita usiku na kusafirishwa kwenda mahali ambako hakujajulikana bado.

Shughuli ya uchaoaji huo imefanywa na watu wat maalumu,kwani wafanyakazi wa kiwanda hicho, kilichoko Dar es Salaam, eneo la Chang’ombe, Barabara ya Dakawa, walipewa likizo ghafla ya wiki moja, na kuacha usimamizi wa kiwanda mikononi mwa maofisa kadhaa wa serikali wanaodhaniwa kuwa makachero wa idara ya usalama.

Taarifa zinasema wafanyakazi hao walielezwa kuwa likizo hiyo imesababishwa na “matengenezo makubwa” yanayofanyika kiwandani hapo.

Hata hivyo, taarifa zaidi zinaeleza kwamba kuondolewa kwa wafanyakazi hao ilikuwa mbinu ya kutoa nafasi ya kuchapishwa kwa karatasi za kupigia kura. Haikufahamika mara moja idadi ya karatasi hizo na wapi zilikuwa zikipelekwa.

Wachache waliobakizwa ni wale wa kitengo cha uchapaji wa karatasi nyeti – security printing unit (SPU) – pekee.

Uchapaji huo umekuwa ukifanyika usiku pekee, na hakuna mtu aliyeruhusiwa kuingia na simu wala kuondoka na kipande chochote cha karatasi.

Hali hiyo imesababisha wasiwasi kwa baadhi ya wadadisi, na tayari baadhi ya wadau wa uchaguzi, wakiwemo chama kikuu cha upinzani, Chadema, wamelalamika na wasiwasi huo kuhusu uwepo wa karatasi za kupigia kura ambazo zitakuwa zimetengenezwa kinyemela kwa shabaha ya kuhujumu uchaguzi kama mbinu ya dola kumnusuru mgombea wa CCM, John Magufuli.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, aliituhumu NEC kwa kushirikiana na chama kilicho madarakani, CCM, kuiba kura jwa ajili ya Magufuli.

Awali Chadema ilidai karatasi hizo zinachapishwa na kiwanda cha Jamana, lakini watoa taarifa wetu wamesema sicho kilichohusika kuzichapa.

Mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda hicho, Mehbooob Kasum, alisema kiwanda chake hakiwezi kufanya kazi hiyo kwani ina lawama sana. Lakini alithibitisha kuwa jitihada za serikali kutaka kichape karatasi hizo zilikuwepo.

“Hii kazi sisi tuliikataa, kwani tunajua ina lawama sana. Tuliikataa, hata tuliposhawishiwa kuomba tenda. Hatukuomba sisi,” alisema.

SAUTI KUBWA inatambua kuwa waliopewa kazi “rasmi” ya kuchapisha karatasi hizoni kampuni iitwato MS Ren-Forms ya AfrikaKusini, kwa gharama za Sh bilioni 14.4.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekanusha tuhuma hizo za Chadema zilizotolewa na Mnyika.

Like